Vitabu vipya vya taasisi vinaokoa au kudhalilisha elimu ya Tanzania?

Unadhani maoni haya yanawaonea TIE?

  • Ndio

    Votes: 0 0.0%
  • Hapana

    Votes: 9 100.0%

  • Total voters
    9

Teleskopu

JF-Expert Member
May 5, 2017
702
765
Nahisi hatujajua thamani ya elimu. Tumezoea kusikia kwenye soka Tanzania ikiitwa “kichwa cha mwendawazimu.” Nahisi kama kwenye Elimu nako hakuna tofauti.

Lakini nisiseme sana, labda teleskopu yangu ina ukungu. Mniwie radhi kama nitakuwa nimekosea. Nina tu-swali tuchache naomba mchango wa mawazo.

Endapo nitakuwa sahihi kama ninavyohisi, basi, “Somo hilo hapo juu lahusika!”

Vyombo vya elimu vilisema kuwa kuwapo kwa vitabu mashuleni toka kwa wachipishaji wengi (viliitwa ‘utitiri wa vitabu’) ni tatizo --- JAPO MTU ATAJIULIZA, UNAEPITISHA VITABU SI NI WEWE? KWA NINI USITEUE KIMOJA KWA KILA SOMO UNACHOONA KIMEKIDHI VIGEZO ULIVYOWEKA WEWE MWENYEWE?

Basi, suluhisho likatangazwa kuwa ni Taasisi ya elimu (TIE) ndiyo inatakiwa kuandika hicho kitabu kimoja kwa kila somo kwa ajili YA NCHI na “future” yake.

Mantiki ya tamko hilo ni kuwa: TIE ndio WENYE UWEZO wa kuandika vitabu (na sio “Makanjanja” – yaani waandishi binafsi kama walivyoitwa wakati ule).

Sasa naomba nizungumzie kitabu ambacho sasa ndio kimeandaliwa na TIE chenye jina: Najifunza Kusoma Darasa la Kwanza Kitabu cha Kwanza, kisha wadau tusaidiane kubainisha iwapo hiki: (a) kinatimiza malengo yale (b) kinafaa kutumiwa na watoto wetu (c) kinabeba hatma tarajiwa ya Tanzania.

Haya ni MACHACHE kati ya mengi niliyoyabaini kwenye kitabu hiki:

1. Uk 3 wameandika: “Tusimulie matendo tunachofanya tunapoamka. ---------- tunachofanya??
upload_2017-5-10_12-52-40.png
2. Uk 6 swali la 1: Taja majina yawanyama hawa. ---- “yawanyama” ni neno moja??
upload_2017-5-10_12-52-56.png
3. Uk 10 swali la 2: Ni jina la picha ipi lenye sauti ya mwanzo isiyofanana na sauti ya mwanzo ya jina la picha nyingine? --------- Hivi hii ni sentensi ya mtoto wa Darasa la 1? Imerudiwa mara nyingi kwenye kurasa mbalimbali.
upload_2017-5-10_12-53-9.png
4. Uk 26: “tamka za herufi” ni Kiswahili sahihi? Neno “Silabi” --- Haya ndiyo matumizi ya herufi kubwa? Swali la 5, neno “bima” kwa mtoto wa Darasa la 1? Akiuliza, "Bima ndio nini mwalimu?" mwalimu atajibuje hadi aelewe?
upload_2017-5-10_12-53-23.png
5. Uk 37 swali la 9 linasema: Tazama picha zifuatazo kisha kamilisha sentensi hizo. ---- “sentensi hizo”????
upload_2017-5-10_12-53-36.png
6. Uk 39 swali la 3 linasema: Soma habari hii kisha jibu maswali yafuatayo: ------- Hivi unaweza kutumia neno “yafuatayo” kwa mtindo hii? Sentensi mwisho wa habari inasema: “Bei ni mia.” ---- duh!!!!!
upload_2017-5-10_12-53-52.png
7. Uk 67 swali la 2 linasema: Keki na pilau ni nini? ----- Hivi unaweza kuuliza hivi ili mtoto aseme “ni tamu”? (maana ndilo jibu wanalotaka)
upload_2017-5-10_12-54-10.png
8. Uk 117 swali la 7 linasema: Baba yake ina nguvu. -------- Are we serious? Hata Wakenya nadhani hawaandiki hivi.
upload_2017-5-10_12-54-24.png
9. Uk 119 swali la 2 kumeandikwa: “Unda na tusome silabi …” -------- Sijui wewe msomaji unaonaje hapo?
upload_2017-5-10_12-54-53.png
10. Uk 125 kuna embe imekatwa nusu halafu imeitwa “kokwa”
upload_2017-5-10_12-55-11.png
11. Uk 127 kwenye habari kuna sentensi inasema: Mimi ni zaidi yako, bila mimi huwezi kwenda nchi za mbali.-------- Hii ni sentensi moja kweli?
upload_2017-5-10_12-55-28.png
12. Uk 128 swali la 10: Soma habari hii. Kisha jibu maswali. ---------- Hizi ni sentensi mbili kweli? Sentensi mbili za mwisho zinasema: Mwalimu Limo alimwambia Furaha asikate tamaa. Aendelee kusoma kwa bidii atafaulu. ---------- Ndugu msomaji, wewe unazionaje ladha yake?
upload_2017-5-10_12-55-44.png
13. Jambo la mwisho kwa hapa, angalau mojawapo kwa upande wa usanifu, ni kuwa: unaonaje ukisoma kitabu ambacho kimejaa BOLD, BOLD, BOLD letters kila sehemu? Je, huo ni uandishi mwafaka kweli?
upload_2017-5-10_12-56-54.png
Sasa, kitabu chote kiko kimtindo huu.

……………….

Kama nilivyosema, “HAYA NI MACHACHE TU.”

Please, somebody do something about our education!

Maoni yangu:

1. Serikali waendelee kusimamia ubora wa vitabu kupitia EMAC.

2. Kama TIE wanaandika, nao washindane na wachapishaji wengine kwa usawa lakini sio kupitisha sheria ya kufungia wengine, kisha wanaleta vitu kama hivi - vinginevyo basi waboreshe kwelikweli.

3. Kama vitabu vingi ni utitiri na ni tatizo, basi chagua kimoja KILICHO BORA kwa kila somo toka kwa mchapishaji YEYOTE – kwa mujibu wa vigezo unavyotaka mwenyewe – ambavyo sina uhakika kama kipimo cha vigezo hivyo ni vitabu hivi vinavyoandikwa na TIE kwa sasa.

4. TIE wanawezaje kuwa waandishi na hapohapo ndio mahakimu wa kuhukumu kazi za wachapishaji wengine? (kwa maana kwamba EMAC imekuwa ni sehemu ya TIE)? Je, watatenda haki kwa watu ambao hawangependa wawazidi? Je, wao wanahakikiwa na nani? BAKITA wanawahikiki? EMAC gani inawahakiki wao?

Ni hayo tu Watanzania wenzangu.
 
Nafikiri kuna kukosa weledi hapo. Kitabu hicho ni dhahiri hakija haririwa (not edited). Na wataalamu wa kiswahili tunao. Sasa huko kwenye masomo mengine sijui mambo yakoje. Ndio maana mimi sikubaliani na wale wanaosema tukifundisha kiswahili watoto watafanya vizuri. Inaelekea hata kiswahili chenyewe ni shida.

Wangeweza kutengeneza miongozo kwa watungaji/waandishi wa vitabu, halafu wanavipitia kutokana na vigezo vilivyo wazi kwanza kila kitabu kinapewa pasi au shindwa, pili vile vilivyoshinda vinalinganishwa na kilicho bora kinatumika. Tatizo hua inakuwa 10% nafikiri-kuandika na kuchapisha. Lakini wakiwa serious inawezekana kupata vitabu bora.

Kama ni lazima TIE waandike basi kuwe na jopo lingine la kutathmini kilicho andikwa lakini hii inapunguza umakini na swali nani atachagua hilo jopo. Wao wasimamie kazi watu wengine waifanye.
 
mtoa thread badilisha kwanza heading yako kisha ndo uwakosoe wengine
 
Mkuu mleta mada, kwanza nikupe pongezi kwa uchambuzi wako na kuona hili.
Kwa kweli nimesikitika jinsi ambavyo watendaji mbali mbali katika nchi hii hawapo makini kabisa katika kazi zao, hicho kitabu unaweza ona ni namna gani kimepita chini ya wasimamizi mbali mbali wa idara mpk kikachapishwa namna hiyo tena kwa rangi na nakshi mbali mbali bila watu kupima yaliyomo, huu ni uozo na aibu, Mheshimiwa Rais tupia jicho lako hapo kuna majibu sugu.
 
mtoa thread badilisha kwanza heading yako kisha ndo uwakosoe wengine
Teh teh. Asante manchoso. Nilijaribu kweli lakini ilishindikana. Nilitafuta mahali pa ku-edit heading nikakosa bhana. But all in all, hii huwezi linganisha na KITABU ambacho kinakuwa na editorial team na ambacho unaingiza pesa lukuki only to end up with a pile of errors kama hivi.
 
Mkuu mleta mada, kwanza nikupe pongezi kwa uchambuzi wako na kuona hili.
Kwa kweli nimesikitika jinsi ambavyo watendaji mbali mbali katika nchi hii hawapo makini kabisa katika kazi zao, hicho kitabu unaweza ona ni namna gani kimepita chini ya wasimamizi mbali mbali wa idara mpk kikachapishwa namna hiyo tena kwa rangi na nakshi mbali mbali bila watu kupima yaliyomo, huu ni uozo na aibu, Mheshimiwa Rais tupia jicho lako hapo kuna majibu sugu.
Nakubaliana nawe kabisa kluger. Inasikitisha. Elimu imekuwa ni mahali pa kuchezea. Anakuja huyu anasema ondoa masomo ya biashara, ondoa michezo; anakuja huyu anasema yarudisheni. Mara mwingine anasema private publishers waondoke. Lakini watoto wanaendelea kusogeza miaka; haiwangoji. Hadi sasa naamini shuleni hakuna vitabu maana purchases za mwisho zilikuwa ni zile fedha za radar. Nobody cares.
 
Teh teh. Asante manchoso. Nilijaribu kweli lakini ilishindikana. Nilitafuta mahali pa ku-edit heading nikakosa bhana. But all in all, hii huwezi linganisha na KITABU ambacho kinakuwa na editorial team na ambacho unaingiza pesa lukuki only to end up with a pile of errors kama hivi.
ni kweli mkuu nimeona wamemchemka sana hawako serious
 
Nafikiri kuna kukosa weledi hapo. Kitabu hicho ni dhahiri hakija haririwa (not edited). Na wataalamu wa kiswahili tunao. Sasa huko kwenye masomo mengine sijui mambo yakoje. Ndio maana mimi sikubaliani na wale wanaosema tukifundisha kiswahili watoto watafanya vizuri. Inaelekea hata kiswahili chenyewe ni shida.

Wangeweza kutengeneza miongozo kwa watungaji/waandishi wa vitabu, halafu wanavipitia kutokana na vigezo vilivyo wazi kwanza kila kitabu kinapewa pasi au shindwa, pili vile vilivyoshinda vinalinganishwa na kilicho bora kinatumika. Tatizo hua inakuwa 10% nafikiri-kuandika na kuchapisha. Lakini wakiwa serious inawezekana kupata vitabu bora.

Kama ni lazima TIE waandike basi kuwe na jopo lingine la kutathmini kilicho andikwa lakini hii inapunguza umakini na swali nani atachagua hilo jopo. Wao wasimamie kazi watu wengine waifanye.
Masiya, miongozo ipo. Hicho kinachoitwa EMAC ni chombo rasmi chenye miongozo inayotaka kitabu kiwe na standards fulani. Bila hivyo hakiwezi kupitishwa. Lakini hawa wenzetu kwa kuwa wao ni serikali, huwa hawapeleki kule. Ukiweza kuangalia hata syllabus walizoandika, ni aibu tupu. FULL OF ERRORS. Sasa sijui kitu gani kitawafanya wabadilike hivi sasa na ukichukulia kazi yenyewe is even bigger and complex. Ni kudanganyana tu.
 
kama watoto ndo wanaenda kusomeshwa hivi vitabu basi shida ipo wizara ilitazame hili janga
Hivyo ndio vitabu RASMI (Kiada) machoso. Vingine vyote wanasema ni vya ziada. Kitabu cha ziada maana yake ni mwalimu tu mwenyewe atanunua kupanua ujuzi wake, lakini serikali ikinunua na kusambaza, basi vinakuwa ni hivi ya TET.
 
kama ni hivyo hilo ni tatizo kwa makosa hayo basi hakuna elimu hivyo vitabu vitaenda kutuharibia watoto wetu
 
kama ni hivyo hilo ni tatizo kwa makosa hayo basi hakuna elimu hivyo vitabu vitaenda kutuharibia watoto wetu
ni kweli kabisa. State monopoly tangu zamani ilishashindwa. Sijui kwa nini iweze leo.
 
Masiya, miongozo ipo. Hicho kinachoitwa EMAC ni chombo rasmi chenye miongozo inayotaka kitabu kiwe na standards fulani. Bila hivyo hakiwezi kupitishwa. Lakini hawa wenzetu kwa kuwa wao ni serikali, huwa hawapeleki kule. Ukiweza kuangalia hata syllabus walizoandika, ni aibu tupu. FULL OF ERRORS. Sasa sijui kitu gani kitawafanya wabadilike hivi sasa na ukichukulia kazi yenyewe is even bigger and complex. Ni kudanganyana tu.
Nashukuru kwa taarifa. Kama ni hivyo wawe compelled kupeleka EMAC-kitabu chochote kinatakiwa kipate independent reviewers. Ni kukosa weledi kama hawafanyi hivyo. Hivi hakuna njia ya kumuandikia waziri husuka na evidence uliyoweka hapo juu ayaone mwenyewe.
 
I wish it were possible. Sijajua endapo kuna njia ya kufanya hivyo Masiya. Nimeweka tu humu hoping kwamba kuna mtu aliye significant ataweza kuona; yamkini na wabunge ambao wako bungeni sasa.
 
Isipokuwa tatizo kubwa ni kuwa EMAC ambayo zamani ilikuwa wizarani, siku hizi wanayo wao. Imo ndani ya utawala wao. Kwa hiyo, siamini kama inaweza tena kuwakagua wao fairly.
 
Isipokuwa tatizo kubwa ni kuwa EMAC ambayo zamani ilikuwa wizarani, siku hizi wanayo wao. Imo ndani ya utawala wao. Kwa hiyo, siamini kama inaweza tena kuwakagua wao fairly.
Kama ni hivyo basi waalike watunzi wa nje ya TEA na wao through EMAC wafanye kazi ya quality control badala ya kuwa watunzi.
 
I wish it were possible. Sijajua endapo kuna njia ya kufanya hivyo Masiya. Nimeweka tu humu hoping kwamba kuna mtu aliye significant ataweza kuona; yamkini na wabunge ambao wako bungeni sasa.
Kama unaweza kuiconnect na jukwaa la siasa inaweza kupata wider audience na probably ku-land in good hands. Jukwaa hili sijui kama hao jamaa wanapita sana.
 
Qumermake elimu ya Bongo. Kasikilize wimbo wa Bonta kamshirikisha Baraka unaitwa Zero, ameelezea sababu ya ukweli ya wanafunzi kufeli.

Kuna watu walidai eti sababu ni madawati.
 
Kama unaweza kuiconnect na jukwaa la siasa inaweza kupata wider audience na probably ku-land in good hands. Jukwaa hili sijui kama hao jamaa wanapita sana.
Nimeiweka hata kule. Natumaini itakuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom