Vitambulisho vya uraia TZ viwe hivi

mbasamwoga

Member
Jul 6, 2011
70
12
habari zenu wana jamvi, sasa hivi serikali iko mbioni kuandaa vitambulisho vya uraia. lkn cha kushangaza hawajasikiliza maoni ya watanzania ili kuona ni kipi hasa wangependa pia kiwepo kwenye ID hizo. kwa uzoefu wangu suala la upotevu linachukua sana nafasi kwa ID za benk, vyuo, NEC yaani kadi za kupigia kura n.k.hizi zimezagaa mitaroni, vituo vya polisi,maofisini n.k ambako wenye navyo wameshinda kujua kuwa viko huko hivyo kulazimu mmiliki kuingia gharama ya kutengeneza ID mpya kwa gharama kubwa, kupoteza muda na hata kupoteza haki zake za msingi kutokana na kukosa hicho kitambulisho.
Lakini serikali katika mchakaro wa kutengeneza ID za uraia hilo hawalioni kabisa ama labda wanasubiri hoja iibuliwe na waziri ama Rais ndio ipewe kipaumbele, lakini ukweli ni kwamba hivi vitambulisho imefikia hatua sasa viwekwe namba za simu za wenye navyo ili vinapopotea iwe rahisi kumpata na kumrudishia. Ama wanajamvi wenzangu mnayapi!! nawasilisha
 
Nadhani visiwe na namba but wakati wa usajili namba tuzisajili pia kwa sababu kitambulisho itakuwa ni mali ya serikali kikipotea atarudishiwa mwenye mali na kumpa mtumiaji!
 
ukiweka kitambulisho namba ya simu ni kwamba unayapa haya mamkampuni ya simu kipande kikubwa cha keki ambacho hawastahili...cha msingi kuwepo na kampuni ya simu ya kizalendo ambayo ina flat charging rate....au ikiwezekana zain inunuliwe kabisa then wananchi wawe na share..ukisema utumie makampuni ya njee ya simu kwenye vitambulisho hiyo sio sahii...lakini wazo lako zuri.
 
Back
Top Bottom