Vita ya urais kwa tiketi ya CCM ni kubwa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Taifa linayumbishwa na wanasiasa waroho ambao wameshaona njia rahisi ya kutoboa kimaisha ni kupitia siasa na si vinginevyo! Kwa kuipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma kumewafanya wanasiasa uchwara kupitia CCM wajione wana uwezo wa kupata nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi kwa maana ya urais.

Na kwa bahati mbaya sana hawafanyi hivyo kwa uzalendo wala kulipenda sana taifa bali kwa maslahi binafsi na ya watu wao wa karibu wakiwepo ndugu, jamaa na marafiki(wazuri na wabaya)

Kupitia siasa wanajaribu kulinganisha wastaafu wa siasa waliobahatika kupata nafasi za juu za uongozi maisha ya neema wanayoishi na wastaafu wa kitaaluma maisha ya dhiki wanayoishi wao na familia zao.

Kiuhalisia kanuni ya maisha inasema hakuna anayeonja asali kisha atamani kumeza shubiri

Kuipa siasa thamani na umuhimu mkubwa na kuipa kipaumbele kwenye kila jambo la kitaifa vinaliangamiza taifa na kila mtu anaota sharubu na kudhani yeye ndio yeye na wengine si mali kitu.

Taifa linapoteza dira, taifa linapoteza mwelekeo na hii si lawama ya kupewa awamu hii bali ni tangu pale hayati Mwalimu Nyerere alipokabidhi madaraka kwa Mzee Mwinyi.. Pale ndio taifa lilipoanza kuyumba na kukosa mwelekeo na dira yenye maono ya mbali kwa faida ya wote kama taifa..!

Pengine kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine ndio kilizima ndoto za maono mengi ya hayati baba wa Taifa.. Moringe alikuwa cream ya Kambarage, aliyetegemewa kwa asilimia nyingi kumpokea Mwalimu kijiti baada ya kung'atuka.. Je kifo cha chake kilikuwa ni mpango kamili wa kuzima maono hayo? Muda utakuja kusema!

Kitabu cha Mwalimu Nyerere cha HATIMA YA TANZANIA NA UONGOZI WAKE kiliangazia mengi na kubeba ufunuo mkubwa unaojidhihiri sasa... Uongozi wetu sasa umetawaliwa na siasa zisizo na chembe ya utu, uzalendo na weledi kwa manufaa ya nchi

Cream ile ya Mwalimu imepigwa ngwara na mweleka mkubwa kabisa.. Waliobaki hawana nguvu ya maamuzi tena na hata walipojaribu kukosoa hapo nyuma walikipata kile kilichompata mtema kuni huko mwituni hapo zamani.. Vijana chipukizi wa wakati huo ndio hawa leo hii waliotengeneza mifumo, matabaka na mirija inayolinyonya na kulidhoofisha taifa

Kwasasa kila mwanasiasa anaota kutengeneza mrija wake utakaomfaidisha yeye na watu wake kwa miongo mingi ijayo
Hii ni mbaya sana kwakuwa kwenye hizo harakati hutafuta wafadhili wasiolitakia mema taifa bali matamanio binafsi

Kwasasa nafasi inayotolewa macho ni kiti cha urais kupitia chama chao, wanamuona mama si kwamba hatoshi la hasha bali keshakula kipande chake! Kila mtu anapambana kivyake kuelekea 2025.. Na wengi wao ni wateule na wateuliwa na mama mwenyewe!

Tuhuma na tetesi kwamba kuna ambao wako ughaibuni kukusanya pesa kwa ajili ya mbio za urais ni hatari ni mbaya kwa taifa.. Anayekubali kukupa elfu kumi anatarajia kupata milion

Kwasasa vifurushi vinapanda kila uchao
Kamari zinazidi kutamalaki mpaka vichochoroni.. Mengine hayaandikiki

Hao waliokasimiwa madaraka ndio viongozi vinara wa kuliangamiza taifa kutokana na kuunda mitandao inayonyukana ndani kwa ndani na chini kwa chini... Ni mtafutano na mitifuano. Ni kuwindana na kuwekeana mitego.. Kila mtu anakula kivyake na kukusanya kivyake..

Tutafika 2025 tukiwa tumechoka sana! Mmoja kwa kujiamini kabisa kasema waziwazi MIMI NDIO WAZIRI MPAKA 2030!
Ukimuona tumbili mjini usimrushie mawe!
 
Niko pale nimekaaa.
Wakuu Kuna. sauti ya Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Mkoa wa Pwani Ramadhani Mlao akizungumza na Makatibu wa Vijana wa Mkoa wa Pwani.

Kuwaambia kuwa ametumwa na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa ndugu. Kenani Kihongosi awape maelekezo ya kumchagua Mohammed Kawaida

Mlao amewaambia Makatibu kuwa Kenani Kihongosi mwenyewe atawasilina nao Makatibu kuwaambia wamchague Kawaida

Ni ajabu na kweli

Mkurugenzi wa Uchaguzi anamfanyia Kampeni mgombea

Nimeshindwa kuiweka hyo sauti ya dogo Mlao.
Linguistic
 
Hili kundi lililopo madarakn ni hatar Kwa afya, JPM alijitahid kuliondoa hatimae limerudi tena, hili kundi halina huruma hata nusu na hii nchi yaan utazan wakolon au wahamiaji ni kundi la watu wenye tamaa kupita kias,
Yeah JPM alijitahidi lakini kosa lake kubwa naye ni kujaribu kuunda lingine jipya ambalo nalo sasa lilinogewa nalo limejiingiza kwenye huu mnyukano kwa gia ya kuenzi mazuri ya mwendazake lakini kiuhalisia wote ni walewale tuu
 
"Ukimuona tumbili mjini usimrushie mawe"
Mkuu tuhimizane sana kujenga familia bora na siyo bora familia
Hao ccm uliowaongelea hapa hili linalowahusu wao wanachoangalia sasa ni kuwa na familia tuu hawazingatii ubora wake ndiyo maana wanararuana hivi sasa
Mimi pia ninaamini hakuna msaada wa bure karne hii tuishi tukipambana na kujituma.
 
Sijasoma andiko lako mshana,nakuheshimu sana lakini wewe ni shabiki kindakindaki wa Chadema,kuna lipi utakaloongea kuhusu CCM ukiwa na fikra huru?
Asante nakushauri soma lote kwa makini, kisha pembua u CHADEMA wangu uweke pembeni kisha angalia uhalisia wa kile nilichoandika
Hili andiko nimegusia tangu nyuma miaka ya 1985 .. Je wakati huo CHADEMA ilikuwepo?
 
Mbilinge za urais tz ni tangu kale,1985 nyerere alichezewa kekundu keusi,alimtaka mjamaa dk salmin,wajumbe wakamuweka mwinyi...hata hivyo hujaweka kinagaubaga madai yako
Ndio maana nikasema hii michezo ilianzia huko na nikagusia hata kifo cha Sokoine aliyekuwa chaguo la kwanza la mchobga
 
Back
Top Bottom