Vita ya Ndugai ni Dodoma vs Dar es salaam

Binadamu tumeumbwa kuwa na kinyongo kwa wale ambao tunahisi hawatufanyii mazuri

Saikolojia ya Spika Ndugai imeathirika baada ya SSH kufanyia shughuli nyingi za kitaifa Dar es salaam kuliko Dodoma tofauti na mtangulizi wake

Ndugai ametumia kigezo cha mikopo kumshambulia lakini mikopo hii ilikuwepo tangu mwendazake akiwepo na hakusema,kwa nini hakusema? Ni kwa sababu mwendazake ametimiza ndoto za Dodoma kuwa makao makuu ya nchi baada ya serikali kuhamia Dodoma

Mama ameingia madarakani shughuli zikarudi Dar es salaam kitu ambacho kinamuumiza Ndugai kisaikolojia na amewahi kuhoji "Kwa nini viongozi wa serikali hawakai Dodoma?

Mama SSH kinachokuumiza siyo mikopo ni kwa nini shughuli zote za serikali hazifanyikii Dodoma kama alivyokuwa anafanya mwendazake?

Wadau hii nadharia unaiunga mkono au la!

mpumzisheni Mzee wa watu sasa!
 
Saikolojia ya Spika Ndugai imeathirika baada ya SSH kufanyia shughuli nyingi za kitaifa Dar es salaam kuliko Dodoma tofauti na mtangulizi wake - wala sidhani kama ni ukweli Mh. Magufuli alitumia muda mwingi Dodoma, kuna vikao vingi sana vilifanyika Dar, wageni wengi tu walipokelewa Chato, na muda mwingi tu raisi alikuwa Chato bila maelezo yoyote. Leo kwa nini Mama akiamua kufanyia kazi Dar ambapo ndiyo ikulu iliyokamilika kwa upande wa miundombinu iwe nongwa?
Mama akafanyie kazi zake Kibandamaiti kabisa ili Ndugai afure zaidi
 
Tatizo ni pale ambapo viongozi kushindwa kujua dhamana zao kama viongozi na kutafuta huruma ya wananchi wakati wao wanayo nafasi kubwa ya kubadilisha hali ya mambo.
Ni ujinga ujinga tu ambao hauna kichwa wala miguu.
 
Hiyo nadharia haina mashiko mkuu
. Ishu hapa ni kuwa kwanin tuliambiwa tunajenga madarasa kwa tozo zetu. Lakin inashamgaza kuona madarasa yanajengwa kwa hisani ya mikopo ya COVID-19...? Je pesa za tozo zinaenda wapi .?
 
Mji wa Dodoma una changamoto nyingi sana.Mimi binafsi sishauri Dodoma iwe mbadala wa Dar .Issue ya kuipendelea Dodoma imekaa kisiasa zaidi kuliko kiuhalisia.Dodoma tuwaachie wanasiasa na maamuzi yao ya kiduanzi.Mjanja yeyote lazima aipe kipaumbele Dar.
Ni kweli Dar ni jiji kubwa lenye hadhi ya kuwa makao makuu ya nchi, lakini kijiografia limekaa pembezoni mno mwa nchi. Imagine kutoka kagera hadi Dar, Dodoma ni Center ya mikoa mingi.

JPM aliweka mikakati mizuri ya kujenga miundo mbinu ya kisasa katikati ya mji ambayo ingechochea mji kukua kwa haraka, ilikuwa suala la muda tu. Tangu serikali ihamie Dodoma angalau Dar panapumua it was too congested, misafara kila wakati ilisababisha jam kila pahala.

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Binadamu tumeumbwa kuwa na kinyongo kwa wale ambao tunahisi hawatufanyii mazuri

Saikolojia ya Spika Ndugai imeathirika baada ya SSH kufanyia shughuli nyingi za kitaifa Dar es salaam kuliko Dodoma tofauti na mtangulizi wake

Ndugai ametumia kigezo cha mikopo kumshambulia lakini mikopo hii ilikuwepo tangu mwendazake akiwepo na hakusema,kwa nini hakusema? Ni kwa sababu mwendazake ametimiza ndoto za Dodoma kuwa makao makuu ya nchi baada ya serikali kuhamia Dodoma

Mama ameingia madarakani shughuli zikarudi Dar es salaam kitu ambacho kinamuumiza Ndugai kisaikolojia na amewahi kuhoji "Kwa nini viongozi wa serikali hawakai Dodoma?

Mama SSH kinachokuumiza siyo mikopo ni kwa nini shughuli zote za serikali hazifanyikii Dodoma kama alivyokuwa anafanya mwendazake?

Wadau hii nadharia unaiunga mkono au la!
Ndugai ametumia kigezo cha mikopo kumshambulia lakini mikopo hii ilikuwepo tangu mwendazake akiwepo na hakusema,kwa nini hakusema? Ni kwa sababu mwendazake ametimiza ndoto za Dodoma kuwa makao makuu ya nchi baada ya serikali kuhamia Dodoma
 
C&P kuna watu wanafunguka
SAMIA NA NDUGAI NI GENGE MOJA LILILOFITINIKA

1. Kauli za Job Ndugai Dhidi ya Rais Samia zinaweka wazi tunu ya Uhuru wa Bunge na Wabunge kwa niaba ya Bunge dhidi ya Serikali katika kuendesha Serikali kwa maslahi ya Umma na Taifa.

2. Lakini Makosa ya Rais Samia Suluhu kulingana na Kauli za Spika wa Bunge hayaondoi Makosa makubwa alioyafanya Ndugai kwa umma wa nchi hii kupitia mgongo wa Bunge la Chama kimoja.

3. Makosa ya Spika wa Bunge kwa miaka 5, dhidi ya Demokrasia, Utawala wa Haki (sheria zote kandamizi) ziliundwa chini yake, hayaondoi Makosa ya Rais Samia Suluhu akiwa Kama Rais wa Tanzania kwa sasa.

4. Rais Magufuli ndie Rais pekee wa Tanzania aliekopa fedha nyingi zenye riba kubwa kwa muda mfupi kuliko Rais yeyote Yule akiwemo huyu Mama. Lakini Ndugai hakuwai kukemea wakati wote huo, lkn Leo amepata wapi ujasiri huo? Unafki mtupu...

5. Hoja ya kwamba, Wanapambana na Samia wanafanya hivyo kwasababu ni mwanamke! Nao ni upotofu, na Kwamba Ndugai ni mgogo kwahiyo anadharauliwa nao ni upotofu mtupu...ni Jaribio la hatari la kuhalalisha matendo mapya ya unyama dhidi ya Binadamu kupitia mamlaka ya Urais.

6. Wanaodai kwamba, Rais anadharauliwa kwasababu ni mwanamke, wanatengeneza kichaka kipya kibaya kwa Taifa hili, kichaka ambacho Rais huyu anaweza kuitumia Kama ngao yake ya kupuuza misingi ya Utawala wa Sheria na Haki na hivyo kutengeneza mfumo Mpya wa unyama dhidi ya Binadamu kuliko wakati wowote ule, watu Hawa wanapaswa kulaaniwa...Rais anapingwa kwasababu ni Rais na sio mwanamke.

7. Ni wazi kwamba Spika Ndugai ni miongoni mwa wafuasi wa Marehemu Magufuli, ambao bado wanaamini kwamba wanaweza kurejea katika uwezo wao madaraka Kama hapo kabla. Ni wazi kwamba, Bashiru, Majaliwa na Mpango wamefungwa midomo Yao kupitia ufisadi wa BOT, na hivyo wanatumia wenzao (Wakina Ndugai na Polepole) kujaribu ku-balance power na kubakia kuwa na influence kwenye Serikali.

8. Vita ya Ndugai Dhidi ya Samia sio Vita ya Uanamke na Ugogo, sio Vita ya Jinsia Wala sio Vita ya ukabila Bali ni Vita ya madaraka na mamlaka. Waliopanga kujaribu kumzuia Mama kuwa madarakani kwenye nafasi hii bado wanapambana kuhakikisha ndoto zao zinatimia..
Alafu wanatuzugazuga sisi...upuuzi mtupu, na wafu wazikane tuu...

9. Ndugai na Samia wote ni walewale, dhambi zote za nchii zilizotendwa na Serikali hii wanawajibika kwa pamoja na hakuna msafi Kati Yao. Wote ni binadamu wakatili na walioshiriki kuhakikisha Haki nchi hii inapotea, watu wanaumizwa, na Hadi sasa ulinzi wa matendo ya uovu dhidi ya Binadamu yameendelea kulindwa na Utawala huu wa mama Kama ambayo ulilindwa kwa nguvu zote na kupaliliwa na Bunge wakati wa Magufuli. Hawa wote hawafai...

10. Dawa ya kuondokana na majanga yote haya mawili ni kupata Katiba Mpya.
 
Suala la Dodoma lafaa lipiganiwe kwa nguvu zote hilo si suala la Magufuli hata kidogo. Hata kama Ikulu ya Dar inag'aa kama mbingu, tukiipigania Dodoma itang'aa pia. Tusipende vilivyojengwa tupende kujenga pia.
 
Hili jambo ni gharama kwa Taifa.

Rais achague mahali atapofanyia shughuli zake.

Kila mara kuchoma mafuta kwa gharama ya nani??

Si sisi wananchi??
Yuko aliyepeleka shughuli nyingi kule kwake Chato na hata kuapisha wateuliwa ikawa kwake.
Japo alisisitiza Dodoma ijengwe alipiga kotokote yaani aliuma na kupuliza.
Hataree!!
 
Hili jambo ni gharama kwa Taifa.

Rais achague mahali atapofanyia shughuli zake.

Kila mara kuchoma mafuta kwa gharama ya nani??

Si sisi wananchi??
IMG-20211230-WA0063.jpg
 
Binadamu tumeumbwa kuwa na kinyongo kwa wale ambao tunahisi hawatufanyii mazuri

Saikolojia ya Spika Ndugai imeathirika baada ya SSH kufanyia shughuli nyingi za kitaifa Dar es salaam kuliko Dodoma tofauti na mtangulizi wake

Ndugai ametumia kigezo cha mikopo kumshambulia lakini mikopo hii ilikuwepo tangu mwendazake akiwepo na hakusema,kwa nini hakusema? Ni kwa sababu mwendazake ametimiza ndoto za Dodoma kuwa makao makuu ya nchi baada ya serikali kuhamia Dodoma

Mama ameingia madarakani shughuli zikarudi Dar es salaam kitu ambacho kinamuumiza Ndugai kisaikolojia na amewahi kuhoji "Kwa nini viongozi wa serikali hawakai Dodoma?

Mama SSH kinachokuumiza siyo mikopo ni kwa nini shughuli zote za serikali hazifanyikii Dodoma kama alivyokuwa anafanya mwendazake?

Wadau hii nadharia unaiunga mkono au la!
Sio kweli,ndugai ni sehemu ya majaliwa,pokepole,bashiru ambao hawakutaka achukue nchi but wamepotea

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom