Vitambulisho vya wamachinga vyaingiza Bilioni 20. Dar yaongoza, RC Makonda apongezwa

Hii pesa yake huwa inaenda wapi?
kununua ndege au magari ya bashite maana kuna masoko imeacha kitimtimu,ile 500 waliyokuwa wantoa per day ilikuwa ianlipia usafi na ulinzi leo haitolewi tena,hiyo 20,000 hela zake zinapoenda haijulikani,halmashauri zipo hoi hata hela ya mabango walikatazwa kuchukua ingawa mabango yenyewe siku hizi matupu hakuna hata anayetangaza tena
 
Unaweza kulinganisha idadi ya wafanya biashara walioko Dar na wale walioko Katavi?!
 
Kwa akili yako ulitaka KATAVI ndio iongoze? Hujui kama Dar ndio chimbuko la wamachinga na asilimia kubwa ya wakazi wa Dar ni wamachinga? Hata hesabu ndogo namna hii mnashindwa kuifanya? Vitambulisho vilivyotolewa jiji la Dar ni vidogo sana kwa kweli, Dar hapakosekani wamamchinga laki tano.
 
Machadema bwana
Heko Bashite, Mkoa wake unaongoza kwa idadi yaya majumba makubwa, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya magari, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya wafanya kazi, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya boda boda, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya barabara zenye lami, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya ofisi za serikali, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya manispaa, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya klabu za michezo, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya watembea kwa miguu, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya makampuni binafsi, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya makao makuu ya mashirika, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya makazi ya mabalozi wa nje, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya wanawake wasio na waume, mkoa wake unaongoza kwa idadi ya mashoga, mkoa wake unaongoza kwa...ningeweza kujaza vitabu mia moja ila naishia hapo.

Kuwa mwana CCM ni laana tosha.
 
Katavi hata wauza matunda tu wanahesabika,
Na biashara ni pale centre karibu na stand na huku sokon pekee
Wangepewa pungufu hata robo ya walichopewa
Kweli nilikuwa kule miezi mitano iliyopita. Pale stand supu ya kutafuta.
 
Kwa akili yako ulitaka KATAVI ndio iongoze? Hujui kama Dar ndio chimbuko la wamachinga na asilimia kubwa ya wakazi wa Dar ni wamachinga? Hata hesabu ndogo namna hii mnashindwa kuifanya? Vitambulisho vilivyotolewa jiji la Dar ni vidogo sana kwa kweli, Dar hapakosekani wamamchinga laki tano.
Unauzungumziaje mkoa wa Tabora?
 
kaka mbona huku madawa bado tunauza kama kawa.Unaamini kabisa na wewe kuwa makonda anazuia madawa.Akili za chekechea huku hata kama gongo kama unahitaji ipo kibao,bangi,mirungi,upo kibao jumla na rejareja.Tunapatikana maeneo yote,kuanzia posta,ferry,keko,kariakoo,mwananyamala,kigogo,kitunda,buguruni,Tandika,ubungo,sinza,Tandale,mpaka gongo la mboto.Kama ulifikiri biashara imekufa basi wewe ndo ulikufa ufufuke sasa katika wafu.Kumbuka bunduki haiui ila watu ndo wanaua hivyo hivyo hata madawa ya kulevya hayana shida watu ndo wanashida ila jiulize kwa nini wanaokuja kununua madawa kwetu ni wengi na vya kutosha na hali wanajua kuwa ni hatari kwa Afya zao?
Ili akuache uuze madawa yako ya kulevya kwa uhuru?
 
Unauzungumziaje mkoa wa Tabora?
Tabora ni sawa kupata hivyo maana pale wajasiriamali ni wengi na hakuna wafugaji wengi wala mapori, Tabora hivyo vimegawanywa Igunga, Nzega, Tabora mjini, Uyui..
 
Hali inazidi kuwa mbaya kwa wasiomtakia mema RC Makonda baada ya kazi zake kuzidi kumnyokea na safari hii ameongoza katika makusanyo ya hela ya vitambulisho vya wamachinga.

Wenye roho ya korosho na Makonda mjinyonge tu sasa maana bado yupo yupo sana kwenye nafasi yake.View attachment 1098052
mmeo kajitahidi
 
Back
Top Bottom