Vitabu vilivyoandikwa na Waandishi wa Tanzania

Hadithi za Madaruweshi - Mwandishi "Dr. Fredrick Joseph". Kiukweli kuna Watanzania wanajitahidi sana kuandika vitabu lakini wanaishia kusoma wenyewe na baadhi ya watu wachache sana kwenye jamii husika. Bado tunamuamko mdogo sana katika nyanja hii ya usomaji vitabu.
 
Niliwahi kuiba kitabu cha Musiba maktaba ya Arusha nikawa nachana karatasi tano tano mpaka kikaisha......aise
Wanunulie uwarudishie.

Kuiba kitabu ni kitu kibaya.

Kuchana kitabu ni kitu kibaya zaidi.

Sisi tulikuwa tunaenda ofisi ya Propaganda ya Urusi, ilikuwa pembeni ya Diamond Jubilee Road hapa Maliki Road.

Basi wanatupa vitabu vya propaganda za Urusi. Vitabu vyenyewe havisomeki, vimetafsiriwa kutoka Kirusi kwenda Kiswahili, vimejaa propaganda za Kikomunisti.

Basi sisi vile vitabu tukawa tunavichukua, tunampelekea Mzee Rashidi, mkaanga mihogo wa Muhimbili Primary.

Ukimoa Mzee Rashidi vitabu, yeye anakupa mihogo. Mzee Rashidi anatumia karatasi za vitabu kufungia mihogo.

Wale Warusi wangejua vitabu vyao vinatumika kufungia mihogo, hata wasingetupa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania hakuna aliyewahi kuandika vitabu vingi kama Shaaban Bin Robert. Vya harakaharaka ninavyoweza kukumbuka kati vile nilivyosoma ni pamoja na :

(1) Adili na nduguze
(2) Mapenzi bora
(3) Kielezo cha fasili
(4) Masomo yenye Adili
(5) Insha na mashairi
(6) Msululu wa vitabu vya Diwani ya Shaaban; nadhani hivi vilikuwa kumi na mbili, yaani Diwani ya Shaaban-1, mpaka Diwani ya Shaaban-12
(7) Kielezo cha Insha
(8) Maisha yangu baada ya miaka hamsisni
(9) Sanaa ya Ushairi
(10) Wasifu wa Siti Binti Saad
(11) Kufikirika
(12) Kusadikika
(13)Koja la Lugha
(14)......................... na vinginevyo vingi

Hivyo tu vinafikia jumla ya vitabu visovyopungua 23; hakuna mwandishi wa kitanzania aliyewahi kutoa vitabu kufikia hata nusu ya hapo.
 
Asante kwa uzi murua.

Hili lijamaa umilisahau :cool:: Mlenge Fanuel Mgendi

Edit 1:
MamaMwajey.jpg
NihameBondeni.jpg
StareheGharama.jpg

Porojo.jpg
 
Kichuguu,
Huyu mtu alikuwa fasaha sana. Kwangu mimi sijawahi kuona fasaha kama huyu katika lugha ya Kiswahili.

Ninavyo vitabu viwili na nina mpango wa kuongeza vingine.

Hicho namba 8 na kingine kina husu misemo ya Kiswahili.
 
Kiranga,
Uandishi wa Aristabalus Elvis Musiba haukuwa na originality yoyote. Alikuwa akitafsri vitabu vya Nick Carter -Spymaster na kuviandika katika mazingira ya kiswahili wakati actions zote ni zile zile. Kwa mfano kama ulisoma kitabu cha Vatican Vendetta ndicho alichotumia kuandika kitabu chake kimoja, nadhani kitabu cha "Kufa na Kupona"
 
Originality is overrated.

There is nothing new under the sun.

Hata huyo character Nick Carter wamemuandika waandishi angalau wanane kutoka mwaka 1886.

Sasa hata huo mfano wako wenyewe unaonesha originality is overrated.

Kwa sababu originality ingekuwa muhimu, muandishi mmoja tu angemuandika Nick Carter, wengine wangekuja na characters wengine kila mtu na wake.

Mimi Musiba amenipa hamasa kubwa sana ya kusoma, kwa wakati ambao hakukuwa na vitabu vya caliber ya alivyoandika yeyr katika Kiswahili.

Hilo tu linatosha kumpa hongera zake, whether alikuwa original or not.

In fact kuona tu mtu anaandika kuhusu spy anayeenda Palm Beach Hotel, sehemu ninapopajua, anatembea Sea View, sehemu ninapopajia etc, aliyeongelea mambo kama ukombozi wa Kusini mwa Afrika, jambo ambalo lilikuwa hot topic kwetu,kulifanya kwangu Musiba awe original.

Hakukuwa na Mtanzania aliyeandika vike kabla ya Musiba kwa watu niliowasoma.

Ukitaka sana mtu awe original mwisho utataka atunge alphabet yake na lugha yake tujifunze upya ili kusoma kitabu original.

Na hata hapo hatakuwa original, maana vitabu vishaandikwa tangu miaka ya falme za ki Babiloni.

Sasa unachora wapi mstari wa originality kusema hiki original na hiki si original?

Wakati watu wameandika kuhusu ujasusi tangu enzi za "The Epic of Gilgamesh" huko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga,
Katika creative writing kuna tofauti sana kati ya topic, na flow of ideas. Wewe unasema kuwa topic ya spying imeandikwa na watu wengi, that is correct, hata essay assignment kwenye creative writing hutolewa topic, halafu kila mwandishi anaandika kivyake vyake.

Vitabu vyote vya nick carter vilikuwa vya spymaster lakini msululu wa matukuo ulikuwa ni tofauti kati ya kitabu na kitabu, kubadili maandiiko kutoa kiingereza na kuyaweka katika Kiswahili, halafu kuhamisha setting ya maandiko hayo kutoka Rome na kuyaweka Dar es Salaam, na vil vile kuhamisha majina ya characters kutoka Nick Carter na kuwa Willy Gamba, na mwishowe kubadili wizi wa siri za Vatican na kuwa siri za ukombozi ni plagiarism!!!

Ni tofauti kabisa na uandishi kama Katalambula na Shaffi ambao pia waliandika kuhusu topiki hiyo lakini uandishi wao hauwi traced kwa mwandishi mwingine.
 
Kichuguu, Nick Carter kaandikwa na waandishi wangapi?

Na kama originality is all that, kwa nini kila muandishi hakuja na character wake tofauti?

Mfano wako mwenyewe wa Nick Carter unaonesha originality is overrated.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kichuguu, Nick Carter kaandikwa na waandishi wangapi?

Na kama originality is all that, kwa nini kila muandishi hakuja na character wake tofauti?

Mfano wako mwenyewe wa Nick Carter unaonesha originality is overrated.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna historia ya utumiaji wa jina la Nicholaus Carter katika vitabu hivyo kutokea New York miaka hiyo ya sitini, ila ni vitabu vilivyokuwa inspired na vitabu vya Ian Fleming vya James Bond-007. Vitabu hivi viliandikwa na watu wengi sana wakitumia jina la Nick Carter, na main Character pia akiwa ni Nick Carter.

Hata hivyo, series hiyo ilikuwa na editor mmoja Valerie Moolmana ambaye ndiye aliekuwa anaauthorize view published au hapana. Siyo kila alienadika Nick Carter alikuwa published, lazima awe edited kuone kuwa hakuna plagiarism ya aina yoyote..

Huwezi kuquestion series ambayo jina la ama author au main character ni fixed. Vitabu vya James Hadley Chase navyo vilikuwa ni series iliyoanzishwa na james Hadley Chase Mwenyewe, lakini baadaye watu wengi waliongana kuendelea kuviandika kwa jina hilo hilo la james hadley chase.
 
Kichuguu, Hujajibu swali langu.

Kama originality ni muhimu sana kwa muandishi, kwa nini waandishi tofauti wote wamuandike character mmoja Nick Carter?

Kwa nini kila muandishi asije na character wake tofauti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujajibu swali langu.

Kama originality ni muhimu sana kwa muandishi, kwa nini waandishi tofauti wote wamuandike character mmoja Nick Carter?

Kwa nini kila muandishi asije na character wake tofauti?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nafikiri huelewei maana ya originality katika creative writing na hivyo inawezekana huwezi kutofautiisha kati ya plagiarism na inspiration. Kuwa inspired kuandika kitabu kuhusu ujasusi lakini ukaja na hadithi tofauti, hata kama umetumia jina la character lile lile siyo plagiarism, ila kukopti hadithi ile ile na kuiweka katika setting tofauti ni plagiarism.

Tukirudi kwenye vitabu vya Nick Carter, wale waandishi wote waliochangia katika series ile walitumia theme ya series hiyo hiyo, ndiyo maana editor alivikubali, na hawakuchukua credit binafsi; kwa hiyo vilikuwa vinajulikana kuwa vimeandikwa na Nick Carter. Mwishowe correspondences zote zinakwenda kwa Nick carter, siyo kwa aliyendika, au mchangiaji.

Kama kungekuwa na Mwandishi akaandika na kuuza kitabu chake kwa jina lake binafsi nje ya series kungeweza kuwa na matatizo, siyo lazima ya plagiarism, bali ya Trade Mark.
 
Nafikiri huelewe maana ya originality katika creative writing na hivyo inawezekana huwezi kutofautiisha kati ya plagiarism na inspiration. Kuwa inspired kuabndika kitabu kuhusu ujasusi lakini ukajana hadithi tofauti, hata kama umetumia jina la character lile lile siyo plagiarisma, ila kukpti hadithi ile ile na kuiweka katika setting tofauti ni plagiarism.

Tukirudikwenye vitabu vya Nick Carter, wale wanandishi wote waliochangia katika series ile walitumia theme ya series hiyo hiyo, ndiyo maana editor alivikubali, na hawakuchukua credit binafsi; kwa hiyo vilikuwa vinajulikana kuwa viemandikwa na Nick Carter. Mwihsowe correspondences zote zinakwenda kwa Nick carter, siyo kwa aliyendika.

Kama kungekuwa na Mwandishi akaandika na kuuza kitabu chake kwa joina lake binafsi nje ya series kungeweza kuwa na matatizo, siyo lazima ya plagiarism, bali ya Trade Mark
Una mu accuse Musiba plagiarism?

Kigwangala alifanya plagiarism kutika kitabu cha "Why Nations Fail: The Origins of Power, Prosperity and Poverty", kuna sura inaongelea South Korea.

Nikamuambia hapa ume plagiarize pale, nikamuonesha neno kwa neno alivyo plagiarize.

Kwa hivyo, si kweli kwamba sijui plagiarism ni nini. I take plagiarism seriously.

Sasa Musiba ka plagiarize wapi? Tupe detailed account, neno kwa neno, si maneno ya jumla.

Kitabu gani cha Musiba kime plagiarize kitabu gani kingine?

Weka majina ya vitabu hapa tuchambue neno kwa neno.

Nimekuuliza, unachora wapi mstari wa kutenganisha originality na inspiration, hujajibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una mu accuse Musiba plagiarism?

Kigwangala alifanya plagiarism kutika kitabu cha "Why Nations Fail: The Origins of Power, Prosperity and Poverty", kuna sura inaongelea South Korea.

Nikamuambia hapa ume plagiarize pale, nikamuonesha neno kwa neno alivyo plagiarize.

Kwa hivyo, si kweli kwamba sijui olagiarism ni nini. I take plagiarism seriously.

Wait, aliyegundua hiyo plagiarism ya Kigwangala siyo Companero kweli?

Kama sikosei Companero aliwahi hadi kuanzisha uzi humu kuhusu plagiarism ya Kigwangala...
 
Kwanza nashukuru sama kama ulikamata watu wanatumia plagiarism kujipatia sifa; na pia nashukuru kuwa unavumilia typos ninazofanya kwani mara nyingi vidole vyangu huenda kwa spidi tofauti na mawazo yangu wakati ninatype, ndiyo maana huwa narudia post tena baadaye kurekebisaha makosa.

Watu wengu hudhani kuwa plagiarism ni kukopi neno kwa neno tu, hapana, plagiarism ni pana sana hasa kwenye creative writing. Unaweza kutumia maneno na lugha tofauti kabisa lakini ukawa umerudida creation ile ile, hiyo pia ni plagiarim. Kwa hayati Msuiba (tulikuja kufahamiana kipindi fulani alipoanza biashara baada ya kutoka jela) ni kweli nikifanya fair assessment ya kazi zake nitasema kuwa kuna plagiarism, I am sorry ingawa hata mimi nilisoma vitabu vyake vyote; kuna desa kubwa sana.

Angalia maana ya plagiarim hapa: "the practice of taking someone else's work or ideas and passing them off as one's own." Hapo umuhimu upo kwenye work or ideas siyo words. Of course ukikopi maneno moja kwa moja inakuwa ni plagiarism ya waziwazi, lakini hata ukibadilisha maneno ukabakisha ideas bado pia ni plagiarism.
 
Wait, aliyegundua hiyo plagiarism ya Kigwangala siyo Companero kweli?

Kama sikosei Companero aliwahi hadi kuanzisha uzi humu kuhusu plagiarism ya Kigwangala...
Mimi niliigundua independently.

Kuna pahali nilisoma maneno ya Kigwa, nikaona haya maneno mbona kama nishayasoma pahali?

Nikakitafuta kitabu cha " Why Nations Fail", nikalinganisha.

Voila!

Jamaa alibadili lugha tu, hakujitahidi hata kuchanganya maneno kidogo.

Nikamshika shati aombe radhi.

Akakomaa hakuomba radhi mpaka leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom