Vita ya ufisadi CCM, nani kuchukua jukumu?


Saharavoice

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
2,672
Likes
223
Points
160

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
2,672 223 160
Baada ya Samuel Sitta na Dr. Mwakyembe kupewa uwaziri, nani sasa kuongoza mapambano ya ufisadi ndani ya CCM? tutarajie nini kwenye bunge hili iwapo hawa ndiyo walikuwa wapinzani ndani ya CCM?

Nawasilisha
 

afande samwel

Senior Member
Joined
Mar 13, 2010
Messages
139
Likes
0
Points
33

afande samwel

Senior Member
Joined Mar 13, 2010
139 0 33
Baada ya Samuel Sitta na Dr. Mwakyembe kupewa uwaziri, nani sasa kuongoza mapambano ya ufisadi ndani ya CCM? tutarajie nini kwenye bunge hili iwapo hawa ndiyo walikuwa wapinzani ndani ya CCM?

Nawasilisha
.
kupigana na ufisdi sio bungeni peke yake.Kama tatizo ilikuwa sio njaa zao,basi waonyeshe kwenye wizara walizopewa
 

Mzee Dogo

JF-Expert Member
Joined
Nov 13, 2010
Messages
384
Likes
61
Points
45

Mzee Dogo

JF-Expert Member
Joined Nov 13, 2010
384 61 45
Tutarajie wapinzani wa dhati ndio pekee wawe wapiganaji labda na wachache wataokuwa wakitaka madaraka ya baada ya Dr. Fake...
 

kibenya

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2010
Messages
384
Likes
66
Points
45

kibenya

JF-Expert Member
Joined Nov 23, 2010
384 66 45
Hakuna mwingine labda kidogo mama kilango,olesendeka mnafiki kumbukeni alisema eti jk kamanda wa kupinga ufisadi wakati aliwanadi kwenye uchaguzi hii vita tubebe sisi watanzania wote pamoja na CDM
 

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
2,672
Likes
223
Points
160

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
2,672 223 160
Bunge lilopita lilitiwa chachu na wabunge wa CCM wapambanaji. nionavyo mimi hao wengine ndani ya CCM walipata nguvu ya kuongea nyuma ya SITTA na Mwakyembe. CDM pekee wataiweza kazi hiyo bila CCM kugawanyika kama ilivyokuwa bunge lililopita?
 

Keil

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2007
Messages
2,214
Likes
6
Points
135

Keil

JF-Expert Member
Joined Jul 2, 2007
2,214 6 135
Bunge lilopita lilitiwa chachu na wabunge wa CCM wapambanaji. nionavyo mimi hao wengine ndani ya CCM walipata nguvu ya kuongea nyuma ya SITTA na Mwakyembe. CDM pekee wataiweza kazi hiyo bila CCM kugawanyika kama ilivyokuwa bunge lililopita?
Mkuu,

Hao unaowaita wapiganaji unawapa sifa kubwa za bure. Hivi kwani hoja ya Buzwagi ilitiwa chachu na wabunge wa CCM? Wabunge wa CCM ndio waliopiga kura kumsimamisha Zitto kuhudhuria vikao, nini kilitokea baada ya hapo? Walipoona chati ya Zitto imepanda ghafla walijikuta wanalumbana na kulaumiana kwamba walifanya kosa kumsimamisha Zitto kuhudhuri vikao vya Bunge.

Baada ya hapo ilibidi serikali ya CCM ianze kuzunguka mikoani eti wanafafanua bajeti ya serikali, tangu lini serikali ilifanya kazi hiyo? Haikuishia hapo, walizomewa kila walikokwenda, mpaka Mohammed Seif Khatib akawa anasema kwamba kuzomewa ni sehemu ya siasa, so mawaziri wasiogope ama kuona aibu wakizomewa.

Hoja ya EPA ilipopigwa nyundo na Sitta, nini kilitokea? EPA ilibadilika na kuwa List of Shame iliyopelekwa Mwembeyanga, ambako haikuwa EPA peke yake bali na mazagazaga mengine. Ndipo msamiati wa ufisadi ulipoanza kutumika rasmi. Waliotajwa wakajibaraguza kwenda mahakamani, hakuna hata mmoja aliyekwenda zaidi ya kudanganya watanganyika.

Ndipo sasa ilipokuja hoja ya Kamati ya Mzee Shelukindo kwamba wachunguze Richmond. Baada ya EL, Karamagi na Msabaha kuachia ngazi, nini kilitokea? Hoja haikushughulikiwa mpaka mwisho, kama ingeshughulikiwa mpaka mwisho wahusika wote wangekuwa wako Segerea pamoja na Hosseah kuachia ngazi.

Mtazamo wangu ni huu, Richmond iliwatoa CCM ili waonekane kwamba nao wanapigania maslahi ya Taifa. Kama kweli wangekuwa wanapigania maslahi ya Taifa wasingeishia hapo walipoishia, walitakiwa wakamilishe kazi yote.

Bado kambi ya upinzani ikicheza vyema karata zake inaweza kuendelea kuiweka pabaya CCM na serikali yake.
 

Forum statistics

Threads 1,204,543
Members 457,361
Posts 28,162,483