Vita vya Kagera 1979: Kwanini Jeshi letu lilipitia mipaka ya Sudan badala ya kukatiza hapo kati kufika Kampala?

Ziroseventytwo

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
7,974
13,614
Tulizunguka sana. Arua, Kasese, portfot na kwingine kabla ya kufika Kampala. Swali ni kwanini tulizunguka sana badala ya kukatisha tu na kufika hapo kampala na kumtimua huyu nduli?

Screenshot_20200413-134955.png
 
Hawakukatiza mkuu, ni kwamba majeshi ya Tanzania yalitembeza kichapo kwa Idd Amin, wakaingia hadi kaskazini na magharibi mwa nchi ya Uganda, wakafika kwenye mipaka ya Uganda na Zaire(DRC), mipaka ya Uganda na Sudan. Mji wa Arua uliopo kaskazini mwa Uganda ndio kipo kijiji cha Koboko, kijiji alichozaliwa Idd Amin Dada.

Waliingia huko wakiwa na mzuka wa mapambano. Amin akasalimu amri, akakimbia Uganda na kuacha majeshi ya Tanzania (Wakombozi) yakiikamata Uganda.
 
Kwa taarifa yako majeshi ya Uganda yalikuwa vizuri sana kabla ya uasi.

Vita ilipoanza tulipoteza wanajeshi wengi mno japo taarifa zilifichwa, binamu yangu amepigana na amesimulia mengi mno ambayo serikali haikuweka na haitaweka wazi.

Hivyo unaposema kwani tulizunguka, unafikiri hao jamaa walikuwa dhaifu kiasi hicho?

Vita ina mbinu nyingi, moja wapo ni kumzunguka adui wakati yeye anapambana na wale waliom face... ghafla anashangaa anashambuliwa eneo ambalo hakutegemea.
Tulizunguka sana. Arua, Kasese, portfot na kwingine kabla ya kufika Kampala. Swali ni kwanini tulizunguka sana badala ya kukatisha tu na kufika hapo kampala na kumtimua huyu nduli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa taarifa yako majeshi ya Uganda yalikuwa vizuri sana kabla ya uasi.
Vita ilipoanza tulipoteza wanajeshi wengi mno japo taarifa zilifichwa, binamu yangu amepigana na amesimulia mengi mno ambayo serikali haikuweka na haitaweka wazi.
Hivyo unaposema kwani tulizunguka, unafikiri hao jamaa walikuwa dhaifu kiasi hicho?
Vita ina mbinu nyingi, moja wapo ni kumzunguka adui wakati yeye anapambana na wale waliom face...ghafla snashangaa anashambuliwa eneo ambslo hskutegemea.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikuwa katika mazingira ya jeshi la akiba wakati huo, na siyo kweli kuwa Jeshi la Uganda lilikuwa liko vizuri sana kuliko la Tanzania. Wale askari wetu waliokufa wengi kwa kipindi kimoja ni wale waliotumwa na Brigadia Yousufu Himid ambaye wakati huo ndiye aliyekuwa Brigade Commander wa Brigedi ya Magharibi kabla ya kuondolewa (kwa kosa hilo) na nafasi yake kukaimiwa na Kanali Kotta - baba yake na Faraja Kotta.

Brigedia huyo aliituma battalion kadhaa zivuke mto kwa mitumbwi kuingia hilo enelo lililokuwa limetekwa baada ya daraja kuvunjwa. Kwa vile upande ule uliokuwa umetekwa ni high tactical ground ndiyo maana askari wa Tanzania waligundulika na kuuwawa kwa vile walikuwa wanajiandaa kuvuka na bunduki tu, bila ya kuwa na silaha kubwa.

Askari wetu wa kwanza kuingia Uganda kukomboa ile sehemu iliyokuwa imetekwa na kusaidia ujenzi wa daraja la muda walipitia Rwanda. Ni vivyo hivyo pia kwa kupitia Rwanda ilikuwa ni rahisi wao kuingia ndani zaidi ya Uganda kwa upande wa Magharibi, hivyo hata mashambulizi makubwa ya kuingia Kampala yalitokea huko Magharibi, na ni kweli askari wetu wengine walishafika mbali karibu na Sudan kabla ya kuja kushambulia Uganda.

Kikosi Kikikubwa cha Idi Amini ni kile kilichokuwa kinaitwa Simba Batallion kilichokuwa na makazi yake pale Masaka (siyo Mbarara) ambacho baadaye kilikuja kusaidiwa na askari wa Libya wakati wa yale mapambano ya Lukaya. Kikosi kile cha Simba Batallion kilizingirwa pia na majeshi ya Tanzania kutokea Magharibi kikiongozwa na Brigadier Imran Kombe na Major General Marwa, ndipo Amini alipotuma wale askari wa Libya waje kusaidia na kufanya mapambano ya Lukaya kuwa makali sana lakini mwishowe Simba Batallion na askari wa Libya wakasalimu Amri na kuiacha Baracks ya Masaka mikononi mwa Imran Kombe. Ukishaondoa hiyo Simba batallion na Askari wa Libya, sehemu kubwa ya jeshi la Amin lilikuwa ni "maharage ya Mbeya tu"

Rangi ya nyekundu ndiyo iliyokuwa ruti ya kwanza kuingilia Uganda, halafu ruti ya kijani ndiyo ilikuwa ruti ya pili baada eneo la kaskazini mwa mto Kagera kusafishwa na daraja la muda kujengwa.

1592123135425.png
 
Tulipoteza wanajeshi wengi, acha kutetea
Walipotea wapi; si ajabu unasikia hadithi tu; ni kweli tulipoteza wanajeshi karibu 500 ( siyo 2000 ingawa sina namba kamili) ambayo ni karibu batallion moja, na nimekuambia kuwa katika hatua za kwanza za vita kuna karibu Batallion nzima iliyopotea kwa sababu ya uamuzi mbovu wa kamanda mmoja.

Vile vile vita ya Lukaya iliua waganda na walibya wengi sana lakini pia watanzania walikufa. Mimi nilikuwa karibu sana na taarifa za mapambano yale kuanzia mwezi Octoba mwaka 1978 (siyo 1979) kabla hata Rais hajatangaza vita yenyewe kwa vile nilikuwa kwenye Brigedi ya Magharibi ambayo ndiyo iliingia vitani kwanza.

Vita iliendelea kwa miezi saba katika mazingira magumu kama niliyosema hapo, hivyo ni kweli watu walikufa. Huwezi kupigana vita ya ardhini bila askari wako kufa. Jeshi la Uganda halikuasi bali lilielemewa nguvu na jeshi la Tanzania licha ya kuwa walikuwa wanasaidiwa na askari wengi sana kutoka Libya.

Unaposema kuwa watu wetu walielemewa sana ila baada ya hapo jeshi la Uganda likaasi ndipo tukapata unafuu- ni wazi hujui vita nini- ile siyo ngoma ya mdundiko ndugu yangu, ni kazi ya kurushiana risasi za moto, sema pia ni askari wangapi wa Uganda waliokufa kama hutapatwa na ugonjwa wa moyo iwapo unaliangalia jeshi la Tanzania wakati huo katika negative lens;

Jeshi la Uganda lilikuwa kubwa sana, Amini alikuwa anawekeza sana katika jeshi kuliko sehemu nyingine yoyote, ila sasa JWTZ ilikuwa inawafuta kama sisimizi ndipo wakafikia kukata tamaa ya kuendelea na vita ile.
 
Walipotea wapi; si ajabu unasikia hadithi tu; ni kweli tulipoteza wanajeshi karibu 2000 (sina namba kamili) ambayo ni kama batallion moja, na nimekuambia kuwa katika hatua za kwanza za vita Kuna karibu Batallion nzima iliyopotea kwa sababu ya uamuzi mbovu wa kamanda mmoja...
Jamaa anajibu from story za kwenye kahawa we unamchapa na facts tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walipotea wapi; si ajabu unasikia hadithi tu; ni kweli tulipoteza wanajeshi karibu 2000 (sina namba kamili) ambayo ni kama batallion moja, na nimekuambia kuwa katika hatua za kwanza za vita Kuna karibu Batallion nzima iliyopotea kwa sababu ya uamuzi mbovu wa kamanda mmoja..

Unaweza ukanipa straight fact (sio porojo) kwamba kwa nini immediately after Kagera War uchumi wa TZ ulishuka mpaka negative 3% (rejea mahindi ya Yanga kutoka Marekani na mchele wa Thailand)

Unaweza kutaja sababu moja plain (usipige story) kwamba kwa nini Nyerere baada ya kuona vita inamshinda, aliamuru Migambo Wote wa mitaani wapelekwe frontline vitani kupigana vita. Wanajeshi walikua hawatoshi?

Ahsante. 1979 ulikua una umri gani kaka?
 
Usimuite kaka. Huyo ni mzee wako.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Mwenzako anatoa ushahidi wa maneno we unamwambia tu anatetea

Ingebidi na wewe usememe hivi
Mkuu unakumbuka wakati askari wetu wanang'ang'a kutengeneza daraja kuna askari wa kiganda waliku wamejificha wakiwaua au wakati jamaa wanavuka mtu walikuwa wanashambuliwa...,

Back
Top Bottom