Vita ya pili ya dunia katika picha (WW2), tupia uliyonayo

Teknologist

JF-Expert Member
Oct 20, 2018
1,082
2,000
Mkuu naona umeiva sana kuhusu vita ya pili ya dunia...Swali langu je kati ya russia na muunganiko wa british na u.s.a ni nani alikua tishio kwa Nazi.Pia ni nani kati yao alie sababisha kwa kiasi kikubwa kwa kushindwa vita kwa ujerumani?
Kwa mchakato mzima wa vita vya pili vya dunia, Hitler aliweza kuwamudu muunganiko wa UK na US, vizuri tu, ila aliharibu pale alipoanzisha vita ya "Operesheni Barbarosa" na Muungano wa Kisoviet,

Hii alisababisha kukunyongea kwa uwezo wa kuhimili na kumudu kuhudumia pande zote mbili za kivita.
Pia kutokana na Ukubwa wa nchi na jeshi la muungano wa kisoviet, hii ilimbidi apeleke huduma zaidi kwenye hii vita na kudharau muungano wa UK na US ambao walitumia mwanya huu na kuweza kufanya uvamizi kwenye fukwe za ufaransa kwenye operesheni ijilikanayo kama D-DAY.

Hitler aliwaaona wa Soviet kama watu dhaifu na sio binadamu kamili na wanatakiwa watawaliwe na kutumikia muendelezo wa ndoto za Third Reich, hapo ndipo alipoingia cha kike alivyoanza vita nao.
 

scooman

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
3,080
2,000
Hawa ni sample ya watoto wa kiyahudi waliochukuliwa na dakitari wa NAZI ajulikanaye kama joseph mengele kwa ajili ya kufanyiwa medical experiment. Huyu mdau alikuwa anafanyia binadamu moja kwa moja majaribio ya kitabibu badala ya kutumia wanyama kama panya(Guinea pigs) View attachment 1866450
Mengele aka angel of death
 

Seawhale

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
808
1,000
Claus von Stauffenberg
View attachment 1865210

Huyu ndio Lt Colonel Claus von Stauffenberg aliyeongoza jaribio la kumuua Hitler ndani ya ngome ya Hitler inayojulikana kama Wolf's Lair (Ngome ya Mbwa Mwitu)
Baada ya Lt Colonel Claus von Stauffenberg kujeruhiwa na bomu kwenye vita ta Afrika kaskazini, akaanza kuingiwa na maluweluwe ya kuamka na kujua Hitler analipoteza taifa la ujerumani.
Akapanga na kuwasuka majenerali kadhaa wa Jeshi la Ujerumani wa vikosi vya ardhi vinavyojulikana kama "Wehrmacht", walikuwa hawampendi Hitler kwa sababu ya upendeleo wake na kikosi cha SS Division(kikosi cha mauaji) kilichokuwa na jukumu la kumlinda Hitler na kilihusika na mauji ya kimbari ya wa israel chini ya shabiki asiyekuwa mwanajeshi wala uzoefu wa kijeshi ajulikanae kwa jina Heinrich Himmler.View attachment 1865209
Aina hii ya miwani inaitwaje!?.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom