Vita mpya: CHADEMA watuhumiwa kumfadhili Abdul Nondo kumng'oa Zitto Kabwe Kigoma Mjini

Ndugu zangu,

Vita mpya ya kisiasa kati ya vyama vya upinzani imeshika kasi mjini Kigoma ambapo mara hii kijana Abdul Nondo anayeaminika kufadhiliwa na Chadema kanyanyua silaha za kisiasa dhidi ya Zitto Kabwe.

Chadema ambayo sasa inatamani kurudi katika zama za kuungwa mkono na vijana baada ya kupoteza hadhi hiyo miongoni mwa Watanzania katika miaka ya karibuni.

Kijana Abdul Nondo alitokea kuwa maarufu baada ya kuwa kiongozi wa mtandao wa wanafunzi wa elimu ya juu na zaidi baada ya kuibuka na kashfa ya "kujiteka" ili kupata umtaarifu wa kisiasa tuhuma ambazo alisafishwa na korti na hatimaye kurudi kuendelea na masomo ya shahada ya kwanza UDSM ambapo anatarajia kumaliza mwezi Juni mwaka huu (2019).

Abdul Nondo ambaye yupo mjini Kigoma amekuwa akipita katika magenge maarufu kutafuta uungwaji mkono kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2020 ambapo inaaminika anapata ufadhili kutoka Chadema.

Katika hatua nyingine CCM imeendelea kujiimarisha katika mji wa Kigoma kiasi cha kujiiliza mantiki ya harakati za Chadema kupitia Abdul Nondo zina maanisha nini katika mustakabali wa Jimbo la Kigoma.

Baada ya Zitto kuulizwa kuhusu anavyochukulia harakati za Chadema na Abdul Nondo alisikitika huku akilalamikia Nondo kukata simu zake.

Muda utatujibu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo wewe shida yako hasa ni nini? Una maajabu kama haya tunayoyaona ya Makombo na Zahera wa Yanga kuvaa fulana za rangi ya Simba
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom