Vitambulisho vya NIDA vinaweza kuchapwa na kampuni binafsi za kizalendo, sio lazima NIDA yenyewe

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
36,570
44,227
NIDA wameshindwa kabisa kuendana na kasi ya wahitaji vitambulisho nchi.Wanaoomba kupewa vitambulisho kwa mara ya kwanza au waliopotelewa na vitambulisho hivyo wote kwa sasa wanapewa namba tu. Utasubiri kwa muda mrefu sana kupata nakala halisi ya kitambulisho chenyewe, wengine hadi miezi mitatu!

Tatizo hili linaweza kumalizika kwa kufanya 'outsource' ya kampuni binafsi za kizalendo katika kila mkoa ziweze kuchapisha vitambulisho. Sheria itunguwe kampuni binafsi za kizalendo zipewe tenda ya kuchapisha nakala za vitambulisho vitakavyotoka NIDA.

NIDA waendelee na kazi yao ya kuhakikisha watu wote wanaoomba vitambulisho ni raia halali wa Tanzania au wanakidhi vigezo vya kupewa kisha kwa wale waliokidhi vigezo nakala zao za vitambulisho zinapelekwa huko kwenye kampuni binafsi kuchapwa.

Vinginevyo NIDA waache kutoza elfu ishirini za vitambulisho kama wanatoa namba tu.
Wabunge pia pigeni kelele kazi ya kuchapisha Vitambulisho vya Taifa iweze kufanywa na kampuni binafsi.
 
Makampuni binafsi yangepewa hiyo kazi ingependeza sana, itangazwe tender highest bidder apewe hiyo kazi, akiwa na mashine za kutosha atazalisha vitambulisho vingi kwa siku, hao NIDA wanaonesha wazi wamezidiwa kwani wameshindwa kuendana na kasi ya mahitaji ya vitambulisho, sio sawa miezi sita mtu asubiri kitambulisho.
 
Tatizo wameshindwa kuwatumia vizuri vijana wa IT, wanatumia watu wao wao ujua wamewatoa wapi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom