Vita ya kujivua gamba yamgeukia Idd Azzan; Vijana wakimtaka Azzan kutoa ufafanuzi kuhusu elimu yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita ya kujivua gamba yamgeukia Idd Azzan; Vijana wakimtaka Azzan kutoa ufafanuzi kuhusu elimu yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 11, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]


  na Mwandishi wetu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  KAULI ya ujasiri iliyopata kutolewa na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan, ya kutaka viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Dar es Salaam wajivue gamba kutokana na mkoa huo kufanya vibaya kwenye uchaguzi mkuu uliopita, ndiyo chanzo cha fitna dhidi yake, Tanzania Daima Jumatano limebaini.


  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa ingawa mzozo huo uliozimwa kiaina, katika siku za hivi karibuni mbunge huyo amekuwa akiandamwa na tuhuma za kuchakachua taarifa za elimu yake.

  Wiki hii mahasimu wa mbunge huyo kisiasa, wameendeleza mnyukano huo kwa kumtaka mbunge huyo avunje ukimya dhidi ya tuhuma hizo.


  Mmoja wa viongozi wa Umoja wa Vijana wilayani Kinondoni, (UVCCM), aliliambia gazeti hili kwamba wanamtaka mbunge huyo kutoa ufafanuzi kuhusu madai ya ‘kuchakachua’ taarifa za elimu yake ya msingi na sekondari.


  Mbali na suala la elimu ya msingi na sekondari, vijana hao pia wamemtaka kuweka bayana taarifa kuhusu chuo alichosomea mafunzo ya stashahada (diploma) ya Uongozi na Utawala, kwani chuo alichokitaja kinadaiwa kuwa hakitoi mafunzo hayo.


  Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti, vijana hao walidai kuwa taarifa hizo zimewasikitisha na kumtaka asikae kimya, kwani hatua hiyo inawafanya kuanza kukosa imani naye.


  “Unajua mbunge ni mtu mkubwa; ni kiongozi anayetokana na wananchi, sasa taarifa zake binafsi zinapotiliwa shaka, huku yeye binafsi akibaki kimya ni hatari sana,” alisema Haruna Kisamba.


  Kwa upande wake, Hilda Ngiwe alisema ukimya wa mbunge huyo kuhusu suala hilo umewafanya baadhi ya wana CCM kuamini kwamba amechakachua.


  “Kuna mbunge mmoja huko Temeke aliondolewa madarakani baada ya kubainika kuwa amechakachua taarifa zake za elimu, sasa hili nalo limekuja kwa staili hiyo, tunadhani ni vyema hatua zikachukuliwa,” alisema Hilda.


  Wiki iliyopita baadhi ya vyombo vya habari vilimkariri mbunge huyo akiwataka wanaoshuku elimu yake, waende mahakamani kwani hana wasiwasi.


  Alisema anajua taarifa hizo zimetoka kwa mahasimu wake kisiasa ambao wameamua kumchafulia kwa lengo la kumdhoofisha katika uchaguzi mkuu ujao.


  “Hayo yote ninayajua na kuyasikia, ninaelewa kinachotaka kufanyika na wanaofanya ni kina nani,” alisema mbunge huyo.


  Wakati vijana hao wakimtaka Azzan kutoa ufafanuzi kuhusu elimu yake, baadhi ya madiwani wa Manispaa ya Kinondoni, wamemtaka kuacha kuitumia vibaya Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayohusika na Hesabu za Serikali za Mitaa.


  Madiwani hao wamefikia hatua hiyo baada ya Azzan kudaiwa kupenyeza hoja yenye dalili za chuki dhidi ya diwani mwenzake, akimhusisha na ufisadi wa ujenzi wa shule moja wilayani humo.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Viongozi wote wa ccm ukiwachunguza sana utawamaliza wote. Wengi wamechakachua elimu zao kuanzia pale juu kileleni kabisa pale Magogoni hadi chini kabisa uchakachuaji mtindo mmoja. Hiyo ni sifa mama ya magamba.
   
Loading...