Vitabu vya Kezilahabi, sasa vinapatikana madukani na mtandaoni

Tanzania Nchi Yetu Sote

JF-Expert Member
Mar 12, 2017
483
787
MWITO KWA WATAALAMU WA FASIHI
Mchapishaji mashuhuri wa vitabu vya Kiswahili nchini Tanzania, APE Network, ana Mpango wa kutangaza na kuhifadhi kazi bora za fasihi ya Kiswahili kwa kuchapisha, kusambaza, kuweka mtandaoni, kuhifadhi na kuchambua kazi hizo kifasihi.

Shughuli hiyo imekwishaanza na inaendelea. Zaidi ya vitabu 30 vilivyokuwa vimepotea, vikiwamo vitabu vya Kezilahabi, vimekwishahuishwa na sasa vinapatikana madukani na mtandaoni. Aidha, vitabu 500 vya Kiswahili sasa vinapatikana mtandaoni kwa gharama ndogo ya Sh. 2000/= tu (tembelea www.lantern.co.tz).

Ili kufanikisha Mpango huu, Mchapishaji angependa kushirikisha wadau wa Fasihi, hasa wataalamu, wachambuzi, wahakiki na walimu, ambao watapenda kushiriki. Madhumuni ya Tangazo hili ni kukualika wewe mdau mwenye nia na raghba ya kukuza, kutangaza, kuhifadhi na kuendeleza Fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania, ujitokeze na kushiriki katika Mpango huu adhimu. Mtu yeyote ambaye amepata kuhakiki, kufundisha au kuandika tasnifu au kazi maalum kuhusu kazi yoyote ya Fasihi ya Kiswahili anaweza kushiriki.

Namna ya kushiriki
Wasiliana na Mratibu, M.M. Mulokozi (0788-260760) kikashani; au mwandikie kwenye anwani pepe zifuatazo: mugyam@gmail.com na/au tamulokozi50@yahoo.co.uk ukitaja kitabu au vitabu ambavyo ungependa kuvizungumzia. Unaweza kuchagua kitabu chochote kati ya vitabu bora vya Kiswahili unavyovifahamu, na pendekezo lako likikubaliwa utapangiwa siku na saa ya kuhojiwa na kurekodiwa kwa njia ya sauti na video kwa muda usiozidi dakika 30. Mpango huu ni endelevu na hakuna tarehe ya mwisho ya kuleta mapendekezo, japo kuwahi ni muhimu.
KARIBUNI WADAU WOTE TUENDELEZE FASIHI YETU!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom