Vita ya Syria sasa yaelekea kuwa vita ya dunia kati ya Waislamu wa Suni na Shia!

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,566
Vita kati ya serikali ya Syria ya Assad na waasi wa serikali imezidi kuchukua sura mpya na kuanza kuenea duniani kama vita kati ya Waislamu wa Suni na Shia baada ya nchi za mlengo wa kiislamu kuaza kuunga mokno pande zinazopigana kama ifuatavyo;

Majeshi ya serikali ya Assad - Shia; Syria, Hezbollah (Lebanon), Iran

Majeshi ya waasi Syria - Suni; Turkey, Saudi Arabia na Qatar

Wananchi wa Kuwait wamekuwa wakiandamana kulaani Lebanon na kuonyesha kuunga mkono waasi wa Syria, kukiwa na habari kwamba Misri, Jordan na Iraq hawako mbali na kutaka kuwasaidia majeshi ya uasi.

Ikumbukwe kwama wakati Urusi inaelekea kumuunga mkono Assad, Marekani na Mataifa ya Ulaya wana lengo la kuyasaidia majeshi ya Uasi Syria

Source: Reuters
 
Hao Reuters ni waongo wakubwa,hakuna mtu anaweza akaendela kuchagua upande wa kuunga mkono kwa hali ilipofikia syria.watu wote tunataka hizo fujo ziishe hata kesho asubuhi.

Maisha yanayopotea syria ni hayana tofauti na haya tunaoishi sisi.pande zote zinazopigana ni washenzi na wapumbavu yaani hakuna akili kabisa.
 
Nawaonea huruma mno watoto wazee kina mama nawote wasiojiweza wanavyoumia na kuteseka kila uchao kwasababu tu ya kugombea madaraka lakini sasa kama hiyo vita imeingiliana na mambo ya imani suluhu iko mbalivau haipo kabisa
Halafu hao wanaopiganisha hivyo vita wala hawako mstari wa mbele vitani bali wako mbali kabisa mahali salama huku damu za wasio na hatia zikizidi kumwagika kila uchao
 
Hapo mataifa ya nje yanagombea raslimali wanawatumia tu hao wananchi wa Syria ili wathibiti Mafuta
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom