Vita ya zile 'hewa' imeondoka na awamu ya tano au itaendelea tena tukiingia awamu ya saba?

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Nimekumbuka namna hayati JPM alivyoanza kupambana na mishahara hewa mara tu baada ya kuapisha baraza lake la kwanza la mawaziri. Ikawa ni vita iliyochukua sehemu kubwa ya awamu yake.

Mishahara hewa, kodi hewa, malipo ya ustaafu hewa. Alikuwa akirudia sana katika hotuba yake namna nchi hii ilivyojaa wapigaji wa kila aina. Kikawa ni kibwagizo kilichozoeleka kila anaposimama na kuhutubia kundi fulani la watu akawa mwishoni akiongelea mapambano yanayoendelea wakati huo dhidi ya wafaidikaji wenyewe wa hizo hewa zote.

Mishahara ikawa inachelewa kupandishwa na sababu ya msingi ni kuwa serikali ilikuwa ikiendelea na michakato ya kuziondoa hizo hewa kwani ni nyingi na zinaharibu mfumo mzima wa mapato na matumizi. Kila siku ya Mei Mosi pakawa na uhairishwaji wa upandaji wa mishahara kwa watumishi wa kada mbalimbali.

Ametangulia mbele za haki, hatuna naye tena miongoni mwa walio hai. Sasa tunayo awamu ya sita, najiuliza kwa sasa hatuna tena hiyo michoro ya wizi kama ule wa awamu ya tano kurudi nyuma?. Rais SSH ameweza kuziba hiyo mianya ya wizi wa pesa za umma uliochelewa upandishwaji wa mishahara wa awamu ya tano?

Au labda yanayoendelea awamu hii tutakuja kuyafahamu kwa kina baada ya SSH kuondoka madarakani?. Siku zote serikali zetu zinakuwa na wapambe wanaofanya kazi ya kuichafua awamu inayokuwa imeondoka na kuisafisha inayokuwepo, pengine wanakuwa na ujira kwa kazi hiyo.

Ningependa tu kufahamu wale waliochora ile michoro ya wizi katika mawizara na taasisi mbalimbali kama wamedhibitiwa moja kwa moja, au wameshagundua njia nyingine za wizi wa mali ya umma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom