Vitambulisho vya Wajasiriamali Arusha, hadi Mafundi gereji wanatakiwa kuwa navyo?

Mbalamwezi1

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
2,071
2,010
Wakuu Swaalamaaah......

Watu wangu wa Arusha nina hii habari/kero kuhusu vitambulisho vya wajasiriamali Arusha!

Nina dogo wangu nimempeleka gereji moja mkoani Arusha akajifunze ufundi wa magari kwa vitendo mimi nipo mkoa mwingine. Sasa juzi kati hivi kanipigia simu eti inatakiwa elfu 20 kwa ajili ya kununua kitambulisho cha wajasiriamali na Polisi wanakuja mpaka gereji kuwakamata kama hauna kitambulisho!

Naomba mnijuze, je, ni kweli sasa hivi vitambulisho hivyo wanauziwa hata wasio wajasiriamali?
(Fundi gereji-mwanafunzi na ujasiriamali wapi na wapi?)
 
Kitambulisho cha wajasiliamali ni kwa mtu yeyote ambaye hajaajiriwa na kipato chake hakifiki kiwango cha kuwa na TIN ya biashara au Leseni ya biashara.

Miaka mingi tumekuwa tukilalama kwamba Tanzania wigo wa kodi ni mdogo sana. Sasa inabidi tuanze change mindset yetu, tujue kila tufanyalo yatupasa kuweka kodi in equation.
 
Ni kweli lakini anayejifunza ufundi ni mjasiriamali?
 
Narudia tena, watanzania tunahitaji badilishwa mind set yetu, kwenye dunia ya kwanza vijana wadogo wanaanza file tax return zao wenyewe, in return wanakuwa wakijua kodi ni wajibu.
Hapa kwetu mwanafunzi anaonekana hastaili lipa kodi, wakati si sawa waweza kuwa mwanafunzi ukawa unafanya kazi zinazokuingizia kipato, hivyo kodi unatakiwa ulipe.

Issue moja nnayoiona kwa wengi ni kwamba kwenye pricing, watu wengi hawaweki kodi into consideration. Kama kubadili tairi moja ni TSh 500/=, huyo kijana itambidi aanze charge TSh 600/= ku offset kodi anayolipa kupitia kitambulisho chake. Hivyo ndivyo maisha huenda.
 
Mie nasikiaga huku TRA ukihitaji TIN Namba in bure he nikiwa na hiyo TIN ya TRA Bado nitaulizwa kitambulisho cha mjasiriamali? Hebu nielewesheni mnaojua Haya mambo ya TIN NA VITAMBULISHO YAKOJE?
 
Kitambulisho cha wajasiliamali ni kwa mtu yeyote ambaye hajaajiriwa na kipato chake hakifiki kiwango cha kuwa na TIN ya biashara au Leseni ya biashara.

Miaka mingi tumekuwa tukilalama kwamba Tanzania wigo wa kodi ni mdogo sana. Sasa inabidi tuanze change mindset yetu, tujue kila tufanyalo yatupasa kuweka kodi in equation.
Yeye sio fundi, ila yupo pale ni mwanafunzi anajifunza ufundi
 
Sidhani Kama ni sawa. Mwenye garage anatakiwa kuwa na vibali pamoja na kulipa Kodi, huyo dogo Kama mfanyakazi. Nahisi dogo anadanganya
Ila kuna mtu wa pembeni nimemuuliza amenambia ni kweli wanatakiwa kuwa na vitambulisho, sasa najiuliza hela ya kitambulisho atatoa wapi wkt yeye hana kipato pale bali anajifunza
 
Narudia tena, watanzania tunahitaji badilishwa mind set yetu, kwenye dunia ya kwanza vijana wadogo wanaanza file tax return zao wenyewe, in return wanakuwa wakijua kodi ni wajibu.
Hapa kwetu mwanafunzi anaonekana hastaili lipa kodi, wakati si sawa waweza kuwa mwanafunzi ukawa unafanya kazi zinazokuingizia kipato, hivyo kodi unatakiwa ulipe.

Issue moja nnayoiona kwa wengi ni kwamba kwenye pricing, watu wengi hawaweki kodi into consideration. Kama kubadili tairi moja ni TSh 500/=, huyo kijana itambidi aanze charge TSh 600/= ku offset kodi anayolipa kupitia kitambulisho chake. Hivyo ndivyo maisha huenda.

Nafikiri hujanielewa mkuu, nchi za wenzetu unazozungumzia ni kwamba, kwa mfano, mtu ni mwanafunzi anasoma UDSM lkn ktk muda wake wa ziada anaenda beba box Mlimani City, huyu sawa anapaswa kulipa kodi coz anapata kipato!! Sasa huyu anajifunza ufundi hapo yeye halipwi bali anapata ujuzi tu!

Gari ikiletwa matengenezo anayechukua hela ni fundi mkuu sio yeye!!

Gari ikiletwa kubadilishwa tairi malipo ya hyo kazi hachukui yeye!! Nadhani umenielewa sasa!

Ebu nikuulize swali, je, wanafunzi wanaosomea ufundi huo huo wa magari VETA wanahivyo vitambulisho?!
 
Tatizo watu wanapenda kujifanya wanaiga nchi za wenzetu bila kujua kwenye nchi yoyote hakuna kodi inayotozwa bila kufuata sheria. Muulize anaweza kusema ni sheria gani inayomtaka kijana anyejifunza ufundi kulipia kitambulisho cha mjasriamali? Pia akupe maana ya mjasiriamali
Nafikiri hujanielewa mkuu, nchi za wenzetu unazozungumzia ni kwamba, kwa mfano, mtu ni mwanafunzi anasoma UDSM lkn ktk muda wake wa ziada anaenda beba box Mlimani City, huyu sawa anapaswa kulipa kodi coz anapata kipato!! Sasa huyu anajifunza ufundi hapo yeye halipwi bali anapata ujuzi tu! Gari ikiletwa matengenezo anayechukua hela ni fundi mkuu sio yeye!! Gari ikiletwa kubadilishwa tairi malipo ya hyo kazi hachukui yeye!! Nadhani umenielewa sasa! Ebu nikuulize swali, je, wanafunzi wanaosomea ufundi huo huo wa magari VETA wanahivyo vitambulisho?!
 
Nilichogundua wakuu Wa mikoa,wilaya na watendaji wanalazimisha watu wanunue vitambulisho hata kama hawastahili ili waonekane mikoa yao imeuza vitambulisho vingi hususani baada ya ripoti ya performance kutolewa na baadhi ya mikoa kuonekana ipo chini, kwa hili lisipoangaliwa kwa umakini nimoja ya sababu itakayo mpa mh. Rais wakati mgumu hapo 2020.
Ila kuna mtu wa pembeni nimemuuliza amenambia ni kweli wanatakiwa kuwa na vitambulisho, sasa najiuliza hela ya kitambulisho atatoa wapi wkt yeye hana kipato pale bali anajifunza
 
Nilichogundua wakuu Wa mikoa,wilaya na watendaji wanalazimisha watu wanunue vitambulisho hata kama hawastahili ili waonekane mikoa yao imeuza vitambulisho vingi hususani baada ya ripoti ya performance kutolewa na baadhi ya mikoa kuonekana ipo chini, kwa hili lisipoangaliwa kwa umakini nimoja ya sababu itakayo mpa mh. Rais wakati mgumu hapo 2020.
Yap! Ni kweli mkuu, maana naskia(tetesi) kuwa huko Arusha kuna walimu pia wamepewa hvyo vitambulisho wauze! Mimi nafikiri wenye mamlaka waliangalie vizuri hili suala maana litamfitinisha Mh. Rais na wananchi wake
 
Kwa Mimi nilivyomuelewa rais watu wanaotakiwa kua na tin hawapaswi Kuna na kitambulisho cha mjasiriamali. Ila watendaji wetu wengi hawakumuelewa rais
Mie nasikiaga huku TRA ukihitaji TIN Namba in bure he nikiwa na hiyo TIN ya TRA Bado nitaulizwa kitambulisho cha mjasiriamali? Hebu nielewesheni mnaojua Haya mambo ya TIN NA VITAMBULISHO YAKOJE?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom