Vita vya chama cha nyerere dhidi ya ukali wa maisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita vya chama cha nyerere dhidi ya ukali wa maisha

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Mwigamba son, Apr 2, 2012.

 1. Mwigamba son

  Mwigamba son Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ni ukweli usiopingika kuwa ushindi wa gwanda dhidi ya tawalaaaa ktk jimbo la Arumeru mash, umetokana na wananchi hasa wale wa vijijini ambao kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiipatia tawalaaaa ushindi, kwa mgongo wa ukosefu wa elimu ya uraia katika maeneo ya vijijini. Sasa kilichotokea arumeru ni kuwa vita vikali vilikuwa vikipigana ndani ya mioyo ya wana-arumeru ambapo umeme wa mgao na wa gharama kubwa kushinda uwezo wa wananchi na unaolekea kutoweka kabisa, mfumuko wa bei kila uchwao, ukosefu wa ajira za vijana kwa watoto wao, kunyimwa mikopo kwa mature age, equivalent na watoto wa wakulima, rushwa katika ofisi na taasisi za kiserikali, suala la ubinafsi na upendeleo mchafu katika ajira pamoja na ukosefu wa maji safi na salama katika jimbo hilo ndiyo yaliyopelekea wana wa arumeru kuondoa ile hofu ya siku zote ya kusema chama cha Nyerere na badala yake wamebadili mfumo huo kutokana na miiba na mateso makali ya ukali wa maisha unaoletwa na sera mbovu za serikali ya tawalaaa. Hakika ni imani yangu kuwa hata kama elimu ya uraia haitafika kwa kiasi kikubwa maeneo ya vijijini ukali wa maisha ndio utakao amua ushindi.
  Hongera saaaaana gwanda na wakati mna shereheka chondechonde tafuteni suruhu ya kudumu kuhusu umeme wa uhakika na wa gharama nafuu ikibidi undeni tume itakayokuja na majibu sahihi A-z maana tawalaaa hawana uwezo huo tena.
  MWENYEZI MUNGU AWATANGULIE KATIKA UADILIFU WELEDI UAMINIFU UMAKINI NA USANIFU WA HALI YA JUU KATIKA UJENZI WA CHAMA NA TAIFA NA HASA UCHAGUZI WA 2015. KUSHINDWA HAKUPO KWANI WALE WALIOKUWA NA HOFU YA CHAMA CHA NYERERE HOFU HIYO IMEONDOLEWA NA UKALI WA MAISHA. TUMIENI UKALI WA MAISHA KAMA SILAHA YA USHINDI HUKU KWA MAKINI MKIELEZA NI NAMNA GANI MTAKAVYOBORESHA MAISHA YA WATANZANIA

   
 2. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  wafipa mnasemaje? chama tawala kinajali sana matatizo ya wapalestina na kuhakikisha wapalestina wanapata nchi yao huku wakulima na walalahoi wa kitanzania hawana kazi wala umemem vijijini. Chama tawala kinalaani sana mmarekani akiingia iraq na Afghanistan kutafuta maslahi yake lakini hakilaani uwezo mdogo wa Tanesco wa kutotosheleza mahitaji ya umemem tanzania. Haya sasa Arumeru mashariki imeshatoa onyo, tungoje uchaguzi mkuu 2015!
   
Loading...