Vitabu 54 nilivyosoma na kuchambua kwa kina mwaka 2019, na jinsi ya kuvipata

Mi nahitaji vitabu kama hivi lakini hard copy nijisomee mwenyewe nyumbani nikimaliza nibaki navyo kwa ajili ya watu wengine kusoma na pia kiwa na library yangu mwentewe nyumbani. Pia kupunguza addiction yangu na electronic devices kama simu na computer maana vinaharibu macho na macho yangu yameshaanza kuwa na shida. Msaada tafadhali kama naweza kuvipata popote tuwasiliane PM. Asanteni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Someni vitabu vya true billionaires achaneni hao waandishi maskini wakuwajaza ndoto hewa. Ni maoni tu
 
Rafiki yangu mpendwa,

Tangu mwaka 2014 nimejiwekea utaratibu wa kusoma angalau vitabu viwili kila wiki ambavyo vinafikisha idadi ya vitabu visivyopungua 100 kwa mwaka.

Kwa vitabu ninavyosoma kwenye wiki, nimekuwa nachagua kimoja na kukichambua kwa kina ili wengine nao waweze kujifunza kupitia kitabu na uchambuzi huo.

Kwa mwaka huu 2019 unaoisha, katika vitabu zaidi ya 100 nilivyosoma, hapa kuna vitabu 54 ambavyo nimevichambua kwa kina.

soma vitabu zaidi


Unaweza kupata vitabu vyote hivi 54 pamoja na chambuzi zake kwa kujiunga na channel ya SOMA VITABU TANZANIA, kwa kufungua hapa; SOMA VITABU TANZANIA

Karibu kwenye orodha ya vitabu hivi 54 vya mwaka 2019 na ujiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kupata vitabu hivi pamoja na chambuzi zake.

  1. THE SCIENCE OF GETTING RICH Kilichoandikwa Na Wallace D. Wattles; Kila mtu anaweza kuwa tajiri bila ya kujali mazingira, kipato, kipaji au hata shughuli anayofanya. Ipo namna ya kufikiria na kufanya ambayo kila mtu anaweza kuitumia na akapata utajiri mkubwa kwenye maisha yake.
  2. THE MASTER KEY SYSTEM Kilichoandikwa Na Charles Haanel. Hiki ni kitabu ambacho kinatufundisha jinsi ya kutumia nguvu kubwa iliyopo ndani yetu kuweza kupata chochote tunachotaka kwenye maisha yetu. Nguvu hii kubwa iliyopo ndani yetu, ni fikra zetu.
  3. THE 5 AM CLUB; Own Your Morning, Elevate Your Life kilichoandikwa na Robin Sharma ambaye anatushirikisha umuhimu wa kuianza siku yako asubuhi na mapema, wakati watu wengine bado wamelala. Anasema kwa kuimiliki asubuhi yako, utaweza kuyainua zaidi maisha yako.
  4. MILLIONAIRE SUCCESS HABITS: The Gateway To Wealth & Prosperity Ambacho Kimeandikwa Na Milionea Dean Graziosi. Kitu pekee kinachokuzia wewe usipate yale matokeo ambayo wengine wanayapata, ni tabia ambazo unaziishi sasa. Kama ukijua tabia za waliofanikiwa na ukaziishi, basi utaweza kupata matokeo ambayo wanayapata.
  5. HABITS OF A HAPPY BRAIN: Retrain Your Brain to Boost Your Serotonin, Dopamine, Oxytocin, & Endorphin Levels ambacho kimeandikwa na Loretta Graziano Breuning. Ubongo unazalisha kemikali nne ambazo ndizo zinaleta furaha kwenye maisha yetu. Kemikali hizi zinatofautiana kwa ufanyaji wake wa kazi, lakini mwisho wa siku zote zinaishia kuleta furaha. Kemikali hizo ni dopamini, serotonini, oksitosini na endofini.
  6. THE BLUE ZONES; Lessons For Living Longer From The People Who’ve Lived The Longest ambacho kimeandikwa na Dan Buettner. Kupitia utafiti wa mwandishi wa kitabu cha THE BLUE ZONES, yapo maeneo manne duniani ambayo yameonesha kuwa na watu wanaoishi miaka mingi kuliko maeneo mengine. Maeneo hayo ni Sardinia nchini Italy, Okinawa nchini Japan, Loma Linda Calfornia nchini Marekani na Nicoya nchini Costa Rica. Mwandishi ameshirikisha masomo ambayo ameondoka nayo kwenye kila eneo na jinsi ya kuyatumia kwenye maisha yetu ili tuweze kuishi miaka mingi.
  7. FLOW: The Psychology of Optimal Experience kilichoandikwa na Mihaly Csikszentmihalyi. Kitabu hichi kinatufundisha jinsi ambavyo tunaweza kufikia ufanisi mkubwa na furaha kwenye chochote ambacho tunafanya, iwe kikubwa au kidogo, tunakipenda au hatukipendi.
  8. PEAK; Secrets from the New Science of Expertise kilichoandikwa na Anders Ericsson. Kitabu hiki kinatupa siri za kisayansi za kuweza kufikia ubobezi mkubwa kwenye kitu chochote tunachochagua kufanya kwenye maisha yetu. Kitabu hiki kimetokana na tafiti mbalimbali ambazo zimefanywa kwenye eneo la ubobezi na hivyo kimekuja na majibu sahihi ya hatua unazopaswa kuchukua ili kufikia ubobezi.
  9. 21 LESSONS FOR THE 21ST CENTURY ambacho kimeandikwa na mwanahistoria Yuval Noah Harari. Kwenye kitabu hiki, Yuval amezichambua changamoto kubwa 21 zinazotukabili kwenye karne hii ya 21 na kupendekeza hatua tunazopaswa kuchukua ili tusiachwe nyuma na mabadiliko yanayotokea kwa kasi kubwa.
  10. BECOMING SUPERNATURAL: How Common People Are Doing the Uncommon kilichoandikwa na Dr. Joe Dispenza. Hiki ni kitabu ambacho kinatufundisha namna ya kutumia nguvu kubwa iliyopo ndani ya kila mmoja wetu kufanya makubwa na miujiza kwenye maisha yetu.
  11. STEALING FIRE: How Silicon Valley, the Navy SEALs, and Maverick Scientists Are Revolutionizing the Way We Live and Work kilichoandikwa na waandishi Steven Kotler na Jamie Wheal. Hiki ni kitabu kinachotuonesha mapinduzi makubwa ya kiutambuzi yanayoendelea duniani, ambayo wachache wanaoyaelewa wanayatumia kufanya makubwa sana kwenye kazi zao na hata maisha yao kwa ujumla.
  12. THE CODE OF THE EXTRAORDINARY MIND: 10 Unconventional Laws to Redefine Your Life and Succeed On Your Own Terms ambacho kimeandikwa na Vishen Lakhiani. Hiki ni kitabu ambacho kinatupa mtazamo wa tofauti kabisa wa namna tunavyoyachukulia maisha yetu. Katika kitabu hiki tunajifunza kwa nini sheria na kanuni nyingi tunazoziishi siyo sahihi au zimepitwa na wakati. Na muhimu zaidi, kitabu kinatufundisha jinsi ya kuwa na maisha yasiyo ya kawaida, yaani kuwa na maisha ya kipekee kwetu, kwa namna tunavyotaka sisi wenyewe.
  13. CAN’T HURT ME: Master Your Mind and Defy the Odds ambacho kimeandikwa na Mwanajeshi mstaafu David Goggins. Kupitia historia na magumu aliyopitia kwenye maisha yake mpaka kufikia ukomando, Goggins anatushirikisha jinsi ya kutangaza vita na maisha yetu wenyewe ili kufanikiwa. Kwenye kitabu hiki tunajifunza jinsi ya kwenda kwenye vita dhidi yetu wenyewe, yaani tunakwenda kupambana na sisi wenyewe, ili tuache kujihujumu na kujirudisha nyuma, tufungue uwezo wetu mkubwa na kuutumia kufanikiwa zaidi.
  14. SEEKING WISDOM; From Darwin to Munger kilichoandikwa na Peter Bevelin. Mwandishi amefanya kazi kubwa ya kukusanya hekima za watu mbalimbali walioweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yao na kwenda kinyume na mazoea. Kuanzia mwanabaiolojia Charles Darwin ambaye alileta mapinduzi makubwa kwenye baiolojia kwa kufikiri tofauti, mpaka kwa mwanafalsafa mwekezaji Charles Munger ambaye pamoja na mshirika wake Warren Buffett wameweza kupata mafanikio makubwa sana kwenye uwekezaji, kuliko wawekezaji wengine wote.
  15. THE LAWS OF HUMAN NATURE ambacho kimeandikwa na Robert Greene. Kwenye kitabu hiki, Green ametupa sheria 18 za kuijua asili ya binadamu, akitupa mifano halisi iliyowahi kutokea kwa watu waliozingatia sheria hizi na wakafanikiwa au walizipuuza na kushindwa.
  16. HOW TO GET RICH: One of the World’s Greatest Entrepreneurs Shares His Secrets ambacho kimeandikwa na Felix Dennis. Felix Dennis alikuwa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa sana katika sekta ya uchapishaji wa majarida. Felix alianzia chini kabisa, bila ya elimu kubwa wala mtaji, lakini aliweza kuingia kwenye biashara ya uchapishaji wa majarida na kuweza kuwa tajiri mkubwa sana nchini Uingereza. Katika kitabu hiki, Felix anatushirikisha safari ya mafanikio yake, makosa aliyofanya, bahati alizopata na ushauri muhimu kwa wote ambao wanataka kupata utajiri kwenye maisha yao.
  17. YOUR BRAIN AT WORK: Strategies for Overcoming Distraction, Regaining Focus, and Working Smarter All Day Long ambacho kimeandikwa na David Rock. Kwenye kitabu hiki, David ametushirikisha yale muhimu unayopaswa kujua kuhusu ubongo wako, jinsi unavyofanya kazi na njia bora ya kuutumia ili kuondokana na usumbufu, kuongeza umakini na kufanya kazi zako vizuri pamoja na kuwa na utulivu siku nzima.
  18. TRACTION; Get A Grip On Your Business kilichoandikwa na Gino Wickman. Kwenye kitabu hiki, Gino anatuambia kama tutazingatia maeneo sita muhimu ya biashara ambayo ameyafundisha, biashara zetu zitakua na kuwa huru, kiasi kwamba hazitegemei uwepo wetu wa moja kwa moja ndiyo ziweze kwenda.
  19. THE BULLETPROOF DIET: Lose Up to a Pound a Day, Reclaim Energy and Focus, Upgrade Your Life, Kilichoandikwa na Dave Asprey. Kwenye kitabu hiki, Dave siyo tu anatupa dayati ya kufuata, bali anatusaidia kujenga mfumo mpya wa maisha kwenye ulaji. Huu ni mfumo ambao mtu ukiufuata, unapunguza uzito wa mwili bila ya shida, unakuwa na nguvu muda wote na afya yako inakuwa bora. Mpangilio wa ulaji aliouweka kwenye kitabu hiki unaupatia mwili virutubisho sahihi unavyohitaji na kuzuia mwili kwenda kwenye hali ya uhitaji mkubwa ambao unawasukuma wengi kula zaidi na kuongeza uzito.
  20. THE E-MYTH REVISITED: Why Most Small Businesses Don’t Work and What to Do About It, mwandishi Michael E. Gerber anatupa maarifa sahihi ya kutuwezesha kuanzisha na kuendesha biashara zetu kwa mfumo ambao zinafanya vizuri na kutupa uhuru mkubwa. Michael anasema uhuru kwenye biashara upo kwenye mfumo. Kama unaendesha biashara na huna mfumo, huna biashara, bali una kazi, na hiyo ni kazi mbaya kuliko zote.
  21. WHAT GOT YOU HERE WON’T GET YOU THERE: How Successful People Become Even More Successful mwandishi Marshall Goldsmith anatuonesha jinsi ambavyo tabia zetu zinatuzuia kufanikiwa zaidi. Anaanza kwa kutuonesha jinsi ambavyo tabia zetu zinakuwa kikwazo kwetu, kisha anatupa hatua saba za kujenga tabia bora kwa mafanikio yetu.
  22. DIGITAL MINIMALISM: Choosing a Focused Life in a Noisy World ambacho kimeandikwa na Cal Newport. Mwandishi Cal Newport baada ya kuona changamoto kubwa ya simu janja na mitandao ya kijamii kwa wengi, amekuja na falsafa bora ya matumizi mazuri ya mitandao hii, ambayo itakuwa na manufaa kwetu na kuondokana na madhara ya mitandao hii. Falsafa hii haibadili kitu kimoja kwenye matumizi yetu ya simu janja na mitandao ya kijamii, bali inabadili mfumo wetu mzima wa maisha na jinsi tunavyoichukulia na kuitumia mitandao hii. Falsafa hii anaiitwa DIGITAL MINIMALISM na ameieleza kwenye kitabu hiki.
  23. THE URBAN MONK: Eastern Wisdom and Modern Hacks to Stop Time and Find Success, Happiness, and Peace ambacho kimeandikwa na Pedram Shojai. Pedram amekuwa mtawa wa falsafa ya Taoism na pia daktari wa tiba za mashariki. Kupitia uzoefu wake wa utawa na kutibu watu, amegundua kuna changamoto kubwa kumi ambacho tunazipitia binadamu kwa zama tunazoishi. Changamoto hizo ni msongo, muda, nguvu, usingizi, mtindo wa maisha wa kukaa, ulaji, kutengana na asili, upweke, fedha na kukosa kusudi la maisha. Kupitia kitabu chake, Pedream amejadili kila changamoto na kutupa hekima za kuzikabili changamoto hizo kutoka kwenye falsafa za mashariki.
  24. HIGH PERFORMANCE HABITS: How Extraordinary People Become That Way ambacho kimeandikwa na kocha wa mafanikio Brendon Burchard. Kwenye kitabu hiki, Brendon ametushirikisha hatua sita za kujijengea kama tunataka kufanikiwa zaidi. Pia ametutahadharisha na tabia tatu zinazoharibu kabisa mafanikio yetu na tabia moja kuu inayobeba tabia zote za mafanikio.
  25. BUILT TO SELL: Creating a Business That Can Thrive Without You ambacho kimeandikwa na mwandishi John Warrillow. Kupitia kitabu hiki, John ametushirikisha hatua nane za kutengeneza biashara inayoweza kujiendesha bila ya uwepo wako na pia unayoweza kuiuza na kupata fedha zaidi.
  26. THE CHECKLIST MANIFESTO: How to Get Things Right ambacho kimeandikwa na Daktari bingwa wa upasuaji Atul Gawande. Kwenye kitabu hiki, Atul ametuonesha jinsi ambavyo sisi binadamu tunafanya makosa kwenye kazi zetu za kila siku, na njia rahisi ya kupunguza makosa hayo ambayo ni kutumia orodha (checklist).
  27. 101 CRUCIAL LESSONS THEY DON’T TEACH YOU IN BUSINESS SCHOOL kilichoandikwa na Chris Haroun. Kwenye kitabu hiki tumejifunza siri 101 za mafanikio kwenye biashara na maisha kwa ujumla ambazo hazifundishwi kwenye shule ya biashara.
  28. JUST RUN IT!: Running an Exceptional Business is Easier Than You Think kilichoandikwa na Dick Cross. Kupitia kitabu hiki tunajifunza mfumo rahisi wa kuendesha biashara yenye mafanikio makubwa huku ukiwa na uhuru.
  29. THE MIRACLE MORNING: The Not-So-Obvious Secret Guaranteed to Transform Your Life: Before 8AM, ambacho kimeandikwa na Hal Elrod. Kupitia kitabu hiki, Hal anatuonesha kwamba nguvu ya kuyabadili maisha yetu, kutoka umasikini na ukawaida mpaka kufika utajiri na mafanikio ipo ndani yetu. Na kwa kuwa kila mtu analalamika kwamba hana muda, Hal ametuonesha jinsi ambavyo kwa kutenga saa moja tu kila siku na kufanya vitu sita muhimu sana, maisha yako yanaweza kubadilika.
  30. STAND OUT: How to Find Your Breakthrough Idea and Build a Following Around It ambacho kimeandikwa na Dorie Clark. Kwenye kitabu hiki mwandishi anatushirikisha jinsi ambavyo tunaweza kujitofautisha na wengine kwa kile tunachofanya. Mwandishi anatufundisha njia ya kubobea sana kwenye kile tunachofanya kwa namna ambayo tutakuwa viongozi ambao wengine wanatuangalia na kujifunza kutoka kwetu (thought leader).
  31. GETTING EVERYTHING YOU CAN OUT OF ALL YOU’VE GOT: 21 Ways You Can Out-Think, Out-Perform, and Out-Earn the Competition ambacho kimeandikwa na kocha wa biashara Jay Abraham. Kwenye kitabu hiki, Jay ametushirikisha njia 21 za kuweza kufikiri, kufanya na kutengeneza kipato zaidi kuliko wengine kupitia kazi au biashara tunazofanya.
  32. THE ART OF PUBLIC SPEAKING ambacho kimeandikwa na waandishi Dale Carnegie na J. Berg Esenwein. Kwenye kitabu hiki, waandishi wametushirikisha maarifa na mbinu sahihi za kuweza kuongea mbele ya wengine kwa kujiamini na kwa ushawishi ili tuweze kupata kile tunachotaka na hata kuwanufaisha wengine pia.
  33. HOW TO WRITE COPY THAT SELLS; The Step-By-Step System For More Sales, to More Customers, More Often kilichoandikwa na Ray Edwards. Mwandishi Ray ni mmoja wa waandishi mashuhuri wa matangazo na nakala za mauzo. Kupitia kitabu hiki anatushirikisha siri na mbinu muhimu ambazo tukizielewa na kuzitumia tutaweza kuandika nakala bora kabisa za kuuza chochote tunachouza.
  34. TO SELL IS HUMAN: The Surprising Truth About Moving Others kilichoandikwa na Daniel H. Pink. Kwenye kitabu hiki, mwandishi anatuonesha kwamba kila mtu sasa yupo kwenye mauzo na kwamba mauzo kwa sasa yamebadilika sana. Anatushirikisha misingi mipya ya kufanikiwa kwenye uuzaji pamoja na mbinu sahihi za kupata ushawishi kwa wengine.
  35. HOW TO BE A STOIC: Using Ancient Philosophy to Live a Modern Life kilichoandikwa na mmoja wa wastoa wa zama zetu Massimo Pigliucci. Ustoa ni Falsafa ambayo imekuwepo kwa zaidi ya miaka elfu mbili sasa, ambayo lengo lake kubwa limekuwa kuwafanya watu kuwa na maisha bora, kwa kuishi kwa misingi sahihi. Hii ni falsafa ambayo kila mtu akiweza kuielewa na kuiishi basi lazima atakuwa na maisha bora.
  36. RICH DAD’S BEFORE YOU QUIT YOUR JOB: 10 Real-Life Lessons Every Entrepreneur Should Know About Building a Multimillion-Dollar Business ambacho kimeandikwa na Robert Kiyosaki. Kwenye kitabu hiki, Kiyosaki ametushirikisha mambo 10 ambayo mtu anapaswa kuwa na maandalizi nayo kabla hajatoka kwenye ajira na kwenda kujiajiri. Wapo watu wengi ambao wapo kwenye ajira, wanatamani sana kutoka na kwenda kujiajiri, lakini wakiwaangalia wale waliowahi kutoka kwenye ajira na kwenda kujiajiri, wanapatwa na hofu kubwa. Kwa sababu wengi wanakuwa hawajapiga hatua kubwa. Sasa iwe upo kwenye ajira na unataka kwenda kujiajiri au tayari umeshajiajiri, masomo haya kumi tunayokwenda kujifunza hapa yatakusaidia sana kuanzisha na kukuza biashara yako.
  37. FREELANCE TO FREEDOM: The Roadmap for Creating a Side Business to Achieve Financial, Time and Life Freedom kilichoandikwa na mpiga picha aliyeweza kutoka kwenye ajira mpaka kujiajiri mwenyewe na kufikia mafanikio makubwa. Mpiga picha huyo ni Vincent Pugliese akishirikiana na mke wake Elizabeth katika safari ya kutoka kwenye utumwa wa ajira pamoja na madeni mpaka kufikia uhuru wa kifedha, muda na hata maisha kwa ujumla. Kwenye hiki, Vicent anatushirikisha safari nzima ya maisha yake ya kutoka kwenye utumwa mpaka kwenye uhuru.
  38. RANGE: Why Generalists Triumph In A Specialized World kilichoandikwa na David Epstein. Kwenye kitabu hiki, David ametuonesha jinsi ambavyo hadithi ya kubobea haraka ambayo imekuwa inatumiwa na wengi kama mfano wa mafanikio isivyo sahihi. Ametushirikisha kwa kina jinsi ambavyo kutokubobea kwenye jambo moja kuna manufaa makubwa kwa mtu, hasa kwa maisha na mafanikio ya baadaye.
  39. STREET SMARTS: An All-Purpose Tool Kit for Entrepreneurs kilichoandikwa na waandishi na wafanyabiashara wawili ambao ni Norm Brodsky na Bo Burlingham. Norm na Bo wana uzoefu wa muda mrefu katika kuanzisha na kukuza biashara, na kupitia kitabu hiki wametushirikisha uzoefu wao katika biashara, wametupa mafunzo muhimu ambayo tukiweza kuyatumia tutapiga hatua sana kwenye biashara zetu. Kitabu hiki kina sura 17 na mwisho wa kila sura kuna mambo manne muhimu ya kuondoka nayo na kwenda kuyafanyia kazi.
  40. PROFIT FIRST: A Simple System To Transform Any Business From A Cash-Eating Monster To A Money-Making Machine kilichoandikwa na Mike Michalowicz. Mike anatuambia biashara nyingi zimekuwa zinaendeshwa bila ya kutengeneza faida, kitu kinachopelekea biashara hizo zife. Hivyo anatuambia njia pekee ya kuendesha biashara yenye mafanikio, ni kwa kuanza kupata faida kwanza kabla ya mengine yote. Mike anasema, faida kwenye biashara inapaswa kuanza kupatikana siku ya kwanza unapoanza biashara, na siyo kusubiri mpaka siku zijazo.
  41. SMALL GIANTS: Companies That Choose to Be Great Instead of Big ambacho kimeandikwa na Bo Burlingham. Kitabu hiki kimeandikwa kupitia utafiti uliofanyika kwa biashara ambazo zimechagua kuwa bora badala ya kuwa kubwa. Hizi ni biashara ambazo zilikuwa na nafasi ya kukua zaidi lakini wamiliki wa biashara hizo kuchagua kuzifanya zibaki kuwa biashara ndogo ambazo ni bora zaidi. Kwenye kitabu hiki utajifunza jinsi ambavyo tunaweza kuendesha biashara yako kwa ubora hata kama ni ndogo.
  42. FINANCIAL INTELLIGENCE; A Manager’s Guide to Knowing What the Numbers Really Mean kilichoandikwa na waandishi na washauri wa biashara Karen Berman, Joe Knight na John Case. Kupitia kitabu hiki tunajifunza kwa kina kuhusu namba za biashara na taarifa za kifedha unazopaswa kuzijua na kuzielewa. Haijalishi kama umeajiriwa, unafanya biashara au umejiajiri mwenyewe, bila ya kuzijua namba za biashara kwenye kile unachofanya, huna tofauti na mtu anayetembea gizani huku amefungwa kitambaa machoni.
  43. THIS IS MARKETING: You Can’t Be Seen Until You Learn To See kilichoandokwa na Seth Godin. Seth Godin anasifika kama mmoja wa wabobezi wa masoko katika zama tunazoishi sasa. Seth amekuwa akihubiri aina ya tofauti ya masoko, ambayo haimlengi kila mtu, bali inachagua kulenga watu wachache. Kwenye kitabu hiki, tunajifunza namna bora ya kufanya masoko yenye tija kwenye biashara zetu na maisha kwa ujumla, kwa sababu kila kitu kwenye maisha yetu kinahusu masoko.
  44. TRILLION DOLLAR COACH: The Leadership Playbook of Silicon Valley's Bill Campbell, kitabu hiki kimeandikwa na Alan Eagle, Eric Schmidt, na Jonathan Rosenberg. Hawa ni wakurugenzi wa makampuni ya teknolojia ambao waliwahi kufanya kazi na Kocha Bill Campbell ambaye ana mchango mkubwa sana kwenye ukuaji wa makampuni makubwa ya teknolojia duniani ambayo ni Google, Apple, Amazon, Facebook, Intuit na mengine mengi. Kitabu hiki kimeeleza maisha ya Bill pamoja na misingi yake ya ukocha wa mafanikio.
  45. THE INTELLIGENT ENTREPRENEUR: How Three Harvard Business School Graduates Learned the 10 Rules of Successful Entrepreneurship kilichoandikwa na Bill Murphy Jr. Kitabu hiki ni tofauti kabisa na vitabu vingine vya ujasiriamali, kwani kimetushirikisha sheria kumi za kufanikiwa kwenye ujasiriamali, kupitia hadithi za wajasiriamali watatu waliofuatiliwa kwa kipindi cha miaka kumi. Wajasiriamali hao walikuwa wahitimu wa shahada ya uzamili ya biashara (MBA) kutoka shule ya biashara ya chuo kikuu cha Havard (Havard Business School).
  46. START SMALL FINISH BIG: 15 Key Lessons to Start and Run Your Own Successful Business. Kitabu hiki kinaelezea hadithi ya aliyekuwa mwanzilishi wa migahawa inayoitwa SubWay ambayo ni migahawa maarufu duniani kwa vyakula vya haraka. Mwanzilishi huyo ambaye alikuwa ni Fred DeLuca aliweza kuanzisha biashara hiyo akiwa na umri wa miaka 17 pekee, kwa mtaji mdogo wa dola elfu moja (mwaka 1965) ambao alikopeshwa na rafiki yake.
  47. IT STARTS WITH PASSION: Do What You Love and Love What You Do ambacho kimeandikwa na Keith Abraham. Kupitia kitabu hiki Keith anatufundisha kwamba, hatuwezi kufanikiwa kwenye maisha kama hatupendi kile ambacho tunakifanya. Kama ndani yetu hakuna msukumo mkubwa unaoanza na upendo, hatuwezi kuhimili mikiki mikiki na changamoto tutakazokutana nazo kwenye safari ya mafanikio. Hivyo tunapaswa kujua kile ambacho tunakipenda na kukifanya na kama hatujui tunachopenda, basi chochote ambacho tunakifanya, tukipende sana.
  48. INDISTRACTABLE: How To Control Your Attention And Choose Your Life, ambacho kimeandikwa na Nir wa Eyal. Nir ni mtaalamu teknolojia na mwanasaikolojia pia, mtu ambaye amesoma tafiti nyingi zinazohusisha jinsi saikolojia wa mwanadamu inavyoweza kutekwa na kuwa tegemezi wa teknolojia. Kwenye kitabu chake cha INDISTRACTABLE, Nir anatuonesha jinsi ambavyo tunaweza kuondokana na mitego ya kisaikolojia iliyowekwa na makampuni ya teknolojia na kuweza kunasa umakini wetu na kuleta usumbufu kwetu.
  49. STILLNESS IS THE KEY ambacho kimeandikwa na Ryan Holiday. Ryan amekuwa akiandika vitabu vyake kutoka kwenye msingi wa falsafa ya ustoa na kuiweka kwa namna ambayo tunaweza kuiishi na kunufaika nayo kwenye zama tunazoishi sasa. Kwenye kitabu cha STILLNESS IS THE KEY, Ryan ametuonesha nguvu kubwa iliyopo kwenye utulivu, ambayo tukiijua na kuweza kuitumia basi itakuwa ufunguo wa mambo mengi kwenye maisha yetu. Tangu enzi na enzi, ukiangalia kila aina ya falsafa au dini, utulivu umekuwa unasisitizwa sana. Ni kupitia utulivu ndiyo tunaweza kufikiri sawasawa, kuiona picha kubwa na kujua hatua sahihi za kuchukua.
  50. THE SUBTLE ART OF NOT GIVING A F*CK: A Counterintuitive Approach to Living a Good Life ambacho kimeandikwa na Mark Manson. Kama jina lilivyo, mwandishi anatufundisha jinsi ya kuacha kujali yale yasiyotuhusu. Anachotuambia ni kwamba, maisha yetu yanakuwa magumu kwa sababu tunahangaika na mambo yasiyotuhusu au yaliyo nje ya uwezo wetu. Pia ameeleza jinsi ambavyo ushauri wa wahamasishaji wengi unavyowafanya watu wengi kuwa watumwa na kushindwa kuwa na maisha bora.
  51. SAPIENS: A Brief History of Humankind kilichoandikwa na mwanahistoria Yuval Noah Harari. Yuval amefanya kazi kubwa ya kuchimba historia kamili ya binadamu tangu miaka 70,000 iliyopita ambapo ndipo historia ya binadamu imeanza kuhesabiwa wakati mapinduzi ya kifikra yalipotokea. Miaka 12,000 iliyopita ndipo mapinduzi ya kilimo yalipotokea na miaka 500 iliyopita, mapinduzi ya sayansi yalianza, ambayo ndiyo tunayaishi mpaka sasa. Kwenye kila mapinduzi ambayo tumepitia, Yuval ameonesha mafanikio na changamoto mbalimbali.
  52. FOOLED BY RANDOMNESS: The Hidden Role of Chance in Life and in the Markets kilichoandikwa na mwanahisabati, mwanafalsafa na mwekezaji Nassim Nicholas Taleb. Taleb ameandika kitabu hiki kwa kushirikisha uzoefu wake kwenye uwekezaji kwenye soko la hisa, ambapo wachache wanaochukuliwa wamefanikiwa sana siyo kwa sababu ya ujanja wao au juhudi zao, bali ni kwa bahati tu. Taleb anakwenda mbali zaidi na kuonesha kwamba katika kila eneo la maisha, kuna bahati ambazo watu wanakutana nazo na zinawasaidia kupiga hatua. Lakini wakishapiga hatua wanasahau bahati hizo na kuona ni juhudi zao wenyewe. Kwa sisi kujua mchango wa bahati kwenye maisha yetu, tunaweza kujiweka kwenye upande mzuri wa bahati kuwa na manufaa kwetu.
  53. ATOMIC HABITS: An Easy & Proven Way to Build Good Habits & Break Bad Ones kilichoandikwa na James Clear. Mwandishi James Clear baada ya kupitia tafiti mbalimbali za kisayansi, kisaikolojia na kijamii, ameweza kuja na mfumo bora sana wa kujenga au kuvunja tabia yoyote ile. Mfumo huo una hatua nne ambazo mtu ukiweza kuzifuata, hakuna tabia itakayokushinda. Mfumo huo unapatikana kwenye kitabu hiki cha ATOMIC HABITS.
  54. HOOKED: How to Build Habit-Forming Products, kilichoandikwa na Nir Eyal ambaye anatuonesha jinsi ambavyo makampuni makubwa yanatumia saikolojia yetu sisi binadamu kutengeneza bidhaa na huduma ambazo tunasukumwa kuzitumia muda wote.Kupitia kitabu hiki unajifunza vitu viwili kwa wakati mmoja; kutengeneza bidhaa au huduma ambayo watu watasukumwa kuitumia muda wote na kuepuka kuwa mtumwa wa bidhaa na huduma ambazo zimetengenezwa kwa lengo la kukusukuma wewe kuzitumia, hasa pale zinapokuwa hazina manufaa kwako.
Vitabu vyote hivyo 54 pamoja na chambuzi zake za kina vinapatikana kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA. Ukijiunga leo utaweza kupata mafunzo yote ya nyuma ya vitabu na chambuzi zake, karibu sana ujiunge kwa kufungua; SOMA VITABU TANZANIA

Rafiki yangu mpendwa, mwaka 2020 nitakwenda kukushirikisha vitabu bora zaidi na chambuzi zake, lengo ni wewe upate maarifa sahihi na kuweza kufanya maamuzi sahihi kwa mafanikio yako.

Hakikisha unajiunga na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua hapa; SOMA VITABU TANZANIA kisha bonyeza JOIN na tutakwenda pamoja kwa mwaka mzima, tukipata maarifa sahihi kwa mafanikio yetu.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

Doctor nakukubali na nakuombea uendelee kutusaidia viumbe wa Mungu kama sisi.Hata yesu ahakuaminiwa na bado alisalitiwa ,kuna watu hapa duniani wamekuja kwa ajili moja ya kutothamini na kujifanya wanajua sana,lakini pia dharau kwa wengne eendelea kuwapuuza.Nataka siku moja nifungue shule yangu kuanzia chekechea mpaka secondary.Naweza soma vitabu gani vya kunisaidia?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda mi mnifundishe kusoma vitabu.Maana kwa miezi takribani 6 nimesoma kitabu 2 tu ndivyo nimevimaliza vizuri.1.The richeat man in Babelone
2.Who moved my cheese?
Sasa ivi niko nasoma vitabu vya who will cry when you die,power of positive thinking,Rich Dad poor Dad.

Lakini ninyi mnawezaje kusoma vitabu zaidi ya 15 wakati hapohapo mna majukumu mengine.?maana mimi huwa naenda msitari kwa msitari.Mistari ya muhimu naisoma zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao ni wale wamama wa nyumbani wana muda mwingi wa kurelax ndio maana wana uwezo wa kusoma vitabu vingi.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom