Vita ya Uganda Crude Oil Pipeline (Tanzania vs Kenya)

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,873
Hii vita ni lazima Tanzania tushinde kwa vyovoyte vile. Kwani mara baada ya bomba hilo kujengwa nchi hizi mbili Tanzania na Uganda zitafaidika sana. Na ikumbukwe kwamba Uganda na Tanzania zimekuwa na mahusiano mazuri ya mda mrefu.

Nimejaribu kufikiria sana na kugundua huu mradi una manufaa makubwa sana ndio maana Kenya wanaupigia kelele. Hebu check hapa picha kidogo nadhani utanielewa.

UgandaPipeline.png

Mara baada ya bomba hilo kujengwa itakuwa ni rahisi kwa south Sudani kuunganisha usafirishaji wa mafuta yao kupitia bomba hilo. Na hapo hapo itakuwa rahisi kwa East Congo kuunganisha kwenye bomba hilo. Pia Ethiopia inaweza kuunganishwa na Bomba hilo.
Baadae Sudani nayo inaweza kuunganishwa na bomba hilo. South east Congo inaweza kuunganishwa na bomba hilo. Kutoka tanga kuja Dar sio mbali linaweza kuunganishwa na pia kuungani na bomba la TAZAMA. Kisha Central Africa inaweza kuunganishwa na Bomba hili.

Hii vita sio ndogo wale wa kuchungulia mbele wameshaliona. Kenya walikuwa na nafasi kubwa sana. Lakini kile kihere here cha kukaa Somalia kina wacost sana. Na ile conflict yao na Uganda na Kenya malipo yake ndio haya sasa. Ilifikia Kenya waka ng'oa reli ili kwamba tu Uganda asiweze kusafirisha mizigo yake kupitia Kenya.

Huu ni wakati wa kuonesha Tanzania tunaweza
 
Kwa hili aisee. Uzalendo ulazimishwe. Maana faida ni kubwa kuliko hasara. Na inatakiwa mjadara ufungwe kuhusu mazungumzo ya hili deal.
Uzalendo unarithishwa! Ccm ilikatisha tamaa kila mtu
Kenya wazuri kwenye lobbying but nasafi tunayo,
Pressure ipelekwe kwa M7
 
Uzalendo unarithishwa! Ccm ilikatisha tamaa kila mtu
Kenya wazuri kwenye lobbying but nasafi tunayo,
Pressure ipelekwe kwa M7
Hii inaitwa must win project. Mambo ya uvyama sio wakati wake. Vizazi vijavyo vitatucheka kwa kushindwa kusimamia maslahi ya nchi kwa kuendeza mambo ya kijinga.
 
Kwa hili aisee. Uzalendo ulazimishwe. Maana faida ni kubwa kuliko hasara. Na inatakiwa mjadara ufungwe kuhusu mazungumzo ya hili deal.

Tatizo watanzania hatuna uzalendo,zikitoka bilioni kadhaa wasomi wetu wote watakuja na zile za MAZINGIRA oh MAZINGARA basi ujue kuku kesha liwa
 
tunasubiria maafsa wa ug waje tufanye negotiations maafsa wetu kwenda ug haiwezekani raisi amezuia safari za nje..!
nchi ya ajabu sana hii nasikia kinana, mkapa na jk , wanalazimisha ccm iwe na share kwenye mradi, pia kuna watu wataukwamisha mradi kwa kutaka wapewe 10%, pia wanalazimisha, eti wale madalali feki akina jeetu ndo waiwakilishe serikali kwenye hili dili
 
Hii issue ya kusikia kwakweli mimi siikubali. Hapa ni kuwaambia serikali kuwa hii deal ni ya maana sana. Na wajue kuwa vita vya sasa ni vya kiuchumi. Inabidi kupambana kufa na kupona. Issue unazozileta za kusikia hizo ni issue za kitoto, Leta nondo zenye evidence.
 
Hii inaitwa must win project. Mambo ya uvyama sio wakati wake. Vizazi vijavyo vitatucheka kwa kushindwa kusimamia maslahi ya nchi kwa kuendeza mambo ya kijinga.
Kwenye kuiba kura ndiyo wakati wa uvyama ..................!!?
 
Annael serikali inafanya juhudi gani ili hii deal wakenya wasilichukue? Tumeona juhudi za wakenya wanavyohangaika.. Sisi tunafanya nini? muhongo yuko wapi?
 
Annael serikali inafanya juhudi gani ili hii deal wakenya wasilichukue? Tumeona juhudi za wakenya wanavyohangaika.. Sisi tunafanya nini? muhongo yuko wapi?
Kwa kweli mimi sijui. Ila mimi naonesha namna gani kunafaida katika hili bomba.
 
Back
Top Bottom