Peter Agostino
Senior Member
- Sep 23, 2016
- 105
- 226
Mpaka sasa hivi sijasikia Taifa lolote la Kiafrika likitaja waziwazi kusimama na Taifa la Ethiopia katika vita yake na Waasi wa Tigray zadi ya kila mtu kufuata mkumbo wa Mataifa ya Magharibi kudai , OO... haki za binadamu zinavunjwa Tigray, Aby Ahmed akae meza moja na Waasisi kusuluhisha na hata kufikia hatua ya kuondoa raia zao Adis Ababa kwa propaganda za waasi kuwazidi nguvu Serikali halali. Hivi wakati Abraham Lincoln alipokuwa akipigana na Waasi Marekani karne ya 19 kuna mahali ulisikia alikaa nao meza moja kujadiliana? Mbona Wamarekani walipigana hadi Taifa lao leo ni moja na wanatetea umoja huo kwa udi na uvumba?
Waafrika hebu tuamke tuwe kitu kimoja. Tulimwacha Muamar Gadafi akauwawa hivihivi na hatuoni Libya mpaka leo ikiwa salama, hali ni hiyohiyo katika Mataifa mengine mengi Mataifa ya Magharibi walikojidai wanapeleka demokrasia yao. Hata Mataifa ya jirani kabisa kama Tanzania, Kenya, Uganda nK. ambayo kimsingi yalipaswa angalao hata kuonyesha mshikamano wao kwa kuwakemea waasi wanaotaka kuisambaratisha Ethiopia wamenyamaza kimya wakiogopa Marekani na wenzake. Kwanini Mataifa ya Afrika tusisimame na China kukataa Nchi zetu kuingiliwa na Mataifa ya nje?
Hakuna Taifa Duniani lingekubali hata siku moja uasi wa eneo lake moja kujitenga, hata Umoja wa Ulaya wenyewe japo siyo nchi lakini Uingereza ilipoamua tu kujimega EU iliweka vipingamizi kibao. Marekani hata sijawahi kusikia mtu aliyejaribu kuzungumzia jimbo fulani kujitenga sembuse kutumia vikosi vyake kushambulia serikali kuu ya Washington. Sasa iweje uasi ukitokea tu Afrika Rais Halali akiukandamiza ananyang'anywa hadi nishani ya Nobeli waliyompa wenyewe? Kumbe ilikuwa ni janja yao kumnyamazisha aendelee kutetea maslahi yao. Aby awarudishie linishani lao, Waafrika tuungane naye kuitetea Ethiopia moja na wala siyo vipandevipande vya Ethiopia.