Vitabu vyangu bora vya nyakati zote. Vipi vyako?

Nimemaliza kitabu hiki cha Diamond. Nitakireview kesho, as always Jared Huwa hazingui. Hata kama usipokubaliana na mawazo yake, lakini ana uwezo mzuri sana wa ujenzi wa hoja na ushawishi. Red Giant nakuongezea hiki kwenye orodha yako
Screenshot_20211203-220555.jpg
 
Img_395_0-book_reader_ReadEra.jpg


Hebu fikiria, unayo matatizo yanakuzonga ya kimaisha, unaenda kwa mshauri wa kisaikolojia, anakuainishia mambo 12 ambayo yatakuongoza katika kutatua matatizo yako; lakini jamii, iwe familia, kijiji, wilaya, mtaa, timu, Biashara, makampuni au hata mataifa wakati mwingine ulimwengu mzima, nayo hukumbwa na matatizo, unaweza fikiria njia zile 12 ulizopewa ndio zinaweza tumika pia kutatua matatizo ya mataifa mbalimbali!?. Inafikirisha, lakini Jared Diamond kwenye kitabu hiki, ametueleza kuwa inawezekana.

Ukisoma vitabu vya Diamond (mfano GGS, The World Untill Yesterday au Why Sex is fun), utaona Diamond hutumia uzoefu wake binafsi wa kimaisha au matukio ambayo yanawagusa watu binafsi moja kwa moja ili kujenga Ushawishi katika hoja zake.

Katika kitabu hiki ametumia pia njia hii kama msingi wa kujenga zake ili kutoa majibu/mwangaza/uelekeo katika Swali kuu la kitabu chake; Ni vipi mataifa yanakabiliana na majanga mbalimbali yanayowakabili na kuweza kufanya mabadiliko yanayohakikisha ustawi wa mataifa hayo.

Mwandishi anaanza kwa kuelezea Janga la moto lilotokea Usiku wa Jumapili ya November 8 mwaka 1942 majira ya saa 4 na Robo hadi saa 5 na dakika 10, ambapo Club ya Usiku iitwayo Coconut Groove iliwaka moto na watu 492 kufariki huku mamia wakijeruhiwa. Kwenye ajali hii ya moto ukumbi huu ulikuwa umejaa kuliko uwezo wake, hivyo kusababisha uokoaji kuwa mgumu sana, kiasi cha watu kuzuia mlango wa kutokea, uliokuwa mmoja tu.

Tukio hili liliumiza sana maisha ya wamarekani kiuchumi, kifamilia—wayatima na wajane, na mbaya zaidi kisaikolojia—maumivu na kutojua hatma ya maisha baada ya kundokewa na ndugu, marafiki, workmates, business partners, wapenzi n.k

Some of those survivors and relatives remained traumatized for the rest of their lives. A few committed suicide. But most of them, after an intensely painful several weeks during which they could not accept their loss, began a slow process of grieving, reappraising their values, rebuilding their lives, and discovering that not everything in their world was ruined. Many who had lost spouses went on to remarry. Even in the best cases, though, decades later they remained mosaics of their new identities formed after the Cocoanut Grove fire, and of their old identities established before the fire. [ukurasa wa 9, Upheaval]

Tukio hilo, ndio lililozaa huduma ya kiafya ya akili kwa watu waliopitia matatizo ya akili baada ya majanga kutokea—CRISIS THERAPY. Binafsi, kisa hiki cha Coconut, kimenipa kumbukumbu ya ajali ya Meli ya MV Bukoba, iliyotokea nchini mwetu mwaka 1996. Katika ajali hii, taarifa rasmi yaelezwa ni kujazwa kwa watu na mizigo kuliko kiasi. Mfano, uwezo wa meli ulikuwa ni kubeba abiria 430, lakini meli hii waliofariki ni zaidi ya watu 800. Wapo waliosema kuwa meli hii haikuwa mara ya kwanza kubeba watu waliozidi. Lakini kwa kawaida, ajali sio tukio la ghafla, bali ni mkusanyiko wa vitukio vidogo vidogo ambavyo baada ya muda fulani hufika ukomo na kutokea kwa ajali. Mfano, inapotokea ajali ya barabarani na gari kupinduka, huanza kwa dereva, kunywa pombe usiku wa awali, au kufanya mapenzi kwa muda mrefu hivyo kuchelewa kulala, hivyo huamka akiwa na uchovu, humfanya ashindwe kutimiza wajibu wake ipasavyo mfano kukagua gari lake kwa umakini, hivyo hata kama gari hilo huzoea kubeba watu kuliko kiasi, basi dereva siku hiyo huweza liingiza gari mtaroni na kupata ajali.
—Hadi leo, maeneo ya kanda ya ziwa mikoa ya Mwanza, kagera, musoma na Shinyanga, bado zipo familia nyingi ajali hii ni kumbukumbu ya karibu, na wanao watu wanaowakumbuka, au iliwawia ugumu kiasi gani kurejea kwenye hali ya kawaida na wengine hadi leo wanaishi na machingu hayo ya miaka 25 iliyopita.

Tukio jingine nchini mwetu ni la ajali ya Treni iliyotokea mkoani Dodoma mwaka 2002.

Mheshimiwa Spika, kutokana na ajali ya treni ya abiria iliyotokea kilomita 388/9 kati ya stesheni za Igandu na Msagali Jumatatu tarehe 24 Juni 2002 saa 2.30 asubuhi, Taifa limekumbwa na msiba mkubwa. Siku hiyo hiyo jitihada za uokoaji wa abiria na utoaji wa maiti zilianza mara moja. Kazi hiyo ilikamilika Jumatano tarehe 26 Juni 2002 saa 12.30 jioni. Aidha, matengenezo ya njia ya reli yalikamilika saa 4.30 usiku na kuruhusu usafiri wa treni kurejea katika hali yake ya kawaida. 2. Maiti waliotokana na ajali hii walikuwa 281 ambapo maiti 193 walitambuliwa na kuchukuliwa na ndugu ili kuzikwa na maiti 88 tuliwazika kwenye mazishi ya halaiki katika makaburi ya Maili Mbili Kata ya Miyuji mjini Dodoma tarehe 27 Juni 2002 saa 5.00 asubuhi. Utoaji wa maiti ulifanywa kwa saa 24 kila siku”

—M.Mwandosya, WMU Bungeni, Tarehe 24.Juni.2002 [Chanzo; Jamiiforums)

Mimi binafsi, tukio hili la ajali ya Treni ya Dodoma kuna kisa cha Ndugu yangu mmoja aliyekuwa akitegemea kufunga ndoa huko Tabora na Mmewe mtarajiwa ambaye alifariki kwenye ajali hiyo. Shangazi yangu huyu ilimchukua takribani miaka mitano kuja kukubali kuwa mmewe amekwishafariki, kukaa sawa na hatimaye kuolewa tena.

Matukio hayo ya ajali hizo; za moto Coconut Groove club, ajali za MV Bukoba, Ajali ya Treni Dodoma, ndio yamezaa Crisis Therapy.

Crisis au Upheaval ni nini?

Maneno mawili yametumika kwenye kitabu hiki; Crisis na Upheaval! Crisis kwa tafsiri ya Kiswahili ni Mgogoro na Upheaval ni mtikisiko.

Kwa mujibu wa Kamusi Kuu ya Kiswahili Mgogoro ni hali ya watu kukosa masikilizano inayosababisha vurugu, Ghasia au mtafaruku, huku neno Mtikisiko lina maana ya hali ya kuyumbayumba inayotokana na kutingishwa au kusukwasukwa. Hivyo neno Upheaval/Mtikisiko huashiria forces za nje zinazoleta shida ndani; mf uvamizi, magonjwa ya mlipuko, vita, wakimbizi n.k Huku Mgogoro likiakisi mambo ya nje na ya ndani. Hivyo, kwa muktadha wa kitabu hiki, Migogoro inayowakumba watu au jamii huwa yanaweza kuwa yametokea ndani au nje ya nchi.

Katika Sura ya kwanza kabisa ya kitabu hiki, mafunzo makuu ni mambo 12 ambazo Crisis Therapists huzitumia katika kumsaidia mtu kuweza kukabiliana na migogoro/mitikisiko inayomkumba.


1. Kukubali kuwa Uko kwenye mgogoro.
—Hii ni hatua ya kwanza kabisa ambayo mtu lazima aifanye. Bila kukubali kuwa uko kwenye mgogoro/shida fulani, basi huwezi itatua hali wala kubadilisha mambo.

2. Kukubali kuwajibika.
—Ni hulka ya wanadamu kukubali kuwa wako na tatizo fulani, lakini hawataki kukubali kuwajibika. Wengi husingizia au kualumu wengine. Bila kukubali kuwa wewe mwenyewe unabeba lawama za matatizo fulani, basi huwezi badilika.

. Kuainisha tatizo unalotakiwa kulibadili.
—Ukishakubali kuwajibika, ni vyema utazame kipi hasa unatakiwa ukibadili na kipi hakina haja ya kukibadili—SELECTIVE CHANGE.

4. Kupata msaada kutoka kwa wengine.
—Katika hatua hii unapokumbwa na migogoro, basi unaweza pata msaada kutoka kwa watu wako, ili kuweza kukupa msaada ya hali na mali. Mf, mtu mwenye msukosuko wa ndoa, anaweza pata msaada wa Nyumba kutoka kwa ndugu, kipindi ndoa haijakaa sawa.

5. Kutazama nini wengine walifanya.
—Majanga si kitu kipya, hivyo kuna watu ambao wameshapitia hali kama yako, hivyo unaweza watazama wao na kujifunza pia nini wamefanya ili kujinasua kwenye hali zao, ni sehemu muhimu ya kutatua Migogoro yako.

6. Kuwa na ujasiri.
—Ujasiri kwa maana ya uwezo wa mtu kujisimamia maamuzi bila kuwa kuwaza mtazamo wa wengine, kutokuwa na uoga wa kukubali mabadiliko.

7. Ujasiri wa kujitathmini.
—Kuna msemo kuwa ‘soga ni asali pale wanapozungumziwa wengine, lakini ni shuburi pale mnapojizungumzia wenyewe’. Ukweli wa msemo huu ni kuwa, wanadamu ni wepesi katika kutazama na kuwakosoa watu wengine. Lakini si rahisi kujikosoa wao. Ili mtu aweze kubadili hali, ni lazima aweze kwa dhati kabisa kujitathmini yeye mwenyewe, nini uimara na udhaifu wake.

8. Uzoefu binafsi.
—Mtu mzima huweza kujichanganya na hali mpya kwa urahisi zaidi kuliko kijana, kwa sababu moja, uzoefu wa nyuma. Nakumbuka binafsi, mwaka 2016 wakati Utawala wa Rais Magufuli ndio ameanza kuchukua hatua kadhaa ambazo zilikausha mzunguko wa fedha na kuleta mtikisiko mkubwa; siku moja nilikuwa nimekaa na rafiki yangu mmoja [yeye yuko karibu 25 yrs zaidi yangu kiumri], aliniambia, ‘hii hali bwana mdogo, kwangu si ngeni, hivyo tutavuka tu. Nakumbuka wakati wa utawala wa Nyerere hali ilikuwa ngumu, ilibidi tujibane sana matumizi, lakini tulivuka vizuri tu’. Hivyo, wanasaikolojia wanasema uzoefu binafsi wa mtu katika migogoro fulani, huwasaidia kuweza kuyakabili kwa urahisi zaidi.


. Uvumilivu.
—Mara nyingi, njia za kuyatatua matatizo huusisha kujaribu na kushindwa, pia huchukua muda mrefu au huchukua muda mrefu matokeo yake kuonekana. Hivyo, huhitaji uvumilivu. Mwenye uvumilivu huwa nafasi kubwa ya kukabiliana na majanga.

10. Wepesi wa kubadilika.
—Kuwa na fikra mgando, ni kuona kuwa kuna namna moja tu ya kukabiliana na mambo. Ili kuweza kukabiliana na migogoro, unahitaji uwe na fikra zenye kuweza kukubali mabadiliko.

11. Misingi mikuu.
—Kila mwanadamu anayo mambo anayoyaamini au kuyasimamia ambayo hayo ndio humtambulisha. Yakitoweka hayo mambo, basi naye ni hayupo, hivyo ni lazima yawepo na hayawezi badilika au achwa. Haya ni kama vile imani ya dini, mila, familia n.k. Hivyo mtu anapokabiliana na migogoro, basi ni lazima aainishe kipi kwa kweke ni misingi mikuu, hii itamuongoza kufanya uchaguzi wa nini cha kubadili.

12. Kuzongwa na vikwazo.
—Mambo yanayomzunguka mtu wakati mwingine humpa urahisi au ugumu wa kufanya mabadiliko fulani. Mf, nimeshuhudia migogoro mingi kwa wanandoa, kiasi watu hushindwa kufanya maamuzi ya kutoka kwenye ndoa hiyo, kwa sababu tu ya kuwa na watoto.

Mambo hayo 12 ndio ambayo Diamond ameyaanisha kuwa yanamuongoza mtu binafsi kutatua mitikisiko ya kimaisha inayomkumba.

Kama nilivyoeleza hapo awali, Diamond anajenga hoja kuwa njia hizi zinaweza tumika pia kutatua migogoro inayoikumba nchi.

Kwenye kitabu hiki Sehemu ya kwanza, ameelezea nchi saba na kuonyesha jinsi gani muongozo huo umefanya kazi. Nchi hizo ni Finland, Japan, Chile, Indonesia, Australia, Ujerumani na Marekani. Kwa kweli nilisikitika kwanini hajaelezea nchi hata moja ya Afrika, lakini nilimuelewa Methodology aliyoitumia katika kuchagua nchi hizo—Amechagua nchi ambazo yeye binafsi anazifahamu vyema i.e amezitembelea mara kwa mara na kuishi muda mrefu.

Kwa ufupi-kwa nchi chache; Chile mtikisiko wake ulitokana na Utawala wa kijamaa na kidemokrasia wa Rais Allende na baadae kuingia kwa utawala dhalimu na katili wa kibepari wa Rais Pinochet. Anasema, Chile waliokuwa na misingi ya kidemokrasia, ilibidi wafanye mabadiliko kwa makini, na kuchagua mambo kutoka tawala zote mbili za Allende na Pinochet; Ujerumani yenyewe mgogoro wake mkubwa ulikuwa ni kutoka 1930 hadi 1945 katika utawala dhalimu wa Hitler ambao ulichochea misingi ya kiimla—ambayo kwa mujibu wa Diamond ilikuwa ni asili ya wajerumani wote kijamii— iliyoshushwa karibu na kiuchumi, na kijeshi na hatimaye wajerumani kufanya mabadiliko kutoka 1948 hadi 1990 na kuwa nchi yenye uchumi wa juu ulaya yote na yenye Demokrasia ya juu; Marekani inakumbwa na Migogoro mikubwa: Utengano mkubwa wa kisiasa na kijamii, Hali kubwa ya utofauti wa kimaisha na Kushuka kwa Demokrasia.

Sehemu ya pili ya Kitabu hiki anaelezea migogoro inayoikumba dunia kwa ujumla na jinsi gani tunaweza kukabiliana nayo i.e Silaha za Nuklia, Mabadiliko ya Tabia nchi, Kuzidi kupungua kwa rasilimali za kuhimili idadi ya watu na kuongezeka kwa tofauti ya kimaisha kati ya masikini na matajiri. Nadhani haya si matatizo makuu pekee yanayoikabili dunia kwa sasa na pengine miaka kumi ijayo; Yapo kama Magonjwa ya mlipuko kama Ebola, Kipindupindu, Malaria, Ukimwi bado yanaisimbua dunia hasa Nchi masikini—kwa sasa tuna Covid19 ambayo hadi mwaka 2022 tunategemea itaendelea kuisumbua dunia na madhara yake—hasa kiuchumi— kudumu kwa miaka si chini ya kumi; Ugaidi pia ni janga linaloikabili dunia na pia wakimbizi. Migogoro kama ya Sahel, Pembe ya Afrika, Mashariki ya kati inazidi kuzalisha mamilioni ya wakimbizi kila mwaka. Hivyo, nadhani maeneo haya pia yalihitaji umakini wa mwandishi.

Katika mapitio haya ya kitabu hiki, nitazielezea nchi ya Finland na nitapitia eneo la uelekeo wa dunia katika migogoro inayoikabili.

Finland; Kwa kweli sikuwahi ijua Finland hapo awali, hadi niliposoma kitabu hiki. Kwa wafuatiliaji, wanajua Finland ndiyo nchi yenye watu wenye furaha zaidi dunia, lakini ajabu ni nchi yenye sheria ya ulazima wa kujiunga jeshini. Ni kitendawili! Kwa sababu unategemea mtu mwenye furaha, basi atakuwa na amani, hana matishio; kuwa na ujeshi wa lazima, inaashiria kuwa taifa hilo liko kwenye wasiwasi wa vita. Ni kweli; Finland wako kwenye hali ya hadhari wakati wote kwa sababu ya historia na jiografia yao. Wao husema; “We are a small country; and Our geography will never change.”



Sera ya mambo ya ndani na Nje ya Finland toka miaka ya 1940, walijifunza jambo moja, ni lazima iwe na mtazamo wa kirusi. Ili Finland, iwe salama ni lazima ihakikishe Urusi inajiona iko salama kutokea Finland.

Kihistoria, Finland imekuwa ikigombewa na kutawaliwa na Sweden na Urusi kutoka miaka ya 1100, na Sweden ilikuwa ikitawala hadi mwaka 1809 pale ilipochukuliwa na Urusi chini ya Tsar. Kwa miaka yote Finland ilikuwa na uhuru mkubwa wa kujiamulia mambo yake kama kuwa na Utawala, bunge na fedha yake. Lakini Tsar Nicholas II alibadili hali ya mambo mwaka 1894 na kumteua Bobrikov kuwa Gavana wa nchi hiyo, ambaye aliitawala kikatili sana, hadi alipouliwa mwaka 1904 na wafinland waliokuwa na mazoea ya uhuru wao na Demokrasia. Mwaka 1917, Yalipotokea mapinduzi ya wabolshevicks na Lenin kuwa Rais wa Urusi, Wafinland walitumia fursa hiyo kujitangazia uhuru. Matokeo yake ilitokea vita ya wenyewe kwa wenyewe kugombania madaraka. Vita hii ilikuwa kati ya white [mabepari] waliofunzwa na kusaidiwa na wajerumani na Reds [wakomunist] waliofunzwa na kusaidiwa na Wasoviet. Baada ya whites kushinda, waliwaua Reds 8,000 na wengi 20,000 kufa kwa njaa na mateso. Wafinland, walikaa mezani na kufanya Maridhiano, na mkomunist akawa Waziri Mkuu. Lakini, bado wafinland waliishi kwa kumuhofia Msoviet.

Miaka ya 1920 hadi 1930, Utawala wa Stalini ulizidi kujiimarisha kijeshi na kimiundombinu, ambayo ilielekea mpakani mwa Finland, tena kwenye miji yenye wakazi na muhimu. Kwa wafinland, huu ulikuwa ni ujumbe wa uvamizi. Yaani, ni sawa sasa hivi, Tanzania ianze kujenga reli, barabara kwenda Arusha na kuweka vifaru, kambi za jeshi zikiwa mpakani mwa Kenya . Wafinland chini ya utawala Jenerali Mannerheim, walikuza na kuimarisha jeshi lao. Wafinland wengi walijitolea kufanya kazi ya kujenga mpaka imara wa kijeshi uitwao Mannerheim Line mjini Karelian Isthmus, ulio kusini Mashariki mwa Finland, na kupakana na Leningrad. Wasoviet na wafinland, wote waliendelea kuishi kwa kuhofiana kwa sababu


kijiografia na kihistoria. Hofu nyingine ya Stalin ilikuwa ni Ujerumani. Ujerumani ilikuwa imeziteka nchi za Austria, Poland n.k kwa hofu ya Stalin kuwa Hitler ana lengo la kujitanua zaidi [Stalin anasema alimjua Hitler kutoka kwenye kitabu chake chake Mein Kempf—Harakati zangu]. Hivyo Stalin aliona kuwa punde ataichukua Finland, na hiki kingekuwa ni kitisho zaidi soviet.

Mambo yalikuwa magumu zaidi mwaka 1939 mwezi wa Nane, ambao Ujerumani na Soviet zilisaini mkataba ulioitwa Molotov-Ribbentrop Pact. Katika mkataba huu, Ujerumani, iliitambua kuwa Finland, inapaswa kuwa chini ya himaya ya soviet. Oct 1939, Soviet ilitangaza inazitaka nchi za Baltic [Lithuania, Latvia, and Estonia, plus Finland] ziwe chini yake na kuweka Kambi za Kijeshi. Hii maana yake zingesurrendee uhuru wao. Kwa sababu ya udogo wao, nchi hizo tatu zikakubali. Lakini baadae Soviet walitoa tena matakwa mawili, kambi za Finland mjini Karelian Isthmus zirudi nyuma ili Leningrad isishambuliwe kirahisi na pili Soviey iweke Kambi ya Jeshi la Maji kwenye bandari ya Kusini Finland mji wa Helsinki na ingine kwenye Ghuba ya Finland. Matakwa haya ya soviet, warusi wote waliyakataa, kwa hofu kuwa lengo kuu la Soviet, ni kuichukua Finland yote hivyo wangepoteza uhuru wao. Wafinland walijifunza kwa Czechoslovakia, ambao walikubali kuachia mji wao mkuu wakijeshi wa Sudeten borderland wajerumani mwaka 1938, na kuwafanya wawe dhaifu kijeshi na hatimaye nchi yao yote kutekwa na wajerumani. Wafinland pia walikataa masharti ya Msoviet, kwa kudhani kuwa Msoviet alikuwa akitishia tu. Msoviet naye alihisi kuwa Finland nchi ndogo hivyo haiwezi kumvimbia. Pia Finland alijiaminisha kuwa marafiki zake wangemsaidia. Hesabu za wafinland, hazikuwa halisi kuwa wangeweza dumu vitani kwa miezi zaidi ya Sita, kitu ambacho hata Mkuu wao Wa jeshi aliwasihi kuwa haiwezekani.

Siku ya Jumatatu, ya Tarehe 30, Mwezi wa 11 mwaka 1939, Soviet iliivamia Finland baada ya Soviet kutengeneza False-flag attack, na kuisingizia Finland. Soviet walipoivamia Finland, walitambua Kuusinen, mkomunist kama Kiongozi wa Finland, ili kuhalalisha uvamizi wao, kuwa wanaingia kumlinda. Hii ilikuwa ni vita David na Goliath.

At the time that war broke out on November 30, 1939, the details of this absurd military mismatch were as follows. The Soviet Union had a population of 170 million, compared to Finland’s population of 3,700,000. The Soviet Union attacked Finland with “only” four of its armies, totaling 500,000 men, and keeping many other armies in reserve or for other military purposes. Finland defended itself with its entire army, consisting of nine divisions totaling only 120,000 men. The Soviet Union supported its attacking infantry with thousands of tanks, modern war planes, and modern artillery; Finland was almost without tanks, modern war planes, modern artillery, anti-tank guns, and anti-aircraft defenses. Worst of all, though the Finnish army did have good rifles and machine guns, it had very limited stocks of ammunition; soldiers were told to save ammunition by holding fire until Soviet attackers were close. [Ukurasa wa 76, Upheaval]



Unaweza dhani wafinland ni wehu, lakini walikuwa na hesabu zao.

“Our aim was instead to make Russia’s victory as slow, as painful, and as costly for the Russians as possible.”

Pia walikuwa wakivuta muda ili waweze pata msaada wa nchi marafiki. Wafinland walikaza na walipata faida ya uzoefu wa kupigana kwenye barafu, na kuwa na nguo za baridi ambazo warusi hawakuwa nazo.

Misaada michache walipata mf wanajeshi wachanga kutoka kwa sweden 12,000, Bunduki za zama za Vita ya Dunia ya kwanza, VDK kutoka Italia. Lakini mataifa makubwa marafiki kama Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Marekani na Sweden.

While Germany had sent troops to support Finnish independence and had long-standing ties of culture and friendship with Finland, Hitler was unwilling to violate the Molotov-Ribbentrop Pact by helping Finland. The U.S. was far away, and President Roosevelt’s hands were tied by U.S. neutrality rules resulting from decades of American isolationist policies. [Ukurasa wa 78, Upheaval]



Waingereza na wafaransa, wao walikuwa busy na vita dhidi ya Ujerumani, lakini wote walikuwa na lengo moja. Ujerumani alikuwa akipata madini ya chuma kutoka Sweden Kupitia Bandari ya Narvik huko Norway, hivyo waingereza na wafaransa, walitaka idhibiti Narvik, so walipeleka wanajeshi wengi eneo hilo na wachache Finland.

Baada ya vita kwenda muda mrefu, Stalin alibadili mkakati na kuitosa serikali ya Kikomunist aliyoitambua, hivyo kuitambua serikali ya Finland, na kujikita zaidi kwenye eneo la Karelian Isthmus lenye faidia zaidi kijeshi kwa Urusi.

Kumaliza vita, ilibidi wafanya makubaliano ya amani;

The Soviets now demanded the entire province of Karelia, other territory farther north along the Finland/Soviet border, and use of the Finnish port of Hanko near Helsinki as a Soviet naval base. Rather than remain in their homes under Soviet occupation, the entire population of Karelia, amounting to 10% of Finland’s population, chose to evacuate Karelia and withdrew into the rest of Finland.

Baada ya makubaliano hayo, kwa msaada wa Ujerumani, Finland ilivunja makubaliano ya amani na Soviet ya mwaka 1940 na ilivamia mji wa Karelia, ili kuukomboa mwaka 1944, lakini vita iliyoisha kwa Finland kuchapwa na kisha kulipishwa faini.

Katika vita hizo, wafinland 100,000 waliuawa, watoto 55,000 walibaki yatima, watu 615,000 walipoteza makazi yao.

Mkataba wa amani uliwata wafinland kufanya yafuatayo;

i. Iwashitaki yenyewe maafisa wake walioanzisha vita. Vinginevyo wangefungwa kikatili huko Soviet. Ilibidi utunge sheria, na kuwafunga watu wake wenyewe kwa kuipigania nchi yao.

ii. Kulipa faini Dola Mil 300, na baadae kuipunguza hadi Dola Mil 226. Ajabu, faini hii iliwasaidia wafinland kuendelea, maana iliwafanya wajenge zaidi uchumi wao ili kulipa deni hilo.

iii. Finland ilipaswa ifanye biashara na Soviet, karibu 20%.

Wafinland walikubali, wakaingia makubaliano na Soviet, na wakahakikisha kuwa haikiuki tena makubaliano na Soviet (kama walivyofanya 1940). Walihakikisha makubaliano yoyote na mataifa ya magharibi, ni lazima waishirikishe usoviet. Kwa namna hii Finland waliendelea kufanya biashara na mataifa ya magharibi na kukuza uchumi, huku ikilinda kwa wivu wote uhusiano wake na Urusi hadi leo. Hivyo Finland ikageuka daraja la Soviet na magharibi; Usoviet waliwaamini wafinland na kuhisi wako salama kabisa, ndio maana Stalin alipoulizwa kwanini Hakuweka serikali ya kikomunist nchini Finland kama nchi zingine za ulaya magharibi, alijibu; “When I have Paasikivi [Finland Prime Minister, loyal to Stalin], why would I need the Finnish Communist Party?”

Hivyo wafinland, wanaiita mwaka 1945 hadi 1948 kuwa mwaka wa mtikisiko (Year of great Upheaval). Lakini walisurvive. Kwa vipi?

Muongozo ule mambo 12, una sura hii inapokuja kwenye namna mataifa yanakabiliana na mitikisiko. Hapa mwandishi anaelezea ni kwa vipi njia hizo 12 unaweza ziweka kwenye migogoro ya mataifa/dunia.

1. Kukubali kuwa Uko kwenye mgogoro.
Wananchi kukubali kuwa wako kwenye mgogoro.

2. Kukubali kuwajibika.
Taifa kukubali kuwa wanawajibika kwa matatizo. Wamarekani wao, hawakubali kuwa wanatatizo la Demokrasia, bali wanatupia lawama warusi na wachina

3. Kuainisha tatizo unalotakiwa kulibadili.
Kuanisha nini kinafanya kazi nini hakifanyi katika taifa mf sera, Sheria n.k

4. Kupata msaada kutoka kwa wengine
Kupata msaada kutoka kwa mataifa rafiki au mashirika au watu.

5. Kutazama nini wengine walifanya.
Kujifunza mataifa mengine yamefanya nini kutatua matatizo yao ya aina hiyo.

6. Kuwa na ujasiri.
hapa taifa lazima lijianishe utambuzi wake ukoje.

7. Ujasiri wa kujitathmini.
[https://s0] Maridhiano ya kitaifa ya kujitathmini kwa dhati mapungufu na uimara.

8. Uzoefu binafsi.
[https://s0] Historia ya taifa katika kupambana na matatizo kama hayo.

9. Uvumilivu
[https://s0]Uwezo wa kisiasa wa taifa kukabiliana pale wanaposhindwa jambo fulani.

10.Wepesi wa kubadilika.
[https://s0]Wepesi wa nchi kubalika kisera na kisheria.

11. Misingi mikuu.
[https://s0] Kuitambua misingi mikuu ya taifa.

12. Kuzongwa na vikwazo.
[https://s0]Kuwa huru na vikwazo vya kijiografia.

Hebu tuone sasa ni kwa vipi, Historia ya Finland inatupa sehemu ya kufanya majaribio ya njia hizo.

i. #7, Wafinland waliweza kujithamini kwa dhati na kukubali kuwa wao ni nchi ndogo na wamepakana na Wasoviet ambao usalama wao ni hadi waamini kuwa Finland ni tiifu kwao. Ndio maana Serikali ya Paasikivi, ilijenga mahusiano ya juu kabisa na Soviet, hadi leo.

ii. #3, wafinland waliaminisha kuwa sera zao za kusigana na warusi haziwasaidii na hivyo kuweza kubadili elekeo na kuunda Paasikivi-Kekkonen doctrine iliyolenga kukuza uhusiano na Dunia huku ikimuhakikishia Mrusi usalama.

President Kekkonen’s explanation of his own and Paasikivi’s policy, from his political autobiography: “The basic task of Finnish foreign policy is to reconcile the existence of our nation with the interests which dominate Finland’s geopolitical environment.… [Finnish foreign policy is] preventive diplomacy. The task of this diplomacy is to sense approaching danger before it is too close and take measures which help to avoid this danger—preferably in such a way that as few as possible notice that it has been done.… Particularly for a small state which harbors no illusions that the stances it takes can swing the scales one way or another, it is vitally important to be able in good time to form a correct conception of the strength of those factors on which future development in the military and political sector will depend.… A nation should rely only on itself. The war years taught us an expensive lesson in this respect.… Experience also taught us that a small country purely and simply cannot afford to mix emotions—be they feelings of sympathy or antipathy—into its foreign policy solutions. A realistic foreign policy should be based on awareness of the essential factors in international politics, namely national interests and the power of relationships between states.” [Ukurasa 90, Upheaval]

iii. #6, Finland licha ya mavamizi na tishio la usoviet, bado utaifa wao hawauachi. Lugha yao, music wao, sanaa zao, na Demokrasia.

iv. #9, uvumilivu wa kuanguka awali.
Wafinland walijaribu mwaka 1940, na kumkacha Msoviet, lakini walishindwa. Waliweza vumilia, na kuweza jaribu tena mwaka 1940.

v. #10, uwezo wa kubadilika na kukubalia na hali.

Wafinland, walipaswa wawashitaki watu wao wenyewe. Yaani mfano, sisi Watanzania, tulipovamiwa na Iddi Amin 1978, kama tungeshindwa ile vita, kisha Iddi Amini atuamrishe tuwashtaki na kuwafunga viongozi wote kama kina Msuguli walioongoza vita vinginevyo angewachukua mwenyewe na kwenda kuwafunga kwenye jela zake za mateso makali huko Lubiri. Ni jambo la aibu na fedheha, lakini viongozi walitumia busara, kuanzisha kesi na kuwafunga, sababu hawakua na namna.

vi. #10, misingi ambayo lazima ilindwe. Wafinland wanapenda uhuru na hawataki kutawaliwa. Ndio maana Baltic states zingine zilipokubali kuwa chini ya soviet, wao walikataa. Na kusimama katika vita zote mbili.

Yapo mambo yalikuwa kinyume kwao;

vii. #4, Finland walikosa misaada toka kwa mataifa rafiki.

Viii. #5, hawakuwa na mataifa ya kuiga njia zao.

Ix. #12, hasara ya kijiografia. Kupakana na Urusi, kumewanyima Finland uhuru wa kufanya sera za nje kwa utashi wao, ni lazima mara zote wahakikishe sera zao, hadi leo, hazimuathiri mrusi.


Jambo moja lilikuwa na pande mbili;

X. #1, awali hawakukubali kama taifa kuwa wako kwenye crisis, ndio maana walivunja mkataba na Soviet 1940, lakini mwaka 1944 waliafikiana na kukubaliana.

MIGOGORO YA DUNIA; MTAZAMO WENYE KUKATA TAMAA.

Kwenye kitabu hiki amegusia migogoro inayoikumba dunia kwa sasa; Tishio la silaha za Nuklia, Mabadiliko ya Tabia nchi, Kuzidi kupungua kwa rasilimali za kuhimili idadi ya watu na kuongezeka kwa tofauti ya kimaisha kati ya masikini na matajiri.

Ni vipi tunaweza yatatua kwa njia zile 12.

Katika jicho la uhalisia, ni kweli kabisa dunia inakabiliwa na matishio hayo. Mf Suala la Ugaidi; Sisi Tanzania wenzetu wa Kusini wameshudia vitendo vya mauji ya kutisha huko Mtwara na majirani zetu Msumbiji. Pia nchi kama Nigeria wanasumbuliwa na Ugaidi wa Boko Kharam. Ukipitia njia hizo 12, unaona ni kama Diamond anaungana na wengi waliokata tamaa juu ya uwezekano wa dunia kuyatatua matatizo haya.

i. #4, Hatuna watu wengine wa kuwaomba msaada. Sisi ni sayari pekee kati ya Tisa yenye kuishiwa na watu. Tofauti na matatizo ya Ujerumani mwaka 1945-48, aliweza pata msaada kutoka Marekani na Uingereza, sisi kama dunia hatuna sehemu ya kupata msaada.

ii. #5, Sambamba na hilo, hatuna watu wengine tunaoweza kuwaegelezea njia za kutatua matatizo kama Mabadiliko ya Tabia nchi.

iii. #6, Dunia hatuna utambuzi wa aina moja. Mfano, Dini zimetugawa, siasa na matarajio ya maisha.

iv. #7, Hatuna maadili ya kufanana. Nini sahihi kwa afrika, sio sahihi ulaya.

v. #8, Hatuna uzoefu wa Nyuma wa majanga kama Mabadiliko ya Tabia nchi.

vi. #9, pia hatuna mahala pa kuyaangalizia majaribio yetu yaliyoshindwa. Mifumo kama ya League of Nation na UN, imethibitika kushindwa hadi sasa.

vii. #1, hatuna makubaliano ya pamoja juu ya matatizo. Hapa naomba nitoe mfano binafsi wa Nigeria. Nigeria wao wanashida kubwa ya ugaidi. Lakini changamoto kuu ni moja, hakuna maelewano ya kitaifa kuhusu ugaidi kuwa ni tatizo. Wapo watu wengi ndani ya Serikali wanaunga mkono Boko Haram. Pia katika level ya dunia, wapo mamilioni ya watu wanawaunga mkono magaidi wa namna zote.

viii. #2, Dunia haina Maridhiano ya kukubali kuwajibika. Mf, mabadiliko ya Tabia nchi, mataifa makubwa hayako tayari hadi sasa kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa, Mfano mabadiliko ya Tabia nchi, mataifa makubwa hayako tayari hadi sasa kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa.

ix. #7, Hatutaki kufanya tathmini ya dhati juu ya mchango wetu katika migogoro ya dunia ya sasa.

Ukisoma kitabu hiki, unaona mwandishi naye hana matumaini, ingawa mshumaa wake wa matumaini bado haujazima kwani anaona ipo njia ya kufanya.

Anamini Makubaliano ya kikanda ni uelekeo wa dunia kufikia Maridhiano ya pamoja, akitolea mfano Wa EU. Lakini ukitazama sawa sawq, EU haiko stable kwa sasa, mfano Uingereza tayari imekwisha jitoa. Afrika imekuwa na AU kwa miaka mingi, lakini unyonywaji bado umetawala.

Pia anaamini mataifa mawili ya India na China yenye ⅓ ya watu duniani, yakiungana kupitia Bilateral agreements, basi wanaweza punguza athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa zaidi ya 30%. Lakini eneo hili mimi bado sina matumaini kabisa, sababu mataifa haya hayako tayari kuacha faida za kiuchumi na hadi sasa dunia imekuwa na makubaliano ya kila mwaka, lakini bado hakuna usimamizi wa maadhimio.

Na tatu anaamini makubaliano ya dunia kwa ujumla yatasaidia kutatua migogoro yetu. Lakini UN imekuwepo kwa ziaidi ya miaka 70 sasa, lakini amani ya dunia kwa masuala kama Ugaidi bado yanaitesa dunia.

Mtazamo wangu; Matatizo ya dunia yote manne—ugaidi, utofauti wa maisha, mabadiliko ya tabia nchi na tishio la silaha za Nuclear, linatokana na mfumo wa hodhi wa kichumi wa dunia ambao ni wa kinyonyaji na unaolenga faida tu, ndio chanzo cha matatizo hayo manne. Ukitazama takwimu, Waharibifu wakubwa wa hali ya hewa na tabia nchi kwa ujumla ni mataifa makubwa yaliyoendelea kiviwanda

Hivyo, bila kurekebisha mfumo wa kiuchumi na kuwa na sera za Dunia zinafanyia manufaa watu na Ustawi wa dunia na sio makampuni, migogoro hiyo mikuu ya dunia, haitorekebishika.

Kwa ujumla kitabu hiki kina hoja zinazochokoza akili na kuongeza mambo ya muhimu katika mjadala wa hatma ya ulimwengu. Mwandishi ana mtazamo kuwa dunia kama jinsi tunavyoifahamu, huja ikaanguka ifikapo mwaka 2050. Cc: Red Giant Kiranga MALCOM LUMUMBA Iceberg9 Elungata Paula Paul Nowonmai
 
Nimesoma hii hadi nikahisi nasoma kitabu chote. Nilivyofika nusu nikawaza, "baada ya hii nitatakiwa nisome kitabu tena"?

Thanks for distilling the key insights. Una uandishi/Lugha nzuri nimependa sana japo ni ngumu kidogo.

Okay, Wakati nasoma hii nikakumbuka nimewahi kusikia interview ya Jared kuhusu hii "Upheaval" ila nilisahau kabisa hadi nilivyo soma. IIRC, alisema angeweza kuandika zaidi kuhusu hizi zinazokumba dunia lakini wasiwasi wake ni watu wasingekizingatia kitabu chake kwa sababu ya ukubwa. Lakini pia kuandika kidogo inaonekana ameacha mambo mengi. Nahisi alitamani pia kuandika kuhusu hayo magonjwa ya milipuko n.k.

Asante kwa kurahisisha, sasa nikisoma hiki kitabu sitasoma (nitaruka) Finland chapter. Nimeelewa vizuri sana kutoka kwa summary yako na inatosha.
 
Nimesoma hii hadi nikahisi nasoma kitabu chote. Nilivyofika nusu nikawaza, "baada ya hii nitatakiwa nisome kitabu tena"?

Thanks for distilling the key insights. Una uandishi/Lugha nzuri nimependa sana japo ni ngumu kidogo.

Okay, Wakati nasoma hii nikakumbuka nimewahi kusikia interview ya Jared kuhusu hii "Upheaval" ila nilisahau kabisa hadi nilivyo soma. IIRC, alisema angeweza kuandika zaidi kuhusu hizi zinazokumba dunia lakini wasiwasi wake ni watu wasingekizingatia kitabu chake kwa sababu ya ukubwa. Lakini pia kuandika kidogo inaonekana ameacha mambo mengi. Nahisi alitamani pia kuandika kuhusu hayo magonjwa ya milipuko n.k.

Asante kwa kurahisisha, sasa nikisoma hiki kitabu sitasoma (nitaruka) Finland chapter. Nimeelewa vizuri sana kutoka kwa summary yako na inatosha.
Asante kwa kusoma Sista.

Kwa kweli napenda sana vitabu vya Diamond, namna yake ya kuitazama dunia ni ya uhalisia sana, na angle yake ya kutazama mambo magumu na kuyavunja vunja kwenye ideas nyepesi kueleweka na zenye mantiki sana. Subtle!

Mf, kwenye hiki kitabu ameelezea sana juu ya matatizo nchi ya Marekani, kubwa moja ni ubaguzi wa kisiasa uliopo kwa wanasiasa na wamarekani kwa ujumla. Anasema Marekani kuna utengano mkubwa kati ya Reps na Dems, lakini ndani ya Reps kuna msimamo wa wastani na msimamo mkali, ndani ya Dems nao wako liberal na radicals pia. Na hali hii anasema imeanza kujitokeza miaka ya 80. Katika kutafuta sababu; ameeleza Sababu kadhaa, moja ni Maendeleo ya usafiri wa ndege. Usafiri wa ndege umewafanya maseneta na congressmen wasiishi na familia zao Washington kama zamani, ambapo mtu anaweza kuspend siku nne ofisini, Weekend anasafiri kwenda say California kuungana na familia yake then jumatatu akarudi kazini. Anasema zamani, familia za wabunge na maseneta zilikuwa zikiishi Washington, faida yake ilikuwa wabunge walitengeza mahusiano makubwa kati yao na familia zao. So, hata waliposuguana kisiasa, waliweza kuridhiana kwa sababu ya mahusiano hayo ya kifamilia waliyokuwa nayo.

Hii ni hoja unaweza iona nyepesi lakini ina mashiko sana ukizielewa na kuitafsiri kwenye siasa zetu hapa nchini. Moja ya sababu kwanini Tanzania imekuwa na utulivu wa kisiasa ni mahusiano ya kindugu, kikazi, kifamilia kati ya wanasiasa wa vyama vyote. Kumekuwa na mahusiano personal ambayo hufanya watu wapingane kisiasa tu lakini sio vurugu kati ya Viongozi.

Asante kwa kutaja Interview hiyo ya Diamond, nitaifauta niitazame. Kitabu kizuri sana, chapter nyingine yenye kuvutia sana ni kuhusu Ujerumani! Imenipa taswira ya kijamii ya Ujerumani ambayo ni huwezi ipata shuleni. Mfano, kuna sehemu anaeleza kuwa Hitler alikuwa ni mtawala wa kiimla, lakini anasema, Hitler alikuwa ni reflection ya wajerumani, wajerumani hata katika maisha ya kijamii ni watu madikteta na wenye maisha ya kiimla hata kwenye ngazi ya familia. Anagusia mfano matumizi ya viboko. Hii ilikumbusha kuhusu ukoloni. Wajerumani ni moja ya wakoloni katili sana, ukiangalia mambo waliyofanya Namibia, unaweza elewa hoja ya Diamond ina ukweli kiasi gani.
 
Hiki kitakuwa kitabu changu cha mwisho kwa Diamond, nilipanga mwaka huu nisome vitabu vyake vyote ambavyo sikua nimevisoma.

Sababu ya kukisoma, nataka nizisome kwa undani hoja za Evolution ya mwanadamu.
61kr15s3E5L.jpg
 
Mwenye vitabu vya shuleni kama physics, chemistry, biology na geography tafadhali naomba aviweke humu tusome.
 
38 Reactions
Reply
Back
Top Bottom