Takriban askari 33 wa Uturuki wameuawa katika mashambulio ya anga ya "vikosi vya Syria" Kaskazini-Magharibi mwa Syria, amesema afisa wa ngazi ya juu wa Uturuki.
Wengi waliumizwa katika jimbo la Idlib, amesema Rahmi Dogan, Gavana wa jimbo la Uturuki la Hatay. Taarifa nyingine zinasema idadi ya vifo ni ya juu zaidi.
Uturuki kwa sasa inajibu kwa kuyalenga kushambulia dhidi ya maeneo ya vikosi vya Syria.
Vikosi vya Syria vinavyoungwa mkono na Urusi vinajaribu kurejesha jimbo la Idlib ambalo kwa sasa linadhibitiwa na waasi wanaosaidiwa na wanajeshi wa Uturuki
Maafisa nchini Syria bado hawajatoa kauli yao wazi kuhusu mapigano ya sasa ya Idlib, ambalo ni jimbo la mwisho lililosalia mikononi mwa upinzani.
Jeshi la Uturuki lilianza kupiga maeneo ya Syria baada ya Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan kufanya mkutano na maafisa wa ngazi ya juu wa usalama mjini Ankara.
Kiongozi wa Uturuki anataka vikosi vya Syria virudi nyuma kutoka kwenye maeneo ambayo Uturuki imeweka vituo vya uchunguzi na awali ilitishia kuvishambulia kama haitaacha mashambulio yake.
Lakini serikali ya Syria na Urusi zimekataa madai yake ya kurudi nyuma kwenye mistari ya usitishaji mapigano iliyokubaliwa mwaka 2018. Urusi pia imeishutumu Uturuki kwa kukiuka makubaliano ya mwaka 2018 ya usitishaji mapigano kwa kuwaunga mkono waasi kwa kufyatua makombora.
Waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria wenye makao yao makuu nchini Uingereza,The UK-based monitor, the Syrian Observatory for Human Rights, wamesema kuwa wanajeshi 34 wa Uturuki waliuawa Alhamisi katika mashambulio ya anga jana jioni.
Waliojeruhiwa wamerudishwa nchini Uturuki kwa ajili ya matibabu, amesema Bw. Dogan.
"Yote yanajulikana"maeneo ya serikali ya Syria yalishambuliwa na ndege za Uturuki na vikosi vya ardhini, Mkurugenzi wa mawasiliano wa Uturuki Fahrettin alinukuliwa na Shirika la habari la taifa Anadolu akisema. Uturuki ilikua imeamua ku "jibu kwa ukarimu" mashambulio, alisema Bw, Altun.
Wakati huo huo ,Uturuki ambaye ni mjumbe wa Muungano wa kujihami wa nchi za Magharibi Nato imesema waziri wake wa mambo ya nje Mevlut Cavusoglu amezungumza na katibu mkuu wa muungano wa Nato -Generali Jens Stoltenberg.
Uwanja sasa umewekwa tayari kwa ajili ya makabiliano kamili baina ya Uturuki na Syria
Sent using Jamii Forums mobile app