Vitambulisho vya Wachinga ni leseni halali kwa mujibu wa Sheria Namba 6 ya 2014

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,037
9,953
Katika Sheria ya leseni sura 208 ya 1972 na marekebisho yake (Act Supplement Number 6 of 2014, Ibara ya 7) imewatambua wafanyabiashara wadogo na kuweka viwango vya leseni vya elfu 20.

Hivyo vitambulisho vya machinga ni lesseni halali kwa mujibu wa Sheria, na wala sio hisani ya mtu hivyo halmashauri zinapaswa kuendelea kutoa leseni/vitambulisho hivyo.

Kwa sasa vitambulisho hivyo vinaonekana ni hisani ya rais. Ni wakati sasa halmashauri kuweka utaratibu mzuri wa kutekeleza hii sheria.

Marekebisho hayo sura namba sita ibara ya saba ada ya leseni kwa hair saloon na barber shop ni elfu 5 tu unabeba leseni yako halali kabisa, migahawa maarufu kama Tea Room nayo ada ya leseni ni elfu tano.
 
Back
Top Bottom