Vita ya siasa Tanzania inapopelekwa India | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita ya siasa Tanzania inapopelekwa India

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Oct 30, 2011.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Napenda kumpa pole Mh Zitto Kabwe kama mwananchi yeyote anayeumwa malaria na kichwa kikali, lakini nina tatizo moja hapa na la kimsingi.

  1.Zitto amepelekwa India kwa kuumwa malaria ugonjwa ambao unatibika kirahisi hapa hapa katika hospitali zetu nchini
  2.Zitto kwa wale waliobahatika kumuona hospitali wanasema alikua kwenye hali ya kawaida isiyotishia maisha yake na kwa hili kwenda India halikua na maana
  3.Zitto alishaumwa kama hivi mwaka 2010 na akalazwa Aga Khan, lakini hakupelekwa India kwa matibabu zaidi
  4.Amekua akitembelewa na viongozi wengi wa CCM akiwa hospitalini (sasa sijui urafiki wao ni nini haswa maana yake kama ni protocol za kibunge au kiuongozi-katibu wa bunge au naibu spika wangetosha kwenda kumuangalia na siyo wote hao walioenda huko ina maanisha walitaka kupata media coverage, au kutupotosha kwamba ugongwa ni mkubwa sana)

  Kwa wakati huu kukiwa na baadhi ya viongozi wanaotishia maslahi ya wengine ndani ya CCM wakiwa hoi India kwa magonjwa yaliyowajia ghafla yenye kila uwezekano wa kuchafuliwa kwa mfumo wa damu na sumu hili la Zitto kama kiongozi maarufu wa upinzani, kiongozi aliyejimulika wakati fulani(hii kabla umaarufu haujamzidi na kuanza kua karibu na wanaserikali ya CCM) katika kumulika maovu kwenda India kutibu malaria kukiwa na media fanfare kwangu mimi hii ni siasa tupu na ni kusudio la watu kuficha ukweli uliowakumba akina Mwakyembe na Mwandosya.

  Wanachotaka kufanya ni kuonyesha kwamba India anaenda yeyote anayeumwa chochote, na Zitto atakaporudi itaonekana wengi walienda na wanaweza kurudi kwa hiyo Mwakyembe na Mwandosya chochote kitachowajia (kama ni mauti au ulemavu fulani) ni kawaida ya maisha na siyo mchezo mchafu. Vile vile Zitto atatumika angalau kupunguza mjadala wa kipi haswa kilimfika Dr Mwakyembe baada ya hivi karibuni Mh Sitta kuliongelea hili kwenye vyombo vya habari na polisi kudokezea kuhusu suala hili.
   
 2. akilimtindi

  akilimtindi JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 423
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
Loading...