Vitabu 3 mwaka huu vitakavyokupa mafanikio makubwa kimaisha

Peter Agostino

Senior Member
Sep 23, 2016
105
227
Ni vitabu vya ujasiriamali, biashara na maendeleo binafsi vilivyoandikwa kwa lugha ya kiswahili. Kila kimoja kina mada za kipekee, havifanani. Unaweza ukanunua kimoja, viwili au hata vyote vitatu. Vipo katika mifumo yote, vya karatasi, hardcopy na PDF, Softcopy

1. MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI. (SH. 20,000/=)

2. SIRI YA MAFANIKIO. BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA, SH. (10,000/=)

3. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA. (SH. 5,000/=)

Vinapatikana kwa njia ya e-mail kama softcopy(PDF), na bei zake katika softcopy ni sh. 10,000/= kitabu cha 1, sh. 5,000/= kitabu cha pili na sh. 3,000/= kitabu cha 3. Tuma pesa na anuani yako ya e-mail kwenye namba za simu hapo juu tutakutumia kitabu/vitabu.
 
Mwandishi wa vitabu hivi ni nani? Unaweza pia kunidokeza kidogo kuhusu mafanikio yake ya kimaisha? Hata kama siyo tajiri napenda kujua mambo aliyopitia ili kukusanya uzoefu unaompa credibility kubwa kuhusu mada hii nyeti hasa wakati huu wa kubana matumizi. Ukifanya hivyo nitanunua vitabu 1 - 2.

Mimi ni pragmatist na huwa sipendi nadharia zisizo na maana. Unakuta motivational speaker anakwambia eti "Haya ndiyo mambo 7 yatakayokufanya uwe milionea chini ya mwaka mmoja" wakati mwenyewe maisha yake hayamwendei vizuri hata kidogo. Ni afadhali nihudhurie semina ya Shigongo nikajifunze biashara ya udaku na kumbi za starehe kuliko kwa 'msomi' mwenye nadharia za vitabuni!
 
Nadhani ingekuwa vizuri zaidi kama ungehukumu credibility wakati umeshasoma kitabu, hapo ndiyo unakuwa umetenda haki, wewe umeanza kusoma kazi za Shigongo miaka mingapi? alipoanza kuandika magazeti yake miaka ya 97/98 alikuwa na credibility gani? mbona ulikuwa unayasoma na mpaka leo hii unasema ni heri uendelee kuhudhuria "semina zake za udaku", hapa mimi naona unachoangalia wewe siyo maarifa bali ni pesa, pengine wewe tayari maarifa unayo, basi waache wale waliokuwa na njaa ya maarifa wasome.

Siyo kila mtu amebarikiwa fursa ya kupata elimu kubwa kama yakwako. Watu wa aina yako huwa wanatazama kila kitu kwa mtazamo hasi, kitabu kinachotaja pesa wasiposikia kimeandikwa na Mengi, Bakhresa, Dewj, Bill Gates au matajiri wakubwa, basi kitabu hicho hakifai kabisa kusomwa. Lakini kwa bahati mbaya utakuta Matajiri wakubwa ni nadra sana kuandika vitabu hasa vinavyozungumzia namna ya kupata pesa.

Hata hivyo Mzee wa Vitendo zaidi kuliko maneno, nashukuru kwa challenge yako uliyotoa hapa, watu tunatakiwa tuhoji vitu namna hiyo hasa hasa nyakati hizi ngumu za kiuchumi, ila basi angalao jipatie kakitabu kamoja ili hata ukosoaji wako nao uonekane na watu kuwa ni wa kivitendo zaidi na wala siyo wa nadharia tu. Asante.
 
Mbona uko full of negativity mkuu? Mbona povu namna hii? Umejuaje kuwa mi nina elimu kubwa? Nikikwambia kuwa ni darasa la 7 kutakuwa na tatizo?

Samahani kama nimekukwaza kwa sababu naona umeghafilika kwelikweli. Nilichokuwa najaribu kusema ni maoni yangu tu na principle yangu binafsi: Sipendi nadharia na blah blah nyingi na huwa naegemea zaidi kwenye experience na mambo tangible. Kuliko mchumi aniambie eti uchumi umekua kwa asilimia 8 (na magraph meengi) wakati mtaani na vijijini hali iko vile vile ni afadhali aniambie uchumi umekua na tumeweza kuchimba visima 10,000 vya maji vijijini, tumenunua madawati milioni mbili .....vitu tangible. Hali kadhalika kwenye haya mambo. Kama mtu ana uzoefu kutokana na ku-hussle mwenyewe inasaidia sana kuliko mtu aliyesoma tu haya mambo kutoka vitabuni. That's what I was trying to articulate mkuu na sikuwa napinga vitabu vyako. Samahani kama umenielewa vibaya.

Pamoja na yote haya, unaweza angalau kuniambia jina la mwandishi/waandishi? Au hii nayo ni siri? Unaonaje kama ungeweka picha za maganda ya mbele na nyuma ya vitabu hivi ikiwezekana na orodha ya topics zilizomo katika kila kitabu? Ungefanya hivi tangazo lako lingekuwa limekamilika sana hata angalizo langu hapo juu nisingelitoa. Is this too much to ask?

Happy New Year...
 
Mkuu samahani wewe umefanikiwa kiasi gani kutokana na kusoma hivyo vitabu!!??
Mimi nime-imply kitu kama hicho hapo juu amenijia juu balaa. Pengine wewe atakujibu vizuri. Ingekuwa vizuri pia kama angeweka maganda ya mbele na nyuma ya vitabu hivi na orodha ya topics zilizomo katika kila kitabu badala tu ya kusema "Hivi hapa vitabu vizuri vya utajiri nunueni"
 
Jamani tatizo ni hiyo lugha ya kibiashara niliyotumia kwenye hilo tangazo? Ndiyo maana post hii sikwenda kuiweka kwingine nikaiweka hapa kwenye matangazo na hii ndiyo maana hasa ya matangazo, mbona mnauliza kana kwamba hamjawahi kuona matangazo? Hivi hebu samahani naomba na mimi kabla sijamalizia kukujibu nikuulize swali moja, eti ni kwa nini watu hununua kitabu kutokana na kutazama cover lake?.

Kazi za vitabu kama zilivyokuwa kazi nyingine zozote zile za kiutafiti au tuseme kitaaluma sidhani kama zina uhusiano wowote na maendeleo ya kiuchumi ya mtu, sisemi hivyo pengine kujitetea hapana nitakupa mifano. Wanataaluma wakubwa walioibadilisha dunia hii kama kinaAlbert Einstain usidhani eti walifanya mambo makubwa sana tofauti na taaluma zao, hata mtu kama Napoleon Hill mwandishi wa kitabu maarufu cha Think and Grow Rich, kasome kwa umakini historia yake ni mpaka miaka yake ya mwishoni kabisa ndipo alikuja kutulia kipesa. Watu kama hao mafanikio yao makubwa ni kuona taaluma wanazotafiti zikisaidia watu wengine na wala siyo wao wenyewe.

Unataka kuniambia kuwa Profesa wa majengo anayefundisha chuo kikuui basi ni lazima amiliki skyscraper au daktari anatakiwa asiumwe ili wagonjwa wamuamini kuwa yeye ni daktari kweli? Bado si kama najitetea bali nataka tu uelewe dhana nzima ya kazi za kitaaluma kwanza kabla sijakujibu swali lako. Naomba nikuulize swali jingine tena, hivi leo hii akitokea mtu akasema amegundua dawa ya ukimwi, na wewe kwa mfano ukawa unaumwa ukimwi, utamuuliza eti tuthibitishie kwanza kama wewe uliwahi kuugua ukimwi ndipo ukubali kutumia dawa yake?
 
Mkuu hilo suala la elimu hapo sikuwa namaanisha kwamba wewe una elimu kubwa hapana , nilikuwa namaana kuwa wapo wasomaji wenye kiu ya maarifa na pengine wengine elimu yao ni ya kawaida kwa hiyo anachoweza kuona mwenye elimu kubwa kuwa ni blahblah yeye anaweza kuona kuna kitu cha kujifunza. Wala sikuja juu Mkuu umenielewa vibaya tu na kuhusiana na macover nitayaweka usijali.
 
Wewe ulieleta uzi inabidi uwe na maendeleo kwa title za hivyo vitabu.
 
vitabu-vya-ujasiriamali.jpg
miferejitoleojipya2017.jpg
 
Jamani tatizo ni hiyo lugha ya kibiashara niliyotumia kwenye hilo tangazo? Ndiyo maana post hii sikwenda kuiweka kwingine nikaiweka hapa kwenye matangazo na hii ndiyo maana hasa ya matangazo, mbona mnauliza kana kwamba hamjawahi kuona matangazo? Hivi hebu samahani naomba na mimi kabla sijamalizia kukujibu nikuulize swali moja, eti ni kwa nini watu hununua kitabu kutokana na kutazama cover lake?.

Kazi za vitabu kama zilivyokuwa kazi nyingine zozote zile za kiutafiti au tuseme kitaaluma sidhani kama zina uhusiano wowote na maendeleo ya kiuchumi ya mtu, sisemi hivyo pengine kujitetea hapana nitakupa mifano. Wanataaluma wakubwa walioibadilisha dunia hii kama kinaAlbert Einstain usidhani eti walifanya mambo makubwa sana tofauti na taaluma zao, hata mtu kama Napoleon Hill mwandishi wa kitabu maarufu cha Think and Grow Rich, kasome kwa umakini historia yake ni mpaka miaka yake ya mwishoni kabisa ndipo alikuja kutulia kipesa. Watu kama hao mafanikio yao makubwa ni kuona taaluma wanazotafiti zikisaidia watu wengine na wala siyo wao wenyewe.

Unataka kuniambia kuwa Profesa wa majengo anayefundisha chuo kikuui basi ni lazima amiliki skyscraper au daktari anatakiwa asiumwe ili wagonjwa wamuamini kuwa yeye ni daktari kweli? Bado si kama najitetea bali nataka tu uelewe dhana nzima ya kazi za kitaaluma kwanza kabla sijakujibu swali lako. Naomba nikuulize swali jingine tena, hivi leo hii akitokea mtu akasema amegundua dawa ya ukimwi, na wewe kwa mfano ukawa unaumwa ukimwi, utamuuliza eti tuthibitishie kwanza kama wewe uliwahi kuugua ukimwi ndipo ukubali kutumia dawa yake?
Tangazo lako halijakamilika. Hapa ni JF na tegemea maswali. Ukipenda unayajibu au unakausha.

Ili tangazo lako likamilike linahitaji vitu vifuatavyo:

(1) Picha za cover za mbele na nyuma. Cover hizi zisomeke vizuri.

(2) Orodha kamili ya topics zote zilizomo katika kila kitabu.

(3) Historia fupi ya mwandishi au waandishi mf. elimu yao, uzoefu wao na hata mafanikio/mahusiano yao (kama yapo) katika mada zinazozungumziwa humu.

(4) Siyo lazima sana - Mwaka viliochapishwa, publisher na sehemu mbalimbali zingine vinakopatikana mbali na huko WhatsApp. Watu wengine humu wameshatapeliwa sana na wana wasiwasi na biashara za mtandaoni. Kama kuna maduka yanauza vitabu hivi katika miji mbalimbali hapa Bongo yataje.

Mtu unasoma na unajiridhisha ni kitabu gani ununue. Na watu kuomba ufafanuzi zaidi katika matangazo humu ni jambo la kawaida. Huwezi tu kuripuka "nauza gari" au "nauza nyumba" bila kuweka taarifa muhimu. Na wewe hali kadhalika. Bila taarifa hizi mtu huwezi hata kujua ni kitabu gani kati ya hivyo vinafaa zaidi. Maswali mengi yaliyoulizwa (na yatakayoulizwa) naamini kuwa yanasababishwa na ukosekanaji wa habari hizo muhimu. Na usipoziweka maswali haya yataendelea kuulizwa na utakuwa na kazi ngumu ya kukoromea kila muuliza swali. JF - the Home of GT
 
Nimekuelewa vizuri nitajitahidi kutimiza hivyo vigezo, na mimi njia ninayotumia kuuza vitabu vyangu siyo kupitia mtandaoni tu peke yake hapana, kama ulivyoona kwenye tangazo nimesema pia nawapelekea wateja vitabu walipo, hivyo siyo rahisi kumuuzia mtu kitu cha uwongo wakati mnaonana ana kwa ana.
 
Profesa wa uchumi Ibrahim Haruna Lipumba anayepiga ramli asinyanganywe uenyekiti wa chama maana bila ruzuku za chama uchumi aliosomea unayeyuka kama mshumaa.
 
me siamini kutoka kimaisha kwa kusoma vitabu vya wanaovifanyia biashara.

na sijawai kushuhudia alietoka kimaisha kwa kusoma vitabu kama hivo
 
Na vitabu kama vitabu havina uwezo wa kukutoa kimaisha, bali utatoka kimaisha kwa kuyafanyia kazi yale unayoyasoma kutoka kwenye vitabu. Pia sidhani kama dunia hii kuna mwandishi au kampuni inayotunga kitabu kwa gharama halafu lengo lake la msingi liwe ni kwenda kukigawa bure, utunzi ni biashara kama ilivyokuwa biashara nyingine yeyote ile, kuna gharama tena nyingi tu mtu anazoingia anapotunga kitabu. Ingelikuwa hivyo basi hata wanaogundua madawa ungesema nao wayagawe bure kwa wanadamu wenzao kwa kuwa tu ni kitu ambacho amekibuni kwa kutumia akili yake.
 
jamani nunueni pdf mtupe bure...wengine tupo choka mbaya
Profesa wa uchumi Ibrahim Haruna Lipumba anayepiga ramli asinyanganywe uenyekiti wa chama maana bila ruzuku za chama uchumi aliosomea unayeyuka kama mshumaa.

Kama ya akina profesa kama Lipumba huyataki na hata yanayoandikwa na watu wa kawaida kama mimi pia huyataki sasa wewe unataka Malaika ashuke ndipo umuamini?
 
Nadhani ingekuwa vizuri zaidi kama ungehukumu credibility wakati umeshasoma kitabu, hapo ndiyo unakuwa umetenda haki, wewe umeanza kusoma kazi za Shigongo miaka mingapi? alipoanza kuandika magazeti yake miaka ya 97/98 alikuwa na credibility gani? mbona ulikuwa unayasoma na mpaka leo hii unasema ni heri uendelee kuhudhuria "semina zake za udaku", hapa mimi naona unachoangalia wewe siyo maarifa bali ni pesa, pengine wewe tayari maarifa unayo, basi waache wale waliokuwa na njaa ya maarifa wasome.

Siyo kila mtu amebarikiwa fursa ya kupata elimu kubwa kama yakwako. Watu wa aina yako huwa wanatazama kila kitu kwa mtazamo hasi, kitabu kinachotaja pesa wasiposikia kimeandikwa na Mengi, Bakhresa, Dewj, Bill Gates au matajiri wakubwa, basi kitabu hicho hakifai kabisa kusomwa. Lakini kwa bahati mbaya utakuta Matajiri wakubwa ni nadra sana kuandika vitabu hasa vinavyozungumzia namna ya kupata pesa.

Hata hivyo Mzee wa Vitendo zaidi kuliko maneno, nashukuru kwa challenge yako uliyotoa hapa, watu tunatakiwa tuhoji vitu namna hiyo hasa hasa nyakati hizi ngumu za kiuchumi, ila basi angalao jipatie kakitabu kamoja ili hata ukosoaji wako nao uonekane na watu kuwa ni wa kivitendo zaidi na wala siyo wa nadharia tu. Asante.
Mkuu acha story nyingi,taja mafanikio uliyonayo kwenye maisha ili tuamini hizo mbinu za kwenye kitabu chako.
 
Na vitabu kama vitabu havina uwezo wa kukutoa kimaisha, bali utatoka kimaisha kwa kuyafanyia kazi yale unayoyasoma kutoka kwenye vitabu.

ufafanuzi kwa haya machache:

a. mkuu ina maana wewe hujayafanyia kazi uliyoyaandika?

b. na kama hujayafanyia kazi ni kwa kuwa hupendi kutoka kimaisha au ugumu wa kutekeleza nadharia ulizozitafiti?

ahsante nikipata ufafanuzi nitarudi.
 
Mkuu acha story nyingi,taja mafanikio uliyonayo kwenye maisha ili tuamini hizo mbinu za kwenye kitabu chako.

Mkuu mimi hivi vitabu siyo biography yangu, ni facts zinazotokana na utafiti nilioufanya kwa muda mrefu, hapa ningelazimika kuorodhesha mafanikio yangu kama ningelisema vitabu hivi ni historia ya maisha yangu. Vitabu nimevinadi ili kama kuna anayeona vinaweza kumsaidia basi anunue, ikiwa unaona ni blaablaa mimi siwezi kukulazimisha uvisome.

Vitabu duniani ni vingi na vingine hata vinatungwa na watu huko ng'ambo wala hatujawahi kuwaona lakini watu huvisoma wala hatuulizi wana mafanikio gani. Hebu nikuulize mtu kama Robert Kiyosaki kabla hajawa maarufu walioanza kusoma vitabu vyake kama wangeamua kuwa na attitude kama ya kwako ya kusema eti hawawezi kusoma vitabu vya waandishi wasiokuwa na majina leo hii ungemsikia wapi Kiyosaki? Tubadilike Wabongo, hata kama kitu cha mwenzako hukipendi au unaona hakikufai basi siyo vizuri kumkatisha tamaa. Hata hivyo mimi binafsi naona hizi ni changamoto za kawaida haiwezekani kila mtu kukubaliana na mawazo yako ama kile unachokifanya, kikubwa zaidi ukosoaji au rejections ziwe ni zenye nia njema ya kujenga na siyo kukatishana tamaa.

Kutaka mimi nianike mafanikio yangu hapa hamna tofauti na wale wanaotangaza kazi huku wakimtaka muomba kazi awe kwanza na uzoefu wa miaka kadhaa, kama ndiyo katoka chuoni huo uzoefu ataupata wapi?. Kila bidhaa au huduma mtengenezaji anacho kitu ama kauli yake kuu ya kuuzia hiyo bidhaa/huduma(Unic selling proposition) au USP, kile kitu kinachobeba faida au hamasa kwa mteja, kwa mfano mwandishi vitabu mkonge na mwenye jina kubwa tuchukulie mfano hapa kwetu, Shigongo, yeye USP yake huwa ni jina lake ndiyo maana hata utakuta vitabu vyake jina lake ndicho kiini cha mauzo ya vitabu vyake na huliweka mbele ya kitabu kwa maandishi makubwa kabisa, mtu anapoona tu jina SHIGONGO mara moja hununua kitabu pasipo hata kuuliza ndani kuna kitu gani. Lakini hakuanza mara moja kutumia jina kama USP indi tu alipoanza kutoa vitabu, ilimchukua muda kidogo.

Tajiri mkubwa kama Donald Trump anapotoa vitabu vyake yeye USP yake pamoja na kwamba inaweza ikawa jina lake lakini pia Mali au utajiri wake ni factor muhimu. Sasa mimi unavyoniambia nifanye USP yangu kuwa mafanikio niliyokuwa nayo si unanionea? kwanini usinunue vitabu vyangu ukanipa nguvu ili nitakapofikia hatua hiyo na mimi nikajitangaza kwa mali nilizokuwa nazo?
 
Back
Top Bottom