Vita kati ya Tarime na Rorya

Cynic

JF-Expert Member
Jan 5, 2009
5,144
1,648
Hivi kuna Vita kati ya Tarime na Rorya? Au ni utengenezaji wa news? Maana nimesikiliza recorded BBC Swahili News bulletin, na kama kawaida news kwa vyombo vingi vya habari huwa ni habari mbaya mbaya tu, waka'cover' Irak na mabomu yao, Somalia na kukatana miguu na mikono, Iran na vurugu zao, kesi ya kuuwawa kwa mwandishi wa habari wa kirusi, etc. na hatimaye wakamaliza na Vita kati ya Tarime na Rorya (ambapo wanadai mtu kauwawa na kuna majeruhi).
 
Nisikiavyo mimi ni kuwa kuna Rorya vs Rorya kwenye yale mambo yao ya wapi kujengwe makao makuu ya wilaya. Haya ya vita sijayasikia, labda kama kuna habari zaidi. Lakini kwa muda mrefu hawa jamaa pande mbili wamekuwa wakiishi raha mustarehe kabisa ukiacha wizi wa mifugo wa hapa na pale.
 
TUKUBALIANE kitu kimoja kwanza. Nacho ni kuwa serikali, vyombo vya dola na dini zimeshindwa kuleta amani mkoani Mara. Sawa ?

Kuna jamaa kapendekeza kuwa mkoa huo utawaliwe kijeshi. Mimi ninapinga hilo. NIkitazama ramani za wilaya Tanzania karibu nusu yake viongozi wake ni wanajeshi wastaafu. Wataleta lipi jipya.

Vita hii inaelekea n ya chini chini na hata Watanzania wenyewe hawana habari nayo. Maana kama wanavyopeleka majeshi Comoro, Darfur, Seychelles na kwingineko na kuunda tume za kutafuta amani kulia na kushoto basi miaka mingi iliyopita tungelishakuwa na Koffi Anan hapa au Joachim Chissano kuwapatanisha wakazi wa mkoa wa Mara. Lakini inavyoelekea kwa sababu moja au nyingine kuna mtu au chama mahala fulani kinachotaka hali hii iendelee.


Kisha nimeona huko Misri jinsi Jeshi lilivyojiingiza katika kila sekta ya uchumi kuanzia kutengeneza magari, friji mpaka kuuza mayai na vitumbua lakini badala ya kuongeza tija kwa kuwa shughuli zao zote zinafanyika kiujanja ujanja na wao wanataka kujionesha baada ya kuaibishwa na kajeshi kavitoto vidogo vya Kiisraeli kuwa bado ni miamba wamehamishia ubabe kwa wananchi wao wenye utapiamlo na kwashiorkor ya kila aina kuanzia ile ya chakula, uchumi, siasa na utamaduni na sasa wanaambukiza soka ambalo limeanza kudidimia kwa sababu hamna uhuru wa mawazo, fikra, akili wala kuzungumza na kwenda unapotaka nchini humo.

Kadhalika, menejimenti ya kijeshi sio tu inafanya kila kitu kwa siri kwa faida zao wenyewe na wala mtu asikudanganye kwamba ni faida kwa wananchi wote. KIla rais anayetaka kubaki madarakani lazima ale na wakuu wa jeshi. Lakini ukiwaachia mno jmaa hawa watakuachia ile hadithi ya ngamia na mwarabu au mmeisahau.

NI NINI KIFANYIKE:
Ninapendekeza ili kuleta amani mkoani Mara :
1. kila Wilaya iwe na Baraza lake la Wawakilishi. Mabaraza hayo yataundwa na wenyeviti na makatibu wa kila kijiji na wajumbe toka koo zote katika kila kijiji;
2. Kila kijiji haraka haraka kijengewe kiwanja cha michezo ambacho kitakuwa na karibu maeneo ya michezo yote;
3. Michezo itumike kuleta amani mkoani humo kwa kuwa na mashindano mbalimbali kati ya vijiji;
4. Kijengwe kiwanja kikubwa cha Golfu ili mastaafu wakijaluo waanze kujifunza na hivyo kupata kazi mbadala ambayo ni starehe pia;
5. Kujengwe kiwanja cha basketiboli kwa kila mtaa na ikiwezekana cha voleboli na kriketi pia;
6. Kujengwe kiwanja cha mbio za magari ya formula 1na mbio za pikipiki na mashindano mengine ya kihatarihatari na kidamudamu ili ajra pendwa na uchu wa Kikurya wa damu utulizwe;
7. Kujengwe kituo cha michezo ya majini katika Ziwa Victoria ili vijana wa Mara wapate ajira na kuwa na michezo inayochangamsha damu zao;
8. Waitwe wana michezo wa Kitanzania na wa nje kugundua vipaji vya wakazi mkoani humo na wawapige msasa kwamba kuiba ng'ombe na wanawake sio kazi tu iliyopo duniani. Bila shaka mastaa Kama Hasheem wa Memphis na kina Tiger Woods na Louis Hamilton watawachochea Wakurya na Wajaluo wareeefu kucheza basketiboli, wakimbiza ng'ombe kukimbiza magari na boti, na warusha mishale na mikuki kucheza golfu na wengineo kujihusisha na mbio fupi kwa refu, kurusha mkuki na tufe, futiboli, kriketi na kadhalika, na kadhalika na ninaamini Matinyi huko Marekani atawasaidia kwa mawazo zaidi, the idea ni kwamba there is more in life than fighting for women, land and cattle and it is sheer blindness to believe you are born to live forever where your parents are;
9. Wakorofi wote wakamatwe na kulazimishwa kujiunga na JWTZ au Polisi au JKT;
10. Labda hao walioshindwa sasa baada ya kusoma kpande hiki cha fikra nzito zinazoweza kubadilisha kabisa jamii husika mkoani Mara watakuwa wamepata mwangaza wa kile kinachoweza kufanyika.

Ninamshukuru Mungu kwa kunipa akili ambazo wenzangu hamna. Na nitawashangaa kunionea wivu na kuzikataa kuzitumia fikra zangu. Na katu sitegemei kwa tabia na hulka mlizonazo kutoa shukrani wala asante. Wakupewa ni wakupewa tu hata afike juu kiasi gani. Na wa kutoa ni wa kutoa tu hata awe chini kiasi gani. Na hakika waliozoea kula kibudu cha halali kwao ni anasa tu.
 
Nipo Musoma kwa shughuli binafsi toka 26july09 nilichokipata kwa wenyeji ni kuwa kuna mapigano makali kati ya wajaluo na wakulya yaliyosababishwa na wajaluo kutokubali kuibiwa ng`ombe zao na wakulya nimepita maeneo ya Musoma Air Port nimeona Helcopta yenye maandishi POLISI na wenyeji wanasema ni ya kamanda TOSS sina hakika sana ila ni habari ambazo zimesambaa sana hapa musoma mjini
 
Last edited:
Nipo Musoma kwa shughuli binafsi toka 26july09 nilichokipata kwa wenyeji ni kuwa kuna mapigano makali kati ya wajaluo na wakulya yaliyosababishwa na wajaluo kutokubali kuibiwa ng`ombe zao na wakulya nimepita maeneo ya Musoma Air Port nimeona Helcopta yenye maandishi POLISI na wenyeji wanasema ni ya kamanda TOSS sina hakika sana ila ni habari ambazo zimesambaa sana hapa musoma mjini

Niliwahi kufika maeneo wanayoishi hawa jamaa zetu (wakurya). Ninachokumbuka ni wanaume kutembea na sime, marungu upinde/mshale .. yaani lawlessness na ubabe wa hali ya juu. Dunia/Tanzania ya huko ni nyingine/tofauti kabisaaa..
 
Back
Top Bottom