Elections 2010 Vita umeya CCM ni moto ........................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,173
Vita umeya CCM moto
Thursday, 09 December 2010 20:55

Ramadhan Semtawa na
Raymond Kaminyoge

KAMATI Kuu (CC) ya CCM leo itakutana kujadili majina ya wagombea nafasi za umeya wa majiji na manispaa, huku kambi mbili za watuhumiwa wa ufisadi na wapambanaji zikiumana kila moja kutaka kusimika washirika wao kisiasa.

Tayari mchuano huo umekwishapandisha joto katika hatua ya mchujo wa awali, huku kwa upande wa meya wa Jiji la Dar es Salaam kambi hizo zikionekana kuvutana zaidi.
Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba, jana aliliambia gazeti hili kwamba CC itakutana Ikulu chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kwa ajili ya kupitisha majina yasiyopungua matatu kupeleka kikao cha chama cha madiwani.

Makamba alifafanua kwamba, kwa mujibu wa kanuni za chama hicho kikao hicho cha madiwani ndicho cha mwisho chenye mamlaka ya kupigia kura jina moja litakalowakilisha chama.

"Kesho (leo) kamati kuu itakutana Ikulu kuanzia asubuhi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, ajenda kuu ni moja tu kujadili na kupitisha majina yasiyopungua matatu ya wagombea ambayo yatapelekwa katika kikao cha chama cha madiwani," aliweka bayana Makamba.

Mtendaji mkuu huyo wa CCM aliongeza kwamba, majina yanayojadiliwa na kupitishwa ni ya mameya wa majiji na manispaa huku majina ya wenyeviti wa halmashauri yakiishia katika ngazi ya siasa ya mkoa.

Kauli hiyo ya mtendaji mkuu wa CCM inakuja wakati zikiwepo taarifa za genge la watuhumiwa wa ufisadi likianza kutoa fedha kiasi cha Sh 500,000 kwa kila diwani anayeingia katika vikao vya chama vya madiwani ambavyo vitatoa majina yasiyopungua matatu yatakayopendekezwa na Kamati kuu ili washirika wao washinde.

Genge hilo ambalo linatuhumiwa kujilimbikizia mabilioni ya fedha chafu, linatajwa na duru mbalimbali za kisiasa ndani na nje ya CCM, kwamba zimekuwa zikifanya kampeni kubwa katika kiti cha umeya wa jiji la Dares Salaam.

Dar es Salaam imekuwa ikichukuliwa kama kitovu kikuu cha shughuli mbalimbali za kiserikali, kidiplomasia na kibiashara, hivyo vita kubwa ya umeya imekuwa ikielekezwa katika kiti cha meya huyo na wenzake wa manispaa zake tatu.

Mchuano mkali katika umeya wa jiji la Dar es Salaam unatarajiwa kuwa kati ya Dk Didadas Masaburi, Jerry Slaa na Hashim Sagaf huku wengine ni Abuu Jumaa, na Bisalala Salum.

Vikumbo hivyo vya kambi hizo vikiendelea, tayari baadhi ya madiwani wilayani Ilala, wameomba CC ya CCM kupendeleza watu wenye uwezo na siyo wapiga porojo.

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wagombea hasa wenye nguvu za mafisadi, kuanza kutumia baadhi ya vyombo vya habari kuwapaka matope wenzao ili waonekane hawafai kushika nafasi hiyo.

Wakizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam, kwa sharti la kutotajwa majina yao, madiwani hao walisema, kuna baadhi ya wagombea ambao wanawapaka matope wenzao ambao wanahisi ni watu wenye uwezo ili waenguliwe kwenye kamati kuu na wao kuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda.

“Halmashauri yetu ndiyo imejaa fitina, majungu, kuna mgombea mmoja ambaye anahangaika kuchafua wenzie kwenye vyombo vya habari, kwa nini anafanya hivyo sasa na si zamani, huyu anachafua wenzie ili kujenga mazingira ya kuteuliwa na kamati kuu,” alilalamika mmoja wa madiwani.

Aliongeza, “ Tunaiomba kamati kuu ifanye maamuzi yake kwa kufuata vigezo vilivyowekwa na siyo kuangalia propaganda zinazoenezwa kuwachafua wagombea, vinginevyo tutapata meya hatari,

Diwani mwingine, alisema kamati ya maadili ifanye kazi ya ziada kuwaibua baadhi ya wagombea waliowekwa na matajiri ili kulinda maslahi kwenye biashara zao.

“ Unajua Ilala, ndiyo Dar es Salaam, kuna shughuli nyingi za kiuchumi ambazo zinafanyika, kamati kuu ipendekeze majina ya wagombea wenye uwezo ili waweze kusimamia ipasavyo rasilimali zilizopo,” alisema

Alisema inashangaza mara nyingi propaganda chafu zinaenezwa kupitia vyombo vya habari kuhusu halmashauri hii hali inayoonyesha kuna baadhi ya wagombea hawajiamini kutokana na uwezo wao kuwa mdogo.

Hivi karibuni madiwani wengine katika halmashauri hiyo waliitahadharisha kamati kuu, kuwa makini wakati wakupendekeza mameya kutokana na baadhi ya wagombea kufadhiliwa na matajiri ili waweze kulinda maslahi yao.

CCM itapita katika hatua hiyo ngumu kisiasa baada ya kutikiswa na mbio za uspika ambazo genge la mafisadi lilituhumiwa kuweka mkakati wa kumwangusha Spika aliyejijengea umaarufu mkubwa kwa umma, Samuel Sitta.
 
Kamati Kuu CCM kukutana Dar

Thursday, 09 December 2010 20:00 newsroom
NA MWANDISHI WETU
KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, inakutana leo katika kikao maalumu kuteua majina ya wagombea umeya wa jiji na manispaa. Kikao hicho kitafanyika mjini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete. Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, Yussuf Makamba, ilisema ajenda kuu ya kikao hicho ni uteuzi wa wagombea hao. Kwa mujibu wa taratibu za uchaguzi wa wenyeviti wa halmashauri za serikali za mitaa, kila chama chenye madiwani katika halmashauri husika kina fursa ya kusimamisha wagombea. Mameya ni wenyeviti wa halmashauri katika eneo la jiji na manispaa. Wagombea wa CCM katika kinyangíanyiro cha umeya wa jiji na manispaa watakaopambana na wagombea kutoka vyama vya upinzani wanapaswa kuteuliwa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
ccm-bendera.jpg

Katiba ya CCM ya 1977, toleo la 2010, ibara ya 109 kifungu cha 6 (h) inaelekeza kazi ya kufikiria na kufanya uteuzi wa mwisho wa wana-CCM wanaoomba kugombea nafasi ya meya katika jiji na manispaa itafanywa na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
 
Vita umeya CCM moto
Thursday, 09 December 2010 20:55

Ramadhan Semtawa na
Raymond Kaminyoge

KAMATI Kuu (CC) ya CCM leo itakutana kujadili majina ya wagombea nafasi za umeya wa majiji na manispaa, huku kambi mbili za watuhumiwa wa ufisadi na wapambanaji zikiumana kila moja kutaka kusimika washirika wao kisiasa.

Tayari mchuano huo umekwishapandisha joto katika hatua ya mchujo wa awali, huku kwa upande wa meya wa Jiji la Dar es Salaam kambi hizo zikionekana kuvutana zaidi.
Katibu Mkuu wa CCM Yusuph Makamba, jana aliliambia gazeti hili kwamba CC itakutana Ikulu chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, kwa ajili ya kupitisha majina yasiyopungua matatu kupeleka kikao cha chama cha madiwani.

Makamba alifafanua kwamba, kwa mujibu wa kanuni za chama hicho kikao hicho cha madiwani ndicho cha mwisho chenye mamlaka ya kupigia kura jina moja litakalowakilisha chama.

"Kesho (leo) kamati kuu itakutana Ikulu kuanzia asubuhi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete, ajenda kuu ni moja tu kujadili na kupitisha majina yasiyopungua matatu ya wagombea ambayo yatapelekwa katika kikao cha chama cha madiwani," aliweka bayana Makamba.

Mtendaji mkuu huyo wa CCM aliongeza kwamba, majina yanayojadiliwa na kupitishwa ni ya mameya wa majiji na manispaa huku majina ya wenyeviti wa halmashauri yakiishia katika ngazi ya siasa ya mkoa.

Kauli hiyo ya mtendaji mkuu wa CCM inakuja wakati zikiwepo taarifa za genge la watuhumiwa wa ufisadi likianza kutoa fedha kiasi cha Sh 500,000 kwa kila diwani anayeingia katika vikao vya chama vya madiwani ambavyo vitatoa majina yasiyopungua matatu yatakayopendekezwa na Kamati kuu ili washirika wao washinde.

Genge hilo ambalo linatuhumiwa kujilimbikizia mabilioni ya fedha chafu, linatajwa na duru mbalimbali za kisiasa ndani na nje ya CCM, kwamba zimekuwa zikifanya kampeni kubwa katika kiti cha umeya wa jiji la Dares Salaam.

Dar es Salaam imekuwa ikichukuliwa kama kitovu kikuu cha shughuli mbalimbali za kiserikali, kidiplomasia na kibiashara, hivyo vita kubwa ya umeya imekuwa ikielekezwa katika kiti cha meya huyo na wenzake wa manispaa zake tatu.

Mchuano mkali katika umeya wa jiji la Dar es Salaam unatarajiwa kuwa kati ya Dk Didadas Masaburi, Jerry Slaa na Hashim Sagaf huku wengine ni Abuu Jumaa, na Bisalala Salum.

Vikumbo hivyo vya kambi hizo vikiendelea, tayari baadhi ya madiwani wilayani Ilala, wameomba CC ya CCM kupendeleza watu wenye uwezo na siyo wapiga porojo.

Hatua hiyo inatokana na baadhi ya wagombea hasa wenye nguvu za mafisadi, kuanza kutumia baadhi ya vyombo vya habari kuwapaka matope wenzao ili waonekane hawafai kushika nafasi hiyo.

Wakizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam, kwa sharti la kutotajwa majina yao, madiwani hao walisema, kuna baadhi ya wagombea ambao wanawapaka matope wenzao ambao wanahisi ni watu wenye uwezo ili waenguliwe kwenye kamati kuu na wao kuwa na uwezekano mkubwa wa kushinda.

"Halmashauri yetu ndiyo imejaa fitina, majungu, kuna mgombea mmoja ambaye anahangaika kuchafua wenzie kwenye vyombo vya habari, kwa nini anafanya hivyo sasa na si zamani, huyu anachafua wenzie ili kujenga mazingira ya kuteuliwa na kamati kuu," alilalamika mmoja wa madiwani.

Aliongeza, " Tunaiomba kamati kuu ifanye maamuzi yake kwa kufuata vigezo vilivyowekwa na siyo kuangalia propaganda zinazoenezwa kuwachafua wagombea, vinginevyo tutapata meya hatari,

Diwani mwingine, alisema kamati ya maadili ifanye kazi ya ziada kuwaibua baadhi ya wagombea waliowekwa na matajiri ili kulinda maslahi kwenye biashara zao.

" Unajua Ilala, ndiyo Dar es Salaam, kuna shughuli nyingi za kiuchumi ambazo zinafanyika, kamati kuu ipendekeze majina ya wagombea wenye uwezo ili waweze kusimamia ipasavyo rasilimali zilizopo," alisema

Alisema inashangaza mara nyingi propaganda chafu zinaenezwa kupitia vyombo vya habari kuhusu halmashauri hii hali inayoonyesha kuna baadhi ya wagombea hawajiamini kutokana na uwezo wao kuwa mdogo.

Hivi karibuni madiwani wengine katika halmashauri hiyo waliitahadharisha kamati kuu, kuwa makini wakati wakupendekeza mameya kutokana na baadhi ya wagombea kufadhiliwa na matajiri ili waweze kulinda maslahi yao.

CCM itapita katika hatua hiyo ngumu kisiasa baada ya kutikiswa na mbio za uspika ambazo genge la mafisadi lilituhumiwa kuweka mkakati wa kumwangusha Spika aliyejijengea umaarufu mkubwa kwa umma, Samuel Sitta.

CCM chama tawala mnatia aibu sana!!!!!!!!!!!!!!! Mna TAKUKURU_ kazi yake ni nini??????????????????????? Ni aibu kubwa-pesa za kuhonga zipo tena billions, lakini pesa za kufanyia mambo ya maslahi kwa taifa kama kuandaa katiba ya nchi waziri mufilisi wa uzalendo selina kombaini anasema hakuna pesa!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mtawachezea watanzania wote lakini siyo siku zote-saa hizi wanawataimu tu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Jina la JK latumiwa `vibaya' kampeni za Umeya

Imeandikwa na Mwandishi Wetu,Tabora; Tarehe: 10th December 2010 @ 23:30

MAJUNGU, fitna, fedha kumwagwa hovyo huku jina la Rais Jakaya Kikwete likitumiwa vibaya kwa baadhi ya madiwani ni baadhi ya vitimbi vilivyojitokeza katika kinyang'anyiro cha kusaka umeya wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.

Jumla ya madiwani sita walijitokeza kuchukua fomu na majina hayo yalishawasilishwa Dodoma kwa ajili ya mchujo, lakini hali ya sintofahamu imezidi kushika kasi baada ya madiwani wawili kuapa na kuhakikisha diwani mmoja ambaye anaonekana atapita endapo jina lake litarudi hashindi kiti hicho kwa sababu zao binafsi.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kupitia baadhi ya madiwani ambao hawakuchukua fomu kwa ajili ya kugombea umeya huo huku wakikataa majina yao kutajwa gazetini, walisema hali ni tete katika kipindi hiki cha muda mfupi cha kusubiri majina hayo yapitishwe.

Walisema yupo mgombea mmoja ambaye ana nguvu (jina linahifadhiwa) ambaye amekuwa akimwaga fedha ili kuhakikisha mmoja wa madiwani hao hapiti kwenye nafasi ya umeya endapo Kamati Kuu ya CCM, itarejesha jina lake kati ya majina matatu yatakayorudi.

"Huyo mwenzetu amekuwa akija na fedha na kututaka tuhakikishe endapo jina la mgombea huyo halipiti, kwani yeye alikuwa kwenye kampeni nzito za kitaifa hivyo, ametumwa na Rais kuhakikisha anapatikana meya makini na mahiri chini ya utaratibu anaotaka yeye, " alinukuliwa diwani mmoja alipozungumza na gazeti hili.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwepo na vikao vya usiku na mchana katika baadhi ya hoteli kubwa mjini hapa vinavyoendeshwa na diwani huyo mwenye chuki binafsi na kwamba baadhi ya madiwani waliochukua fomu kuomba umeya wamekuwa wakipishana benki kuchota fedha kwa ajili ya kuwapa wapiga kura ili wakamilishe wakitakacho siku ya siku.

Katika kinyang`anyiro hicho cha umeya, yumo Diwani wa Kata ya Kanyenye, Gulamdewji Remtulah, Diwani wa Kata Cheyo, Mathias Ndaki na Furaha Ikunji Kata ya Chemchem.

Wengine ni Diwani Kata ya Mbugani, Idd Kapama ambaye pia ni Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Tabora wa CCM, Mrisho Kaombwe Diwani wa Kata ya Isevya na Meya wa zamani, George Mpepo wa Kata Ng`ambo.
 
Back
Top Bottom