vita ikianza tutawashinda wakristo...kauli ya ajabu hii. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

vita ikianza tutawashinda wakristo...kauli ya ajabu hii.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ubungoubungo, Sep 26, 2008.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2008
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Jamani, jana sikwenda kazini, nikafungulia radio fulani hivi, sijui inaitwa radio heri au nini ile, ya waislam. kulikuwa na shehe mmoja hivi alikuwa anaongoza mjadala wa "kwanini wakristo wanakuwa wazungumzaji wakuu wa mambo ya kiislam kuliko waislam wenyewe", jambo walilokuwa wakisimamia ni kuhusu "mahakama za kadhi" na pili ni "kujiunga na OIC". niliacha vitu vyote nikaanza kusikiliza. sikuamini macho yetu kutokana ya yale yaliyokuwa yakiongelewa.

  nitakoti vitu vichache tu, nilimsikia yule shehe kwa masikio yangu akisema"WAKRISTO WAKIONA WAISLAM TUMEANZISHA VITA, LAZIMA TUTAWASHINDA TU KWASABABU WAO HAWANA HISTORIA YA KUTUSHINDA VITA SISI WAISLAM, NA HAPA TZ HATABAKI HATA MKRISTO MMOJA. watu wengi walipiga simu sana, wakawa wanatoa lugha za chuki na sumu huwezi amini kwamba sisi wote ni watz. wengi walikuwa wakongea kuwa, wakristo wanapendelewa na selikali ndo maana wamepewa majengo mengi ya kujenga shule na vyuo ndo maana vyuo vingi hapa tz ni vya wakristo na shule pia. wakawa wanasema kupewa jengo la Tanesco morogoro kuwa chuo kikuu haitoshi. pia, walikuwa wanasema kuwa, walifikiri kwasababu raisi wetu ni mwislam, walifikiri atafanya chochote kwaajili ya waislam, na wakawa wanaongea kama ku influence kuwa rais anatakiwa afanye hivyo. na kwamba waislam wanaonewa na makafiri ndo maana wengi wao hawajasoma kama walivyo wakristo.

  jamani, nadhani kuna watu wengine mtakuwa mlisikia huu mjadala, hivi hii tz tunaenda wapi kwa kuhubiri chuki na vita kama hizi? hivi kweli watz tunaiweza vita kweli? tunaweza kuishi kwenye vita kweli?tukawaulize wenzetu wa lebanon walipopigana wenyewe kwa wenyewe kwa vita ya kidini wakristo na waislam wamefaidika na nini?, na wakristo huwa hawasikilizi kabisa hizi radio za waislam, muone namna ambavyo tunafanywa target, is this fair?radio gani ya waikristo inahubiri chuki na kuanzisha vita na waislam? is this a tz that we need?

  watu wengine kama mimi, naogopa sana vita,hivi kama wataendelea na mambo kama hayo, ni bora nianze kuhamisha vitega uchumi vyangu nipeleke hata zambia tu au nchi yoyote ile ambayo nitalala bila shida. kauli za kusema kuwa, wakristo hatabaki hata mmoja, na selikali haichukui hatua yoyote ile kwenye kauli kama hizo,ni mbaya sana. Mungu ibariki Tanzania, tuepushe na watu wakatili wanaotaka tuingie kwenye vita ya kuuana. na shetan ameshindwa kwa Jina la Yesu ktk hili, na wafuasi wake wote wameshindwa vilevile. Naamuru kwa jina la Yesu, hakuna vita itakayotokea Tz. amina.
   
 2. M

  Mafuchila JF-Expert Member

  #2
  Sep 26, 2008
  Joined: Apr 29, 2006
  Messages: 752
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Unapoona viongozi wetu wanashinda Kilimani kwenye nyama choma, na kwenye kumbi za mikutano ya kimataifa; mauti na hatihati zinazojongea sio rahisi kwao kuziona; hata kiama cha moto wa Sodoma na Gomora wanaweza kukipokeo kwa vifijo wakidhani ni moto wa kuokea nyama. Kwa kifupi hali ni ngumu, na viongozi wetu wako busy kuirudisha Tarime kundini bila kujua nini cha kuifanyia baada ya kuirudisha kundini.
   
 3. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #3
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,197
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mimi ni Mkristo lakini sijui kuhusu dini ya Kiislamu.
  Naomba kueleweshwa jambo;
  Kwani Mtume Mohamed alileta dini ili watu wapendane au wachukiane na kutukanana?
  Alisema watu wauane na kuua wasio na hatia?
  Vipi kuhusu kusameheana, amekataza hii kitu?
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  iyo kitu mimi pia nilisikia, sio vita ya tarime kama unavyoelewa, ni hate speech za radio moja hivi ya kiislam hapa bongo. this is not good at all, wakristo hatutaki kupigana,kwasababu Mungu wetu tunayemwabudu anakataza kuua. labda kam wenzetu wanaruhusiwa kufanya hivyo,ndo tutakuwa na doubts about their god. lol!.
   
 5. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Kuna msemo "zima moto ungali cheche". Natumaini kuna watu wanaofuatilia suala hili. Kama watu waliweza kumshitaki mahakamani mtu aliyesema "Yesu si Mungu" (sentensi ambayo kwa mtazamo wangu haina athari yoyote, ni expression tu ya imani kama wengine wanavyoamini Mohammad si mtume), nitashangaa kama watanyamaza kimya juu ya jambo kama hili ambalo linaweza kueneza hofu na kutoaminiana miongoni mwa wananchi.
   
 6. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2008
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  ni upungufu (in the their upper chambers)
   
 7. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mimi nilisikia kwa masikio yangu pia,na nilishangaa sana kusiki hivyo. mara nyingi mimi nimekuwa nikisikiliza radio za waislam ili kujifunza kutoka kwao yale wanayoamini na kufikiri. hate speeches kama hizi hazijaanza leo, nashangaa mkuu ndo umesikia tu jana, hii imeanza muda mrefu sana, na viongozi wetu wamenyamaza kimyaa wanalea haya majipu, yakija kuiva ndo yataanza kuuma watu watashindwa hata kukaa...nafikiri mnajua jipu likiwa limeota kunako au kwenye makalio, mwanzoni unaweza kudharau, ila baadae, utajikuta hata kukaa na kutembea unashindwa. prevention is better than cure.
   
 8. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waislam kama mtoto mkorofi.Hata awe na glasi ya maziwa mkononi atalia tu.
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Jamani tuishi kwa kuvumiliana sana....jamani tukifika huko heeee hatutafika popote...
   
 10. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakianzisha vita, wakristo na waislam wote kwa pamoja watakuwa kwenye risk. watakaopona ni wahindu na wabudha kule uhindini tu...hahaha. manake, waislam tz ni asilimia 35% wakati wakristo ni asilimia 45%. go to cii fact book na data zingine utapata. waliobaki ni watu wasiokuwa na dini kama maasai na wengine. it is interesting kwamba, wataanza kutuua wakristo asilimia zote hizo wakamaliza wakati wakristo hawajajibu. one can imagine hali itakavyokuwa mbaya hapo. na je, waislam watapata faida gani hapo? au ndo watasali vizuri kukiwa na vita? jibu ni kwamba, ndio maana inaitwa vita, wakristo nao watadefend themselves na itakuwa hali mbaya kwa wote, na kidonda hicho hakitakuja kupona milele, chuki hiyo haitakuja kuondoka milele. vishehe vya ajabu kama hivi ni vya kufunga kabisa. vinasababisha tuwaelewe vibaya waislam wote,kumbe kuna waislam wengine hata hawapendi hate speeches kama hizo. naomba selikali ilichukulie makini hili jambo,na radio hizi zifuatiliwe na usalama wa taifa. period.
   
 11. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,959
  Trophy Points: 280
  "Show me just what .... brought that was new, and there you will find things only evil and inhuman, such as his command to spread by the sword the faith he preached" - Byzantine emperor Manuel II Paleologus
  Na
  "Religion and violence do not go together but religion and reasoning do" - Benedict XVVI
   
 12. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Tuzuie vita vya kidini Tz,na Mungu atusaidie. wanaohubiri chuki wote watakufa wao, sisi tutabaki.
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2008
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  kuna mamlaka ya kuregulate vyombo kama hivi. TCRA . Wako wapi ? Kama na wao wameshindwa kazi tuambiwe wazi ili tujue la kufanya kama alivyofanyiwa Mtikila.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Sep 26, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wanabodi,
  Mada hii haifai kuletwa hapa hata kidogo kwa sababu ni kuchangia na kusambaza maelezo ya mtu mmoja mpumbavu ktk redio...
  Huyu mtu hata kama anaitwa sheikh haina maana ni kiongozi wa kiislaam. Kwanza inabidi mfahamu hakuna kitu kiongozi ktk dini ya kiislaam hasa dhehebu la Sunni isipokuwa kuna viongozi wa sala, ama jambo lolote kwa wakati huo tu...Waislaam hawana mtu mbora kuliko mwingine mbele ya Mungu isipokuwa yule mwenye kufanya ibada hivyo hakuna kitu kiongozi wa waislaam.
  Huyo mhusika aliyepewa nafasi kuzungumza ktk redio ni mjinga mmoja kama yule wa Rwanda na wapo wengi sana aina hii kwani nimewahi kusikia redio za kikristu zikizungumzia Uislaam kama ni dini ya mashetani na kadhalika...lakini sikuyachukulia maanani kwa sababu ni Wajinga tu ndio waliwao...
  Mtu mzima mwenye akili zake hupuuza ujinga na kuendelea kusikiliza ujinga ina maana unaanza kuamini ujinga....
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...