Vita Janga la Corona, Rais Magufuli Aanza Kusifiwa Duniani!, Jarida la The Economist 'Lamsifu' JPM Kumtegemea Mungu!, Ni Uamuzi Sahihi?, Utatuokoa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
38,402
2,000
Wanabodi,

Asubuhi ya leo, nimepata tena fursa, kuendelea na zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", ambazo ni makala za kuhamasisha uzalendo na huendeshwa kwa mtindo wa maswali, yakifuatiwa na hoja, kisha majibu uyatoe wewe msomaji mwenyewe. Mada ya leo ni kuhusu hatua mbalimbali zinazochukuliwa na nchi tofauti tofauti na viongozi tofauti kupambana na Corona, wakati nchi nyingi zikikumbatia kitu kinachoitwa lockdown, uamuzi wa rais wa Tanzania, Dr. Joseph Pombe Magufuli kugomea lockdown, kwanza uliwashangaza wengi, huku wengine wakiusifu na wengine wakiukosoa katika vita ya kupambana na janga la Corona, Jee uamuzi wa Rais Magufuli sasa waanza kusifiwa Duniani?, Jee Jarida la The Economist 'Lamsifu' rais JPM kwa kitendo chake cha kugomea lock down na kumtegemea Mungu katika kukabiliana na Corona?!, na jee uamuzi huu ni sahihi na utatuokoa na kuliokoa taifa?.
Maswali haya ni kufuatia Jarida la The Economist la wiki hii lililotoka jana usiku, kumsifu kiaina rais Magufuli katika makala maalum ya jinsi viongozi wa Afrika, wanavyopigana na Corona.

Kwa sisi tuliosoma shule za St Kayumba, wakati fulani kuelewa hizi lugha za mabeberu ni issue, hili jarida la mabeberu la the Economist, ambalo kila siku linaitukana Tanzania na kumtukana rais wetu Magufuli, lakini katika hali isiyo ya kawaida, toleo la wiki hii la hili jarida la Mabeberu linaloongoza duniani kwa circulations ambalo siku zote huwa halioni jema lolote kutoka Tanzania, wala kwa rais wetu, lenyewe siku zote likiona mabaya tuu, mapungufu tuu, na kutukana tuu kwa kutuhumu, kukashifu na kushutumu tuu, lakini toleo la leo, japo limeibuka na shutuma lukuki kwa viongozi wengi wa Africa jinsi wanavyo respond kukabiliana na janga la Corona, lakini kwa upande wa Tanzania na hatua alizochukua Rais Magufuli kukabiliana na Corona ni kwa kugomea lockdown na kumtegemea Mungu, naona kama Jarida hili ni kama limemsifu kiaina Rais Magufuli kwa kumtegemea Mungu huku likiwabeza, kuwashutumu na kuwalaumu viongozi wengine wengi wa Africa kwa hatua walizochukua!.

Hebu jisomee mwenyewe,
Some African politicians risk spreading covid through quackery
Kumhusu rais wetu Magufuli, wameandika hivi,
"John Magufuli of Tanzania insists that “we are not closing places of worship. That’s where there is true healing because it is a country that has put God first,”
Jee huku ni kumsifu au ni kumbeza?.

Jarida hili la mabeberu la The Economist kama kawaida yake siku zote, huwa haliwezi kuzungumzia baya lolote la Bara la Africa bila ya kuitolea Tanzania mfano, na kumtaja rais Magufuli kwa ubaya, lakini safari hii, limewashutumu viongozi mbalimbali wa bara la Africa kwa hatua walizochukua kukabiliana na janga la Corona, kwa kuwataja baadhi ya marais na hatua walizochukua kwa kuzibeza kwa kuchagua hatua ambazo zinaonekana kama ni kichekesho, lakini kwa Tanzania, wamemtaja rais Magufuli vizuri na kwa uzuri kuwa kaamua kumtegemea Mungu!.

Ila this time kwa upande wa hatua zilizochukuliwa na Rais Magufuli wa Tanzania, kugomea kufanya lockdown, angalau sasa ametajwa kwa uzuri, kuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, kaamua kumtegemea Mungu, maana kama wange weka ule uamuzi wa kuwapima mbuzi, mapapai, mafenesi hadi oil za magari, kiukweli wangetufanya tuonekane kama kichekesho, lakini wametumia angle ya kumtegemea Mungu, ambayo ni angle nzuri.

Kama The Economist this time wamemtaja rais Magufuli kwa angle nzuri ya kumtegemea Mungu, kwa kulinganisha na jinsi jarida hili linavyompondaga na kumkandia, hii angle ya Corona ni kama linamsifu ila limeshindwa kumsifu waziwazi, jee huu ni uthibitisho wa mwanzo wa mwelekeo mpya na mwelekeo mzuri wa jarida hili kuanza kumwandika vizuri rais Magufuli, kwasababu huko nyuma walikuwa wakimtukana sana, na kuashiria huku sasa ni ishara za mwanzo za Rais Magufuli kukubalika kimataifa?.

Hitimisho.
Namalizia kwa lile swali la msingi la bandiko hili, kuhusu uamuzi wa rais wa Tanzania, Dr. Joseph Pombe Magufuli, JPM , kugomea lock down na kumtegemea Mungu katika kukabiliana na Corona, Jee uamuzi huu ni sahihi na utatuokoa na kuliokoa taifa?.

My Take.
Siku ya Jumamosi asubuhi kwenye kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kinachorushwa live na Star TV, tutakuwa na Waziri wa Habari, Dr. Harrison Mwakyembe, pia tutazungumzia kuhusu negative coverage ya nchi yetu na rais wetu katika media za nje, majirani zetu na za kimataifa, nini kifanyike?.

Viva Magufuli
Viva Tanzania
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
13,016
2,000
That's our President H.E John Magufuli,The best President currently...

Huwa nawaambia Watanzania
Tanzania tumebarikiwa kuwa na kiongozi bora kama Magufuli

Ni kichaa pekee yake anayeweza kupinga Au kumpinga Rais Magufuli
Kwa mara ya kwanza nchi imepata Rais mbovu kuliko wote!Aibu kabisa kuwa na Rais kama jiwe!
 

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,209
2,000
Paskali nchi ngumu hii. pambana tuu mkuu..huwezi jua hata Mwigulu amekumbukwa.

Otherwise itabidi vijana uwaondoe private.....
 

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
13,016
2,000
Aisee... kweli nimeamini mwandishi ni mnafiki, yaani rais wetu anadharauliwa kwa kukosa jinsi ya kupambana na covid na kumuachia Mungu, na bado mtu anasema rais wetu anasifiwa🤔😷
Aibu kweli,hata mimi namshangaa mletq mada!Mtu kadhihakiwa yeye anaona ni sifa,what a shame!
 

Marshall plan

JF-Expert Member
Nov 3, 2019
648
1,000
That's our President H.E John Magufuli,The best President currently...

Huwa nawaambia Watanzania
Tanzania tumebarikiwa kuwa na kiongozi bora kama Magufuli

Ni kichaa pekee yake anayeweza kupinga Au kumpinga Rais Magufuli
Inawezekana huwa usomi na kuelewa kabisa. Kuna mahala amesifiwa au kadhalaulika?😂
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
11,130
2,000
"John Magufuli of Tanzania insists that “we are not closing places of worship. That’s where there is true healing because it is a country that has put God first,”
Jee huku ni kumsifu au ni kumbeza?.
Hiyo ni kumbeza kwa sababu Mabeberu wote, na sie Washika mikoba wao sio tu tunaamini bali tunajua pasi na shaka si kanisa wala kanisa limepata kuwa kinga au tiba ya janga lolote duniani!

Nyie Wazalendo ndie mnaamini hayo, na amini amini nawaambia, yeyote mwenye kuliamini neno la Bwana basi corona itakuwa inamuogopa na kumkimbia haidhuru hata kama mmoja wa Makuhani Wakuu wanaoliamini Neno la Bwana hivi sasa amejificha Chato, kwa maana hayo hutokea ili maandiko yatimie!!
 

kigogo warioba

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
5,720
2,000
Aibu kweli,hata mimi namshangaa mletq mada!Mtu kadhihakiwa yeye anaona ni sifa,what a shame!
hiii ni kwakua kila mtu anataka sifa kwa mkulu au kujiona wa kwanza kujipendekeza na kumsifia, na sasa wengi wao wanashindwa kutambua kati ya sifa na fedheha, hii sio sifa ni fedheha kwa kushindwa na coronya eti tumemwachia Mungu, huu ni upuuzi,
kwanza Mungu ana kazi nyingi na sio za kusikiliza wapiga nyungu
 

kukumweupe

JF-Expert Member
Apr 18, 2020
440
1,000
Mkuu p kama hutojari tuwekee hiyo habari kama ilivyo sisi tunaifahamu English tuweze kunufaika na nakala hiyo maana tangu kabendela apigwe pin the economist linatuheshemu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom