Vitabu vipya vya TIE na hatma ya Tanzania

Je, unadhani maoni haya ni uonevu kwa Taasisi?

  • Ndiyo

    Votes: 0 0.0%
  • Hapana

    Votes: 16 100.0%

  • Total voters
    16

Teleskopu

JF-Expert Member
May 5, 2017
702
763
Kama ilivyokuwa kwenye post yangu iliyotangulia kuhusu kitabu cha Taasisi ya Elimu: Najifunza Kusoma Darasa la Kwanza Kitabu cha Kwanza, ambacho ndio kimeandaliwa kusambazwa Tanzania nzima kama kitabu cha Kiada kwa ajili ya MAISHA ya wanafunzi na taifa, leo nitaendelea kubainisha makosa MACHACHE TU KATI YA MENGI ndani ya kitabu chao kingine: Najifunza Kuhesabu Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Pili, ambacho ISBN yake kwenye uk i ni 978-9976-61-537-7 lakini kwenye uk ii ni 978-9976-61-535-7.


Ni maombi yangu kuwa watatokea wahusika watakaoweza kufanya kinachopaswa maana, kimsingi, vitabu hivi VINALETA MASHAKA MAKUBWA kwa hatma ya nchi yetu. Siamini kuwa suluhisho ni kuanza kuvitetea vitabu hivi.


Yafuatayo ni hayo makosa MACHACHE TU kati ya mengi kwenye: Najifunza Kuhesabu Kitabu cha Mwanafunzi Darasa la Pili


1. Uk 8 pameandikwa: “Siku moja alinunua daftari nyingi …” ---- Je, wingi wa ‘daftari’ ni ‘daftari’? Kosa hili limerudiwa uk 23, 45, 64.
upload_2017-5-11_11-24-55.png
2. Uk 9 pameandikwa: “Angalia mchoro ufutao …”
upload_2017-5-11_11-25-21.png
3. Uk 19 pameandikwa: “Kujumlisha bila kubadili kwa wima” --- “kubadilini kwa wima” ndio kitu gani? Kilicho cha wima ni ‘kubadili’ au ni ‘kujumlisha’? Kosa hili limerudiwa uk 24, 40.
upload_2017-5-11_11-25-40.png
4. Uk 22 swali la 3 pameandikwa: “Wakaungana na wenzao 427 wa shule ya msingi mapambano.” --------- kwani japo ni Hesabu, ndio usizingatie matumizi sahihi ya herufi kubwa?
upload_2017-5-11_11-25-59.png
5. Uk 23 swali la 7 pameandikwa: “… mitihani yake ya darasa la kwanza na la pili?.” -------- sentensi inawezaje kuishia na alama ya kuuliza na nukta? Swali la 8 nalo hivyohivyo.
upload_2017-5-11_11-26-27.png
6. Uk 24 hatua ya kwanza inasema: “kuna makumi 1 …” lakini ya 2 inasema: “Jumlisha hiyo kumi 1…” -------- Kwa nini hapa useme “kumi 1”? Kosa hili limerudiwa uk 27, 40, 42, 43, 44.
upload_2017-5-11_11-26-47.png
7. Uk 26 kuna “Zoezi la 6” na wa 27 nako ni “Zoezi la 6”. Kosa la namna hii limerudiwa uk 28, 53, 66, 73, 74, 88, 93.
upload_2017-5-11_11-27-11.png
8. Uk 28 swali la 2 linaishia hivi: Shule hizo Jumla ya wanafunzi wangapi? --- wrong sentence.
upload_2017-5-11_11-27-31.png
9. Uk 29 wanasema: “Chati hii ina miraba ya ulalo na wima kama inavyooneshwa na mistari ya ulalo na wima” --- Hivyo, kuna miraba (square boxes) na mistari (arrows).

Mtu atajiuliza:

MOJA: Mraba kama mraba mmoja unawezaje kuwa wa ulalo au wa wima?

MBILI: Aya ya pili inasema: “Ukichunguza mstari wa kwanza wa ulalo una namba 101, 102, 103, 104 na 105.” ----- kwa kuwa hapo juu umetofautisha kati ya mraba (square) na mstari (arrow), je, namba ziko kwenye mstari (arrow) au ziko kwenye mraba (square)?
upload_2017-5-11_11-28-49.png
10. Uk 38 swali la 1 linasema: “Kaka alikuwa na mayai 649, Akauza mayai 415. Alibaki na mayai mangapi? ----- “Alibaki”???

Swali la 6 linasema: “… alikuwa na midoli 888 akauza midoli 573. Alibakiwa na midoli mingapi? --------- hongera kwa kusema “Alibakiwa”. Lakini neno “midoli” ni Kiswahili sanifu?
upload_2017-5-11_11-29-31.png
11. Uk 54 wameandika: “Tunashikana mikono na kufanya duara.” ------- duara huwa linafanywa???
upload_2017-5-11_11-30-9.png
12. Uk 63 Zoezi la 1 limeshatimia na maswali yake na fremu yake, kisha nje ndio unaweka picha za sarafu na kusema: “Chunguza michoro ya sarafu zifuatazo.” Huoni kuwa hizo sarafu ndio zilitakiwa zianze, ndipo useme “Jibu maswali yafuatayo”?
upload_2017-5-11_11-34-43.png

Mtu mmoja akajibu akaniambia kuwa “nyingi ya hizi ni typing errors tu”. Japo si kweli, lakini hata kama zingekuwa ni typing errors peke yake, basi ndio mnataka kutuambia hamna mpango wa kuzisahihisha? Au mnamaanisha kuwa zinakubalika? Na kama mna mpango wa kuzisahihisha, mnaona ni sawa tu kutumia mabilioni ya fedha kuchapa upya vitabu ambavyo tayari mmeingiza makosa lukuki na vimeshazamisha fedha nyingi? Je, na hivi mnavyosambaza au mlivyosambaza mtavirudisha na kuvitupa?


Tunaponya taifa au tunaliangamiza?
 
Bado kuna ombwe kubwa sana katika mamlaka zinazoshughulikia elimu. Hapa nashauri wahusika waviondoe mashuleni hivyo vitabu ili kuondoa mkanganyiko
 
Bado kuna ombwe kubwa sana katika mamlaka zinazoshughulikia elimu. Hapa nashauri wahusika waviondoe mashuleni hivyo vitabu ili kuondoa mkanganyiko
Ni kweli kabisa Kwezisho. Gharama yake mbeleni itakuwa ni kubwa sana.
 
Mtunzi, mpiga chapa na mhakiki wamepungukiwa weledi katika sarufi za kiswahili.

Maneno katika lugha hujengwa kwa viambishi anuwai pia hawakuzingatia njeo. Ni makosa ya kimazoea mfano neno “midoli” mwandishi alipaswa kutumia neno "Wanasesere"

Tuamini ukosoaji huu utachukuliwa kama changamoto ya kufanywa masahihisho.
 
Back
Top Bottom