Vita vya maneno Ufaransa na Uingereza,Sarkozy aonyesha dharau | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita vya maneno Ufaransa na Uingereza,Sarkozy aonyesha dharau

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Jan 31, 2012.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,276
  Likes Received: 19,423
  Trophy Points: 280
  Vita vya maneno baina ya Ufaransa na Uingereza vyaongezeka,Sarkozy aonyesha kudharau Uchumi wa Uingereza!


  Ugomvi na vita vya maneno kati ya wakoloni wakongwe wa Ulaya yaani Ufaransa na Uingereza vimeongezeka baada ya Rais wa Ufaransa kuufanyia istihzai uchumi wa Uingereza akisema kuwa, nchi hiyo hata viwanda haina.

  Jana Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa alizungumza na waandishi wa habari kupitia televisheni kwa lengo la kutetea mpango wake wa kuongeza kodi nchini Ufaransa na kudai kuwa mpango huo una nia ya kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.
  Wakati mwandishi mmoja wa alipomuuliza Rais huyo wa Ufaransa kwamba ni vipi anatetea mpango wake huo wakati kabla ya hapo mpango kama huo umetekelezwa nchini Uingereza na kushindwa, Sarkozy amesema mpango huo umeshindwa nchini Uingereza kwa sababu nchi hiyo haina viwanda.
  Mwaka 2009 pia Sarkozy alitabiri kuwa, mpango wa Uingereza wa kuongeza kodi ungelishindwa tu, matamshi ambayo hayakuwafurahisha viongozi wa Uingereza ambao nao baadaye walikwamisha mpango wa Ufaransa na Ujerumani katika eneo la Euro jambo ambalo lilitishia vibaya kulisambaratisha eneo hilo.
  Matatizo makubwa ya kiuchumi yanayozikabili nchi za Ulaya hivi sasa yanazidi kuonesha uadui na sura halisi ya viongozi wanaochekeana mbele ya vyombo vya habari barani humo.
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Wagombane tu.
  Ila rekodi zinaonesha kuwa uchumi wa nchi fulani huko Ulaya ukiyumba, basi na Ulaya yote kunakuwa na matatizo. Sijui kama Uingereza ni mojawapo?
   
Loading...