Vita vya mafisadi vinapopiganwa na watuhumiwa wa ufisadi wa ccm!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita vya mafisadi vinapopiganwa na watuhumiwa wa ufisadi wa ccm!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kigugumizi, Sep 11, 2009.

 1. k

  kigugumizi Member

  #1
  Sep 11, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  VITA VYA MAFISADI VINAPOPIGANWA NA WATUHUMIWA WA UFISADI WA CCM!!
  Chadema ilitoa shame of list – 11, ambapo namba kumi na moja alikuwa ni Jakaya Kikwete. Hoja hiyo sasa inaanza kuondolewa na mafisadi wanaobakia ni Balali, Lowassa, Rostam, Jeetu patel, Karamagi. Watu kama akina Mkono, Kikwete wanaonekana wako safi. Ni vyema ajenda ya Ufisadi wa JK ikarudishwa badala ya kuonekana yeye ndiye kinara wa kupinga ufisadi.
  · JK ni Edibily Jonas Lunyamila wa Orodha ya Mafisadi.
  · “Makamanda wa Ufisadi – ccm wanalinda kitumbua cha Ubunge.
  · Mkapa ni Mohamed Hussein “mmachinga” wa Orodha hiyo.
  · Makamanda waipongeza Chadema kwa kuwapatia muziki wa kucheza ili kulinda “ubunge wao”
  ……….Hebu tujikumbushe……….Orodha ya Mafisadi (List of Shame)
  11. FISADI NAMBA KUMI NA MOJA NI RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE

  Rais Jakaya Kikwete amekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Desemba 2005. Kabla ya kuwa Rais, Mheshimiwa Kikwete alikuwa Waziri wa Mambo Nje na Uhusiano wa Kimataifa kuanzia 1995 hadi 2005, Waziri wa Fedha 1994 hadi 1995 na Waziri wa Maji, Nishati na Madini kuanzia mwaka 1990 hadi 1994.

  Kama Waziri wa Maji, Nishati na Madini, Mheshimiwa Kikwete alishiriki moja kwa moja katika kusaini mikataba mibovu ya madini na makampuni ya madini ya kimataifa ambayo kwayo taifa limeendelea kupoteza utajiri mkubwa na kuinyima Serikali uwezo wa kifedha wa kuhudumia wananchi. Kwa mfano, mnamo tarehe 10 Aprili 1990, Major Jakaya Mrisho Kikwete aliingia mkataba wa madini ya kampuni ya SAMAX Limited ambapo kampuni hiyo ilipewa leseni ya kuchimba dhahabu katika eneo la Lusu, Wilayani Nzega Mkoa wa Tabora.

  Matokeo ya mkataba huo, maelfu wa wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu waliokuwa eneo hilo waliondolewa kwa nguvu na vikosi vya FFU na bila ya kulipwa fidia yoyote.

  Hadi leo wananchi hao hawajalipwa fidia yoyote licha ya miaka zaidi ya kumi ya kufuatilia haki zao. Baada ya kutwaa utajiri wa dhahabu wa eneo hilo, SAMAX Limited iliuza eneo hilo kwa kampuni ya Ashanti Goldfields ya Ghana kwa dola za Marekani milioni 253.

  Ashanti Goldfields nao wakauza eneo kwa kampuni ya Resolute Limited ya Australia kwa kiasi kisichojulikana cha fedha za kigeni. Resolute Limited ndio waliojenga na wanamiliki Mgodi wa Dhahabu wa Golden Pride ulioko eneo la Lusu, Nzega hadi sasa na ambao ulifunguliwa mwezi Novemba 1998.

  Mnamo tarehe 5 Agosti 1994 Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete aliingia tena mkataba na kampuni ya madini Kahama Mining Corporation Ltd., kampuni tanzu ya kampuni ya Sutton Resources ya Canada. Ijapokuwa mkataba huu unaonyesha wazi kwamba ulikuwa unahusu eneo la Butobela Wilaya ya Geita Mkoani Mwanza, mwezi Agosti mwaka 1996 Kahama Mining Corporation wakisaidiwa na vikosi vya FFU walivamia eneo la Bulyanhulu, Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na kuwaondosha kwa nguvu watu takriban laki nne waliokuwa wakiishi na kuchimba dhahabu katika eneo hilo. Baada ya kutwaa eneo hilo kwa nguvu za kijeshi, Sutton Resources iliiuza Kahama Mining Corporation na Bulyanhulu kwa Kampuni ya Dhahabu ya Barrick Gold Corporation ya Toronto, Canada kwa dola za Marekani milioni 280. Leo hii Bulyanhulu ni moja ya migodi tajiri kwa dhahabu katika Bara la Afrika.

  Dr. Slaa na Chadema - mpo wapi? Makamanda wa Ufisadi wengine kuucheza ngoma ya chadema - mbona mnampongeza fisadi Kikwete?!!
   
 2. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2009
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kikwete siyo fisadi mzee mbona unamsingizia au unachuki binafsi nn........acha hizo.
   
 3. F

  Facts Member

  #3
  Sep 12, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli, kwa yaliondikwa hapa na hata kutamkwa hadharani wakati ule, JK hawezi kukwepa tuhuma kuwa amechangia uporaji wa maliasili za taifa. Na kutokana na serikali yake kushindwa kuvunja mikataba hii ya kinyonyaji au kuirekebisha, inadhihirisha kwamba JK huyu wa sasa na yule aliyesaini mikataba hii, ni yuleyule. Safari bado ndefu ndugu zangu. Vita ya ufisadi haiwezi kupinganwa na mafisadi walewale...
   
Loading...