Vita ya uenyekiti na ngazi nyingine kikanda zinavyominya demokrasia ndani ya CHADEMA

Oct 7, 2019
51
156
Uchaguzi wa chama cha demokrasia na maendeleo unaoendelea mpaka sasa tumeanza kushuhudi uminywaji wa demokrasia, ukabila na ukanda vimeshika kasi kubwa.

Kwa wazoefu wa uchaguzi ndani ya chama hicho wameeleza wazi kuwa ndani ya chama kumekuwa na ngazi za uongozi zimeonekana kuwa ni za baadhi ya watu na mtu mwingine akijaribu kuziwania nafasi hizo hukumbana na vita vikali.

Wameeleza zaidi kuwa ngazi kama nafasi ya mwenyekiti wa chama taifa nafsi hii imenasibishwa kuwa ni ya mtukufu Freeman Mbowe tangu akabidhiwe chama kama Mwenyekiti na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mzee Mtei 1992.

Kiti hiki kimetengenezewa mazingira ya Mhe. Mbowe kukikalia kila awamu ya muhula miaka 5 kama ilivyo sasa kumetengenezwa makundi ya kuweza kuwa fifisha wenye nia na kiti hicho.

Tumeona wanaojiita Bavicha kuchanga fedha za fomu za kumchukulia Mbowe fomu na wanazunguka nchi nzima kuwashawishi wanachama kusaini kama hatua ya kuunga mchakato wa Mh. Mbowe kuendelea na uongozi mbali na hilo pia kumetengenezwa kundi ambalo huwaa attack wanachama wanaoonyesha nia ya kukitaka kiti hicho.

Ambapo wengi hutengenezewa mizengwe kwa kuitwa wasaliti, kutengenezewa nakuwafukuza uanachama.

Licha ya nafasi ya uenyekit taifa pia zipo nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho zinzonekana ni za watu fulani na wengine hawastahili kuomba kugombea.

Mfano uenyekiti wa Kanda ya Kaskazini anagombea Godbless Lema pia Komu ameonyesha nia ya kuutaka uenyekiti na tayari ameshaanza kupewa majina ya usaliti na kuitwa alishanunuliwa na CCM hii ni mbinu tu za kumtaka na kufifisha jitihada zake.

Hivyo katka uchaguzi huu demokrasia inaonekana kuimbwa nje na kwenye majukwaa na si kuitendea katika chama.

Mbali na Komu yupo pia Mbunge wa Jimbo la Ubungo Kubenea ni miongoni mwa wanachama wanaoitwa wasaliti kwa sasa kisa wanapinga kinachoendelea ndani ya chama Mh Msigwa amewasema na kuwaonya.
 
CHADEMA wengi ni empty head, hivyo hawana mwenyekiti anaefaa zaidi ya Mbowe acha aendelee kuwaongoza kwani hawana mbadala.
 
Kama Mbowe anangangania uenyekiti basi kuna hatari na siyo vizuri kabisa kwa chama lakini kupingana kwa waliochukua fomu kwenye nafasi nyingine ni jambo zuri na hiyo ndiyo tunasema demokrasia. Demokrasia ni kusema kwa mabaya na mazuri ktk kutetea nafasi lakini siyo kuwa kuna nafasi ambayo mtu mwingine hawezi kuomba kama mwanachama na ana vigezo hitajiki kama mwingine.

Watu wafanye kampeni kwa hoja na kwa uhuru na kuacha mambo ya usaliti bali waelezee jamii nini watakifanyia chama endapo watachaguliwa kuongoza chama
 
Wameeleza zaidi kuwa ngazi kama nafasi ya mwenyekiti wa chama taifa nafsi hii imenathibishwa kuwa ni ya mtukufu Freeman Mbowe tangu akabidhiwe chama kama Mwenyekiti na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mzee Mtei 1992

****************************

Unadhani ukiandika utumbo kwa kuwa unawaelekezea wapinzania tutakuacha?

Hivi bando kakuwekea nani buana,?
 
Yaani Mbowe amekuwa Mwenyekiti tangu 1992? Hebu muwe mnaona soni na uzushi wenu. Kazi yenu ni kuokoteza vihabari na kujifanya wachambuzi. Propaganda husomewa. Bure kabisa!
 
Mbona nyote mnapambana na Mbowe kuwa mwenyekiti, Kuna kasoro gani??
Vibaraka wa Lumumba mnataka mtu wa kununua apewe wenyekiti, basi mmefeli, mlimchukua Slaa shauri ya njaa lakini Mbowe hamtaweza.
Mambo ya CDM waachieni CDM BAVICHA wameona mbali, Kamanda Mbowe tosha!!
 
Wajanjanjaa tu ndo wanaoelewa dhiki kuu na manyanyaso yatakayo kuwepo kwa wananchi baada ya wapinzani kuondolewa, Hivi kwa nn watu hawajitambui!? Upinzani unaleta changamoto na kuwaogopesha kijani!??
 
CCM ndiyo bingwa na nguli wa mauaji ya demokrasia nchini...kila mwenye wazo mbadala ni adui....ni wakala wa mabeberu...!!
 
Mwaka 2015 ilikua mwisho wa neno "UFISADI" ndani ya CHADEMA.
Naona sasa ndo mwisho wa maneno "DEMOKRASIA, UDIKTETA na UKOMO WA UONGOZI" ndani ya CHADEMA
Hahahaha chadema ni genge lililojitokeza kwa mwamvuli wa chama ilihali syo kweli Mbowe muungwana kinoma anakula pesa kwa miaka yote hii kiufundi mpk watu wanatamania asiache kula huyu Baba kabarikiwa si kidogo atakuaja kuachia uenyekiti pale tu wabunge watokanao na chama chake kupungua au kuksekana bunge maan ruzuku haitakuweko tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom