Vita vya Syria: Magari ya kijeshi ya Urusi na Marekani yagongana

mohamedidrisa789

JF-Expert Member
Jun 20, 2015
5,110
21,646
Vikosi vya Urusi na Marekani vimelaumiana kwa mgongano wa magari ya kijeshi ya nchi hizo mbili kaskazini mashariki mwa Syria ambapo wanajeshi kadhaa wa Marekani wamejeruhiwa.

Video inayoonesha mgongano huo imepeperushwa na tovuti ya taifa ya Urusi, Rusvesna.su, na kusambazwa mara nyingi tu kupitia mtandao wa Twitter.

Video hiyo inaonesha gari la kijeshi la Urusi katika msafara wa jangwani ukigongana na gari la kijeshi la Marekani, Helikopta ya Urusi ilipaa umbali wa chini kabisa.

Urusi inasema kuwa Marekani ilizuia doria.

Taarifa za kutokea kwa tukio hilo zimejulikana Jumatano na waziri wa ulinzi Urusi ilisema kwamba ilitoa onyo kwa jeshi la Marekani kwamba itakuwa inashika doria eneo hilo.

"Licha ya hilo, ukiukaji wa makuabliano yaliyopo, wanajeshi wa Marekani walijaribu kuzuia ushikaji doria wa Urusi," kulingana na taarifa iliyonukuliwa na shirika la habari la Tass.

"Kujibu hilo, jeshi la polisi la Urusi lilichukua hatua kuzuia tukio hilo na kuendelea kutimiza walichokuwa wamedhamiria."

Baraza la Taifa la Usalama Marekani limesema gari la Urusi liligonga gari la Marekani, "na kusababisha majeruhi kwa waliokuwa ndani ya gari".

Vyanzo vya jeshi la Marekani ambavyo havikutajwa vimeambia tovuti ya Politico kuwa wanajeshi wanne wa Marekani wamejeruhiwa kiasi.

Marekani ina wanajeshi takriban 500 katika eneo hilo - kidogo sana kuliko awali - kusaidia kuiokoa dhidi ya vitisho zaidi kutoka kwa kundi la Kiislamu la Jihadi. Jeshi la Marekani linasaidia muungano wa vikosi vya jeshi vya Syria vya Democratic.

Msemaji wa NSC John Ullyot, alinukuliwa na Politico, akisema tukio hilo lilitokea 10:00 saa za eneo Jumatano, wakati wa doria ya usalama ya kawaida ya Urusi karibu na eneo la Dayrick kaskazini mashariki mwa Syria.

Akishutumu jeshi la Urusi kwa mgongano wa magari ya kijeshi ya Urusi na Marekani, alisema wanajeshi waliokuwa wanashika doria pamoja wakaondoka eneo hilo kupunguza makali ya hali ilivyo".

"Hatua ambazo si salama kama hizo zinaonesha ukiukaji wa kanuni zilizowekwa za kuepuka mgogoro, kulikotiwa saini na Marekani na Urusi Desemba 2019," Bwana Ullyot alisema.

Urusi imetoa silaha nyingi za nguvu kwa Rais wa Syria Bashar al-Assad ikiwemo ndege za kivita kusaidia kukabiliana na makundi ya waasi kama vile la IS.

Uchambuzi na maswala ya ulinzi Jonathan Marcus

Kumekuwa na matukio kadhaa yanayohusisha wanajeshi wa Marekani kaskazini mwa Syria. Wiki kama moja hivi iliyopita ilikuwa na makabiliano makali na Urusi, washirika wa Syria.

Februari 2018, kundi kumbwa la mamluki la jeshi la Urusi lilizindua mashambulio dhidi ya eneo la Marekani karibu na eneo kubwa la mafuta na wanajeshi wake wakapata majeraha.

Ingawa tukio hilo la hivi karibuni ni tofauti kidogo. Chanzo chake ni makabiliano ya moja kwa moja kati ya maafisa wa jeshi wa Urusi na vikosi vya Marekani. Marekani inasisitiza kwamba hilo ni sehemu ya matukio ambayo yamekuwa yakitokea. Urusi inakiuka makubaliano ya eneo.

Kwanini hilo limetokea? Urusi inaiona Marekani kama inayokaribia kuondoka Syria. Oktoba mwaka jana, Rais wa Marekani Donald Trump aliamua kuondoa wanajeshi 1,000 ambao walikuwa wakiunga mkono muungano wa Kikurdi, lakini akabadilisha mawazo yake na kubakisha wanajeshi kidogo katika eneo ambalo limewekewa masharti mengi.

Lakini Urusi inafahamu kwamba Bwana Trump anataka kupunguza wanajeshi wa Marekani nje ya nchi. Na vilevile, inaonekana kutaka sana Marekani ijiondoe.

 
Maneno ya vijiweni hatutaki, tunataka ushahidi kama huu au ule wa mashabiki wa Uingereza kuchezea kichapo kutoka kwa warusi
Hii ni habari kubwa Sana usilazimishe kuletewa link ili uione video ! Jiongeze nenda utube, Twitter na kwingine ipo mi nikiona ijmaa
 
Back
Top Bottom