Najiuliza sana kuhusu suala la ubabaishaji unaoendelea kwenye nchi yetu ya Tanzania. Naona mambo hayaendi sawa, huku viongozi wetu wakikabiliwa na kashfa mbalimbali, mikataba mbalimbali hewa, uchumi kudidimia na wananchi kutumbukia kwenye winbi la umaskini na mambo mengine chungu nzima. Hivi kweli nchi yetu ikiingia vitani leo na amiri jeshi wetu Mheshimiwa Kikwete tutaweza kweli kukabiliana na nchi yoyote hapo jirani na kwetu. Kwa mfano Malawi iseme ziwa Nyasa ni lao, na hakuna Wabongo kuvua samaki humo, au Wilaya ya Ngara itekwe na Rwanda au Mlima Kilimanjaro utekwe na Kenya hivi na ubabaishaji unaondelea tutaweza?