Vitalis Maembe: Makonda shika adabu yako, Chuo cha Sanaa Bagamoyo si sawa na wasafi wa nguo

Halafu Makonda hajui kitu, kwasababu chuo cha sanaa Bagamoyo kimefanywa kuwa ni taasisi ya serikali kwa miaka mingi sasa, na yeye kama kama kiongozi wa serikali halikuwa hajui hilo pia.
 
Kwa taarifa yako, walimu wa pale wanatoka sehemu mbalimbali Duniani, na hata Watanzania waliokuwepo wanaijua sanaa kuliko wewe na Makonda.
Sitaki kuwa mbishi mbishi napatembelea week end mi nlionaga hamna lolote 2017
 
Sitaki kuwa mbishi mbishi napatembelea week end mi nlionaga hamna lolote 2017

Labda nikufahamishe tu, tangu Chuo kile kimefanywa kuwa taasisi ya kiserikali (TaSuBa). Yaani taasisi ya sanaa Bagamoyo, hapo ndio mambo yalianza kwenda mrama. Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wasanii.
Wasanii hawapewi kipaumbele tena, si unajua serikali imeshaingia. Rushwa imetawala, ubinafsi na undugu imejaa. Wenye nafasi ndio wanakula keki hata kama hawastahili tofauti na zamani. Serikali imepora nafasi ya wasanii.
Kaa ukijua kuna watu ambao walipita chuo cha sanaa enzi hizo ukisikia majina yao maneno ya Makonda utayaona takataka.
 
Mi 2017 sio tu niliona hayo Bali na mwalimu walikuwa amepitwa na wakati
 
Makonda hakuwa sahihi na hajawahi kuwa kama kawaida yake .
Ila chuo cha bagamoyo hakiendani na kasi ya ulimwengu huu na kwa sanaa zote hakuna kitu tangible tena .
Watumishi wake ni outdated hata computer hawajui kutumia damu changa zinahitajika
Na serikali iwekeze
Kujua kutumia computer sio kigezo, sidhani utasema Marehemu Morris Nyunyusa ambae nina Imani hakuwa anajua kutumia computer au hata kama alikuwa na elimu hii ya kisasa, basi hakuwa msanii Gwiji!!! Hivyo naweza sema Marehemu Dr Hukwe Zawose, Marehemu Mwinamila na magwiji wengine wa Sanaa.
 
Mkuu walikuwa wazuri kwa muda wao kama kwenye bongoflave alivuokuwa mr nice.mkuu james bond alikuwa mzuri ila leo technology ilivyo huwezi tenga sanaa na computer leo tena .

Mkuu nakuelewa vyema kuna Sanaa na Sanaa, hizi za asili za kwetu sijui kama tumefikia wasaani nguli kwenye fani hiyo kuwa na ulazima wa kujua teknolojia za kisasa maana ubunifu wao hautegemee teknolojia. Nakuelewa sana Mkuu. Ila upande mwingine tudumishe Sanaa ie muziki wetu wa asili ambao ndio haswa chimbuko la haya ya kisasa. Pamoja sana...
 
Umeandika kistaarabu na kwa weledi mkubwa .Sina budi kutamka nimezingatia na nitazingatia
 
"MAKONDA SHIKA ADABU YAKO" - MAEMBE .

AMUONYA AACHE KUFANANISHA CHUO CHA SANAA BAGAMOYO NA WASAFI.

Mwanamuziki Vitalis Maembe, amemjia juu Mkuu wa mkoa wa Dar Paul Makonda na kumtaka afute kauli yake na kuomba radhi kufuatia taarifa aliyoitoa kuwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo hakijawahi kuzalisha mtu yeyote maarufu zaidi ya kutafuna fedha za mishahara wanazolipwa bila faida yeyote.

Makonda alitoa taarifa hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye viwanja vya Tandale wakati wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa msanii Diamond Platinumz ambapo ilikwenda sambamba na msanii huyo kutoa misaada mbalimbali ya kijamii.

Kufuatia taarifa yake, Makonda alinukuliwa akisema kuwa Chuo cha Sanaa Bagamoyo ambapo kipo chini ya serikali, hakijawahi kutoa mtu yeyote mwenye tija kwa taifa hili zaidi ya kutumia fedha za serikali wanazolipwa, na kuongeza kuwa ni heri Wasanii wa kundi la Wasafi (WCB) wanafanya vitu vyenye tija kwa jamii na taifa kwa ujumla kuliko chuo hicho.

Kufuatia kauli hiyo, Maembe alionesha kukerwa na maneno ya Mkuu huyo na kutoa maelezo yafuatayo:

" Dogo Makonda, Shika Adabu yako!
Mnapotaka kuongelea vitu vilivyowazidi Umri mkasome kwanza au ulizeni wakubwa zenu wawaambie. Haya! Umezaliwa Mwanza Tarehe 15/02/1982. Chuo Cha Sanaa kimezaliwa Dar es salaam. Kimehamia Bagamoyo na kuanza Rasmi 1981. Serikali ya Tanzania ni kubwa kwako kwa Umri na kila kitu. Ongea lakini chunga ulimi wako!

"Mh. Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mkurugenzi wa BASATA (Baraza la Sanaa la Taifa) Ndugu Lebejo. Mkuu wa TaSUBa (Chuo Cha Sanaa Bagamoyo) Ndugu Makoye.
Mmemsikia Shoga yenu alichokisema kwenye sherehe ya shoga zake wasafi wa nguo?
Mwambieni kuwa yeye ni sehemu ya Serikali, kushindwa kwa Serikali ina maana naye kashindwa, asishabikie kushindwa bali ajirekebishe".

"Kama hajui au hamjui, Mwambieni,
Chuo cha Sanaa Bagamoyo ndiyo Chuo Sanaa pekee cha Umma Afrika kilichopata ithibati ya Ubora uliotukuka. Kwanini?
Chuo kinahistoria ya kutoa mchango mkubwa wa Mapinduzi ya Elimu ya Sanaa ya Afrika Duniani. Imetoa walimu wa sanaa wanao fundisha Vyuo vikuu vya Muziki ndani na nje ya nchi....Dr. Makoye, Dr Nyoni, Dr Kiagho, Dr. Chaya na wengine wengi. Ndiyo chuo pekee cha sanaa kilichowahi kukabidhiwa Zuria jekundu.

"Waigizaji kama Mzee Jangala na wengine wengi. Paul Ndunguru (Mchoraji wa vitabu vingi vya kufundishia Shule za msingi na Sekondari nchini) Mkurugenzi wa Bodi ya Filamu, TaSUBA na hiyo BASATA,
Wataalamu wengi wa Media Tech ktk Vituo nyingi vya TV nchini wamesoma hapo.

"Mwakyembe, Lebejo na Makoye!
Nyinyi ni watumishi mlioaminiwa na Serikali, msinyamaze BOYA Kama huyo anapoitukana Serikali, nawapa siku 7 tuwasikie Mkikanusha au kumuunga mkono wazo lake kama kama 'Walimu wa TaSUBa wanapokea mishahara bure' Kwa sababu ya uzembe wenu na uwoga wenu ndiyo maana hata mafanikio madogo ya juhudi za Serikali hayathaminiwi." Alimalizia.

Maembe Vitali
Nice
 
Halafu Makonda hajui kitu, kwasababu chuo cha sanaa Bagamoyo kimefanywa kuwa ni taasisi ya serikali kwa miaka mingi sasa, na yeye kama kama kiongozi wa serikali halikuwa hajui hilo pia.
Kiazi yule
 
83 Reactions
Reply
Back
Top Bottom