Vita ya Korea 1950-1953

DMCT

JF-Expert Member
Apr 25, 2015
2,276
5,929
Vita ya Korea ya karne ya
20 ilitokea kati ya 1950 hadi
1953.
Ilianzishwa na Korea ya
Kaskazini iliyovamia Korea ya
Kusini. Korea ya Kaskazini
ilisaidiwa na Jamhuri ya Watu
wa China na Umoja wa
Kisovyeti. Korea ya Kusini
ilisaidiwa na Marekani hasa.
Lakini Marekani ilishiriki
katika vita hii kwa jina la
Umoja wa Mataifa pamoja na
wanajeshi wa nchi 16.
Katika miaka mitatu ya vita
hii mapigano ya maadui
yalifika karibu kila sehemu ya
rasi na mateso ya wanachi
raia pia ya wanajeshi kwenye
pande zote yalikuwa mabaya
sana. Si rahisi kutaja idada
ya wahanga wote[1], lakini
makadirio yanataja karibu
milioni 4 watu raia na
wanajeshi hadi milioni 1. [2]
Awamu nne za vita
Shambulio la Kaskazini
Katika awamu ya kwanza
kuanzia mwezi wa Mei 1950
jeshi la kaskazini lilivamia
Korea ya Kusini likateka mji
mkuu wa Seoul na kusukuma
watetezi hadi kusini ya rasi
ya Korea. Lililobaki mnamo
Agosti/Septemba 1950
lilikuwa eneo la Pusan pekee.
Kuingilia kati kwa
Umoja wa Mataifa na
Marekani
30 Julai1950Baraza la
Usalama la UM iliamua
kuingilia kijeshi dhidi ya
uvamizi kutoka Korea
Kaskazini. Azimio hii lilipita
kwa sababu Umoja wa
Kisovyeti hukuhudhuria kikao
hivyo ulishindwa kupiga veto
yake. Jeshi lililoingia kwa
niaba ya Umoja wa Mataifa
liliunganisha vikosi kutoka
nchi 22, jumla askari 500,000
na wengi wao kutoka
Marekani.
Katika awamu ya pili jeshi la
Umoja wa Mataifa lilifika
Pusan kuanzia Agosti 1950.
Ndege za Marekani
zilishambulia barabara,
madaraja na jeshi la
kaskazini kote kwenye rasi.
Korea ya Kaskazini ilikosa
ndege za kijeshi. Jeshi la
Marekani na Korea Kusini
lilelekea kaskazini kwa mbio
na kuteka Seoul tena tar. 21
Septemba 1950. Likaendelea
kuwarudisha Wakorea wa
Kaskazini pia kuteka mji
mkuu wa kaskazini Pyonyang
tar. 19 Oktoba hadi kukaribia
mpaka wa Korea na China
kuanzia mwisho wa mwezi wa
kumi 1950.
Mashambulio
ya ndege za
Marekani
katia Korea
ya Kaskazini
Hapa Wachina walitoa maonyo
Wamarekani wasisongee
mbele zaidi lakini jemadari
mkuu MacArthur hakujali
maonyo haya. Wachina
waliandaa jeshi lao.
Kuingilia kwa China
Katika awamu ya tatu
kuanzia Novemba 1950 jeshi
la China likaingia kati na
kuwasukuma Wamarekani
kusini tena na kuteka Seoul
mara ya pili tar. 3 Januari
1951. Ndege za kijeshi za
Umoja wa Kisovyeti zilisaidia
zikilinda anga nyuma ya
mstari wa mapigano lakini bila
kuwashambulia Wamarekani
juu ya eneo lao. Wakati wa
Januari Wachina waliweza
kusogea mbele ndani ya Korea
ya Kusini lakini walikwama
kwa sababu walishindwa
kupata mahitaji yao kutokana
na nguvu ya Marekani angani.
Kurudi kwa hali ya awali
Katika awamu ya mwisho hadi
Julai 1951 mashambulio ya
Kaskazini na Kusini
yalibadilishana na Wachina
walirudishwa polepole hadi
mpaka wa 38 °C latitudo
uliowahi kuwa mpaka kabla ya
vita. Marekani iliamua
kutosogea mbele zaidi
ikitafuta majadiliano ya
kusimamisha vita.
Mpaka
kati ya
Korea
mbili
ukilindwa
na
wanajeshi
wa
Marekani
mwaka
2001
Majadiliano haya yalianza 10
Julai 1951 yakaendelea hadi
1953. Muda wote vita
iliendelea kwa njia ya
mashambulizi kila upande
lakini kwa shabaha ya kushika
maeneo yaliyowahi kuwa
upande mmoja au mwingine
kabla ya vita lakini kushikwa
na adui kwa sasa.
Tar. 27 Julai1953 mapatano
ya kusimamisha vita
yalifikiwa. Eneo lenye upana
wa kilomita nne pande zote
mbili za mstari wa latitudo ya
38 lilitangazwa kuwa "Ukanda
usio na jeshi".
Hadi leo ni mpaka kati ya nchi
zote mbili za Korea na
kulindwa na wanajeshi wengi
sana.
Marejeo
1. ↑Sehemu ya wa
 
Pamoja na vita zote.leo hii wana maendeleo.sisi vita moja tu.mpaka leo hakuna maendeleo
 
Ili kuvutia wasomaji wako siku nyingine panga vizuri stori yako sio unaiweka kama vile unaainisha vitu!..Halafu penda ushauri!!..
 
Mbona mistari siyo kabisa unaandika kilugha sometimes ila histori makini mwan
 
Ili kuvutia wasomaji wako siku nyingine panga vizuri stori yako sio unaiweka kama vile unaainisha vitu!..Halafu penda ushauri!!..
Nahisi atakuwa ameikopi mahali na kuiweka hapa kama ilivyokuwa kwenye chanzo, bila ya kuihariri....Ila ni habari nzuri sana ya Historia.
 
Back
Top Bottom