Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza; Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita ya Ubunge CCM 2015 yaanza; Pindi Chana adaiwa kumvaa Filikunjombe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 19, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=2]18 SEPTEMBER 2012[/h]Na Mwandishi Wetu, Ludewa

  VITA ya ubunge Jimbo la Ludewa, mkoani Njombe, kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao 2015, imeanza kujionesha wazi baada ya Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bw. Pindi Chana, kudaiwa kufanya jitihada za kumpigia debe mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa UWT, wilayani humo.


  Baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM jimboni humo, wanadai jitihada za Bw. Chana kumpigia debe mgombea huyo ni maandalizi ya kunyakua jimbo hilo ambalo hivi sasa lipo chini ya mbunge wake Bw. Deo Filikunjombe.

  Hata hivyo, mgombea aliyekuwa akipigiwa debe na Bw. Chana, alianguka vibaya katika uchaguzi huo na yule aliyekuwa akiungwa mkono na Bw. Filikunjombe, alipata ushindi wa kishindo.

  Chanzo chetu cha habari kimelidokeza gazeti hili kuwa, kutokana na sakata hilo, viongozi wa juu wa CCM Mkoa wa Njombe na Iringa, walilazimika kufika wilayani Ludewa ili kusimamia uchaguzi huo badaa ya kubaini ukiukwaji mkubwa wa kanuni na taratibu.

  Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa ambaye pia anashikilia Mkoa wa Njombe, Bw. Deo Sanga, alithibitisha kutokea kwa tafrani ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi huo na kudai kuwa, wao kama viongozi wa chama walisimama kidete kuhakikisha misingi na taratibu za chama zinafuatwa.

  Inaelezwa kuwa, chanzo cha mgogoro huo ni Bw. Chana kufanya kampeni ya kuhakikisha mgombea wake Bi. Anna Mlowe, anashinda nafasi hiyo Bi. Mary Mapunda, ambaye alikuwa akiungwa mkono na Bw. Filikunjombe, anaanguka.

  Hata hivyo, katika uchaguzi huo Bi. Mapunda aliibuka kidedea kwa kupata kura 274, wakati Bi. Mlowe akipata 108 na mshindi wa tatu alikuwa Bi. Selina Haule ambaye aliambulia kura 14.

  “Sisi viongozi tunajua wazi kwamba Bw. Chana ana mpango wa kutaka kugombea jimbo hili lakini bado anakabiliwa na upinzani mkali na Bw. Filikunjombe ambaye anakubalika sana.

  “Kiini cha mvutano uliojitokeza juzi katika uchaguzi huu ni baada ya Bw. Chana kutaka kupanga watu wake ili wajijengee mazingira mazuri ya ushindi kkatika Uchaguzi Mkuu ujao.

  “Kama unavyojua mwandishi viongozi wa jumuiya za chama kama UVCCM (Umoja wa Vijana wa CCM), UWT na Jumuiya ya Wazazi wakiwa upande wako ni rahisi kushinda,” kilisema chanzo hicho.

  Chanzo hicho kiliongeza kuwa, mgogoro mkubwa ulizuka baada ya jina la Bi. Mapunda, kutoonekana katika fomu ya kupigia kura huku wakati jina la Bi. Mlowe likiwepo.

  “Tulishangaa kuona jina la mgombea wetu (Mapunda) halipo lakini la (Mlowe), lipo pamoja na wagombea wengine, kutokana na utata huu, Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Njombe, iliamua kuwatuma viongozi wake akiwemo Bw. Sanga na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Njombe, Bw. Hoseah Mpagike kwenda Ludewa kuhakiki mwenendo wa uchaguzi huo.

  “Viongozi hawa walipofika walibaini kuwepo kasoro katika ujazaji fomu za muhtasari kwa wagombea hivyo waliagiza marekebisho yafanywe na majina ya wagombea kutathminiwa upya na ndipo uchaguzi ufanyike ambapo Bi. Mapunda aliibuka kidedea,” alisema.

  Akizungumzia suala hilo, mshindi wa nafasi hiyo Bi. Mapunda, alidai Bw. Chana amemdhalilisha kwa kumtolea lugha ya matusi.

  “Kwa kweli amenitukana sana na pale kulikuwa na watu wa rika zote kuanzia wakina mama, watoto na wanaume, sijajua kwanini aliamua kufanya vile wakati yeye ni kiongozi anayeheshimika.

  “Binafsi nilishiriki kumpigia kura nikiwa Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya UWT Wilaya,” alisema Mapunda.

  Kutokana na sakata hilo, gazeti hili lilimtafuta Bw. Chana, ambaye alikiri kutokea kwa vuta nikuvute katika uchaguzi huo lakini alikataa kulizungumza kwa undani na kudai linafanyiwa kazi na chama.

  “Hivi sasa nipo kikaoni lakini naweza kukupigia nitakapokuwa katika nafasi nzuri ya kulielezea kwa kina,” alidai Bw. Chana lakini hadi jana hakuweza kupiga simu kulizungumzia suala hilo.

  Kwa upande wake, Bw. Filikunjombe alikiri kuwepo kwa taflani hiyo na kudai kuwa, haukuwa mgogoro kati yake na Bw. Chana bali ulihusisha kwa kiasi kikubwa wagombea wa kiti hicho.

  “Si kwamba tulizozana ana kwa ana na Bw. Chana hapana, Kilichotokea ni kwamba mwenzangu alikuwa na mgombea anayemuunga mkono na akina mama wa Ludewa walikuwa na mgombea wao.

  “Yeye alitaka kutumia nguvu kama Mjumbe wa Kamati Kuu kupindisha sheria ili mgombea wake ashinde, lakini sisi tulisimama kidete kuhakikisha kanuni za chama zinazingatiwa kumpata mshindi halali.

  “Kwa mfano, alama alizowekewa Bi. Mlowe hakuna kikao chochote kuanzia Kamati ya Utekelezaji ya Wanawake Wilaya, Baraza la Wanawake Wilaya na Kamati ya Siasa Wilaya waliohusika kuziweka, Bw. Chana alitaka haya yote yapuuzwe na viongozi walipomweleza yeye akaleta ubabe,” alisema Bw. Filikunjombe.

  Kwa upande wake Bw. Sanga, alisema suala hilo limepatiwa ufumbuzi baada ya kurekebishwa kasoro zilizojitokeza.

  “Sisi tulikwenda kuhakikisha uchaguzi huu unafanyika kwa kufuata misingi na taratibu za chama chetu baada ya Halmashauri ya Mkoa kutuagiza twende kulishughulikia kutokana na utata uliokuwepo.

  “Hapa ninapozungumza na wewe uchaguzi umeshafanyika na mshindi halali Bi. Mapunda,” alisema Bw. Sanga.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 19, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Filikumboje... Atahama CCM kama wanamfanyia VISA...PINDI CHANA ni nani?
   
 3. M

  Mazindu Msambule JF-Expert Member

  #3
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 4,322
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu Pindi Chana ni mwanamke au mwanaume? samahani wakuu naomba mnikumbushe, mimi huwa najua ni Mmama na sio men ila article inaosha kitu tofauti na ninavyo fahamu!
   
 4. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #4
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni mama ni zao la mafisadi. Napita tu.
   
 5. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #5
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Alikuwa demu wa Wasira wakazinguanaga.Hope sasa wana date na Makamba Sr.
   
 6. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #6
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,462
  Trophy Points: 280
  ina maana ndio walewale wa vitu maalumu.!
   
 7. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #7
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Pindi chana ni mwepesi mno kwa deo filikunjombe,deo filikunjombe ni mbunge wa kuchaguliwa ana watu ludewa na nje ya ludewa kwa kazi yake anayoifanya,pindi chana ni mbunge wa kuteuliwa kitu maalum kwa watu maalum!!!!!!!!!!!!!,huyu hawezi kutupotezea muda.deo filikunjombe moto mwingine huo kayanza peter pinda anaujua vizuri!!!!!!!!!!!!!
   
 8. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #8
  Sep 19, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  watabaki vipande vipande....kuna uwezekano mkubwa chama kikamsupport Chana, Deo misimamo yake inawanyima raha ndani ya ccm na wasiyopenda mabadiliko
   
 9. Mulama

  Mulama JF-Expert Member

  #9
  Sep 19, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Kwani mgobea wa CDM hayupo katika jimbo hilo mpaka hawa wapange mikakati ya kutoana ngeu hivo?!
   
 10. t

  testa JF-Expert Member

  #10
  Sep 19, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  huyu pindi n mtoto wa mama chana mama yake nae ni kitu maalumu kwa watu maalumu toka kitambo tena inasemekana amechukua tabia ya mama yake kila mtoto na baba yake,hamuwezi deo mpambanaji
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Huyo pinda chama bora akae pembeni kabisa yani hamuwezi hata kidogo mpiganaji filikunjombe.

  Mimi naona anatafuta umaarufu tu hapo!
   
 12. C

  Concrete JF-Expert Member

  #12
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Pindi Chana anajua hata rudi tena bungeni kwa ubunge wa viti maalum kama Sophia Simba atashinda tena uenyekiti wa UWT kwa kuwa ataleta mpango wa ukomo wa viti maalum japokuwa uchaguzi uliopita alimuunga mkono Sophia Simba.

  Pindi Chana inasemekana nafasi za juu alizonazo(Ubunge, uenyekiti wa kamati ya bunge na ujumbe wa kamati kuu) ni matokeo ya kutoa huduma nzuri kwa 'wazee' ukizingatia kwamba 'mtaji' alionao unalipa kwa wanaume wengi tu.
   
 13. C

  Concrete JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mkuu uliza uambiwe maajabu!!

  Ndani ya CCM ukiwa mwanamke huu ni mtaji tosha sana wakufanikiwa.

  Mkuu nikimwaga majina wa 'Wazee' ndani ya chama wanaosadikiwa kula huo mzigo utakimbia hapa JF.
   
 14. C

  Concrete JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ahame aende wapi? Chadema?
  Shibuda anatosha sana kuwapa funzo Chadema kuacha kudandia waganga njaa kutoka CCM.

  Kama anania ya dhati ahame sasa sio kusubiri mpaka maji yamwagike.
   
 15. M

  Malila JF-Expert Member

  #15
  Sep 19, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Mwaga hayo majina mkuu, unaficha nini sasa?
   
 16. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #16
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Achaneni na chama kinachokufa!!!!
   
 17. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 19, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Hapo ndio utajua ubovu wa ccm!
  Wanapenda kuchagua watu kwa haja zao binafsi.
  Yani na asilimia ya wabunge viti maalum wa ccmweli ndio wana patikana namna hii!

   
 18. m

  makelemo JF-Expert Member

  #18
  Sep 19, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona mwandishi anasema Bwana Pindi Chana, Sijaelewa,
   
 19. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #19
  Sep 19, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  hili gazeti mhariri wake ana macho au?huyu pindi chana si mwanamke?mbona kila linapoandikwa jina lake wanaandika Bw.pindi chana?samadi ya ng'ombe waandishi wengine
   
 20. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #20
  Sep 19, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Deo kazungumza vizuri sana, Pinda hasara sana no pindi hazara chana alikuwa na mgombea wake anayempenda, na wananchi wa Ludewa nao walikuwa na mtu wao wanayemtaka so you can imagine nguvu ya kimada mmoja na peoples pawa ya wana ludewa
   
Loading...