Vitambulisho vya Wamachinga kwanini ni lazima vimalizike kwa udi na uvumba ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,563
217,866
Hili jambo limenishangaza sana! kwamba kumbe vile vitambulisho vya machinga si msaada tena bali ni biashara tu kama zingine tena ni biashara iliyowekewa malengo maalum , inavyoonekana hata kile kinachoitwa ni kwa ajili ya wenye mitaji midogo ni uongo tu , hivi kama ni lazima viuzwe huo muda wa kuangalia vigezo vya mitaji midogo utapatikana vipi ?

Hii nchi yaweza kuwa imefirisika bali tunafichwa tu , haiwezekani msaada ugeuke kuwa lazima kiasi cha kufukuzisha viongozi kazi , kuna kitu hatujaambiwa bila shaka
 
Nimekuwa nikiwaza kwa muda mrefu kiasi ni kwanini serikali inatumia nguvu ya ziada kuhakikisha vitambulisho hivi vimekwisha kwa wakati.

Nakubaliana na wewe kuwa suala sio kitambulisho, ila kinachopatikana baada ya kitambulisho 'kuuzwa'.

Machinga na 'wapiganaji' wengine wanauziwa vitambulisho sio kwa sababu ya utambuzi, bali ni biashara ya kuingiza mapato serikalini. Yeyote mwenye uwezo wa kufikiri vizuri atahoji kwanini tunalazimisha vitambulisho hivi na sio vingine vyote.
Hili jambo limenishangaza sana! kwamba kumbe vile vitambulisho vya machinga si msaada tena bali ni biashara tu kama zingine tena ni biashara iliyowekewa malengo maalum , inavyoonekana hata kile kinachoitwa ni kwa ajili ya wenye mitaji midogo ni uongo tu , hivi kama ni lazima viuzwe huo muda wa kuangalia vigezo vya mitaji midogo utapatikana vipi ?

Hii nchi yaweza kuwa imefirisika bali tunafichwa tu , haiwezekani msaada ugeuke kuwa lazima kiasi cha kufukuzisha viongozi kazi , kuna kitu hatujaambiwa bila shaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magu ashafeli kitambo. Hazina vyuma vimekaza makusanyo karibia yote yanaishia kulipa mishahara na madeni.

Huku nyumbani kavuruga uchumi, pesa hamna kwenye mzunguko.

Huko nje kayavuruga mabeberu mpaka yamekata misaada.

Sent using Sukhoi Su-57
 
Hii issue ishabadilika, sio msaada tena bali biashara ambayo wahusika wanaamini kuna kiasi kitakuwa kinaingia kila mwaka. Jiloge jisajili lazima kila baada ya mda fulani ambao bado hatujajua utakuwa unalipia hicho kiasi. Inaweza ikawa kila baada ya miezi 2,3, 4 au vyovyote watakavyoona inafaa.
 
Miaka yote mmeshindwa kuwatambua rasmi wamachinga ...Magufuli did it in a fraction of a second ...sasa hivi wanatambulika
 
Hili jambo limenishangaza sana! kwamba kumbe vile vitambulisho vya machinga si msaada tena bali ni biashara tu kama zingine tena ni biashara iliyowekewa malengo maalum , inavyoonekana hata kile kinachoitwa ni kwa ajili ya wenye mitaji midogo ni uongo tu , hivi kama ni lazima viuzwe huo muda wa kuangalia vigezo vya mitaji midogo utapatikana vipi ?

Hii nchi yaweza kuwa imefirisika bali tunafichwa tu , haiwezekani msaada ugeuke kuwa lazima kiasi cha kufukuzisha viongozi kazi , kuna kitu hatujaambiwa bila shaka
Hapo ilitumika janja ya nyani tu. Kiukweli hakuna cha kitambulisho bali ni ulipaji wa kodi. Nimeshuhudia maeneo kadhaa hata akinamama wauza maandazi wanaambiwa wanatakiwa kuwa na hivyo vitambulisho, na hapo hapo waendelee kulipa ushuru mwingine kwa maeneo wanakouzia. Huu ni mpango maalum wa kuwalipisha kodi watu wote bila kujali uwezo au ukubwa wa kile anachokifanya. Kutoka hapo nadhani vitatolewa vitambulisho vingine vya wakulima na wafugaji muda si mrefu.
Hapa nadhani kuna mdororo wa kifedha serikalini kwa kukosa misaada kutoka kwa wadau wa maendeleo au mabeberu wetu. Na kama ndo hivyo labda wataalamu wa uchumi waje watuambie mwisho wa siku nini kitatokea kama serikali itakusanya hela zote toka kwa wananchi wake bila kupokea hela yeyote toka nje. Huo mzunguko wa hapa hapa ndani utakuwa na adhari gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kusikia watu wanalazimishwa kuchukua vitambulisho. Mbona watu hawalazimishwi kwenda kuchukua vitambulisho vya Taifa?
 
All in all naona sawa tu. Kama ukilipa elfu 20 unafanya biashara bila kero za mgambo ama TRA wenyewe mwaka mzima basi ni mradi mzuri na utakuwa na manufaa sana.

Nilipendekeza pia kuwe na road toll maalum kabisa, watu wanunue wakiwa na safari za mikoani ili tusipigane tochi za kionevu. Ni bora kila mtu atoe mchango kwa hiari tu!
 
Back
Top Bottom