Vita ya Tanzania na Malawi: JK ampinga Lowasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita ya Tanzania na Malawi: JK ampinga Lowasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Aug 19, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  JK amekana kuwa Tanzania haijapeleka majeshi mpakani na Malawi kama Amiri Jeshi mtarajiwa Edward Lowasa alivyoeleza. Soma Habari hii kwa kina

  Tanzania haitapigana na Malawi, asema JK
  Tausi Mbowe

  RAIS Jakaya Kikwete amesema kuwa, Tanzania haina mpango wala nia ya kuingia katika vita na nchi jirani ya Malawi kufuatia tofauti zao kuhusu mpaka katika Ziwa Nyasa.Rais Kikwete alisema hayo jana alipokutana na Rais wa Malawi, Joyce Banda mjini Maputo Msumbiji.

  "Namhakikishia dada yangu (Joyce Banda) na watu wote Malawi kwamba, hatuna nia wala mpango wa kuingia vitani. Hatuna matayarisho ya jeshi wala jeshi alijasogea popote kwa vile hakuna sababu ya kufanya hivyo,”

  "Mimi ndiye amiri Mkuu wa Majeshi ya Tanzania na sijapanga wala kutoa maelekezo ya vita."
  Kauli hiyo inapingana na iliyowahi kutolewa hivi karibuni na Edward Lowassa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, aliyesema kuwa Tanzania iko tayari kwa vita iwapo Malawi itaendelea kushikilia msimamo wake kuwa eneo hilo ni la Malawi.

  Katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini Dodoma hivi karibuni, Lowassa alisema kuwa Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo na kwamba kamati yake imeridhishwa na maandalizi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

  Rais Kikwete, alisema kwa muda mrefu kumekuwa na utata kuhusu suala la mpaka na tayari maofisa wa pande zote mbili wameanza kulizungumzia kwa nia ya kulitatua kwa amani.

  Rais Kikwete aliwalaumu wanasiasa kwa kulikuza suala hilo na kuwataka waandishi wa habari kujiepusha na maneno yanayoleta taharuki na chokochoko baina ya nchi hizo mbili.

  "Tuviachie vyombo vyetu vya umma vifanye kazi. Hebu tuvipe nafasi na wanasiasa na waandishi wa habari wajiepushe na maneno haya yanayosababisha taharuki na chokochoko, kwani hayana maana yoyote katika kujenga uhusiano wetu,” Kikwete alisisitiza na kuongeza:

  “Naomba wanasiasa na waandishi wa habari waiache diplomasia ifanye kazi yake."

  Rais Kikwete yuko mjini Maputo, Msumbiji kuhudhuria mkutano wa viongozi wa
  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), uliofunguliwa juzi na ulitarajiwa kumalizika jana jioni.

  Kutokana na kauli hiyo, Rais Banda alisema kuwa, amefurahishwa na kufarijika kwa Rais Kikwete kumhakikishia kuwa hakuna vita.

  "Nimefarijika sana, suala hili limetusumbua sana," alisema Rais Banda na kuvishukuru vyombo vya habari vya Malawi kwa kuonyesha uzalendo na ukomavu katika suala hilo.

  MY TAKE;

  1: Ni kweli jeshi letu lilisogea mpakani au la?
  2: Je, Joyce Banda anastahili kuaminika au la?
  3: Je, nani mungo? EL kwa kutwambia Jeshi letu limejiandaa kuingia vitani na Malawi, au JK anayetutangazia kuwa hata jeshi halijasogea mpakani na hakuna mpango wa kupigana?
   
 2. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Namuamini EL kwa kauli yake yenye theme ya ulinzi...JK hayupo siriaz,bt anakula kotekote maana jana kajichekesha maputo akija bongo anasema 'membe ebu wapige ka mkwara'
   
 3. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tumieni kichwa kufikiri nyie watu hivi mnajua siasa nyie.Akili ndogo isiendeshe akili kubwa.Mnakurupuka tuu Eti jk ampinga lowasa
   
 4. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Hapo jk kaongea tu kumridhisha. lakini huyo mama ajue iko kazi kumiliki ziwa lote, na hizo diplomasia hapo hazitasaidia chochote maana kila mmoja anamsimamo wake.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,227
  Trophy Points: 280
  EL ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, he was very right 100% kutoa assurance kwa Watanzania kuwa majeshi yetu yako tayari kwa vita kuilinda mipaka yetu 24/7 kwa sababu hiyo ndiyo kazi ya jeshi letu na majeshi mengine yote!. Jeshi letu ni jeshi la Ulinzi na sio jeshi la uwamizi kama yalivyo majeshi ya mabeberu!.

  Ulinzi maana yake nini?, jee jeshi letu la ulinzi, ni jeshi la ulinzi wa kitu gani?, kama kazi ya jeshi ni ulinzi, jee ni lini linakuwa liko tayari kwa ulinzi?, hii ikimaanisha wakati mwingine wote jeshi letu linakuwa limelala usingizi, hivyo haliko tayari kiulinzi?!.

  Wasiojua wameitafsiri ile kauli ya EL kuwa ni kutangaza vita!, no!, vita hutangazwa na Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni JK, alichokisema EL kiko valid kuwa jeshi letu liko na utayari wa vita vya kuilinda mipaka yetu 24/7 kitu ambacho ni true to the very moment!.

  EL just "calls a spade a spade!", JK calls it "a big spoon!".

  Pasco.
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Daima huwa sina imani na JK kabisa. I trust EL, president to be
   
 7. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Katika hili Mh. Rais ameweka bayana kwamba Yeye ndiyo Amiri Jeshi mkuu na hana mpango wa kutupeleka vitani,Mheshimiwa Lowasa hiyo si nafsi yake nafasi yake ni kutoa ushauri kwa viongozi wa serikali ikiwemo Amiri Jeshi Mkuu.
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Hakuna kauli zilizotofautiana. Ni kweli jeshi letu liko standby, na hiyo siyo katika mpaka wa Malawi tu. Mipakani kote jeshi liko macho na tayari kwa chochote.
   
 9. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  JK amekana kuwa Tanzania haijapeleka majeshi ......? Unaruka mkojo unakanyaga mavi. Maana ya sentensi hiyo ni kwamba JK amekiri Tanzania ilipeleka majeshi yake.......Jifunze kiswahili weye
   
 10. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 180
  JK haaminiki,yu kigeugeu siku zote...na EL naye anavizia urais 2015!
  Kazi tupu!
   
 11. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kati yao mmoja lazima awe mnafiki!Au kulikuwa na sababu gani kuelezea hili kwa Joyce Banda? Nani aliyesema tutapigana vita? Kwa nini asingemweleza bayana Malawi waache kufanya kile wanachofanya sasa kwenye ziwa nyasa mpaka wafikie makubaliano?
   
 12. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  namchukia sana mzee wa masifa lowasa, hakuwa na sababu ya kuwaita waandishi wa habari na kutangaza vita, anataka tuache kuzungumza m4c tuanze kujadili vita ambayo haipo
   
 13. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #13
  Aug 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Kwa maoni yangu, JK kasema hivyo ili kupungua presha, lakini Malawi wakijifanya hawasikii watapigwa tu!!
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  Aug 19, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Hivi mnaamini kwamba Rwanda inamsaidia Colnel Makenge wa DRC na M23 yake? Pamoja na wamarekan na waingereza kupiga kelele kwamba Rwanda inawasaidia waasi na wana habari hizo lakini Gen. Kagame amekuwa akikanusha kila kukicha.

  Kwa hiyo mnategemea kwamba pamoja na chokochoko za mpaka jeshi letu limekaa tu kimya wala halijishughulishi na habari za chokochoko hizo?

  Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama alikuwa sawa na Amiri Jeshi Mkuu naye yuko sahihi. Amiri Jeshi hawezi kuutangazia ulimwengu kuwa ameagiza majeshi yajikusanye mpakani hata kama yamejikusanya huko; akisema hivyo ni sawa tu na kutangaza vita. Na siyo lazima majeshi yetu yaambiwe kwamba sasa nendeni mpakani, yenyewe yanatakiwa kutumia inteligensia yake na kujua hali ya kisiasa kati ya nchi yetu na jirani zetu ikoje na hivyo kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha mipaka yetu iko salama.
   
 15. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #15
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana nawe mkuu, JK anauma na kupuliza, kama alivyomuaibisha Pinda kuhusu posho za wabunge, sasa anataka kutwambia EL na Membe wamekurupuka kitu ambacho si kweli
   
 16. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #16
  Aug 19, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  kwa hali ilivyokuwa wakati huo na hofu ya watanzania ilivyokuwa, EL alikuwa sahihi kabisa kutamka vile, hata Membe alikuwa sahihi. JK kawaida yake kujitoa katika mambo mengi, jaribu kumfuatilia JK utagundua hili
   
Loading...