Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 348
- 847
VITA YA OPIUM; KITU KIDOGO KILIVYOWEZA KUSABABISHA BALAA KWENYE TASNIA YA BIASHARA, JAMBO LINALO WAGHARIMU UCHINA MPAKA LEO.
Na. Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Sunday-21/02/2021
Himo, Kilimanjaro, Tanzania
Mwanzoni mwa karne ya 18, China iliibuka kama kituo kikubwa ulimwengu cha bidhaa muhimu duniani kama viungo, nguo za shairi, vyombo vya Nyumbani na bidhaa nyingine za kifahari zilizo pendelewa sana huko Ulaya.
Wakati huo, Uingereza na mabeberu wengine wa Ulaya walikuwa wanakusanya tani na matani ya Dhahabu kutoka Afrika na kuzifanya nchi hizi za Ulaya kuwa tajiri sana, huku wakitumia dhahabu waliyo ikusanya Afrika kununulia bidhaa za kifahari huko Uchina.
Hatimae mwisho wa Karne ya 18, China ilikuwa imeshachukua karibu nusu ya akiba zote za dhahabu ambazo nchi za Ulaya walikuwa nazo, hii ni kutokana na dhahabu nyingi zaidi ilikuwa ikihamia China kutoka Ulaya kila siku kwa sababu ya kununua bidhaa za Wachina ambazo raia wengi wa Ulaya walizitaka bidhaa kutoka Uchina kwa ajili ya anasa huko Ulaya.
Wazungu ni wajanja bwana, huwa awakubali kushindwa toka zamani, Serikali zao zilipo gundua kuwa bila kuwa na mkakati maalumu wa kuizuia China kudhibiti dhahabu ya dunia, ipo siku China itaibuka kuwa taifa kubwa lenye hifadhi kubwa ya dhahabu na kuwapiku mataifa ya Ulaya.
Hivyo Basi..............
Wazungu wakaamua kuanzisha kilimo cha Afyuni (Opium), ikumbukwe kuwa wazungu waliwasoma wachina kuwa ni watu waliopenda Sana ulevi mbalimbali, hivyo njia rahisi ya kuirejesha dhahabu yao ilikuwa ni kuwapelekea kitu ambacho kinge wavutia zaidi, hivyo wakazisha kilimo cha Afyuni (Opium) na kuanza kuipeleka China.
Hii Afyuni (Opium) ni nini?...................
Afyuni ni neno la kiswahili lenye kutokana na lugha ya Kiarabu "أفيون", huu mmea kiasili ulianza kulimwa huko Kemet (Egypt ya Sasa) miaka 4700 iliyopita, huko Kemet mmea huo ulitumika kama dawa, hii Afyuni inapatikana kutokana na utomvu uliokauka wa maua ya mmea wa 'mpopi', jina lake la kisayansi huitwa "Papaver somniferum" kwa Kiingereza ndio huitwa "Opium poppy".
Ndani ya mmea huu kuna kemikali mbalimbali ambazo ni kati ya dawa kali kabisa zenye uwezo wa kutuliza maumivu, lakini pia hutumiwa kama ulevi yani madawa ya kulevya, maana ndani yake ndio utolewa madawa ya kulevya kama heroin.
Sasa Basi..................
Waingereza ndio walioanza kulima mmea wa mpopi na kutengeneza Afyuni (Opium) kwa wingi katika makoloni yao huko India, na kisha kuipeleka China, walipoona soko lake huko China linakuwa kwa kasi wakaanza kuisambaza afyuni huko China kwa bei ndogo.
Kufatia hatua hiyo Wafanyabiashara kadhaa wa Ulaya wakaanza kupeleka bidhaa ya Afyuni (Opium) kwenye Soko la Wachina mnamo 1812 na kwa muda mfupi, Wachina walikuwa ndio soko kubwa la Afyuni (Opium) na ndio walikuwa watumiaji wakubwa duniani wa Afyuni (Opium) kuliko sehemu nyingine yoyote ile ulimwenguni.
Kitendo hiki cha nchi za Ulaya kufanya biashara ya Afyuni (Opium) kwa wingi huko Uchina, hatimae China ikawa Afyuni (Opium) na Afyuni (Opium) ikawa China, jambo hili lilipelekea nchi za Ulaya kuanza kuirudisha dhahabu iliyokuwa China kurejea Ulaya.
Hii ni kutokana na matumizi makubwa ya Afyuni (Opium) huko China, wachina waliitaji Afyuni (Opium) kwa idadi kubwa, hivyo kulazimika kutoa dhahabu yao kuinunua Afyuni (Opium) ili iwafae kwa matumizi yao, kupitia mpango huu hatimae Wazungu wakafanikisha kuirudishwa dhahabu yao Ulaya, mchezo ukaishia hapo.
Kimbembe kingine kikaibuka...............
Kufatia kuongezeka kwa matumizi ya Afyuni huko China kulipelekea raia wengi wa China kuharibika (mateja) kupitia ulevi wa Afyuni (Opium), uzalishaji wao na uchumi ulianza kupungua na uchumi wa China ukaanza kuanguka jambo ambalo halikuwahi kutabiriwa kama uchumi wa China ungeanguka kwa kiasi hicho kufatia hatua nzuri waliyo kuwa nayo mda mfupi nyuma.
China sasa ikashituka, Serikali ya China ikaona hasara ya biashara hiyo kwanza kwa sababu ya hatari kwa afya ya wananchi, pili kwa sababu ya hasara kwa uchumi kutokana na watu kupoteza muda kwa ulevi na pia gharama za kununua afyuni kutoka nje ilikuwa kubwa ambayo iliigharimu China dhahabu nyingi kuiagiza.
Kwa bahati mbaya, hatua hii ya serikali ya China kushituka juu ya madhara ya ulevi huo wa Afyuni ilikuwa tayari imechelewa sana kwa sababu watu wengi karibu 87% walikuwa tayari wameshakuwa maraibu (addicted) na ulevi wa Afyuni (Opium).
Hivyo Serikali ya China ilipotaka kulazimisha kupiga marufuku uingizwaji na matumizi ya ulevi wa afyuni, Uingereza iliizuia China kufanya hivyo, China nayo ikagomwa kuingiliwa Mambo yake ya ndani, kumbuka tayari Uingereza ilikuwa ikipata faida kubwa kwenye biashara hiyo ya Afyuni (Opium) huko China.
Hivyo basi China ilipo goma amri ya Uingereza ya kutositisha biashara ya Afyuni Uingereza iliamua kuishambulia China katika vita maarufu vya afyuni ( Opium War 1840 na tena 1858), tembelea website hii kujua namna Afyuni ilivyo kuwa janga linalo wagharimu wachina mpaka leo www.africanacup.org.
Ajabu ni kuwa vita vilipo anza raia wa China waliungana na Uingereza katika kuisaidia Uingereza kuishambulia China kwa sababu hawakuweza kuishi bila ya Afyuni (Opium), hivyo waliamini kuwa iwapo China itashinda vita hivyo Afyuni itapigwa marufuku, kwa hivyo walipambana na serikali yao Ili Waingereza washinde ili wao waweza kupata Afyuni bila kipingamizi.
Hivyo Vita ikawa kubwa, katika vita hivyo China ilishindwa vita hiyo na ikalazimisha kukubali biashara hiyo ya Afyuni (Opium).
Madhara mengine ambayo China iliyapata kwenye vita hivyo vya Opium (Anglo-Chinese war 1839-1842/Opium War) na inaiumiza mpaka leo ni eneo la Hong Kong kutawaliwa na Uingereza, hii ni baada ya Uingereza kushinda vita iliitawala Hong Kong kimabavu kwa muda wa miaka 56 mpaka June 9, 1898 Uingereza waliposaini mkataba wa kuikodisha ardhi ya Hong Kong kutoka utawala wa China wakati huo ukijulikana kama Qing Dynasty, mkataba uliojulikana kama Convention for the Extension of Hong Kong Territory ulioipa ruhusa Uingereza kuitawala Hong Kong kwa muda wa miaka 99 hadi tarehe 1 July 1997, Mkataba huo Uingereza ilisaini na China kama adhabu ya China kulipa fidia ya gharama ya vita ya Opium War.
Hivyo toka hapo matumizi ya Afyuni nchini China yaliendelea kutumika kwa kasi kubwa na hadi kufikia mwaka 1912 robo ya wanaume wote nchini China walitegemea matumizi ya afyuni katika maisha yao, tatizo hili liliendelea hadi pale biashara hiyo ilipo kuja kukomeshwa chini ya utawala wa Wakomunisti wa Mao Dzedong mwaka 1949.
Hata hivyo biashara hiyo iliendelea kufanyika kwa sili hadi baada ya vita baridi kumalizika ndipo matumizi ya ulevi wa afyuni yalipungua lakini matumizi ya madawa yanayotolewa ndani yake kama heroini yamezidi kuendelea kutumika duniani.
Mpaka Sasa China ni moja ya mataifa 5 ambayo ni soko kubwa la madawa ya kulevya duniani, Hong Kong ni moja ya eneo linalowaumiza kichwa Serikali ya Beijing, Macao ndio kitovu kikuu cha anasa na ulevi duniani, asilimia 60% ya wakazi wa Macao ni walevi wa anasa wa karibu 24% ya walevi wa anasa duniani kote. 30% ya wachina Vijana wanaupenda Uingereza na Umarekani kuliko Uchina ili kuenjoy raha ya Uhuru wa kuishi utakavyo wa dunia.
Cha kijifunza hapa,...............
1- Siku zote watu wanaotunyonya ili kudumisha maisha yao ya kifahari daima watakuwa na mkakati maalumu wa kutuweka katika hali ya unyonyaji, mkakati wao unaweza kujumuisha pia kutuangamiza kabisa, lazima tufikirie kwa kina ili kulinda masilahi yetu.
2- Sio kila ukionacho kizuri mwanzo kinabeba nia njema kwako, kuwa makini na kila kipitacho mbele yako
3- Tamaa ya mwanzo inaweza kukughalimu kwa muda mrefu Sana.
4- Mzungu anatazama faida yenye manufa kwake kiliko utu, kwao "There's no free lunch" no matter mtaathirika kiasi gani.
5- Walicho jifunza wachina baada ya mwaka 1949 ni kuwa hawawezi kuruhusu fikra ya nje kutawala fikra yao.
6- Kitu kidogo kinaweza kusababisha maafa makubwa na kutengeneza jambo kubwa baadae.
7- Watu wako wanaweza kukupiga vita hata kama unafanya kwa manufa yao.
8- Katika amani unaweza kuingiziwa furaha Ili tu kuipoteza amani.