Vita ya Richmond yarejea kwa kasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita ya Richmond yarejea kwa kasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Sep 28, 2009.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  *VIKAO VYA WABUNGE VYAANZA KUJADILI UTEKELEZAJI WAKE

  Na Exuper Kachenje

  MZIMU wa Kampuni ya Richmond Development (LLC), uliowekwa kiporo katika kikao cha Bunge kilichopita, unatarajiwa kuibuka tena kabla ya kikao kijacho cha Bunge, baada ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, kujipanga kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio yake kutoka serikalini.

  Katika Mkutano wa Bunge uliomalizika mwishoni mwa mwezi Agosti, Bunge liliitaka serikali ipitie na itekeleze maazimio yote ifikapo Bunge la mwezi Novemba, ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha maafisa wake waandamizi, walioshiriki kwenye mkataba huo wa kifisadi uliosaniwa Juni 23, 2006.

  Tayari ratiba ya vikao vya Kamati za Bunge ambayo gazeti hili imefanikiwa kupata nakala yake, inaonyesha bayana kwamba, utekelezaji wa maazimio ya Richmond ni moja ya ajenda ambayo itafikishwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, ili kujadiliwa.

  Miongoni mwa maazimio ambayo Bunge iliyarudisha serikalini, ni pamoja na kutaka mamlaka ya juu ya nidhamu (Rais), ichukue hatua za kuwawajibisha maafisa waandamizi baada ya kukataa taarifa ya awali ya serikali, ambayo ilitoa onyo kwa maafisa wake waandamizi badala ya kuwawajibisha.

  Dk Edward Hoseah, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Johnson Mwanyika na Kamishna wa Nishati wa wizara hiyo, Bashir Mrindoko, ni maafisa waandamizi ambao wametajwa kupaswa kuwajibishwa na mamlaka hiyo.

  Pia Wajumbe wa Timu ya Mazungumzo ya Mikataba Serikalini (GNT) nao wanapaswa kuwajibishwa.

  Wakati Bunge likiwa mbioni kuanza mwezi Novemba, tayari ratiba ya vikao inaonyesha kwamba, mjadala kuhusu utekelezaji wa maazimio hayo unatarajiwa kurindima ndani ya kamati hiyo kwa siku mbili mfululizo.

  Kwa mujibu wa ratiba ya vikao vya kamati, taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Richmond itajadiliwa kwa siku mbili ambazo ni Oktoba 6 na 7, mwaka huu.

  "Tarehe 06-07/10/2009, Jumanne na Jumatano, kujadili taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Richmond," ilibainisha sehemu ya ratiba hiyo ya vikao vya kamati hiyo. Ratiba hiyo ya kamati, imebainisha kuwa mjadala huo, utahusisha wajumbe wa kamati hiyo, Sekretarieti, Wizara ya Nishati na Madini na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  Tayari pia Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na wananchi Septemba 9, mwaka huu kwa utaratibu wa maswali ya papo kwa papo, alikiri kwamba, bado kuna hatua zaidi zinapaswa kuchukuliwa kwa maafisa wa serikali waliohusika katika mkataba wa Richmond.

  Rais aliweka bayana kwamba, serikali imekuwa ikilifanyia kazi hilo, ili kuona hatua zaidi zinachukuliwa kwa wahusika, huku akionya hakuna undugu wala urafiki kwenye vita ya ufisadi.

  Katika Mkutano wa Bunge uliopita, sakata hilo lilichukua sura mpya baada ya Bunge kuibana serikali na kwamba ifikapo Novemba mwaka huu, ihakikishe imetekeleza maazimio yake yote.

  Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanaamini kwamba, Bunge la Novemba linatarajiwa kutoa taswira na msimamo thabiti wa mhimili huo,endapo serikali itashindwa kutekeleza maazimio hayo.

  Bunge hilo, linatarajiwa kufuatiliwa kwa karibu na Watanzania wengi pamoja na wahisani, ili kuona endapo wabunge wanaopinga ufisadi akiwemo Spika Samwel Sitta kama wataweza kuendeleza mapambano au kulegeza msimamo baada ya kubanwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Katika mkutano wa mwezi uliopita, Kamati ya Nishati na Madini chini ya Mwenyekiti wake, William Shelukindo, iliwasilisha maoni yake bungeni baada ya serikali kutoa taarifa ya utekelezaji wa maazimio hayo ambayo imewasafisha watu waliotuhumiwa na kashfa hiyo.

  Mwenyekiti huyo, aliwasilisha taarifa hiyo, iliyokataa uamuzi wa serikali uliotolewa kuhusu namna mchakato huo, ulivyowasafisha baadhi ya maafisa wake waandamizi.

  Awali, serikali ilitoa taarifa hiyo ambayo ilizua utata mkubwa baada ya kusema baadhi ya maafisa wake hawakuhusika katika sakata hilo, hivyo hawana hatia jambo lililozua mjadaka mkubwa ndani na nje ya vikao vya Bunge.

  Baada ya Shelukindo ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), kuwasilisha maoni yake, Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk Willibrod Slaa, alimgeukia Rais Kikwete na kuitaka serikali iwe imekamilisha taarifa jinsi inavyolishughulikia suala la Richmond ifikapo Novemba mwaka huu, vinginevyo ajiuzulu na kuitisha uchaguzi mpya.

  Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chadema na Naibu Kiongozi wa Upinzani bungeni, alisema Rais Kikwete amelifikisha suala hilo hapa lilipo kutokana na serikali yake kushindwa kutekeleza maazimio ya Bunge.

  "Hawa ndio waliotufikisha hapa tulipo, na wawajibishwe kwa kupuuza maazimio ya Bunge, ingekuwa nchi ya wenzetu hapa serikali ingejiuzulu na turudi kwenye uchaguzi ili wananchi wachague upya.

  "Novemba serikali itoe tamko kuhusu hili (Richmond), kwa kuwa haiwezekani Hosea (Mkurugenzi wa Takukuru) anatuhumiwa halafu anapewa onyo, sielewi serikali inataka nini?," alihoji Dk Slaa na kuomba Bunge lisiyumbe kwenye jambo hilo.

  Hata hivyo, baada ya wabunge kuzidi kuiwashia moto serikali Spika Sitta, aliingilia kati kuiokoa huku akiiitaka serikali kusitisha kutoa maamuzi hadi Mkutano wa 17 wa Bunge utakaoanza Oktoba ili ijipange vizuri na kuleta majibu sahihi.

  Spika alisimama na kumketisha chini Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ambaye alitaka kutoa ufafanuzi kuhusu hoja za wabunge na akamwambia kuwa, asitoe ufafanuzi huo, kwani anaweza kutoa majibu ambayo hayatawaridhisha wabunge na kuzua mjadala mwingine.

  Mkataba wa Richmond na Tanesco ambao ulisainiwa Juni 23,2007 umekuwa ukiitikisa nchi baada ya Ripoti ya Uchunguzi chini ya Mbunge wa Kyela Dk Harrison Mwakyembe, kusomwa bungeni mwezi Februari mwaka jana na Edward Lowassa kulazimika kujiuzulu, wadhifa wa uwaziri mkuu.
   
 2. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #2
  Sep 28, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hakuna jipya katika hili litapita bunge hili bila maamuzi ya msingi....iam sick with this country
   
 3. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 641
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ngoja tusubili tuone kitakachoendelea .kama demokarasia imekomaa Tanzania au vipi. Je na Rais wetu ataweza kujiuzuru .? Tukifika hapo basi tutegemee makubwa inchini na maisha bora yatakuwa yamekalibia maana jamaa alisha anza kujibu kisanii pale alipoongea na watanzania kwenye kipindi cha maswali na majibu .naamini lazima Richimond iondeke na mtu kama ilivyokuwa kwa mshikaji wake EL. Natamani hiyo siku ifike haraka.
   
 4. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #4
  Sep 28, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Just NATO
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kibubunswa aka Kichukuu, NATO siyo? teteteee

  No Action Talking Olny........ Mambo mswano.
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni vituko katika Kampeni kuelekea uchanguzi mkuu mwakani, Hakuna Jipya hapa wakuu
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Richmond itazikwa rasmi bunge la Nov
   
Loading...