Vita ya kiuchumi katika ngazi ya mtu, familia, ukoo na marafiki

sepema

JF-Expert Member
Jun 13, 2019
591
1,000
Wakuu salaam.

Kuanzia awamu ya5 yaserikali yetu neno vita yakiuchumi limekuwa likitajwa Sana naviongozi wetu wajuu serikalini.

Kwa nilivyowaelewa wanamaanisha kuwa mtu,kikundi,taasisi ama nchi yoyte inayopinga mipango ya maendeleo kwa nchi yetu,hawa watakua wapiganaji wa hii vita ya kiuchumi.

Sasa Mimi huko serikalini napaacha Kama palivyo.

Hii 'Vita ya kiuchumi' katika ngazi nilizotaja kwenye kichwa Cha mada nimbaya na inatafuna zaidi kuliko hii ya serikali na nchi kwa ujumla. Kwanini?

Vita hii inahusisha ndugu,marafiki na kila unayemuamini katika mzunguko wako wamaisha.

Mbinu zitumikazo hapa ni majungu,unafiki na ikibidi uchawi.Lengo la yote niwewe uanguke ili either mfanane kimaisha au wao wawe juu yako.

Ugumu wakupambana na Vita hii katika ngazi tajwa nikwamba wapiganaji(maadui),hawataki uwafahamu hivyo wanakuchekea, wanakushauri na wakati mwingine wanakusaidia pale unalowahitaji Ila mioyoni wamebeba agenda ya kukuangusha.

Wakuu, Hawa watu ni wabaya na Mara nyingi huwa washindi wa hii vita.

Watu wengi Wanashuhuda na mikasa ya kufirisiwa na kutiwa umasikini na watu wa familia zao ikiwemo marafiki.

Ushauri; Kabla hujaanza kupambana kwenye Vita ya kiuchumi kwa ngazi ya juu, mulika kwanza hapo ulipo.

Adui wa mtu ni mtu
 
Hii vita mbona ni nyepesi Sana kuishinda hii. Muhimu ni kujifunza kanuni za kuishi na watu
 
inategemea huo uchumi wako upo kwenye macamera (limbukeni) au veep?
 
Ukijikuta duniani jua tu upo kwenye mapambano, haijalishi una kitu ama huna kitu ni lazima tu utapitishwa kwenye mstari ambao unatakiwa kufikia maamuzi juu ya maisha yako ya sasa na ya baadae.

Mtu asidhani kwamba yupo salama kwa vile yeye hayapitii magumu, hapana, kila mtu ana wakati wake wa kupitia hayo.
 
Inabidi Kama binadamu mtu mzima na mwenye akili utambue kabisa kuwa upo kwenye hatua ya mapambano, usifikiri na kuwaza kwa ufupi tu yani waza kwa upana zaidi,lazima uwafikirie hata watu wako wa karibu na uwajumuishe kama 'threat to your missions', kwani kila mmoja anafahamu yaliyo moyoni mwake, ww ni nani hadi uamini watu kiasi hicho?...usitegemee chochote kutoka kwa binadamu.
 
Tataizo wengi wanapenda kuongea mipango yao hadharani,kila mtu wa karibu anamweleza mipango yake yote
 
Kila unapojitahidi kupiga hatua kuna anaekushika shati kwa nyuma pasipo kutambua. Hii ni vita ya kimyakinya katika ulimwengu wa roho. Watu wengi wanaanguka kwa vita vya namna hii. Ila anaejua kuchezea anasonga mbele. Kivipi? Anarusha kipepsi kilichoenda shule kiasi cha kumvunja mtu meno. Huyo mtu hatarudia tena na anaishia kukuita mchawi. Yote haya ni katika ulimwengu wa roho.
 
Back
Top Bottom