Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita vya Kagera: Nini chanzo? Kulikuwa na ulazima?

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Zero One Two, Jan 23, 2011.

 1. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Wandugu, salam za mida hii.

  Natafuta hotuba ya "SABABU TUNAYO, NIA TUNAYO NA UWEZO TUNAO."


  Nataka kusikia hizo "sababu tunazo" na hoja ya Rais ya kwenda vitani kwa mapana na urefu, badala ya kumbukumbu ya mstari mmoja tuliyokaririshwa toka udogoni.


  Nitangulize ahsante.
   
 2. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  naskia kuna mkono wa waingereza na wamarekani, sina uhakika nahitaji maelezo kwa wanaojua zaidi. Amini alikua na silaha pamoja na jeshi lililojitosheleza zaidi yetu, je ilikuaje tukashinda?tulitumia satelite za nani ku target majeshi ya amini?na kwanini? Kuna siri nyingi wakubwa.
   
 3. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #3
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nilisikia maneno, sina uhakika nayo kwamba ''hiyo ilikuwa njia ya kusambaza ukimwi afrika ya mashariki!" naomba kusahihishwa!
   
 4. N

  Nonda JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Utasikia sababu tano na domo, longo longo tu.
  Mpango ilikuwa ni kumrudisha Obote madarakani!
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sababu ya kwanza ni utawala wa kidikteta wa idd amin uganda kubomoa daraja la mto kagera mtukula na maneno ya kebehi kwa baba wa taifa pia alitangaza kwamba kagera ni sehemu ya uganda na alichoma bendera ya taifa na ya chama cha mapinduzi hadharani vilevile alisema anataka jeshi lake lifike mpaka dar es salaam yaani liiteke dar jamaa alikua anajiamini sana kwasababu alikua anaona tu kwamba sisi watanzania ni wapole sana kumbe uwezo tunao na nguvu tunayo nadhani waganda mpaka leo wanatuogopa maana tulipiga mpaka tukatokezea ethiopia!
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Jan 23, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,606
  Likes Received: 3,908
  Trophy Points: 280
  Kilimasera ukiona mdogo wakoa anampiga ngumi mwezio na mwenzi akarudishia mkorofi ni yule aliyeanza kurusha ngumi??

  Tafuta Literatures, uliza waganda, nenda kulia nenda kushoto......

  Uganda mpaka leo wanamkumbuka Amin! ambaye wewe unamwona dictator

  Amin aliua makumi
  Obote kaua maelfu
  Museven kaua makumi elfu.......


  Kwa kufupi mkuu, Nyerere alikuwa na mtu ambaye anatakwa sana na Amin..Mr.Obote,

  kwa kifupi ulikuwa mpango wa Nyerere kumuweka Obote madarakani!!! yale ya kagera n.k ni hasira za Amin, ukweli NYERERE NDIYE ALIKUWA MKOROFI!!!!!
   
 7. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika na hili lakini nahisi uko very very wrong mkuu gharama ya ile vita ukilinganisha na hiyo sabu du! hapana kama nikusambaza ukimwi wangeweza ku2mia njia ambayo isingeinvolve mauaji kama yale na gharama kama hizo..
   
 8. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #8
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kwa research za harakaharaka mie nadhani amin ndiye aliekua mkorofi man any way ngoja nipitie tena maana hizo nilizitoa kichwani na nikapitia faster literature zangu so wait nitakupa jibu ila kwa ile vita sidhani kama alikua mkorofi ni nyerere man!
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Du haya majibu?

  Ukitaka kujua sababu hasa ni jaribu kuangalia mambo yafuatayo:

  1. Museven ilikuwaje akapigana vita ya kumg'oa Idd Amin?

  2. Akina Paul Kagame ilikuwaje wakapigana vita ya kumg'oa Amin?

  3. Ilikuwaje hao wawili na kundi lao wawe Tanzania kabla ya vita?

  4. Kwa nini walipatia mafunzo ya vita Tanzania na kufanya mazoezi ya kivita Msumbiji?

  5. .....................................................................................

  Sababu ya kuanza vita kamwe haiwezi kuwa ni MOJA tu. Lazima kulichangiwa na vitu vingi sana. Obote ni kipande tu kwani Mzeven na akina Kagame pamoja na vita kuisha, walibaki Tanzania. Hata mie kwa sasa sina uhakika wa sababu ngapi hasa zilisababisha.

  Kuhusu Unyama wa Idd Amini kulinganisha na Mseven, mhhh Tafadhalini wajamani. Nimekaa na jamaa wengi wa Uganda na wengine hadi leo nawasiliana nao na mmoja wao akiwa ni kijana aliyepigana na Mseven kama askari wa Mizinga. Wengi wanasema kuwa Idd Amin alikuwa mnyama sana. Tatizo lake ni kuwa aliuwa hata wasiotaka kujihusisha na siasa. Kila msomi alikuwa ni tishio lake kubwa sana.

  Mseven yupo zaidi kupigana na adui zake. Kama wewe hujihushi na siasa, basi huwezi kupambana naye. Obote pia alikuwa mnyama sana sana na ndiyo maana Amin alipoingia, watu walimshangilia sana. Ila na Amin akawa kama Kikwete kwa kuunguza imani kubwa aliyopewa na wananchi.

  Miaka ya 80 na 90 Waganda walikuwa wakichukia sana Kiswahili. Msifikiri akina Cameleon leo wakiimba Kiswahili basi mkafikiri imekuwa hivyo muda wote. Jamaa walikuwa wakidai kuwa "enzi za Amin ukisema Kiswahili basi Mageti yote yanafunguliwa na unapigigiwa saluti. Kisa ni kuwa Kiswahili kilitumika zaidi na Amini na jeshi lake." Hivyo ukisema Kiswahili tu, watu wanajua kuna mtu anaweza kupoteza maisha sasa hivi au kupigwa sana.

  Ila ukweli mwingine ni kuwa, SIASA za Uganda ni ngumu sana. Utaona mtu analalamika kuwa kaonewa na Mseven na mwisho wa siku ukaja shangaa kaishia mitini na kisa ni kwamba jamaa ni Mpelelezi wa upinzani. Waswidi waliachwa mitini na jamaa mmoja na familia yake. Jamaa alikuja kuomba hifadhi, mwisho akaleta hadi familia yake. Siku moja wameamka jamaa hayupo Sweden na familia yake. Wakaulizia mipakani hakuna data zozote. Walipoenda Kampala kumtafuta, siku moja kawapigia simu na kuwaambia anawaona kwenye Mkahawa na kuwa wasimfuatefuate zaidi. Jamaa (waandishi wa habari) wakasema SIASA ZA UGANDA NI KIBOKO.

  Ndiyo maana nasema "Kama kuna mtu anafahamu hasa sababu, basi huyo ni Mganda. Kama siyo basi ni Nyerere na wengine wachache. Wengine wote wanajua tu sababu kadhaa na siyo zote". Uganda mambo ni mazito sana na sijui yataisha lini. Hata ukiweka katiba mpya na uchaguzi huru, Uganda ni ngumu sana. Wakija zubaa, Uganda yaweza kuwa kama Somalia maana WAJUAJI WENGI SANA UGANDA.
   
 10. S

  Shomy . I JF-Expert Member

  #10
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 222
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Vita ya Kagera na sababu za KIDINI. Nitafafanua. Idd amin alikuwa ni mmoja wa viongozi ambao ni mwiba kwa mataifa ya Marekani na Uingereza. Alikopa fedha WB kwa ajili ya maendeleo ya nchi na badala yake alijenga msikiti ambao unakadiriwa kuwa ni mkubwa ktk A.Mashariki. Na alikuwa mbioni kutangaza Uganda kuwa nchi ya kiislam kitendo kilichowakasirisha mabwana hao wa ulaya.

  Ilikuwa ngumu kwa wao kujiingiza 1kwa1 ktk kumuondoa madarakani na badala yake wakaamua kuitumia tz km walivyofanya kule NJUWANI huku wao wakiwa nyuma ya tz kwa kutoa silaha za kivita. Pia Nyerere alikabidhiwa eneo lote la A.Mash.kuusimamia ukristo na kuuendeleza. Hivyo ilikuwa ni lazma awajibike ipasavyo.

  Kwa kusema ukweli Tz hatukuwa na uwezo wa kumng'oa Idd Amin wala kule NJUWANI. Pia kuhusu kula nyama za watu, hakuna kitu km hicho hata hizo filamu wametengeza haohao(marekani na uingereza) ili kunakshi uongo wao watu waamin kile walichofanya. Mifano mingine ni sudani na angola (huu ni mjadala unaojitegemea).

  Nyerere hakuwa na 'UWEZO' wala 'NIA' Na huo ndio ukweli wenyewe mkuu.
   
 11. M

  Mtemakuni JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Watanzania tupende kuwa tunasoma historia na vitabu na kuanalyse mambo bila emotions. Wala tusitawaliwe na uswahiba au mapenzi just bcaz unampenda mtu bac kila anachofanya is right..!

  Kwa udadisi wangu na uelewa wangu na source zangu za information sababu za vita ya amini zilikua kuu mbili 1st Interest ya nyerere kumpandikiza washikaji zake obote na museveni though alizuga mwanzoni kwa kumpa lule..!

  2nd was interest ya wamarekani na waingereza kutokana na dini ya Amini, uhusiano wake na waarabu na kauli zake dhidi ya israel na baada ya kuteka ile ndege ya waisrael plan zilifanywa chap chap kwa kumuhusisha nyerere na kwasababu nyerere alikua na hiyo plan mambo yalikua mepesi akawezeshwa vita ikapigwa. Though china pia walitupa silaha soo hapa nyerere alitumia ucomunist wake pia kuget other helps...!
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kwa mfano upo kwenye paper ya advanced level hilo shwali unakutana nalo na lina maksi 20 unafikiri mwalimu wako angekupa ngapi kwa point hiyo?
   
 13. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 80
  umenena ukweli mtupu. Mie nilikuwa mji wa Mbarara siku moja nilipokwenda kutafta mahali pa kulala baada ya kujitambulisha kuwa ni Mtz walikataa kunipa rum kisa eti tajiri yao amepiga marufuku kulala watanzania kwani ni waongo sana na walimtia umackni wakat wa vita.
   
 14. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwaka 1977/78 wewe ulikuwa uzaliwa? Kuna sababu gani ya vita zaidi ya nchi kuivamia nchi ingine?

  Amini aliivamia Tanzania, akatangaza mpaka mpya kuwa ni mto kagara kiasi cha kilomita 25 hivi ndani ya mipaka ya Tanzania, wananchi watanzania wenzetu waliokuwa wanaishi maeneo yaliyotekwa walifanyiwa unyama na wengine kuuawawa bila makosa.

  Jina sahihi la vita ya kagera ni "Vita ya Ukombozi wa Kagara" Ndiyo maana Nyerere alipounganisha vita ya ukombozi na vita ya kumwondoa Amini Madarakani Uganda Umoja wa Mataifa haukumlaani kama ilivyo kuwa kwa G W Bush na Sadam Hussein. Actually, Waamerika walii copy Tanzania kama precedent ya nchi kumwondoa madarakani raisi wa nchi ingine wakati wa sakata la iraki huko UN.
  Ukweli wa vita ya kagera unaujua ila hapa umeuliza tu kiunaafiki, una ajenda yako mwenyewe ambayo unaona aibu kuiweka wazi.

  Kama ungekuwa siyo mnafiki ungeuliza ni kwa nini Amini alikimbilia Saudi Arabia au ni kwa nini Gadaffi alileta majeshi kumsaida Amini
   
 15. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #15
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  Wana jamvi nilifanya utafiti kuhusu vita hiyo,pia nikaandika makala yenye kurasa 50,mzee hamad hemed mtz mwenye asili ya kiarabu alikua huko wakati wa vita hiyo na anasema amin alipendwa sana na aliwapeleka maka kuhiji waislam wengi bure.

  Pia urafiki wake na gadaf pa 1 na mataifa ya uislam iliwaudhi wamarekani, pia kitendo cha kuwashinikiza wana diplomasia na viongozi wa uingereza walioenda uganda kumbeba juu na kuzunguka nae kampala kama walivyotumikishwa watu weusi kwenye biashara ya utumwa iliwauzi sana, hivyo nyerere akapewa dili la kumuangusha amin, mzee J Kenyata akamwambia amin dhidi ya mpango huo ndio amini akatangaza vita dhidi ya tz kwani alishajua mpango mzima nyerere na jesh lake masikini halikua hata sare za kutosha na wengine walikua wanafunga kudu kwa kukosa mikanda,alitumia rada na satelite za waingereza kumpiga amini, hakua na uwezo wala sababu ya msingi.

  Naishia hapa wengine waendelee.
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Jan 24, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwa nini isiwe ni kwa sababu ALIWAFUKUZA WAHINDI kwa kuwapa siku 90 wawe wameondoka wote Uganda?

  Yameanza yale ya Vipofu walioenda kumshika Tembo na kila mmoja akawa na story yake ya Tembo alivyo, kwa sababu kila mtu alishika kipande tu cha tembo.

  Kumbuka Wahindi wengi walienda UK na Canada.

  Pia Obote alikuwa na mpamgo wa kurudi madarakani akisaidiwa na akina Museven, Kagame na Tanzania.

  Angalieni film ya RISE AND FALL OF AMIN, iliyotengenezewa Kenya na huku Wakenya wakisaidia kutengeneza.

  Sikujuwa hata hili watu wataleta UDINI. Kaaazi kwelikweli. Hitler angelikuwa Muislaam .........
   
 17. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #17
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  mwl nyerere aliwahi sema kua yeye kama binadam alikua na mazuri pia mabaya hivyo niwajibu we2 kufuata mazuri na kuyapuuza mabaya yake, hili la vita ni baya na alichemsha pia muungano na zanzbar pia alichemsha kwani wakati karume anataka kujitenga baada ya mkataba wa muda kumalizika nyerere huyohuyo anahusishwa na mipango ya kumuua karume ili kulinda mungano, na wanaoutaka zaidi ni ulaya na marekani ili kuudhibit uislam na tishio la ugaidi, wazenj wanalijua hilo sio siri.
   
 18. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #18
  Jan 24, 2011
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Nashukuru sana kwa michango hii wandugu.

  Sababu zilizotolewa zinaleta mantiki na baadhi nimewahi kuzisikia.

  Ambacho sijawahi kukisikia, na ambacho nimetaja kuwa nakiomba, kama kipo, ni hoja ya vita kupitia hotuba ya "Sababu Tunazo, Uwezo Tunao" iliyotolewa Agosti 18, 1978, na Hayati J. Kambarage Nyerere.

  Unaposema "sababu ni kuvamiwa, kwani hujui" hainisaidii. Si kila unapovamiwa unaamkia vitani. Yapaswa, katika diplomasia za vita, uonyeshe, kama ambavyo nasikia Rais alifanya, kuwa njia nyingine zimeshindikana.

  Hiyo hoja ya Rais ndio ninayoitafiti. Kuna mtu anayo?
   
 19. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #19
  Jan 24, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Nyerere alikuwa mkorofi, ni yeye mwenyewe aliyebomoa daraja la Kagera kutafuta chokochoko za kumpiga Idd Amini. Alifanya hivi kumuingiza rafiki yake Obote madarakani kama mnakumbuka kipindi kile Obote alikuwa Dar. Ametuingiza kwenye umasikini wa kutosha kwa kutufungisha mkanda mpaka leo. Nachukia sana vita vile....
   
 20. J

  JokaKuu Platinum Member

  #20
  Jan 24, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,806
  Likes Received: 5,115
  Trophy Points: 280
  Bruce Lee,

  ..ungeisaidia sana jamii forums kwa ku-post paper uliyoandika kuhusu vita vya Kagera.

  ..nadhani sasa hivi kutakuwepo na a lot of de-classified documents toka mashirika ya kijasusi ya nchi za magharibi zinazoweza kutoa mwangaza kuhusu nini kiliendelea.
   
Loading...