Vita Kati ya Maji ya Kilimanjaro na Maji Mengine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vita Kati ya Maji ya Kilimanjaro na Maji Mengine

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by SolarPower, Apr 19, 2011.

 1. S

  SolarPower JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 226
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natumaini wengi wenu mtakuwa mmegundua hali ambayo si nzuri katika biashara ya ushindani kati ya maji yenye chapa ya KILIMANJARO na maji kama UHAI na mengineyo.

  Hali iliyopo ni kuwa katika sehemu nyingi hapa Dar Es Salaam kama vile Baa maarufu mbalimbali, Kumbi za Starehe, Club za Usiku, Mahoteli, Migahawa mbalimbali pamoja na mikutano na semina mbalimbali utakuta sehemu zote hizi maji yanayouzwa ni ya KILIMANJARO. Binafsi nimeishazuiwa kuingia na maji ya UHAI katika baadhi ya sehemu hizi kwa kuambiwa kuwa maji hayo hayaruhisiwi kwa maelezo kuwa maji yanayoruhusiwa ni ya KILIMANJARO tu? Je hii ni haki? na Je FAIR COMPETITION COMMISSION wanalijua hili? na kama wanalijua hili tatizo, je ni hatua gani wamechukua ili kuleta usawa katika ushindani wa biashara hii ya maji ya kunywa?
   
 2. C

  Chogo matata Member

  #2
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Mlima unauzika kwa wageni uhai hayana ishu kwenye mikutano na sehemu muhimu,kwanza maji yenyewe yanachakachuliwa mtaani daily,we nenda sehemu kama arusha alafu uliizia maji ya uhai kama utayapata?sanasana w2 watakushangaa.
   
 3. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #3
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Huwezi mlazimisha mtu kuuza kitu ktk sehemu yake ya biashara.
  Wote tunajua ukweli kuhusu quality ya maji ya klm na mtu mwnye hotel kubwa kihivyo asingependa kuudhi wateja kisa maji yamechakachuliwa. Pia maji ya kanda ya kaskazini yana ladha nzuri sana tu compare na mengine, hii ni fact.

  Kwa walioenda nchi za nje wamekutana na hili na sio kitu cha ajabu kuingia mahali ukaomba coke ukaambiwa wanauza products za pepsi tu, binafsi imenitokea hapa dsm mara kadhaa.
   
 4. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #4
  Apr 19, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  mbali ya kuwa maji ya uhai yanachakachukiwa mtaani pia parking yake sio nzuri chupa zake hazi vutii mbele ya wengi tofauti na kilimanjaro, angalia yale maji ya cool bleu nayo ni mazuri
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Apr 19, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Malalamiko ya huyo jamaa hayana msingi kwa sababu kama ulivyosema kila mtu ana uhuru wa kuchagua product za kuuza sehemu yake ya biashara na inashangaza mtu kubebelea mimaji hadi sehemu hiyo huku akijua kwamba hapo kuna kinywaji kinauzwa. Kwa hili hata angeenda na gold label angefurushwa nayo kama ambavyo mtu angeenda na chakula chake cha kutoka kwa mama ntilia na kuingia nacho hotelini. Mbona hajiulizi kwa nini maji ya Kilimnjaro yalikuwa yanauzwa kwenye world cup Afrika ya Kusini na hakukuwa na hayo maji yake ya Uhai?
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Apr 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Same OLD Stories - FAIR Competition Commission wapo pale ki-maslahi zaidi!!! Sh...
   
 7. C

  Cola Member

  #7
  Apr 19, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 41
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Uhai yanachakachuliwa hata mimi hapa Dar nayanywa nikikosa kilimanjaro au cool blue. kuna kipindi waliwahi kumuuliza mmiliki wa uhai kuhusu ubora wa maji kuwa chini akasema kuwa yeye hafanyi biashara ya maji bali ya chupa ndo kisa kaweka bei chini. akasema maji anaweka kama bonus so endapo yanachakachuliwa aliomba asiulizwe kwa kuwa maji si biashara yake bali chupa.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ushindani wa kijinga namna hii umewahi kuwepo hata kwenye soda na bia. Kuna baa au migahawa fulani ukienda hupati soda ya ukoo wa PEPSI au ya COCA. TBL walijaribu mara kadhaa kuia SERENGETI kwa njia za kikatili kama kununua chupa na makreti yake kisha kuyateketeza. Kinachofanyika ni kwa wenye mabaa kupewa viti, meza na friji halafu wanapewa masharti magumu kutouza bidhaa za washindani.
   
 9. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #9
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mtoa hoja kusema kweli sijaona issue ni nini mbona huo ushindani upo katika bidhaa nyingi? Hujaweza kuonesha foul play sasa Fair Competition wanaingiaje?
   
 10. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #10
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Inasemekana kuwa UHAI ni ya walalahoi,hayana TBS ya kutosha.
   
 11. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #11
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikipiga Kili zangu hafu ukaniletea maji Uhai, lazima nitapike.

  marufuku uhai kuuzwa Bar.

  ukiona bar wanauza maji ua Uhai, ukienda jikoni haukosi kukuta mende.
   
 12. L

  LAT JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Kilimanjaro Water is a registered Trade mark of the Coca Cola Company
   
 13. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #13
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hata ukienda Nairobi utapata maji ya Kilimanjaro my friend..so cool your anger uhai hayauziki kwenye baadhi ya maeneo hiyo ni fact lakini kwetu buguruni ndio hayo hayo uhai tunakatia kiu!
   
 14. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #14
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Si hao tu,hizi agencies zimekuwa kama fashion na mambo ya ulaji tu,toothless.Si mnayaona ya ewura,bei elekezi...blah,blah...
   
 15. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #15
  Apr 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Kula roho yako kitu inataka.TBS unawajua au unawasikia tu?Ukikutana na maji ya mtungini bugia.
   
 16. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #16
  Apr 19, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  majuzi nilimtuma mtu maji akanietea uhai lita mbili yaani ni makubwa mpk nikanawa na uso...
  Kuuliza bei naambiwa ni shilingi mia 8...nikachoka
   
 17. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #17
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,947
  Likes Received: 1,507
  Trophy Points: 280
  Uhai kaka ni low quality kutoka visima vya hapo Kipawa,hata packing yake ni ya kizushi hata mimi kwenye kamugahawa kangu yanaishia nje ya geti basi,pia si maji tu kaka kwenye kumbi au hotel hutakiwa kuingia na vinywaji binafsi kutoka nje ,vinginevyo hizo zitakuwa ni zile hoteli za kariakoo au magomeni kama vile Bismillahi n.k
   
 18. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #18
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asilimia kubwa ya sisi watanzania maji ya UHAI ndio yanatutoa kimaisha maana bei zake ziko chini hata hao watu wa maofisini kwenye vikao vyao tu ndio wanakunywa KILIMANJARO ila majumbani kwao kama kawa tunakandamiza UHAI (KILIMANJARO YANAFANANA NA LILE JINA LA KALE KALAJI CHETU )
   
 19. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #19
  Apr 19, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nayapenda sana maji ya KILIMANJARO tatizo lile jina lake linafanana na kale kabia
   
 20. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #20
  Apr 19, 2011
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kusema ukweli mimi nikiyanywa (Uhai) tumbo huwa linaniuma. Nimeazimia kuachana nayo kabisa vinginevyo niwe sina jinsi ya kupata maji mengine na ninywe kidogo tu kutuliza kiu. Angalau CoolBlue na Maji Afrika yana ubora, Uhai ni mabaya sana na yanachakachuliwa mno na kwa ujumla TBS yake ni karibu na sifuli.
   
Loading...