Vita ya Tundu Lissu vs Magufuli na Vita ya Kambona vs Nyerere, ipi Kali?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831
IMG_20201119_053110.jpg

Jaribio la mapinduzi la mwaka 1964 lilihusishwa kwa sehemu kubwa na Oscar Kambona. Hapa wakituhumiwa Kambona na Lusinde kuvunja kitengo maalum cha intelijensia kilichoitwa SPECIAL BRANCH na kujaza UVCCM (wakati huo TYL) 1 ambao hawakuwa na mafunzo na ujuzi wowote hivyo kukwamisha upatikanaji wa intelijensia ya hasa kilichokuwa kinaendela jeshini.

Soma zaidi kwenye biography ya Nyerere, kitabu cha pili, Development as Rebellion
 
Udhubutu wa kambona ulikuwa mkubwa.. Aliingia uwanjani bila jeshi alitegemea maarifa yake. Kambona hakupenda kodi ya kichwa iliyokuwepo miaka ile. Pengine naye aliitamani nchi ili ajimegee kama ilivyo kwa wengi miaka hii. RIP Osca Kambona.

Tundu ni mpambanaji msomi wa sheria aliyebobea. Kuweza kugombea huku akiwa na matobo ya risasi mwili mzima ni ujasiri mkubwa.

Tundu naamini atajipanga zaidi pengine miaka kadhaa ijayo atakalia kiti.

Wapinzani wapambanie tume huru, japo sijui hata watasemea wapi. Walipopewa jukwaa walideka kama akina junia kidogo nje, kumbe walisahau kuwa WAKATI NI UKUTA. Wote tupo uraiani sasa.

Itachukua muda pia kutengeneza palipobomoka.

Ngoja tuone, naamini Mungu atatunza afya zetu.
 
"Kila nyakati na nabii wake"

Wakati wa kina Oscar it was great although in this time kwa Lissu is more great sababu zama hizi kuna uelevu plus elimu, technolojia ipo juu tofauti na nyakati zile.
 
Kambona alikuwa ndani ya chama kilekile cha Nyerere wakati Lissu ni mpinzani

Nyerere alikuwa dikteta mwenye akili na utu, pamoja na udikteta wake hakuwa radhi kuua mtu kwa sababu za kisiasa, kikubwa ambacho angekifanya ni kumuweka mtu detention au kumfungia kijijini kwake lakini siyo kuagiza wasiojulikana waue!

Si vizuri kumlinganisha Nyerere na watu wasiojielewa.

Na si vizuri kumlinganisha Lissu na Kambona, ni watu wawili tofauti.
 
Kambona Alipendwa zaidi ya Mwalimu Nyerere.
Alikiwa na sera Bora zaidi ya Mwalimu Nyerere.
Alikuwa Msomi Mzuri sana.
KAMA KAMBONA ANGEPATA URAIS TANGANYIKA INGEKUWA ULAYA.

WHILE JIWE.

Dikteta.
mshamba wa Madaraka.
Anaamini hata kuua wapinzani wake kwa Risasi.
Hawezi kabisa mijadala, Kujibu hoja kwa Hoja.

MKAPA APUMZISHWE ANAPOSTAHILI KUTULETEA ADHABU YA JIWE.
 
Kambona alikuwa ndani ya chama kilekile cha Nyerere wakati Lissu ni mpinzani

Nyerere alikuwa dikteta mwenye akili na utu, panoja na udikteta wake hakuwa radhi kuua mtu kwa sababu za kisiasa, kikubwa ambacho angekifanya ni kumuweka mtu detention au kumfungia kijijini kwake lakini siyo kuagiza wasiojulikana waue!

Si vizuri kumlinganisha Nyerere na watu wasiojielewa.

Na si vizuri kumlinganisha Lissu na Kambona, ni watu wawili tofauti.
Bora kuua kuliko kumuweka mtu detention maisha yake yote,hii ni zaidi ya mauaji ya familia nzima...R.ip Jumbe &Temeke Sanga
 
View attachment 1629620

Jaribio la mapinduzi la mwaka 1964 lilihusishwa kwa sehemu kubwa na Oscar Kambona. Hapa wakituhumiwa Kambona na Lusinde kuvunja kitengo maalum cha intelijensia kilichoitwa SPECIAL BRANCH na kujaza UVCCM (wakati huo TYL) 1 ambao hawakuwa na mafunzo na ujuzi wowote hivyo kukwamisha upatikanaji wa intelijensia ya hasa kilichokuwa kinaendela jeshini… soma zaidi kwenye biography ya Nyerere, kitabu cha pili, Development as Rebellion

Kuweka rekodi sawa,

Jaribio la mapinduzi la mwaka 1964 lilikuwa limeandaliwa na Jeshi baada ya kuona wazungu wanathaminiwa na kupewa nafasi kubwa kuliko wazawa, impact yake ni kuzaliwa kwa JWTZ

Jaribio la mapinduzi la mwaka 1969 ndio liliandaliwa na Oscar Kambona akiwa uhamishoni huku akishirikiana kwa ukaribu sana na akina Bibi Titi Mohamed, Lifa Chipaka na wengineo waliokuwepo hapa nchini! Impact ya jaribio hili ndio kulipelekea kuundwa kwa Idara ya Usalama Ikulu, baadae ikaja kuwa Idara ya Usalama wa Taifa!
 
Mbona kichwa cha uzi ni tofauti na maudhui? Hata hivyo huwezi kalinganisha matukio hayo kwa kuwa yako katika enzi tofauti "different political systems". Tukio la kwanza lilitokea ndani ya mfumo wa chama kimoja, jingine ndani ya mfumo wa vyama vingi. Haya ni mazingira tofauti kabisa.
 
View attachment 1629620

Jaribio la mapinduzi la mwaka 1964 lilihusishwa kwa sehemu kubwa na Oscar Kambona. Hapa wakituhumiwa Kambona na Lusinde kuvunja kitengo maalum cha intelijensia kilichoitwa SPECIAL BRANCH na kujaza UVCCM (wakati huo TYL) 1 ambao hawakuwa na mafunzo na ujuzi wowote hivyo kukwamisha upatikanaji wa intelijensia ya hasa kilichokuwa kinaendela jeshini… soma zaidi kwenye biography ya Nyerere, kitabu cha pili, Development as Rebellion
Wote hao ni madikteta tupu
 
Mbona kichwa cha uzi ni tofauti na maudhui? Hata hivyo huwezi kalinganisha matukio hayo kwa kuwa yako katika enzi tofauti "different political systems". Tukio la kwanza lilitokea ndani ya mfumo wa chama kimoja, jingine ndani ya mfumo wa vyama vingi. Haya ni mazingira tofauti kabisa.
Naunga mkono hoja mkuu
 
Back
Top Bottom