Vita ya rushwa/ufisadi na uhalisia wa maslahi ya madiwani katika halmashauri nchini

Zapa RadioFm

Senior Member
Feb 12, 2016
112
171
Itoshe tu kusema hivi..
Ufisadi na Rushwa havitaisha katika Halmashauri zetu hadi pale wawakilishi hawa wa wananchi ( madiwani) wataboreshewa maslahi yao, walau yawe nusu ya posho na mshahara wa mbunge.

Ufanisi hautakuwepo katika maeneo yatu hadi pale utaratibu wakuwawezesha madiwani hao kufanya shughuli zao zakuwaletea wananchi maendeleo.

Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na Makatibu Tawala wanakula "bata" huku kazi wanazofanya nyingi zikiwa za "kisiasa" (sisizo na tija) ukilinganisha na Wenyeviti/Mameya wa halmashauri za majijk, miji na wilaya wanaofanya kazi zenye tija za wananchi.

Mwisho:
"DC au RC hatapata heshima kwakutumia mwanya mbovu wa katiba wakumweka Kiongozi mwenzake ndani masaa 48 bila kosa lolote la msingi, badala yake hao ma-DC au ma-RC watadharaulika na kuwa chukizo mbele za wananchi"
 
Ulichooongea ni kweli kabisa.Lakini kumbuka tumeshagawanywa kwa itikadi zetu.Kwa maana kwamba hata kama upinzani inakiongozi mzuri wanachama wa CCM hawawezi kumchagua sababu tu ni mpinzani,hebu ona kwenye halmashauri zetu,hasa walizoshinda upinzani,hivi kuna sababu gani ya kuvunja halmashauri sababu tu Meya ni mpinzani?

Hivi kuna sababu gani ya kuingiza Siasa za kijinga hata kama chama fulani kimeshindwa,kwanini wasikubaliane kwamba kiongozi mzuri ni fulani huyu ndiyo awe Meya wetu?Mfano mzuri tumeuona Kinondoni tulipata Meya Mzuri sana lakini ni viongozi wangapi wa chama tawala waliappreciate uwezo wake zaidi ya matusi mitandaoni na vijembe kwenye mikutano?

Tujifunze kwa wenzetu pia
 
Back
Top Bottom