Vita ya mamba waWili ilioingiliwa na kenge wasiokuwa na uelekeo.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita ya mamba waWili ilioingiliwa na kenge wasiokuwa na uelekeo..

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Greater thinker, Dec 8, 2011.

 1. Greater thinker

  Greater thinker JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 292
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ilikuwa ni kunako asubuhi tulivu kijua cha mawio kinachomoza na mto ukiwa tulivu na upepo tulivu ukipepea ghafla bin vuu mto ukaanza kuchafuka kilichofanya mto kuchafuka ni ugomvi wa mamba wawili uliokuwa mkubwa kupita kiasi huku baadhi ya watu waliokuwa nchi kavu wakishuhudia ugomvi huo pasipo kujua sababu za mamba hao kugombana ghafla mamba mmoja aliyeonekana kushindwa akaamua kutoka ndani ya mto na kuja nchi kavu.

  Akakaa kidogo nchi kavu na kushindwa kukaa nchi kavu na kuamua kurudi tena mtoni na mwishowe wakapatana na yule mamba mwenzie huku akiwa na hasira za kimoyomoyo za kutaka kulipiza kisasi na hatimaye akaamua kuwashika kenge masikio na kuwaambia kenge kuwa yule mamba mwingine ndiye anayewafanya kuwa masikini na wale kenge kutokana na njaa zao wakaamua kuingilia ugomvi wasioujua na mamba yule aliyepgwa mwanzo akaona bado haitoshi akaanza kumzushia na kuipakazia taasisi yake mambo meng ya uongo mara ooh ananibania hapigi ngoma zangu hv kutopigwa ngoma na clouds pekee ndo itakufanya upotee kwenye game?kwan kuna radio ngap?E.a,radio1,kiss fm,magic,radio uhuru,passion,rfa,times,capital,classic!!!radio zote hzo zisifanye ngoma yako kuwa hit? Kama ngoma yako kali lazima itakuwa hit tu kwan hit nyingi huamuriwa na mashabiki ndio wanaopga simu redion,kutuma msg,e mail n.k.

  Sugu na vinega wake wanashndwa kutambua kuwa style zao ni old fashion,tangu sugu anaanza ku rap mwanzoni mwa miaka ya 90 hadi leo anatumia style yake ile ile hv haoni kuwa style ile imechuja? Ebu mwangalie mwana fa wa 'ingekuwa vp' na mwangalie fa wa 'yalaiti' ni mwana fa wawili tofauti kabsa mwangalie fid q wa 'dot com' na mwangalie fid q wa 'ngosha ze swaga don' ni tofauti kabsa hapa namaansha kubadilika kwa style.Kuna siku nilimuuliza prof Jay kuwa anajua kwa nini ngoma zake mbili za mwisho yan 'msilie' na 'kama ipo' hazkufanya vzur?akanijibu kwa kunisikilizsha ngoma yake mpya ambayo inatarajia kutoka hv karibuni inayoitwa 'kamili gado' ngoma ile nilivoisikiliza nikamwambia vzuri kwa kubadilika.Na sio bongo tu hata marekani wasanii wote wasiobadilika wamepotea yuko wapi method man?twalib?red man?ja rule?black milk?na wengi tu wasiobadilika wameshapotea kwenye industry .

  Vinega hawa wanashndwa kuelewa hiki kitu kinachoitwa Edu-tainment yan education+entertinment yani unaburudika zen unaelimika mimi nikimsikiliza sugu siburudiki hata kidogo bali naelimika tu,yan me nimetoka kazini nimechoka nipo kwenye foleni kubwa tu ya kurudi nyumbani alafu nimskilize sugu au sogy dog khaa!si ndo ntazidi kuongeza stress kwa nini nismsikilize Izo business naburudika huku naelimika pia.

  Kama mziki wako ukiwa na radha+video kali lazima itakuwa hit tu,eti wanasema ruge anampendelea fa,hv yeye ruge ndiye aliyempa fa tunzo ya EA?au ruge ndo alimpeleka fa channel 0 awards?ukifanya video kali km za ay,fa au cpwaa hata clouds wasipozpga ztagongwa tu kwngne tu.Au ruge ndye anayepga video ya Ay MTV?

  Ebu nitajie ni kinega gani mwenye video kali itakayoweza kupgwa channel 0?sugu ana video gani yenye quality ya kuweza kujivunia?Je ana video hata ya Dola 5000?Jibu ni hapana.Sugu huyu anachukua chuki zake binafsi na kuzpeleka bungeni ili kumchafua tu ruge,sugu huyu anachukua maneno ya mitaani na kuyapeleka bungeni!hv huyu ni mbunge makini kweli?alisema kuwa THT wamepewa nyumba na serikali!una ushahid gan wa hili kwel we ni mbunge makini?THT Ile nyumba ni wamepanga na wanalipa kodi kama kawaida usipeleke mambo na chuki zko binafsi bungeni bhana me nilidhani ataongelea kuhusu mauzo ya albamu ndpo wasanii wanaponyonywa sana,badala ya kuiomba serikali kushughurikia tatizo hlo kwa kuwa watapata kodi kwny mauzo hayo,au kufanya harakat kwa wanao ban cd,juke box,na cd fake!!.Me nina uhakika clouds haifanyi wasanii kuwa masikini bali wao ndio wanaowasaidia na kuwainua.

  Vinega hawa ndio wanaopga show mbovu wasiokuwa na mawasiliano mazuri na Dj(speaking of experience kwa kuwa nshahudhuria show nying tu). Kama sogy bdo anapanga lakin diamond ana mjengo wake unaona tofauti hyo?sogy z old diamond z new product.

  Vinega hacheni kufuata mkumbo kwa njaa zenu na kuinglia ugomvi msioujua(Ambao mimi naujua cwezi kuuanka hapa jamvini,kwa kuwa upo kisheria zaid) ki undani na kutumiwa km chambo AMKENII yooI!!.Cha msingi cha gongeni ngoma kali,video kali na mjue kupga show lazma mtatajirika tu hata kama ngoma zenu hazipgwi clouds na mumuangalie sana sugu atawavuruga sana,na najua sugu utakuwa umeshanijua mimi ni nani kwa 7bu nilishawahi kukuambia na hatimaye pia ukaniita ni snitch yoo!..yoo!

  GT hapa yoo.!
   
 2. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  ila kweli .........
   
 3. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Mimi nipo na mzee yusuphu mie alooo hooo wapi mama khadija kopa,isha mashauzi mambo ya vidole juu babuu weee mwanamke reception babuu shep hata la kichina lipo, haloooo hooo tutabanana hapahapa mjini akiwa kwako ni wako akitoka nje ni wetu babuuuuuuuuuu
   
 4. dazipozi

  dazipozi JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 1,143
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hadithi yako ina2fundisha nini?
   
 5. Mwanagandila

  Mwanagandila Senior Member

  #5
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 182
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  **** ni **** tu hata aelimishwe vipi lazima bado ataendelea kuwa **** tu.Diamond kajenga nyumba wapi? tupe picha za hiyo nyumba aliyojenga?Usimfananishe Soggy/Adili/Mapacha na hao wabana pua zako, Wu Tang Clan, ONXY wanafanya HIP HOP lakini mbona wana maisha mazuri??Diamond ana kipi cha kujivunia zaidi ya kupanga Sinza na kutembelea Opa ya milion 8??Radio na Wisel wametoka mwaka mmoja na Diamond unajua wana kiasi gani wanachokimiliki?nimabie kwa nini Radio na Wisel wakija Bongo wanalipwa Dolla 8000- 10000 kwa show excluding accomodation/airticket na usafiri wakati huyo huyo Diamond wa hapa Bongo anatembea kwa basi lao la Fiesta mikoa yote, hotel yatshs 30000 au 50000 na kwa show analipwa laki 7 - mpaka laki 9usidandie profesa jay kanunua kile kiwanja mwaka 2002 wakati wa Machozi Jasho na Damu baada ya miaka 9-10 leo ndio anakamilisha hiyo sehemu ya kukaa, halafu bado unasema muzik unalipa?kwa nini asingekua mbali na zaid ya hapo na kuwapita Radio na Wisel achilia mbali Bob WINE, BEBE COOL & Chamelion??Bw. Misosi wakati anatoka nyimbo yake na album yake ilikataliwa na mhindi kisa alitoka Tanga na hakuwa na mtu wa kumuelekeza afanye nini ili aweze kuuza kazi yake, baadae alipopewa ramani na wadau wa mjini Ruge akampeleka kwa mdosi na album iknunuliwa n aikauza nakala nyingi tu, sasa ni kwa nini usiweze kuuza album mpaka Rugay asimame kati???Rugay yeye ni nani katika medani ya sanaa kiasi kwamba kila kitu mpaka afanye yeye?kwa taarifa yako Sugu alianza kuwaleta wasanii kutoka USA wakati Rugay bado bwana mdogo tu anasoma uzengoaliwaleta LOST BOYS wakapiga show Diamond Jubilee na nyomi ilikuwepo ya kutosha..sasa wewe unasema ooh wasaani wa zamni ni old skul kwa sasa hawana nafasi niambie msanii gani leo anaweza kuzindua album yake Diamond Jubuilee na akajaza ukumbi kama Nature, Daz Nundaz, prof Jay na Sugu???vita sio ya sugu na Rugay vita ni ya Rugay dhidi ya anaowazulumu katika sanaa, haiwezekani yeye ndio awe na uwezo wa kufanya maamuzi yote kwenye tasnia ya sanaaa...kama wasanii wa zamani hawna inshu imekuaje baada ya movemnt za anti virus wawaite Solid Ground Family, LWP, Manzese Crew na Afande Sele???wasanii hao wana nyimbo gani mpya za kuwafanya waweze kupewa nafasi ya kufanya shooo kwa sasa??hauoni kama ni unafiki tu huo?kaa kimya wewe wa juzi
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  nna tatizo la macho na ulivyoshindwa kukidhi viwango vya paragraph nimeshindwa kufuatilia hoja yako.
   
 7. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  kwa mtazamo wako kenge wanatoka upande gani? nna wasiwasi na upstairs yako kamanda!
   
 8. dazipozi

  dazipozi JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 1,143
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  pumba 2,umeandika 2 hapa
   
 9. A

  Akiri JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,453
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  sijui huyu jamaa aliyeandika anaugua ugonjwa gani, yaaani unaandika mambo mengo mpaka hueleweki
   
 10. a

  adolay JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,074
  Trophy Points: 280
  Anamatatizo ya akili.
   
 11. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,892
  Trophy Points: 280
  [h=3][​IMG]
  Soma hotuba hii tafathali.
  HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHE. JOSEPH MBILINYI, (MB) WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO, KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012
  [/h]
  SEKTA YA SANAA
  Mheshimiwa Spika, nianze na sekta ya Sanaa. Na hapa natangaza maslahi, kuwa mimi ni msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva) na nimekuwa kwenye fani hii kwa muda mrefu sasa. Kwa uzoefu wangu na kwa niaba ya Kambi rasmi ya Upinzani, nachukua fursa hii kuieleza serikali kwamba; “Sanaa si mapambo au burudani tu kama ilivyozoeleka, bali Sanaa ni ajira inayoweza kubadilisha maisha ya Mtanzania yeyote anayejihusisha nayo na inaweza kabisa kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya mapato ya Bajeti ya Serikali, ikiwa Serikali yenyewe, itadhamiria kwa dhati kufanya mapinduzi makubwa katika tasnia hii”.
  Mheshimiwa Spika, Ripoti moja nchini Marekani ya mwaka 2007 ilisema, nanukuu; “Makampuni yanayotengeneza na kuuza kazi za hatimiliki yataendelea kuwa moja ya nguvu kubwa za uchumi wa Marekani, kwani mapato yatokanayo na filamu, muziki, michezo ya video, na mifumo ya kompyuta yanachangia zaidi ya asilimia kubwa ya Pato la Taifa na kuajiri takribani watu milioni 5.4…” mwisho wa kunukuu.
  Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa sekta ya Sanaa ikifanyiwa mapinduzi makubwa inaweza kabisa kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya bajeti ya Serikali yetu na kuchangia maendeleo ya taifa hili. Ikiwa Sanaa inachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa taifa kubwa kama Marekani; Je, Tanzania tuna maendeleo gani ya kujivunia hata tupuuze Sanaa? Bado hatujaipa sekta hii umuhimu wake unaostahili;
  Matokeo yake Mheshimiwa Spika, Wasanii pamoja na Serikali bila kujua, wamekuwa wakinyonywa kimapato na Wadhamini, Wazalishaji, na Wasambazaji wa kazi za Sanaa, hususan kwenye biashara ya kuuza muziki na filamu. Kwa mujibu wa utafiti wa Dkt. Jehovaness Aikaeli ambaye ni mchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema sekta ya muziki pekee ikifanyiwa maboresho, inaweza kuiingizia Serikali mapato ya kodi ya wastani wa shilingi bilioni 50 kwa mwaka.
  Mheshimiwa Spika, tafiti chache zilizowahi kufanyika, ukiwemo utafiti wa Taasisi ya RULU/BEST – AC, wa mwaka 2007/08, zimeonyesha kuwa Wasanii na Serikali kwa pamoja, wamekuwa wakipoteza mapato mengi yatokanayo na biashara ya kazi za sanaa, hususan muziki na filamu kama ifuatavyo;
  · Maharamia wameendelea kurudufisha santuri na kanda za muziki, filamu na kazi nyingine za sanaa, na kujipatia mapato haramu kwa jasho la Wasanii, lakini hakuna hatua kali zinazochukuliwa kukomesha hali hii.
  · Wasanii wengi wamekuwa wakiingia mikataba isiyo na manufaa kwao baina yao na Wadhamini, Wazalishaji, Wasambazaji wa kazi za Sanaa na hivyo kunyonywa kimapato, kwa sababu tu ya kukosa uelewa mzuri wa masuala ya mikataba na kutokuwepo udhibiti wa kutosha wa Serikali.
  · Serikali kwa mwaka 2007 pekee, ilipoteza mapato ya muziki, ya jumla ya shilingi bilioni 71 sawa na asilimia 0.5 ya Pato la Taifa.
  · Kodi inayokusanywa na Serikali katika Sekta ya Muziki, inapatikana katika asilimia 12 tu ya kiwango cha mapato kinachotakiwa kulipiwa kodi kwenye sekta hiyo.
  · Hasara inayotokana na ulipaji mdogo wa kodi kwa taifa kwenye sekta ya muziki pekee, inakadiriwa kuwa sawa na asilimia 0.1 ya Pato la Taifa na hasara hiyo ilitegemewa kuongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2007.
  · Wakati wa utafiti iligundulika kuwa ni asilimia 12.5 tu ya Wafanyabiashara wa kazi za Sanaa, ndio waliokuwa wamelipa mirabaha, asilimia 87.5 hawakuwa wamelipa.
  Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na wizi na uharamia huu wa kazi za Sanaa na kuokoa mapato ya Wasanii na ya Serikali, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza yafuatayo;
  COSOTA iwe Mamlaka
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza kuwa Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Na.7 ya mwaka 1999 ifanyiwe marekebisho kwa lengo la kuipa meno zaidi ya kulinda haki na kuhakikisha Wasanii wananufaika na kazi zao. Jedwali zima lenye marekebisho yanayopendekezwa katika sheria hiyo, limo katika Kiambatanisho Na. 1 cha hotuba hii. Moja ya mapendekezo yaliyomo kwenye kiambatanisho hicho, yanalenga kuifanya COSOTA kuwa chombo chenye nguvu zaidi katika kulinda kazi za Wasanii kuliko ilivyo hivi sasa.
  Mheshimiwa Spika, kwa hiyo katika sehemu ya marekebisho tunayopendekeza, Kambi rasmi ya Upinzani tunataka Sura Na. 218 ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki, ifanyiwe marekebisho ili kuunda Mamlaka ya Hakimiliki Tanzania (COPYRIGHT REGULATORY AUTHORITY OF TANZANIA (CORATA) badala ya kuiacha COSOTA kama ilivyo hivi sasa. Mamlaka haya yakishaundwa yatakuwa na nguvu zaidi ya kushughulikia mambo mbalimbali ya kazi za wasanii,yawe ndio msimamizi na mratibu wa masuala ya Hakimiliki kwa kushirikiana na vyama vya msingi vya wasanii vilivyopo chini ya BASATA,kama vile Chama Cha Muziki Wa Dansi Tanzania(CHAMUDATA) na kile cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya yaani Tanzania Urban Music Association (T.U.M.A), tofauti na sasa ambapo COSOTA imebakiwa na kazi ya kusajili kazi za wasanii na kukosa nguvu ya kuzilinda.
  Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa mwenye Hakimiliki ana jukumu la kulinda haki zake kwa kwenda mahakamani pale anapoona haki yake imepokwa na mtu au kikundi chochote, bado ipo haja ya kuhakikisha kuwa Polisi wetu wa upelelezi wanahusika moja kwa moja katika kulinda haki za Wasanii.
  Mathalan, nchini Marekani hawana polisi wa kulinda hakimiliki moja kwa moja, lakini Shirika lao la Upelelezi (FBI), limekuwa likifanya uchunguzi wa mara kwa mara kuhusu hakimiliki za wasanii, kila kunaporipotiwa suala la wizi wa kazi za msanii, na limekuwa linahusika moja kwa moja katika kutoa ushahidi na kusaidia kupatikana kwa haki ya msanii husika.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza kuwa taasisi za Serikali: Polisi na Forodha washirikiane kwa karibu na Mamlaka ya Hakimiliki na Hakishiriki tunayotaka ianzishwe (CORATA), kukomesha uharamia wa kazi za Sanaa. Jeshi la Polisi liunde kitengo cha kukabiliana na wasiotekeleza sheria ya hakimiliki. Forodha watengeneze utaratibu wa kutoza kodi kikamilifu kwenye kazi za muziki, filamu na Sanaa nyingine zote zinazouzwa nje ya nchi. Na mashirika ya uzalishaji wa kazi za muziki –waunde ushirikiano na taratibu zao za kukabiliana na uharamia wa kazi za sanaa kwa mapana yake.
  Mheshimiwa Spika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Februari mwaka huu, wakati akizindua kampeni ya kuzuia malaria ambayo iliwashirikisha baadhi ya wasanii, aliahidi kuundwa kikosi kazi (task force) kitakachowashirikisha COSOTA, Polisi, Tume ya ushindani, TRA, BRELA, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na wasanii mbalimbali wanaojihusisha na sanaa ili kutafuta ufumbuzi dhidi ya uharamia na wizi wa kazi za Sanaa.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inaitaka wizara kuliarifu Bunge hili, je kikosi kazi hicho kiko wapi mpaka leo? Na kama kiliundwa, kiliundwa kwa taratibu zipi, na kwanini suala hilo haliko wazi?
  Mradi wa Stickers kwenye kazi za Sanaa
  Mheshimiwa Spika, mbali na marekebisho hayo ya kisheria na kimfumo tuliyopendekeza, Kambi rasmi ya Upinzani pia tunaitaka Serikali ndani ya mwaka wa fedha wa 2011/2012, itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kuanzisha utaratibu rasmi wa kuwa na Stickers kwa ajili ya kazi zote za Sanaa, hususan kwenye kanda na Santuri za muziki, filamu, na kazi zote za Sanaa zinazoshikika na kuuzika. Hapa tunashauri kuwa mamlaka tunayotaka ianzishwe, yaani COPYRIGHT REGULATORY AUTHORITY OF TANZANIA) ishirikiane kwa karibu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kuandaa utaratibu mzima wa kuwa na Stickers hizo na jinsi ya kuusimamia.Na sio kuwaachia tena watu binafsi kusimamia hili.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inaamini kuwa utaratibu rasmi wa kuwa na Stickers ukitumika sekta ya Biashara ya Kazi za Sanaa inaweza kupata mafanikio ya kuridhisha ndani ya muda mfupi. Mfano mzuri ni Sticker yenye nembo ya TRA inayowekwa kwenye bidhaa za Konyagi. Faida kubwa ambayo itapatikana kwa kuwa na Stickers za TRA kwenye kazi za Sanaa ni kuwa stickers hizi zitawezesha kubaini kazi halisi (Original) iliyofanywa na msanii mhusika dhidi ya kazi za bandia zilizorudufishwa au kughushiwa.
  Sambamba na hilo ni kwamba mapato ya Wanamuziki, Watunzi wa filamu na washirika wao pamoja na Serikali yataongezeka na hivyo mchango halisi ya sekta hii kwenye uchumi wa nchi utakuwa wazi.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inatambua kuwa baadhi ya makampuni ya usambazaji na utangazaji wa kazi za Sanaa, yamekuwa yakijiwekea yenyewe Stickers kwenye kazi zao za Sanaa, lakini bado Stickers hizo hazijaweza kuwasaidia vya kutosha katika kulinda kazi hizo, kwani bado umma hauna taarifa za kutosha, na mbaya zaidi Stickers zenyewe zimekuwa zikighushiwa hivyo kutotoa msaada unaotakiwa.
  Kwa kutilia maanan hilo, Kambi rasmi ya Upinzani inasisitiza kuwa ni muhimu sana utaratibu wa kuwa na Stickers rasmi za kiserikali kwa kazi zote za Sanaa, ukaanzishwa mara moja ndani ya mwaka wa fedha 2011/2012, ili kuokoa mapato ya Wasanii na mapato ya kodi ya Serikali yanayopotea kwenye sekta hii ya sanaa.
  Mheshimiwa Spika, pia tuna taarifa kuwa Wasanii wengi kutoka nje ya nchi wanaofanya maonyesho mbalimbali hapa nchini wamekuwa hawatozwi kodi licha ya kulipwa fedha nyingi. Kwa hiyo, tunaitaka Serikali kuanzia mwaka wa fedha wa 2011/2012, ihakikishe kuwa Wasanii hao wa nje ya nchi ambao wamekuwa wakilipwa dola laki 1hadi dola laki 4 kwa onyesho moja hapa nchini, wawe wanatozwa kodi ya kutosha, ili fedha hizo ziongezee bajeti kuu ya Serikali na kuwasaidia Watanzania wengi maskini.
  Mheshimiwa Spika, tunaitaka Serikali kwa kushirikiana na vyombo husika, iweke utaratibu wa kuhakikisha kuwa pale Msanii wa ndani anapofanya onyesho au kazi ya pamoja na Msanii kutoka nje, basi kuwe na mgawanyo mzuri na wa haki wa mapato kati ya Msanii huyo wa Nje na Msanii Mzawa. Pendekezo hili linazingatia ukweli kuwa kwenye maonyesho ya muziki yanayofanywa kwa kuwashirikisha kwa pamoja Wasanii wa Nje na wale wa Ndani, wa Nje wamekuwa wakilipwa fedha nyingi sana kuliko wale wa ndani, licha ya kuwa kazi iliyofanywa ni moja na wote wameingiza mapato.
  Mheshimiwa Spika, ili kuboresha Sekta nzima ya Sanaa nchini, na kuhakikisha inaongeza ajira zenye tija, na kutoa mchango mkubwa katika ukuaji uchumi, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe;
  · Serikali ndani ya mwaka wa fedha wa 2011/2012,pamoja na kufanyia kazi tafiti zilizokwishafanywa na wadau mbalimbali wa sanaa, ifanye utafiti mahsusi na wa kina kuhusu Sekta nzima ya Sanaa (Feasibility Study), ili kubaini fursa na vikwazo vyote vilivyopo, na kuainisha njia na mikakati kabambe ya kuboresha na kuisimamia sekta husika, kwa manufaa ya Wasanii na uchumi wa nchi.
  · Kupitia matokeo ya utafiti huo, Wizara ndani ya mwaka wa fedha 2011/2012, iandae Mpango mahsusi wa Maboresho ya Sekta ya Sanaa, ambao pamoja na mambo mengine, ulenge kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato ya Sanaa na kuchochea ajira nyingi na zenye tija kwa vijana.
  · Chuo Kikuu cha Sanaa cha Bagamoyo kipandishwe hadhi na kuwa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Kawawa cha Bagamoyo (Kawawa Memorial University – Bagamoyo). Lengo liwe ni kuhakikisha kuwa chuo hiki kinatoa mafunzo yote ya hali ya juu ya mambo ya sanaa, michezo na utamaduni kwa vijana wa Kitanzania na wale wanaotoka ng’ambo, huku tukimuenzi Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa, kwa mchango wake mkubwa katika taifa hili alioutoa kwenye uongozi na Sanaa.
  · Serikali ihakikishe kuwa asilimia 90 ya bajeti zote za Wizara, Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali zinazotengwa kwa ajili ya kunaksisha ofisi, iwe inatumia kazi za sanaa na samani zinazopatikana hapa Tanzania au zinazotokana na ubunifu wa Watanzania. Hii itachochea ajira katika kazi za Sanaa na kuweka ushindani wa kibiashara ambao utainua ubora wa kazi hizo.
  · Masomo ya Sanaa yarudishwe katika ngazi zote za elimu katika shule za binafsi na serikali, ili kuchochea ubunifu na umahiri wa vijana katika kazi za sanaa na kuinua vipaji vyao mbalimbali.
  · Serikali ihakikishe mafunzo ya Sanaa yanatolewa kwa vyuo vya elimu ili kuweza kupata walimu wa kutosha wa sekta hii.
  · Mashindano ya ubunifu wa kazi za Sanaa yaanzishwe yakiwa ni sehemu ya mashindano ya michezo ya UMISHUMTA na UMISETA.
  Kashfa ya Nyumba ya Sanaa
  Mheshimiwa Spika, Nyumba ya Sanaa ilianzishwa mnamo 1972 kwa madhumuni ya kutoa mafunzo ya Sanaa kwa vijana, wanawake na wasiojiweza pamoja na kutafuta masoko ya Sanaa na kazi za mikono. Hata hivyo, kuanzia mwaka 1995 kumekuwepo hali ya kutoelewana baina ya wajumbe wa Bodi ya wadhamini baada ya kutiliana shaka wenyewe kwa wenyewe, pia kati ya Bodi ya Wadhamini na Wanachama waanzilishi wa Nyumba ya Sanaa.
  Mheshimiwa Spika, matokeo ya hali hiyo ni kufunguliwa kwa kesi mahakamani. Katika kesi hiyo, iliyotolewa hukumu tarehe 24 Februari, 2005, Msajili aliamua kufuta rasmi usajili wa Bodi ya Wadhamini ya Nyumba ya Sanaa akiwataka wakabidhi mali na shughuli za NYUMBA kwa asasi mbadala. Uchunguzi uliofanywa na Kambi rasmi ya Upinzani umebaini kuwa tangu kutolewa kwa hukumu hiyo, Bodi haijawahi kukasimisha amali na majukumu ya Nyumba ya Sanaa kwa asasi mbadala, na badala yake imeendelea kuwepo na kupelekea Nyumba hiyo kuendeshwa kama kampuni binafsi kwa faida ya wajumbe wachache wa Bodi.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani ina taarifa kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo iliyofutwa na baadhi ya wajumbe wake wameleta mwekezaji ambaye wameshaingia naye ubia kimkataba, kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa katika eneo lenye jengo la sasa. Izingatiwe hapa kuwa mwekezaji atapaswa kulivunja au kubadilisha mfumo wa jengo la sasa la Nyumba ya Sanaa, ndipo aweze kujengwa la ghorofa.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani, inaitaka serikali na Bunge lako tukufu lizingatie yafuatayo;
  · Tujue kuwa Nyumba ya Sanaa hivi sasa inawanufaisha wachache ambao si walengwa waliokusudiwa. Tufahamu kwamba wanufaika hawa hawana rekodi ya uwekezaji katika Nyumba ya Sanaa, hivyo wanavuna matunda yaliyopandwa na wengine hasa kupitia ushirikiano mwema baina ya serikali ya Tanzania (kupitia Ikulu), Norway (kupitia shirika la NORAD) na Uholanzi (kupitia shirika la NOVIB).
  · Tutambue kuwa Nyumba ya Sanaa ilikuwa ni mlango wa masoko ya Sanaa na kazi za mikono, hivyo kutokuwepo kwake kunakwamisha juhudi za wazalishaji kazi za sanaa wa Tanzania kuweza kushiriki vyema masoko na hasa soko la pamoja la Afrika Mashariki.
  Mheshimiwa Spika, kwa kuyazingatia yote hayo na kwa manufaa ya wadau wote wa Sanaa na taifa zima kwa ujumla, Kambi rasmi ya Upinzani inaitaka serikali ichukue hatua zifuatazo kuhusiana na Nyumba ya Sanaa:-
  Mheshimiwa Spika, kwanza tunataka Nyumba ya Sanaa irudishwe Serikalini kwa Mdhamini Mkuu wa Serikali ili mchakato wa uanzishwaji wa Bodi huru ya kusimamia malengo yake anuai ufanyike. Uhuishaji wa Nyumba ya Sanaa utachangia sana kuongeza ajira na pato la taifa, hivyo kupunguza tatizo la uzururaji na kilio cha masoko ya kazi za sanaa.
  Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tangu kufutwa kwake mnamo mwaka 2005, Nyumba ya Sanaa imeendelea kufanya biashara pamoja na kuingia mikataba ya biashara mpaka sasa, Kambi rasmi ya Upinzani tunaitaka serikali ifanye tathmini na ilipwe kodi kutokana na faida ya biashara zilizoendeshwa mara baada ya kusitishwa uendeshaji wake.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani tunaitaka Serikali isitishe mara moja uvunjwaji wa jengo lililopo sasa, kwani ni utalii na ni alama ya taifa inayoonyesha jinsi serikali za Norway na Tanzania zilivyothamini juhudi za wasanii na wazalishaji kujikwamua kiuchumi na kuchangia pato la Taifa.
  Tunataka Nyumba ya Sanaa ifufuliwe upya bila kubadili malengo yaliyopelekea kujengwa kwake, na badala yake kila kitu kiboreshwe kwa kuheshimu malengo yale yale. Tunaamini Serikali hii inayojiita Serikali sikivu, itaheshimu matakwa ya Watanzania hususan Wasanii ambao pasipo shaka yoyote ile wanataka Nyumba yao irudi kwenye mikono salama kama tulivyopendekeza.
  Ahadi ya Studio ya Wasanii
  Mheshimiwa Spika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kupitia Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano alitangaza kuwa amewapa Wasanii Studio ya kufanyia kazi zao. Hata hivyo, baadaye wananchi na wadau wengi wa sanaa, nikiwemo mimi binafsi, tulishangaa kusikia Studio hiyo wamepewa NGO binafsi ya Tanzania House of Talent (THT)! Pia Rais aliahidi na kutoa nyumba ya Serikali kwa Wasanii ambayo ingetumika kuendeshea Studio husika, lakini nyumba hiyo ya Serikali iliyotolewa na Rais sasa iko chini ya THT na ndio makao ya THT!
  Mheshimiwa Spika,
  Mheshimiwa Spika,
   
 12. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #12
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wewe unafikiria kwa kutumia masaburi, ukwel ni kwamba huyo kirusi Ruge anabaka mziki hapa bongo kwa kushirikiana na jamaa wa serikali wasiokuwa waaminifu, wanaish mjini kiujanja ujanja tu na subirin 2015 akitoka madarakan ndugu yenu patachimbika mali ya serikal mlochukua itarudi.

  Unachekesha kweli ngoma ya SMS ya Nick Maujanja haikuwah kuwepo kwe top twenty ya Wafu FM ka wa jina langu ila ilishashika namba moja, bongo ukienda kwa mdosi kupeleka album mpaka kirusu ruge ashirikishwe ka hujuan nae imekula kwako, ka haupo kambi yao hupat show ma marketing manager wote wamewashika hakuna pa kutokea na ukiwa mjuaji kudai pesa nyingi hutapa show mpaka unaingia kaburini.
   
 13. WAFU FM

  WAFU FM Member

  #13
  Dec 8, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wewe unafikiria kwa kutumia masaburi, ukwel ni kwamba huyo kirusi Ruge anabaka mziki hapa bongo kwa kushirikiana na jamaa wa serikali wasiokuwa waaminifu, wanaish mjini kiujanja ujanja tu na subirin 2015 akitoka madarakan ndugu yenu patachimbika mali ya serikal mlochukua itarudi.

  Unachekesha kweli ngoma ya SMS ya Nick Maujanja haikuwah kuwepo kwe top twenty ya Wafu FM ka wa jina langu ila ilishashika namba moja, bongo ukienda kwa mdosi kupeleka album mpaka kirusu ruge ashirikishwe ka hujuan nae imekula kwako, ka haupo kambi yao hupat show ma marketing manager wote wamewashika hakuna pa kutokea na ukiwa mjuaji kudai pesa nyingi hutapa show mpaka unaingia kaburini.
   
 14. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  KWELI KABISA.. MKUU! SUGU ANADHANI ZAMA HIZI NI ZILE ZA 1990 .... :lol:
   
 15. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Naona ndio mikakati ya kikao cha juzi kuidhoofisha vinega inaanza kutekelezwa,naskia Kinje,somebody Swita wa airtel n.k n.k walikuwepo pia kuunganisha nguvu..ila haujaanza vizuri.vp Kusaga alishaongea kupitia redio yake?kama sehemu ya mkakati.
   
 16. K

  KILOSAA New Member

  #16
  Dec 8, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lakini ikumbukwe kuwa SUGU lengo lake sio nyimbo zake zipingwe redio..........lengo lake wasanii watendewe haki kwa kulipwa malipo staili na kazi yao.Sasa angalia jinsi wachache walivyoshikilia soko la muziki ili waweze kufanya maamuzi yoyote wanayotaka juu ya huu tasnia ya mziki.Pia CLouds na wadau wake wanaokula pesa za wasanii wanaogopa kuwalipa vizuri wasanii kwani wakiwa na nguvu ya kiuchumi watakuwa wabishi kutawalika,SUGU nguvu ya kiuchumi ameipatia sio kwenye Muziki roho inamuuma anapoona muziki aliouangaikia ameishia kuwatajirisha wachache .
   
 17. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Kaka Point yako nimeilewa hapa ila mimi nina Tatizo moja hapa hivi mnavyolalamika kuwa wasanii wa nje kulipwa pesa ya juu kuliko wasanii wetu then mnalalamika kuwa sio sawa kwa kigezo kipi ?? hivi nyinyi mnataka LADY GAGA alipwe sawa na SOGGY DOGGY guys guys guys... tuwe tunafikiria vitu vya kuongea jamani jamani jamani... tuwe tunafikiria basi ...
  mwenzako kagonga mult Platnum, yuko under huge label , video zake zina budget kubwa show yake hayuko mwenyewe kuna dj, light man, dancers, managers na watu kibao mfano hata akilipwa 200,000 usd yeye mfukoni unakuta inaingia 40,000 umeona....

  kwanza ni international artist soggy doggy kaishia tu ... Uganda na Kenya

  tukija katika Uganda wao kama wao serikali yao ndio inawa support so hata hapa sisi ni kazi ya serikali kubadilisha mfumo mzima wa music......

  kama U.s, Nigeria, na Uk wanavyofanya Tatizo sio Ruge. coz ruge yeye ni mmiliki tu wa chombo cha habari

  kuna vyombo vya habari zaidi ya kumi bongo.... umeona kama ruge hapigi nyimbo yako kuna Times fm, ea radio , radio one , Rfa hizi ni redio ambazo zinakufanya uwe maarufu tu so hapa ni kuna conclusion kuwa KAMA HUWEZI HUWEZI TU

  mimi sugu namkubali tena sana, Mapacha, na kundi lote linalojiita vinega ninawakubali tena sana tu coz they come up na kitu ambacho kidogo kinaifanya game ya bongo kuwa na ushindani mkali....

  coz kama ni inshu ya malaria sugu kuporwa na ruge kama alivyosema mimi hapo ninam support sugu ila kwa inshu ya
  pango la Tht ...tuangalie kwa macho mawili ile ni nyumba ya vipaji right? na wengi ambao wapo mle ni watoto yatima...sawa tunaweza sema wamenyonywa its okay.... wananyonywa BUT bila Tht maisha ya barnaba, lina, amin, wale dancer yangekuwa wapi?? sawa wananyonywa sikatai ila wanaingiza hela ambayo hiyo pesa walikuwa hawana uwezo wa kuingiza hapo mwanzo
  japokuwa at the end of the day bosi wao RUGE ndio anaingiza kipato kikubwa .. na hii iko sehemu zote Duniani
  unajua mapato ya lil wayne UNIVERSAL RECORDS wanachukua asilimia ngapi do you think ni 50% kwa 50% BIG NO kuna label zingine zinachukua 60% ya mapato ya msanii ananyonywa au hanyonywi???
  hiyo ni marekani

  sio tu kwenye music hata kwenye movies
  mfano shia labeof alilipwa usd 15 million kwa ajili ya kucheza transofmer -movie iliyoingiza 800 million usd kanyonywa au hajanyonywa??

  so i dont think ni muda wa kurumbana halafu sisi sio wasanii so hatujui makubaliano yao yakoje so tukiona mtu kalipwa pesa na kaenda kufanya shoo na clouds fm tusim judge vibaya coz hatujui kuwa wameelewana nini na watu wa clouds na wamelipwaje...

  kupigwa nyimbo redioni sio suala la wewe kuichukia clouds fm coz kama nilivyosema hapo awali kuna redio kibao na duniani kuna redio zaidi ya 1,000 so nina UHAKIKA uki submit nyimbo yako kwa redio hizo zote am sure KAMA WEWE Nyimbo yako ni nzuri LAZIMA U HIT na utakua juu kila siku..... ila kama nyimbo yako ni mbaya utaishia kulalamika tu kila siku so am sure guys

  ninaomba sugu na ruge wapatane na waangalie ni jinsi gani ya kusuluhisha huu mgogoro wao.....
   
 18. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #18
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mkuu CTU,
  Hapa kinacholamikiwa sio wasanii walipwe sawa na wasanii wa kimataifa,hapa kinacholalamikiwa ni lile gap kuwa kubwa mno,mfano milioni200 na laki 2 ni gap kubwa sana..at least wangevuta kidogo m'bongo apewe ata mil5 kiasi kwamba akitoka kwenye show anauwezo ata wa kununua bati za kuezekea banda lake..

  Pia unasema THT ni watoto yatima,kwa taarifa tu hakuna msanii yatima pale tht,linah ana wazazi wake wazima wako mbeya,barnaba ana wazazi wake wapo dsm na wengine wote,huo ni utapeli tu kwa wazungu.

  Kuhusu kupigiwa nyimbo zao redioni,sidhani kama hizi harakati zote ni hili nyimbo zao zikapigwe cloudsfm,
  we unafikiri Sugu minyukano yote hii ni hili apate airtime cloudsfm?siamini kama propaganda hii inaanza kukuingia.

  Unasema Ruge anaonewa,uhoni kosa lake..mkuu mimi binafsi sikufichi ninamarafiki kibao wasanii,wanalalamika sana kuhusu huyu MWIZI.kadhulumu sana wasanii sema Sugu amethubutu kuongea wazi tena bila uoga,wengine wanaongea chinichini tu.
  Ebu fikiria hadi studio aliyotoa rais kwa wasanii wote wa bongofleva kajimilikisha,studio ni kwa ajili ya wasanii kwani ye Ruge ni msanii?kwani THT ni BASATA?
  Eti kaanzisha chama cha kutetea haki za wasanii(TFU),kwani ye ni msanii?umeona wapi promota(tatizo)akaanzisha chama cha kutetea wasanii(waathirika wa tatizo)?..Tuzo kubwa za muziki kili awards yeye ndio anasimamia kila kitu,uchafu anaoufanya uko ukiusikia unaweza shika ata gun ummalize jinsi anavyochezea akili za wabongo..ukienda kwenye kampuni zinazotoa udhamini ndio u-Mafia mtindo mmoja bila kumpigia magoti yeye haupati udhamini kirahisi,kawashika wadau wote uko..unaweza kukaa chini kutengeneza idea yako ukipeleka kampuni,unaambiwa uiache waitathimini,kesho unasikia inatumika clouds group..
  Ukitaka kupeleka albamu kwa wadosi,bila Ruge kuipitisha haipokelewi,so inabidi umtoe cha juu..
  Sasa hivi kapenya hadi ikulu..haiitaji HATIMILIKI kudeal na wezi kama awa
   
 19. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #19
  Dec 9, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  kidogo naanza kupata picha ya ambayo nilikuwa siyajui......
  Nilifikiri tht ni kwa ajili ya watoto yatima kumbe sio.... (lakini inatangazwa kama ya watoto yatima)
  haya tuje swala la studio ya rais nakumbuka ilikuwa ni sherehe za tht ndio risala ya tht wakaomba studio kama nimekosea naomba nirekebishwe so rais alitoa ile studio kwa tht right?? Chini ya ruge right????
  But maybe katika risala ilisomwa kama wanataka studio ya wasanii ndio watu wakafikiri ni ya wasanii wote but ilikuwa kwa ajili ya tht coz ilikuwa tafrija yao na ndio maana rais alipoulizwa alisema ametoa kwa walioiomba tht....
  Chini ya ruge....
  Am i right???

  So hapa twalalamika nini?????

  Suala la tfu mimi sina chochote ninachojua so nitakaa kimya hapa

  kili music award navyojua ilianziswha na mtoto wa dandu... Ikawa iko chini ya kilimanjaro lager right ??

  Swali langu ni hili mnauhakika wakati mtoto wa dandu anaanzisha hichi kitu hakukuwa na mkono wa ruge????
  Kama ulikuwako katika kum support basi ni haki yake coz ni investors katika business hiyo.....

  Huwezi jua ka invest katika that kili music

  i dont think kibongo bongo mtu unaenda kumshika mtu kichwa na kufanya unavyotaka kama hujaweka pesa yako hapo hicho kitu hakiwezekani yaani wewe uwe na say katika sehemu fulani bila ya kuweka kitu hell no....
  Na kuhusu ruge the gay oooooh sorry i mean the guy lol... He is very smart kwa kusikia habari zake tu ni mtu anaye play card zake kwa plans so ninahisi high probability kuwa jamaa ka invest katika distribution, media, awards, so kama ka invest the guy anafuata mfumo wa nchi yetu ambayo ni capitalist so yeye ana play karata zake kama businessman so akitokea don akaput 5 dices wakati ruge ana 3 dices katika business aliyoinvest jamaa hapa nina maana akitokea don akiinvest kwa asilimia kubwa katika business alizoinvest ruge lazima jamaa awe chini na don aliyekuja ata take over thats how vitu vinavyoenda so mkuu cha msingi lets pray kwani hii vita walioianza kina sugu sio ndogo.... Ni vita kubwa labda atokee mtu abadilishe mfumo mzima wa usambazaji bongo...jamii forum business forum wachacharike na idea ningependa kuona mtu wa jamii forum anakuja na ku innovate kitu kipya ambacho kitu wa kinabadilisha mfumo mzima wa usambazaji wa muziki bongo....na sio mziki tu hata kwenye movies
   
 20. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #20
  Dec 9, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  uko sawa kabisa mkuu,kuhusu maombi ya studio yalifanywa kwenye sherehe za Tht,lakini iliombwa na wasanii wote japo risala iliandaliwa na Ruge,ile risala ilisomwa na lady jaydee baada ya Afande sele kugoma kuisoma baada ya kuipitia na kuona imejaa usanii sana..na Rais alihaidi kuitoa kwa wasanii wote,ila kilichofuata ni studio kukabidhiwa kwa tht badala ya chombo cha serikali Basata..ndio maana waziri alijikanyaga sana alipoulizwa juu ya hili.

  Kuhusu tuzo za Kili,Dandu ndio muhasisi bila Ruge kuweka ata sh.10 yake wala idea,yeye Ruge kaingia juzi hapa na kampuni yake ya 1call baada ya kupewa dili na wadhamini kuratibu tukio zima yani kusimamia mchakato wa kura,kupamba ukumbi,show za siku ya tukio na baada ya tukio n.k n.k ila haki ya killi awards inabaki kwa mke wa Dandu chini ya Basata..

  Kama unavyosema hii vita ni ngumu sana japo watu wanachukulia poa,unajua ikifikia kiwango watu wanakuwa tayari kwa lolote lile ni hatari sana..
  Siombei ila kuna kila dalili hii vita ikamalizwa kwa watu kuzikwa kaburini..

  Kwa taharifa ni kwamba Vinega wameshatoa ratiba yao ya kuzunguka mikoani,uku Cloudsfm wakiendeleza mpango wao kwamba kila jamaa watakapotua kufanya show nao siku hiyohiyo wanafanya show yao tena safari hii bure,wakisaidiwa na kampuni moja ya simu.

  Hii vita unaweza kuwaona Sugu na Ruge ila nyuma yao kuna makundi makubwa sana..kuna mambo mengi sana hapa mkuu.
   
Loading...