Vita UWT yaendelea: Anna Kilango adaiwa kuitisha kikao cha siri na kugawa nauli kwa wenyeviti!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita UWT yaendelea: Anna Kilango adaiwa kuitisha kikao cha siri na kugawa nauli kwa wenyeviti!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Mar 16, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Baada ya Juzi Sofia Simba kukanusha kuhusika moja kwa moja na mabadiliko ya mchakato wa kupata wabunge wa viti maalum, sasa Mama Kilango ametoka UK na kuwawahi wenyeviti wa mikoa na wilaya huhohuko Dodoma na kuwaandalia dinner ambayo iliambatana na manywaji na nauli kwa washiriki wote. Lengo ni kupata uungwaji mkono ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mkuu. Endelea kujihabarisha hapa..........

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Wagombea UWT waanza kupigana vijembe [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 15 March 2012 20:08 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0diggsdigg

  Habel Chidawali, Dodoma
  HOMA ya Uchaguzi ndani ya Umoja wa Wanawake (UWT) wa CCM imepanda huku baadhi yao wakianza kuvurugana ingawa muda wa kampeni haujafika.

  Katika kikao cha Wenyeviti wa Mikoa na Wilaya kilichomalizika juzi usiku mjini hapa, baadhi ya wagombea walikuwa wakipita huku na kule kwa ajili ya kuwasaka wapiga kura huku vikao vya usiku vikifanyika na fedha nyingi zikitembezwa.

  Mbali na hilo, baadhi ya wenyeviti hao kwa nyakati tofauti walieleza kuwa joto liko juu kwa wagombea kwani baadhi yao wameshaanza kampeni hata kabla ya ratiba ya chama huku wakirushiana vijembe vya wazi.

  “Hilo sio la siri, ni kweli tumeitwa katika Ukumbi wa Kilimani Barabara ya Ntyuka ambako tumekula na kunywa na pia tumewezeshwa vijinauli kidogo, lakini hayo siyo ya kuandika gazetini we waambie tulikuwa na mambo yetu,’’ alisema mmoja wa Wenyeviti wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa ambaye hakutaka jina lake liandikwe.

  Mwenyekiti huyo alimtuhumu mmoja wa wagombea kuwa alipanda ndege kutoka Uingereza na kuja nchini kwa ajili ya kukiwahi kikao hicho huku akimwacha mumewe huko lengo kubwa likiwa ni kuwaona wajumbe waliokuwa wakishirikia kikao mjini Dodoma.

  Baadhi ya watu wanaotajwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa UWT Taifa ni pamoja na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecele na Mwenyekiti wa Sasa Sophia Simba huku ikielezwa kuwa kutakuwa na mpambano wa visasi kwa wagombea hao.

  Mmoja wa wenyeviti wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini, alisema “Watu wengine wamekuwa ni wapambanaji wa kupinga ufisadi, lakini wao ndio wa kwanza kutoa fedha, jana kuna mtu alitoa Sh 30,000 kwa kila mjumbe eti kwa ajili ya kutusalimia tu, yaani ndio maana wakizipata nafasi hizi wanatutelekeza kwani fedha wanatumia nyingi mno kuzisaka.’’

  Aliongeza kuwa katika vijembe hivyo, mgombea huyo aliwataka wanawake kuachana na kumchagua Mwenyekiti wa sasa Sophia Simba kwa madai kuwa ameshindwa kuwatetea wanawake tangu alipoingia madarakani miaka minne iliyopita.

  Katika ujumbe wa simu ya mkononi ambao Mwananchi iliuona jana uliandikwa “Huyo kinyogoli wenu ametoka nje ya nchi na kumuacha mumewe, lengo ni kufanya kampeni na leo atakutana na wajumbe katika Ukumbi wa Kilimani mjini hapo hivyo kuweni makini ninyi wa upande wa Mwenyekiti.’’

  Akizungumzia jambo hilo Mwenyekiti wa UWT Sophia Simba alikiri kulisikia jambo hilo na kueleza kuwa mgombea huyo si mara ya kwanza kukutana na wajumbe na kufanya kampeni.

  “Ni kweli hata mimi nimesikia na hizo ‘message’ nimezisoma baadhi, lakini mimi niliwaita Wenyeviti katika kikao halali kabisa cha kazi ili tuweze kupanga mambo yetu lakini kama wenzangu wanatumia nafasi hiyo kufanya kampeni wafanye lakini wakumbuke muda bado,’’alisema Simba.

  Mwenyekiti huyo alisema kuwa wanawake wa sasa si wa kudanganywa kama inavyodhaniwa kwani wanajua kuchagua pumba na mchele na hivyo akasema hana wasiwasi kwa kuwa wanatambua hukumu ya mwisho itakavyokuwa.

  Akizungumzia suala la ukomo wa wabunge wa viti maalumu ambalo limeisumbua UWT kwa muda mrefu sasa alisema hiyo ni ajenda ambayo hata yeye aliikuta lakini kwa sasa ni wakati wake kuzungumzwa.

  “Ajenda hiyo sikuileta mimi lakini naikubali kwa moyo mmoja, shida ni kwamba baadhi ya wabunge wanaogopa kupoteza vitumbua vyao na ndio maana anaipigia debe iondolewe, lakini mimi nataka wajiamini na kugombea majimboni kwani tayari wana nguvu,’’alisisitiza Simba
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Huu moto sijui utazimika vipi? natamani uchaguzi ufike haraka hawa wamama waparuane kucha
   
 3. mgodi

  mgodi JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,303
  Likes Received: 967
  Trophy Points: 280
  Mbona huyu mama huwa anajidai anapinga ufisadi? hapo tena anagawa pesa ili apate ungwaji mkono kwenye uchaguzi!
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni sera kuu ya chama tawala, wanatofautiana kiasi tu lakini wote ndio tabia zao.
   
 5. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ​hakuna asiyetoa rushwa ccm hiyo ni sera yao
   
 6. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka mama Kilango hajawahi kujibu makombola ya Sophia Simba kuhusu ufadhili wa JITU PATEL kwenye harusi yao na Mzee wa Chilonwa. Tutasikia mengi ngoja kipenga kipulizwe.
   
 7. kiroba

  kiroba JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 10, 2011
  Messages: 324
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wenyeviti nawaombeni muwakatae wote hao kwa kuwa hawana uwezo wa kuongoza jumuiya kubwa kama yenu. Badala yake mpitisheni Betty Machangu atawaongoza vizuri sana na jumuiya itapata maendeleo sana.
   
 8. b

  baba koku JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Tunaomjua vyema tunafahamu kabisa kuwa hii ndiyo hulka yake,lakini bahati mbaya tuliowengi tunapenda ku-judge a book by its cover. Nilishuhudi kampeni zake wakati akigombea ubunge wa Ubungo nadhani mwaka 2000 akipambana na Keenja katika kuwania kura za maoni. Niliyoyaona sikuamini Tanzania kwa wakati huo tunao wanasiasa wanaotoa rushwa namna ile.
   
 9. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  hakuna kupinga ufisadi hapo,zile zilikua hasira kwa waliosababisha mumewe akose urais na hivyo akashindwa kuwa first lady! Ikulu ingegeuzwa bonge la pango la walanguzi,wezi,vibaka,majambazi, ........!
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Maisha yao ndio hayo fedha zetu wenyewe wamezihodhi ili kuwanyanyasa wananchi wakubaliane na matakwa yao CCM yote hovyo kabisa hovyo hovyo hawana ujasiri wa kulinda tena haki ya utu,mtu wala wananchi
   
 11. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tafsiri ya ufisadi kwa wana CCM ni tofauti na tunaoijua wote. Tafsiri zao sarakasi tupu.
   
Loading...