Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Hii dhana ya vita vya kiuchumi inachanganya sana. Maana ikiangaliwa kwa upande mmoja watu wengi hudhania kuwa vita hivi huwa vinapiganwa baina ya taifa maskini lenye rasilimali zake dhidi ya mataifa matajiri yenye nia ya kunyonya rasilimali zake.
Tafsiri sahihi vita vya kiuchumi ni mikakati au mbinu zinazoweza kutumiwa na taifa lolote kuweza kudidimiza uchumi wa taifa fulani. Mfano ni kuweka kikwazo au kususa kununua bidhaa za taifa fulani.
Sasa kama ndio hivyo sisi kama Taifa ambalo tunataka tupige hatua kiuchumi tuko kwenye vita kiuchumi na akina nani? Mabeberu? Au jirani zetu waafrika?
Ni wazi kuwa tunaweza kuwa kwenye uwezekano wa either mabeberu wanataka waje hapa kuchota rasilimali zetu tusiambulie chochote na uchumi wetu usikuwe. Pia huenda kuna jirani zetu, waafrika wenzetu hawataki tukuwe kiuchumi nao wanafanya kila mbinu tusifanikiwe.